kahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 23 Aug 2026 07:22:49
MPs Pledge Support for Expansion of Police Training Facilities Across Kenya
The National Assembly Departmental Committee on Administration and Internal Security has pledged to support efforts to secure additional resources for the expansion and improvement of police training facilities across the country. The committee, led by Narok West MP Gabriel Tongoyo, made the commitment on Saturday during an inspection of the Magado Field Campus, operated by [...] The post MPs Pledge Support for Expansion of Police Training Facilities Across Kenya appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 23 Aug 2026 07:30:29
Leading African Institutions, Entrepreneurs and Professionals to Be Honored in Nairobi
Leading institutions, entrepreneurs and professionals from across Africa are set to be honoured at the 2026 Pacesetters International Awards (PIA), a Pan-African recognition programme celebrating excellence, innovation and transformative leadership. The awards ceremony is scheduled for September 25, 2026, in Nairobi, Kenya, and is expected to bring together influential figures from government, business, academia, diplomacy [...] The post Leading African Institutions, Entrepreneurs and Professionals to Be Honored in Nairobi appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 23 Aug 2026 06:55:56
Ruto atua ngome ya Kalonzo na minofu uchaguzi ukikaribia
RAIS William Ruto amewataka viongozi wa upinzani kutafuta hoja bora za kupinga ajenda yake ya maendeleo badala ya kuwagawanya Wakenya kwa misingi ya ukabila. Rais alisema hayo jana alipofanya ziara katika Kaunti ya Machakos, ngome ya kisiasa ya kiongozi wa Wiper Patriotic Front Kalonzo Musyoka, huku akijaribu kuvutia wakazi wa Ukambani kuelekea uchaguzi wa 2027. Rais pia alishutumu upinzani kwa kukosa ajenda thabiti ya kisiasa na kudai baadhi yao wanafanya kazi kwa niaba ya viongozi wengine. "Ingawa umeajiriwa na umekubali kuwa kikaragosi, usijiaibishe. Mnaenda kusema tatizo kubwa la mpango wa nyumba za bei nafuu ni kuku kushindwa kupanda ngazi. Huo ni ujinga. Tafuteni hoja bora," alisema Rais Ruto katika mikutano mitatu aliyoandaa Machakos. Aliongeza: "Mnaendelea pia kusema mtavunja SHA. Tafuteni hoja bora ya kuwasilisha kwa Wakenya." Rais alisema wakati umefika ambapo Wakenya wanapaswa kuwahukumu viongozi kwa rekodi zao za uongozi, mipango na maono badala ya matusi na kauli za kisiasa. "Wakenya hawana haja na wale wanaowagawanya kwa kuwaita wengine binamu, wengine wasaliti na wengine maadui. Kenya inahitaji umoja. Sisi sote ni ndugu," alisema katika mkutano Kimutwa Township.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 23 Aug 2026 05:58:52
Man dies after being mauled by stray dogs in Kiambu
A 35-year-old man died after he was attacked and mauled by several stray dogs while walking home in Githunguri village, Kiambu County, in the early hours of Saturday. The incident occurred at about 3am on August 22, 2026. According to police, George Kimani Gitangia was attacked by several stray dogs while on his way home. [...] The post Man dies after being mauled by stray dogs in Kiambu appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 23 Aug 2026 06:01:44
Carney say Trump started trade war with fresh tarrifs 'attack'
Prime Minister Mark Carney has said a fresh wave of US tariffs on Canada is a miscalculation designed to hurt and divide us, after trade talks collapsed late on Friday. They asked too much and they offered too little, Carney said on Saturday, adding that the US and Canada were now in a trade war. [...] The post Carney say Trump started trade war with fresh tarrifs attack appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 23 Aug 2026 06:04:04
