taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 06 Sep 2026 12:29:25
Ondiek alivyobwaga shemeji yake James Orengo uchaguzi wa 1983
STEPHEN Oluoch Ondiek alikuwa miongoni mwa wanasiasa wa Nyanza waliopitia nyakati tofauti za siasa za Kenya, kutoka enzi ya chama kimoja hadi mfumo wa vyama vingi. Mwaka 2001, Rais wa wakati huo Daniel arap Moi alimteua Ondiek kuwa Waziri wa Maendeleo ya Wafanyakazi, wakati ambapo viongozi wengi wa Nyanza walikuwa wameondoka KANU na kujiunga na upinzani. Baada ya kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, sehemu kubwa ya Nyanza, hasa jamii ya Luo, ilijitenga na utawala wa Moi. Kiongozi wao mkuu alikuwa Jaramogi Oginga Odinga, ambaye mwaka huo aligombea urais kupitia FORD-Kenya. Lakini safari ya Ondiek katika siasa ilianza akiwa ndani ya KANU. Kwa kushangaza, alikuwa kiongozi wa Kanisa la Legio Maria Afrika kabla ya kuingia kwenye siasa za uchaguzi. Alikuwa amehimizwa na Jaramogi kuingia katika siasa za kuchaguliwa mwaka 1983. Wakati huo KANU ilikuwa chama pekee cha kisiasa kilichoruhusiwa nchini na kilikuwa kikitajwa kwa kaulimbiu ya "baba na mama". Ondiek alitumia nafasi yake ya kidini kuwafikia wapigakura na kufanikiwa kushinda kiti cha Ugenya katika uchaguzi wa 1983 akibwaga shemeji yake, James Orengo. Hata hivyo, Ondiek alikaa miaka kadhaa kama mbunge wa kawaida kabla ya Moi kumteua kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Kazi za Umma. Alirejea bungeni mwaka 1988 baada ya kushinda uchaguzi uliofanyika kwa mfumo wa mlolongo, ambapo wapigakura walipanga foleni nyuma ya mgombea waliyemtaka. Lakini mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa mwaka 1992, Orengo alirejea na kumshinda Ondiek katika kinyang'anyiro cha Ugenya. Orengo aliendelea kuwa mbunge wa Ugenya hadi 2013 alipogombea useneta wa Siaya. Ondiek hakurejea tena Bungeni kama mbunge hadi alipofariki mwaka 2011. Kwa kipindi fulani, aliongoza tawi la KANU Siaya. Nafasi hiyo ilikuwa imeshikiliwa na William Odongo Omamo kabla ya kuondoka KANU na kujiunga na National Development Party (NDP) iliyoongozwa na Raila Odinga mwaka 1997. Jina la Ondiek lilipata umaarufu zaidi nchini alipokuwa waziri. Akiwa Bungeni, mara nyingi alijibu maswali ya wabunge kwa niaba ya wizara yake na mawaziri wenzake ambao hawakuwepo. Lakini urithi wake mkubwa ulikuwa katika elimu. Ondiek alikuwa na shauku kubwa ya elimu na aliwekeza katika shule za msingi na sekondari jijini Nairobi, Kisii na eneo lake la Siaya. Hata hivyo, baadhi ya wapigakura wake walimshutumu kwa kutumia vibaya nafasi yake kama mlezi wa Hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge ya Ugenya (CDF). Walidai kuwa alizipendelea shule alizohusishwa nazo wakati wa kugawa fedha za karo kwa wanafunzi wasiojiweza. Mwaka 2002, familia yake ilikumbwa na msiba mkubwa. Watoto wake walikuwa wakirejea Nairobi baada ya kumsaidia kushinda uteuzi wa chama wakati gari lao lilipopata ajali. Watatu kati yao walifariki katika ajali hiyo, katika pigo kubwa kwa familia hiyo. Maisha ya Ondiek yanaakisi mabadiliko makubwa ya siasa za Nyanza kutoka enzi ya KANU na mfumo wa chama kimoja hadi siasa kali za vyama vingi zilizoibadilisha sura ya eneo hilo.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Sun, 06 Sep 2026 12:10:44
Babu Owino: Linda Mwananchi to unveil new party with like-minded leaders
Linda Mwananchi leadership plans to unveil a new political party that will challenge ODM dominance in Nyanza and other parts of the country, Embakasi East MP Babu Owino has said.
read morekenyanews.go.ke
@kna Sun, 06 Sep 2026 11:21:57
MCK to establish modern media workstations in Isiolo, Meru ahead of 2027 polls
The Media Council of Kenya (MCK) plans to establish modern media workstations in Isiolo and Meru counties to strengthen journalism and enhance coverage of development and community issues ahead of the 2027 General Election. MCK board members announced the plans during a meeting with journalists in Isiolo town, where they also visited the Kenya News...
