taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 19 Aug 2026 05:55:36
Linda Mwananchi waapa kuchukua hatua za kisheria na kiraia kukabili serikali kuhusu uhuni
VUGUVUGU la Linda Mwananchi limetangaza mkakati wa kukabiliana na kile inachodai ni ongezeko la ghasia za kisiasa nchini. Mkakati huo unahusisha hatua kali za kisheria mahakamani, kushinikiza idara za usalama, uasi wa kiraia na kuhamasisha zaidi mashirika ya kiraia pamoja na vyombo vya habari. Kundi hilo limesema hatua hizo zitachukuliwa kufuatia vurugu zilizovuruga ziara yake katika Kaunti ya Homa Bay Jumapili iliyopita, ambapo watu walifariki dunia, makumi kujeruhiwa na mali kuharibiwa. Badala ya kujiondoa kwenye shughuli za kisiasa, viongozi wa Linda Mwananchi wanasema tukio la Homa Bay limeimarisha azma yao ya kupinga kile wanachokiita ghasia na vitisho vinavyofadhiliwa na serikali. Kundi hilo linasema kwa sasa litafuata njia za kisheria, lakini limeonya kuwa huenda likalazimika kutumia hatua za kiraia ikiwa serikali haitawawajibisha waliohusika na vurugu hizo. Gavana wa Siaya, James Orengo, ambaye ni mmoja wa viongozi wa vuguvugu hilo, alisema Jumanne kuwa yuko tayari kukabiliana na kile alichokiita "ugaidi wa serikali" na akashutumu serikali ya Rais William Ruto kwa kupanga mashambulizi dhidi ya wapinzani wa kisiasa. "Tuko tayari. Niko tayari kukabiliana na changamoto yoyote inayotokana na ghasia za serikali. Huu ni ugaidi wa serikali unaoendelezwa na Rais William Ruto na lazima awajibike," alisema Bw Orengo nje ya makao makuu ya Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) katika Barabara ya Kiambu, Nairobi. Alikuwa amemsindikiza Bw Oliver Jaoko, maarufu kama Olivetti, ambaye polisi wanamtafuta kuhusiana na vurugu zilizoshuhudiwa katika mkutano wa Linda Mwananchi mjini Homa Bay. Bw Orengo pia alishutumu serikali kwa kuandaa mazingira ya kuahirisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027, ingawaje hakutoa ushahidi wowote kuhusiana na madai hayo. "Rais Ruto anajaribu kutuandaa kuahirisha uchaguzi. Hilo halitawezekana," alisema. Kundi hilo limetaja maeneo manne ya mkakati wake: mahakama, maandamano na uasi wa kiraia, kushinikiza polisi na vyombo vingine vya usalama, na kuhamasisha mashirika ya kiraia na wanahabari kufuatilia shughuli zake moja kwa moja. Njia ya kwanza ni kupitia mahakama. Katika taarifa yake ya Jumatatu, Linda Mwananchi lilisema litashinikiza uwajibikaji kupitia Katiba, mahakama na taasisi nyingine za kisheria. "Kila mhuni na afisa ambaye sura yake ilinaswa kwenye kamera akihusika katika vurugu hizi, alionekana na anatambulika," kundi hilo lilisema. "Tutatumia Katiba, mahakama na taasisi zote za kisheria kuhakikisha kuna uwajibikaji." Pia limetaka Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS), Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi (IPOA) na Idara ya Kitaifa ya Ujasusi (NIS) zifanye uchunguzi kuhusu mwenendo wa maafisa wao wakati wa vurugu za Homa Bay. Linda Mwananchi linadai maafisa wa usalama walitazama tu huku wafuasi wake wakishambuliwa au walisaidia kuvuruga shughuli zake za kisiasa. Madai hayo hayajathibitishwa kwa njia huru na vyombo vya usalama bado havijayakubali hadharani. Kundi hilo linadai msafara wake ulikumbana na vizuizi vya barabarani tangu mpaka wa Kisumu na Homa Bay, na kuendelea kukabiliwa na vizuizi ndani ya kaunti hiyo. Linaongeza kuwa watu wenye silaha waliokuwa wamejipanga kando ya barabara walifyatulia risasi msafara huo. Moja ya madai makubwa zaidi yanahusu mtu aliyekamatwa na wafuasi wake Nyandiwa ambaye alidaiwa kujitambulisha kama afisa wa NIS. Kundi hilo linasema simu yake ilichukuliwa na baadaye watu waliojieleza kuwa maafisa wakuu wa polisi waliwasiliana wakitaka irejeshwe. Nguzo ya pili ya mkakati huo ni shinikizo la kisiasa kupitia maandamano na uwezekano wa uasi wa kiraia. Seneta wa Vihiga, Godfrey Osotsi, alisema kundi hilo linaweza kuchukua hatua za kiraia iwapo Rais Ruto ataendelea kudumisha serikalini maafisa wanaotuhumiwa kupanga ghasia za kisiasa. "Tutarejea kwenye hatua za kiraia ikiwa Ruto ataendelea kuwaweka watu hawa serikalini," alisema Seneta Osotsi. Nguzo ya tatu ni kishinikiza polisi moja kwa moja. Orengo na Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino, walimsindikiza Jaoko kwenda kujisalimisha kufuatia maslahi ya polisi katika uchunguzi wa vurugu hizo. Bw Owino alishutumu polisi kwa kushindwa kuchukua hatua wakati timu ya Linda Mwananchi ilishambuliwa Homa Bay, akisema walipaswa kurejesha utulivu na kulinda wananchi.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 19 Aug 2026 06:55:23