Dozens of people abducted in attacks on villages in Nigeria, police say
More than 100 people have been abducted in attacks on several villages in Nigerias central Niger State, police and residents have told the BBC. The attackers, who were reportedly wearing military-style clothing, targeted communities in the Borgu Local Government Area after Fridayprayers. Police spokesman Wasiu Abiodun said more than 40 people were also killed in [...] The post Dozens of people abducted in attacks on villages in Nigeria, police say appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 23 Aug 2026 05:54:07
Two cousins drown while bathing in river Lusumu in Kakamega
Two children aged seven and 10 drowned while bathing in River Lusumu in Mumias East, Kakamega County, on Saturday evening. The deceased were aged 10, a Grade Three learner at Kamashia Comprehensive School, and 7, a Grade Two learner at St Peter's Mumias Primary School. The two, who were cousins, drowned at Mululi Village in [...] The post Two cousins drown while bathing in river Lusumu in Kakamega appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 23 Aug 2026 05:56:42
Protests after man shot dead at Del Monte Farm in Murang'a
Police in Murang'a are investigating the shooting of a 23-year-old man at a Del Monte farm, an incident that sparked protests along the Thika-Kenol highway on Saturday. A mob moved to the main highway where the body of Peter Kimani Gitau, a 23-year-old man, was taken and blocked the traffic flow for several minutes. The [...] The post Protests after man shot dead at Del Monte Farm in Murang'a appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 23 Aug 2026 05:55:18
Kindiki asema atazima kabisa nyota ya Gachagua Mlimani
NAIBU Rais Kithure Kindiki amesema yuko tayari kumkabili mtangulizi wake Rigathi Gachagua katika vita vinavyozidi kupamba moto vya kudhibiti siasa za Mlima Kenya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027. Prof Kindiki na Bw Gachagua wanadai kuwa wana ushawishi mkubwa katika eneo hilo lenye wapigakura wengi, huku kila mmoja akijigamba kuwa ana uwezo wa kumbwaga mwenzake katika uchaguzi ujao. Bw Gachagua ameapa kumzuia Rais William Ruto kupata uungwaji mkono Mlima Kenya, huku Prof Kindiki akijenga mtandao wa kisiasa wa kuzuia upinzani kutwaa eneo hilo. Jambo moja linalowaunganisha wapinzani hao ni juhudi za kuunganisha Mlima Kenya, lakini kila mmoja akitaka umoja huo umfaidi kisiasa. Jumamosi, Prof Kindiki aliendeleza kampeni zake za kuimarisha ushawishi wake Mlima Kenya Mashariki alipokutana na zaidi ya viongozi 20,000 wa mashinani kutoka Meru, Tharaka Nithi, Embu na Isiolo katika Uwanja wa Kinoru. Mkutano huo uliwahusisha magavana, maseneta, wabunge, wazee wa vijiji, wahamasishaji wa afya ya jamii, madiwani wa sasa na wa zamani. Ulijiri siku moja baada ya Naibu Rais kukutana na maafisa 15,000 wa UDA wanaosimamia vituo vya kupigia kura, ambao aliwataka kuwa mabalozi wa chama hicho tawala. Prof Kindiki alisema atafuta ushawishi wa upinzani katika kipindi cha mwaka mmoja kuelekea uchaguzi, akidai ana uzoefu mkubwa wa kampeni kuliko Bw Gachagua. "Upinzani usithubutu kunichokoza. Gachagua amekuwa akiona mambo ni rahisi Mlima Kenya kwa sababu sisi tulikuwa tumejishughulisha na kazi huku wao wakifanya kampeni," alisema. Alisema amewahi kuendesha kampeni za urais katika Mlima Kenya na kushinda. "Wakati kampeni