kahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 05 Sep 2026 04:55:55
Why are European countries moving their gold out of North America?
When the central bank of the Netherlands confirmed this week that it had moved tonnes of the countrys gold out of North America, it said the relocation would make it better prepared for severe crises. Some 86 tonnes from the combined total of about 313 tonnes held in the US and Canada were relocated to [...] The post Why are European countries moving their gold out of North America? appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sat, 05 Sep 2026 04:58:57
Indian state gives taxi and tuk-tuk drivers a year to learn local language
An Indian state has given taxi and tuk-tuk drivers one more year to learn the local language after a new rule making it mandatory sparked protests. Transport officials in the western state of Maharashtra had begun testing drivers ability to conduct basic conversations in Marathi, the states official language, on 20 August. Those who failed [...] The post Indian state gives taxi and tuk-tuk drivers a year to learn local language appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sat, 05 Sep 2026 04:55:13
Simu zatumika kufuatilia kuenea kwa Ebola DRC
MAAFISA wa afya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wameanza kutumia data ya simu za mkononi kufuatilia mienendo ya watu na kutambua maeneo ambayo Ebola inaweza kuenea. Hii ni kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO). Teknolojia hiyo, ambayo haijawahi kutumika katika kukabiliana na mlipuko wa Ebola, huchanganua taarifa mbalimbali ya mawasiliano ya watu. Hivyo, wataalamu wanaweza kukadiria maeneo ambayo watu husafiri na kutambua maeneo yaliyo katika hatari. Uchambuzi huo unafanywa na shirika la Sweden, Flowminder, kwa kutumia data inayotolewa bila malipo na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom. Taarifa hizo hukusanywa kwa njia fiche bila watafiti kuingilia taarifa binafsi za watumiaji. Kisangani, kitovu muhimu cha usafiri, kilitambuliwa mapema kuwa katika hatari kutokana na idadi kubwa ya wasafiri kutoka maeneo yaliyoathiriwa. WHO iliimarisha maandalizi huko kabla ya visa vya kwanza kugunduliwa. Hadi sasa, mlipuko huo umeenea katika majimbo sita, huku zaidi ya watu 6,250 wakiambukizwa na 3,039 kufariki tangu mlipuko huo kutangazwa Mei 15. Ugonjwa huo unasababishwa na Bundibugyo, ambayo haina chanjo wala tiba iliyoidhinishwa.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sat, 05 Sep 2026 03:55:30
Onyo latolewa kuhusu usalama wa maziwa upungufu ukiendelea
WASIWASI kuhusu usalama wa maziwa umeongezeka huku upungufu wa bidhaa hiyo ukiendelea kushuhudiwa nchini, na kusababisha ongezeko la bei pamoja na kuibuka kwa wauzaji wasio rasmi. Wataalamu wa afya ya umma wameonya kuwa uhaba wa maziwa unaweza kuwafanya baadhi ya wafanyabiashara kutumia mbinu zisizofaa ili kukidhi mahitaji ya soko. Miongoni mwa hofu zilizopo ni uwezekano wa kuuzwa kwa maziwa yasiyopitia ukaguzi unaohitajika au yale yaliyohifadhiwa katika mazingira yasiyo salama. Kutokana na kupungua kwa upatikanaji wa maziwa yaliyosindikwa, baadhi ya watumiaji wamegeukia maziwa yanayouzwa moja kwa moja na wafugaji au wauzaji wa mitaani. Ingawa maziwa hayo yanaweza kuwa salama yakishughulikiwa ipasavyo, wataalamu wanasisitiza umuhimu wa kuyachemsha kabla ya matumizi ili kuzuia magonjwa yanayoweza kuenezwa kupitia maziwa mabichi. Wadau wa sekta ya maziwa wanasema hali ya sasa imechangiwa na ukame na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yamepunguza malisho na maji kwa mifugo. Matokeo yake ni kushuka kwa uzalishaji wa maziwa katika maeneo mengi yanayozalisha bidhaa hiyo nchini. Mamlaka za udhibiti zimewahimiza wananchi kununua maziwa kutoka kwa wauzaji wanaotambulika na kuhakikisha bidhaa wanazonunua zimeidhinishwa kwa matumizi ya binadamu. Pia zimeonya dhidi ya kushawishiwa na bei nafuu kutoka kwa vyanzo visivyoaminika.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sat, 05 Sep 2026 02:55:45
Nchi kukumbwa na janga la ukosefu wa chakula