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 06 Sep 2026 11:24:08
US envoys arrive in Ukraine for talks after meeting Putin in Russia
Two US envoys are hoping for equally productive meetings in Ukraine after holding talks with Russian President Vladimir Putin in Moscow on ending the war, US officials say. Steve Witkoff and Jared Kushner arrived in Kyiv on Sunday, having discussed substantive plans for next steps with Putin on Saturday, according to the White House. It [...] The post US envoys arrive in Ukraine for talks after meeting Putin in Russia appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 06 Sep 2026 11:46:48
Evan Roos Siblings: Getting to Know Taila and Rohland
Evan Roos is a professional rugby union player known for his versatility and physical prowess. Born on 21 January 2000 in Pretoria, South Africa, he stands at an imposing 1.91 metres and weighs around 109 kilograms. He is a product of a strong rugby schooling system, having attended Paarl Boys High School, a renowned institution [...] The post Evan Roos Siblings: Getting to Know Taila and Rohland appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 06 Sep 2026 10:36:21
How Land Buyer Was Conned Sh2.4 Million by Imposter in Machakos
A Machakos land buyer lost Sh2.4 million after a suspected fraudster allegedly posed as the owner of a prime parcel of land along the Nairobi-Mombasa highway using forged identity documents and a fake title deed. Detectives based in Kalama Sub-County have arrested the suspect, identified as David Maitha, who allegedly operated for months using the [...] The post How Land Buyer Was Conned Sh2.4 Million by Imposter in Machakos appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 06 Sep 2026 10:12:18
How Detectives Cornered Suspected Mastermind in Motorcycle Theft Syndicate in Meru
A suspected mastermind in a motorcycle theft and robbery-with-violence syndicate operating in Meru County and its environs has been arrested. Detectives from the Directorate of Criminal Investigations (DCI) Mutuati arrested Evans Munene Kinyua, alias "Mutharimi", following an intelligence-led operation in Ngitana, Mutuati Sub-County. According to the DCI, Kinyua is believed to be a key player [...] The post How Detectives Cornered Suspected Mastermind in Motorcycle Theft Syndicate in Meru appeared first on Kahawatungu.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Sun, 06 Sep 2026 09:47:35
Kenya Railways Issues New Clarification on SGR Tickets Booked Via Mobile Money
Madaraka Express passengers can book SGR tickets by visiting the Kenya Railways Booking Portal to choose their travel details, select seats, and pay via mobile money.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 06 Sep 2026 09:55:13
Siri ya ziara ya Gachagua Amerika
KIONGOZI wa chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP), Rigathi Gachagua, anatarajiwa kuanza rasmi shughuli zake za kisiasa nchini Amerika kesho Jumatatu baada ya kukamilisha mapumziko ya siku 10 akiwa pamoja na mkewe, Mchungaji Dorcas Rigathi. Bw Gachagua, ambaye aliondoka nchini Agosti 26 kuelekea Amerika, alisema aliamua kwanza kutumia muda wa faragha na familia kabla ya kuanza mikutano yake ya kisiasa na wafuasi wa chama hicho walio Amerika. Mwanasiasa huyo amekuwa akichapisha picha akiwa na mkewe wakifurahia mapumziko, ikiwemo safari za boti zenye mwendo kasi na matembezi asubuhi. "Familia ni muhimu sana. Nilihitaji kwanza kupata muda wa kutosha pamoja na mke wangu ambaye ameendelea kunipa nafasi ya kushughulikia siasa nyumbani Kenya. Baada ya mapumziko hayo nitaanza mikutano ya kisiasa kuhusu hali ya nchi, umuhimu wa kujenga DCP, haja ya kuwa na mgombea mmoja wa urais wa upinzani, pamoja na malengo na bajeti yetu," alisema Gachagua. Kiongozi huyo wa DCP alisema atakuwa na mikutano ya hadhara na ya faragha huku akijaribu kujenga chama chake kama mshirika muhimu katika juhudi za kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini Kenya kupitia njia za kidemokrasia. Alisema mojawapo ya malengo yake ni kuhimiza muungano wa upinzani kutafuta viongozi bora watakaowania nyadhifa mbalimbali katika serikali ya kitaifa na za kaunti. "Nitakutana na wafuasi kutoka Mlima Kenya na sehemu nyingine za nchi. Tumeanzisha sera ya kukusanya wote na kutomtenga yeyote ndani ya DCP. Tunauza maono ya chama na ajenda ya kitaifa kuhusu kwa nini ni muhimu kuondoa Kenya katika hali ya sasa chini ya utawala wa Rais William Ruto. Tuna malengo, mikakati na pia pengo la kifedha ambalo tunahitaji kuziba," alisema. Kwa mujibu wa Gachagua, siku 45 zijazo atakazokuwa Amerika zitalenga kutafuta uungwaji mkono kisiasa na kifedha kutoka kwa Wakenya wanaoishi ughaibuni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Ratiba iliyotolewa na DCP inaonyesha kwamba hadi Septemba 10 atakuwa katika mji wa Spokane, jimbo la Washington, ambako atahudhuria mikutano ya hadhara pamoja na vikao vya faragha na watu wanaotajwa kuwa muhimu kwa ajenda ya chama.
read moreRight Column Content