zitaanza, kura zitamiminika kwenye kapu la Rais. Bila kujali yaliyotokea Ol Kalou, tutashinda upinzani 2027," alisema. Prof Kindiki pia alimkejeli kiongozi wa DCP akimtaja kama "simba wa karatasi" na kumtaka akabiliane naye moja kwa moja. "Tuonane ana kwa ana na tushindane kama wanaume ili kutofautisha kiongozi wa kweli na bandia. Wale wanaojigamba ni simba wa karatasi," alisema. Naibu Rais alisema mikutano yake na viongozi wa mashinani inalenga kuunda mtandao wa wafuasi ambao wataweza kueleza mafanikio ya serikali ya Rais Ruto. Alisema viongozi hao watakuwa mabalozi wa serikali katika maeneo yao na kuwafahamisha wananchi kuhusu utekelezaji wa Ajenda ya Mabadiliko kutoka Chini kwenda Juu. Prof Kindiki aliorodhesha mafanikio ambayo serikali inadai imepata katika miaka minne, yakiwemo ruzuku za kilimo, kuajiriwa kwa zaidi ya walimu 100,000 na utulivu wa thamani ya shilingi dhidi ya dola. Pia alitaja kupungua kwa bei ya unga na mabadiliko katika huduma za afya kupitia Mamlaka ya Afya ya Jamii. Katika michezo, alisema serikali inajenga Uwanja wa Talanta na viwanja vingine 33 katika maeneo mbalimbali nchini. Prof Kindiki pia aliwataka wakazi kuunga mkono msimamo wa mabaraza ya wazee wa Mlima Kenya Mashariki wa kutaka eneo hilo liwe na msimamo mmoja wa kisiasa kuunga serikali. "Mlima Kenya ni mmoja kisiasa, kijamii, kiuchumi na kitamaduni. Ni watu wachache wanaotaka kutugawanya," alisema. Magavana Cecily Mbarire wa Embu, Muthomi Njuki wa Tharaka Nithi na Isaac Mutuma wa Meru waliahidi kushirikiana na Prof Kindiki kuunganisha eneo hilo kumuunga mkono Rais Ruto. Gavana Mbarire alisema wakati umefika kwa wakazi wa Mlima Kenya Magharibi kuonyesha ikiwa wanaweza kuthamini uhusiano uliopo kati ya maeneo hayo. Gavana Njuki alisema watasaidia kuimarisha uungwaji mkono wa Naibu Rais na Rais Ruto. "Ni msimamo wetu kwamba Kindiki abaki Naibu Rais hata baada ya 2027," alisema.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 23 Aug 2026 04:55:54
Ndindi Nyoro akoroga hesabu za Gachagua Mlimani
KIONGOZI wa chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP), Rigathi Gachagua anakabiliwa na changamoto mpya katika juhudi zake za kudhibiti siasa za eneo la Mlima Kenya, mwezi mmoja tu baada ya ushindi mkubwa wa chama chake katika uchaguzi mdogo wa Ol Kalou. Katika uchaguzi huo wa Julai 17, mgombeaji wa DCP, Kamau Ngotho alipata kura 35,440, sawa na asilimia 85 ya kura zote, dhidi ya mgombeaji wa United Democratic Alliance (UDA) aliyeungwa mkono na Rais William Ruto, Muchina Nyaga, aliyepata kura 5,450. Ushindi huo ulimpa Bw Gachagua nguvu mpya na kumfanya kujitangaza kuwa kiongozi asiye na mpinzani wa kisiasa katika Mlima Kenya, huku akitaja DCP kama chama chaguo la wakazi wa eneo hilo. Katika uchaguzi huo, Jubilee ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta ilipata kura 198 huku Party of National Unity (PNU) ya aliyekuwa Gavana wa Meru Peter Munya ikipata kura 28. Lakini mwezi mmoja baadaye, Bw Gachagua anakabiliwa na upinzani mpya, huku hatua ya Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro kujiunga na People's Party of Kenya (PPK) na kuwa kiongozi wake ikiwa changamoto kubwa zaidi. Bw Nyoro anasema chama chake ni sehemu ya upinzani na kinalenga kushirikiana na vyama vingine kupata mgombea mmoja wa urais kwa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, pamoja na kuondoa serikali ya Rais Ruto madarakani. Hata hivyo, Bw Gachagua na washirika wake wamemtaja Bw Nyoro kama mpinzani anayelenga kuvuruga juhudi za kuunganisha kura za Mlima Kenya. "Mlima ni mmoja, chama ni kimoja (DCP), na