KENYA inakabiliwa na hatari ya upungufu mkubwa wa chakula huku wakulima katika maeneo yanayolisha taifa wakisita kupanda tena zao hilo baada ya ukame kuangamiza mazao ya awali. Hofu hiyo inatanda licha ya serikali kutumia mabilioni ya fedha kupunguza gharama ya mbolea na mbegu katika juhudi za kuwashawishi wakulima kurejea mashambani msimu huu. Katika maeneo ya North Rift, yanayojulikana kama ghala la chakula la Kenya, hali ya kusubiri na kuona imetawala. Wakulima wengi wanahofia kupanda tena mahindi baada ya kupata hasara kutokana na ukame na magonjwa ya mimea. Serikali imepunguza bei ya mbolea ya ruzuku kutoka Sh2,500 hadi Sh2,000 kwa gunia la kilo 50, huku ikigharamia nusu ya bei ya mbegu bora za mahindi. Hatua hiyo imeshusha bei ya mbegu kutoka Sh300 hadi Sh150 kwa kilo. Lakini kwa wakulima wengi, punguzo hilo halitoshi kuondoa hofu ya kupata hasara nyingine. William Kosgei, mkulima kutoka Ziwa, Uasin Gishu, alisema gharama za kilimo ni zaidi ya mbolea na mbegu. "Kilimo si suala la kupunguza tu gharama ya mbolea na mbegu za mahindi. Bado kuna gharama kubwa za mafuta ya trekta kutayarisha mashamba, dawa za kuua magugu na mishahara ya wafanyakazi. Aidha, hali ya hewa isiyotabirika inafanya kuwa hatari kupanda zao lile lile kwa mara ya pili katika msimu mmoja," alisema. Kwa miaka mingi, wakulima wa mahindi North Rift wamezoea kupanda zao hilo mara moja kwa mwaka. Sasa wengi wao wanaombwa kupanda tena baada ya zao lao kuharibiwa na ukame mkali na milipuko ya magonjwa. Hii imezua swali kubwa kuhusu iwapo wakulima wako tayari kuhatarisha mtaji wao tena. Mkurugenzi wa Chama cha Wakulima Kenya (KFA), Kipkorir Menjo, alisema hofu imeenea miongoni mwa wakulima. "Kuna mashaka makubwa miongoni mwa wakulima kuhusu iwapo wapande tena au wasubiri msimu ujao. Mabadiliko ya tabianchi yamesababisha hali ya hewa kutotabirika na wakulima wanaogopa kupata hasara nyingine kutokana na majanga ya kiasili," alisema. Bw Menjo alisema wakulima wengi bado wanahangaika kulipa mikopo waliyochukua kufadhili mazao yaliyoharibiwa. "Wakulima waliopata mikopo ya mamilioni ya shilingi kutoka taasisi kama Agricultural Finance Corporation (AFC) sasa wanakabiliwa na changamoto ya kulipa madeni hayo huku wakihitajika kuwekeza katika zao jingine," alisema. Hali hiyo inaweka shinikizo zaidi kwa sekta ya kilimo ambayo tayari inakabiliwa na athari za mabadiliko ya tabianchi. Uasin Gishu na Trans Nzoia, ambazo ni miongoni mwa kaunti muhimu katika uzalishaji wa mahindi, zimeathiriwa na ukame, na hivyo kuongeza hofu kuhusu uzalishaji wa chakula katika msimu unaokuja. Serikali, hata hivyo, imeamua kuongeza ruzuku kwa matumaini ya kuzuia wakulima kuacha kilimo. Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo Mutahi Kagwe alisema bei ya gunia la kilo 50 la mbolea imeshushwa kwa Sh500, kutoka Sh2,500 hadi Sh2,000. "Kiini cha mpango huu ni kuhakikisha kwamba mkulima aliyepoteza zao kutokana na ukame hapotezi pia uwezo wa kupanda zao linalofuata kwa sababu ya kushindwa kumudu gharama za mbolea na mbegu," alisema. Hata hivyo, kwa wakulima wanaokabiliwa na madeni, gharama za kutayarisha mashamba na hali ya hewa isiyotabirika, bei ya mbolea pekee huenda isiwe kichocheo cha kutosha. Hofu yao ni kwamba, kupanda tena bila uhakika wa mvua kunaweza kuwa mwanzo wa hasara nyingine. Na ikiwa maelfu ya wakulima wataamua kusubiri hadi msimu ujao, athari zake zinaweza kwenda mbali zaidi ya mashamba yao. Zinaweza kuathiri upatikanaji wa mahindi, bei ya chakula na usalama wa chakula nchini. Kwa sasa, Kenya iko katika mashindano dhidi ya muda: Serikali inataka mashamba yarejee katika uzalishaji, lakini wakulima wanataka kwanza uhakika kwamba hawatapelekwa tena kwenye mzunguko wa madeni na hasara.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 04 Sep 2026 21:54:05
What happens next after Lindsay Clancy's murder case ends in a mistrial?
After a week of mulling Lindsay Clancys fate, a judge has declared a mistrial in the case of the US mother accused of murdering her three young children. It came after the jury said they could not reach a unanimous verdict on whether Clancy was guilty of murder. The declaration opens the door to a [...] The post What happens next after Lindsay Clancys murder case ends in a mistrial? appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content