kiongozi wa eneo ni mmoja (Gachagua)," alisema Kaimu Katibu Mkuu wa DCP John Methu, ambaye pia ni Seneta wa Nyandarua. Bw Nyoro, hata hivyo, amesisitiza kuwa yeye ni kiongozi halisi wa upinzani anayelenga kuimarisha ajenda ya upinzani. "Nitafanya kazi na viongozi wote wa upinzani, akiwemo Bw Gachagua, na chama changu hakitakuwa mahali pa kukimbilia watu waliokataliwa na Mlima ambao wamekuwa wakitukana DCP na uongozi wake," alisema. "Najua kuna wanaonitilia shaka. Lakini baada ya muda mtaona msimamo wangu kamili katika kupinga na kuondoa serikali hii madarakani." Mchanganuzi wa siasa Gasper Odhiambo alisema Bw Nyoro ana haki ya kidemokrasia kuanzisha chama na kujiunga na upinzani, lakini muda na namna alivyoingia kwenye siasa za upinzani huenda zikamfanya akabiliane na upinzani mkali. "Bw Gachagua ana haki yote kumchukulia Bw Nyoro kuwa mpinzani wake. Swali ni kwa nini Bw Nyoro alisubiri hadi Bw Gachagua aondolewe kwa kura ya kutokuwa na imani, akabiliane na makundi ya wahuni na maafisa wa polisi waliopotoka, ndipo aanze kuhamasisha Mlima Kenya kuingia upinzani," alisema. Bw Odhiambo alisema Bw Gachagua mwenyewe alipitia upinzani kama huo baada ya kuondolewa kwenye wadhifa wa Naibu Rais. Alisema wakati huo Jubilee na PNU tayari vilikuwa katika upinzani. "Bw Nyoro ameingia kushindana na Bw Gachagua na DCP. Kisichojulikana ni kama anafanya hivyo kwa niaba yake mwenyewe au kuna nguvu iliyojificha nyuma ya pazia la siasa." Bw Odhiambo pia alikumbusha kuwa kabla ya Bw Gachagua kuondolewa madarakani Oktoba 2024, washirika wa Bw Nyoro katika Kaunti ya Murang'a, wakati huo wakiongozwa na Seneta Joe Nyutu, walikuwa wamemuonya Rais Ruto kuwa angehatarisha kiti chake ikiwa angemwacha Bw Gachagua na kumchagua Bw Nyoro. "Upinzani wa Bw Nyoro dhidi ya Bw Gachagua si jambo jipya. Umekuwepo tangu 2022," alisema. Alisema katika shughuli zote rasmi za Bw Gachagua katika Mlima Kenya akiwa Naibu Rais, Bw Nyoro hakuhudhuria hata moja. "Wakati Bw Gachagua aliondolewa mamlakani na kujitahidi kujijenga kisiasa upya, Bw Nyoro alikuwa amekaa katikati. Sasa kwa kuwa Bw Gachagua anaonekana kurejea kwa nguvu, Bw Nyoro anaingia katika uwanja huo akiwa na chama na azma ya kushindana naye. Bw Nyoro ana mengi ya kueleza," alisema. Katika mkutano wa kisiasa Kiharu Agosti 19, Bw Nyoro aliwaomba wakazi wamuamini na akasisitiza kuwa yeye si msaliti. "Ni kwamba mamlaka huchukuliwa, hayapeanwi. Lazima nijionyeshe kwa njia bora itakayonisaidia kutimiza malengo yangu," alisema. Alisema atawasimamisha wagombeaji katika uchaguzi wa 2027 na pia atamenyania nafasi ya kuwa mgombea urais wa upinzani. "Nina nia njema na nawaomba sote tuvumiliane," alisema. Kuingia kwa Bw Nyoro katika uwanja huo kunatokea wakati Naibu Rais Kithure Kindiki anaonekana kuunga mkono juhudi za kuunda mrengo tofauti wa kisiasa Mlima Kenya Mashariki. Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku ameibuka kama mmoja wa watetezi wakuu wa mpango huo. Bw Ruku anataka Meru, Tharaka Nithi na Embu kuungana chini ya Prof Kindiki na kisha kujadiliana na Rais Ruto kuhusu nafasi yao katika serikali ijayo. Ingawa Prof Kindiki amekuwa akisema hadharani kuwa Mlima Kenya unapaswa kuwa kitu kimoja, wazee kutoka Meru na Embu tayari wamemtangaza kuwa msemaji wao. Katika ishara nyingine ya mgawanyiko huo, Prof Kindiki alisema aliyekuwa Gavana wa Meru Kiraitu Murungi amepewa jukumu la kushirikiana na Rais mstaafu Kenyatta kuhakikisha kuna ushirikiano unaolenga "kuwazuia wapiga kura wa Mlima Kenya kuchagua upinzani mwaka 2027". Wakati huohuo, Mbunge wa Laikipia Mashariki Mwangi Kiunjuri na mwenzake wa Ndia George Kariuki wameanzisha mikakati ya kisiasa inayolenga kupunguza ushawishi wa Bw Gachagua. Bw Kiunjuri anaripotiwa kuratibu vyama vidogo vinavyomuunga mkono Rais Ruto katika eneo la Mlima Kenya, huku Bw Kariuki akijenga mtandao wa viongozi wa mashinani wanaounga mkono msimamo wake.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 23 Aug 2026 03:55:35
Tiketi ya Sifuna–Kalonzo yaendelea kupigiwa debe
UCHAGUZI Mkuu wa 2027 unapokaribia, upinzani unaanza kuashiria mwelekeo wa kuungana na vuguvugu la Linda Mwananchi, huku mjadala kuhusu nani atabeba bendera ya urais ukizidi kupamba moto. Katika ishara ya mwelekeo huo, Seneta wa Kakamega Boni Khalwale ameibua uwezekano wa tiketi ya Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na Kalonzo Musyoka, akidai kuwa muungano huo unaweza kupatia upinzani nafasi nzuri ya kumkabili Rais William Ruto. Bw Khalwale alisema Ijumaa kwamba utafiti aliouhusisha na wasomi kutoka China unatabiri kuwa Sifuna akiwa mgombea wa urais na Kalonzo mgombea mwenza, wanaweza kupata asilimia 68 ya kura dhidi ya asilimia 29 ya Rais Ruto. "Nimesoma utafiti jana usiku ambao umefanywa na Wachina. Umesema kwamba sisi tulioko mrengo wa upinzani tukikufanya wewe kuwa mgombea urais, halafu Kalonzo Musyoka awe mgombea mwenza wako, wewe na Kalonzo mtapata asilimia 68 ya kura, huku William Ruto akienda Sugoi na asilimia 29, " alidai Khalwale. Hata hivyo, Khalwale hakutaja taasisi iliyofanya utafiti huo, ulifanywa lini, sampuli iliyotumika au mbinu iliyotumiwa. Hakuna ripoti ya utafiti huo iliyowekwa wazi ili kuthibitisha takwimu hizo. Licha ya utata huo, kauli yake inaangazia hesabu inayozidi kutawala siasa za upinzani: je, Sifuna anaweza kuwa sura ya kizazi kipya cha upinzani huku Kalonzo akitoa uzoefu na ukomavu wa kisiasa? Sifuna amekuwa akipanda katika kura za maoni na sasa anatajwa miongoni mwa viongozi wanaoweza kupewa nafasi ya kuongoza upinzani. Utafiti wa TIFA uliotolewa Julai ulimweka Rais Ruto mbele kwa asilimia 24, Sifuna akifuata kwa asilimia 15 na Kalonzo akiwa na asilimia 13. Uchaguzi wa Kenya huamuliwa pia na miungano ya kikanda, nguvu za vyama, wagombea wenza na uwezo wa kuvutia wapiga kura nje ya ngome za viongozi. Kwa Sifuna, changamoto ni kugeuza umaarufu wake unaokua kuwa mtandao wa kitaifa. Kwa Kalonzo, changamoto inaweza kuwa kuamua ikiwa yuko tayari kuachana na azma ya kuwania urais na kukubali kuwa mgombea mwenza. Mjadala huo unajiri huku viongozi wa Linda Mwananchi wakiongeza shughuli za kisiasa na baadhi ya viongozi wa upinzani wakionyesha wako tayari kufanya kazi nao. Hata hivyo, bado hakuna makubaliano rasmi kuhusu mgombea wa upinzani, chama kitakachotumika au nafasi ya Kalonzo katika mpangilio huo. Kwa hivyo, tiketi ya Sifuna na Kalonzo bado ni uvumi wa kisiasa kuliko mpango uliokamilika. Lakini mjadala wake unaonyesha mabadiliko yanayoendelea katika upinzani huku 2027 ikikaribia: kutoka mashindano ya mtu mmoja mmoja hadi kutafuta tiketi moja inayoweza kuunganisha nguvu za kisiasa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi. Iwapo Linda Mwananchi itaungana rasmi na makundi mengine ya upinzani, suala la nani atakuwa mgombea wa urais na nani atakuwa mgombea mwenza litakuwa mojawapo ya maamuzi magumu zaidi kuelekea uchaguzi huo. Kwa sasa, jina la Sifuna limeingia katika hesabu hiyo. Kalonzo ana uzoefu na ngome yake ya kisiasa. Swali kubwa ni ikiwa wawili hao wanaweza kugeuza nguvu zao kuwa muungano mmoja wenye mvuto wa kitaifa — na ikiwa viongozi wengine wa upinzani wako tayari kuunga mkono mpango huo.
read moreRight Column Content