Mwanasheria Mkuu akosa kujibu iwapo waliotimuliwa afisini wanaweza kuwania 2027
MZOZO wa kisheria kuhusu iwapo viongozi waliotimuliwa afisini kupitia bunge wanaweza kugombea nyadhifa za kisiasa kabla ya kesi zao kukamilika bado utaendelea kushuhudiwa nchini. Hii ni baada ya Mwanasheria Mkuu Dorcas Oduor, kukosa kutoa jibu la moja kwa moja kuhusu utata huo. Suala hilo lina umuhimu mkubwa kwa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na aliyekuwa Gavana wa Meru Kawira Mwangaza, ambao wote waliondolewa mamlakani na Bunge na wanapinga kutimuliwa kwao kortini. Bi Oduor ameishauri Mahakama ya Juu kutosikiza ombi la kutoa ushauri wa kikatiba kuhusu iwapo viongozi walioondolewa mamlakani kupitia bunge wanaweza kugombea nyadhifa za kisiasa kesi zao zikiendelea mahakamani. Mawakili wa Spika wa Bunge la Kaunti ya Meru, Ayub Bundi, hata hivyo, wamesema Mwanasheria Mkuu hakujibu maswali manane ambayo Mahakama ya Juu ilimtaka kuyashughulikia. Mawakili wa Spika wa Bunge la Kaunti ya Meru, Ayub Bundi, hata hivyo, walisema Mwanasheria Mkuu hakujibu maswali manane ambayo Mahakama ya Juu ilimtaka kuyajibu. Mojawapo ya maswali hayo ni iwapo rufaa au kesi ya kupinga kuondolewa mamlakani inaweza kusimamisha amri ya kikatiba ya uamuzi huo na kumruhusu kiongozi huyo kugombea uchaguzi. "Baada ya kupitia ushauri huo, ni wazi kwamba haujajibu wala kushughulikia masuala hayo," wakasema mawakili hao. Walimtaka Mwanasheria Mkuu kufuata maagizo ya Mahakama ya Juu kwa kutoa ushauri wa kisheria unaojibu kila swali lililowasilishwa. Bw Gachagua aliondolewa mamlakani Oktoba 2024. Mahakama Kuu ilitupilia mbali kesi yake Juni 2026, lakini amekata rufaa katika Mahakama ya Rufaa. Kiongozi huyo wa DCP ametangaza nia ya kuwania urais katika uchaguzi wa 2027. Bi Mwangaza naye aliondolewa kama Gavana wa Meru Agosti 2024 baada ya Bunge la Kaunti kupitisha hoja ya kumtimua na Seneti kuithibitisha. Mahakama Kuu ilikataa kesi yake Machi 2025, lakini amekata rufaa kupinga uamuzi huo. Anaongoza chama cha Umoja na Maendeleo (UMP) na analenga kuwania kiti cha ugavana tena. Bw Bundi aliwasilisha kesi hiyo katika Mahakama ya Juu Aprili 2026, akitaka ufafanuzi kuhusu masharti ya Katiba yanayohusu masharti ya kugombea nyadhifa za kisiasa. Mahakama ilimwagiza kupata ushauri wa Mwanasheria Mkuu ndani ya siku 21. Bi Oduor alisema kesi hiyo haifai kuendelea kwa sababu inahusu maswali yenye msingi na huenda ikaathiri kesi za baadaye. "Afisi hii inaona kwamba kesi hii haikidhi masharti ya Katiba ya Mahakama ya Juu kutoa ushauri wa aina hii," akasema. Hata hivyo, mawakili wa Bw Bundi wanasisitiza kuwa Mwanasheria Mkuu hakutimiza maagizo ya mahakama kwa sababu hakujibu maswali muhimu. Kwa sasa, Mahakama ya Juu bado haijatoa uamuzi kuhusu suala hilo. Hii inaacha swali la iwapo Gachagua na Mwangaza wanaweza kugombea uchaguzi wa 2027 likiwa halijajibiwa.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 19 Aug 2026 07:55:38
Mama mkarimu auawa na aliyempa maji ya kunywa
HUZUNI na mshtuko zimetanda katika kijiji cha Chabuene, Kaunti ya Meru, kufuatia mauaji ya kikatili ya Evelyne Mukiri Mbaabu, mwanamke anayekumbukwa kwa ukarimu wake na juhudi zake za kuhifadhi mazingira. Mkasa huo ulitokea mnamo Agosti 7 majira ya saa moja usiku, baada ya mwanaume asiyejulikana kuingia nyumbani kwake akiomba maji ya kunywa. Kwa mujibu wa familia, Bi Mukiri, mwenye umri wa miaka 65, alimkaribisha mgeni huyo na hata kumualika kwa kula chakula cha jioni. Kisha akamtuma mjukuu wake kwenda kuchota maji kutoka nyumba kuu huku akiendelea kuandaa chakula katika jiko lililojengwa nje ya nyumba. Hata hivyo, muda mfupi baadaye ukarimu wake uligeuka kuwa mkasa. Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, mjukuu huyo alipokuwa akichukua maji alisikia mayowe ya nyanya yake. "Aliporudi mbio jikoni, alimkuta mwathiriwa akiwa amelala katika dimbwi la damu amejeruhiwa," ilisema ripoti ya polisi.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 19 Aug 2026 10:30:08
Serikali yatetea mageuzi katika sekta ya afya licha ya changamoto
SERIKALI imetetea mageuzi yake katika sekta ya afya, ikisema imetekeleza ahadi nyingi ilizotoa wakati wa kampeni licha ya changamoto mbalimbali. Rais William Ruto alisema maendeleo katika sekta ya afya hayapaswi kupimwa kwa idadi ya sheria zilizopitishwa au watu waliosajiliwa pekee, bali kwa uzoefu wa mgonjwa anayepata huduma. "Kipimo halisi cha mafanikio ni ikiwa mgonjwa anapata huduma za afya zinazotegemewa, nafuu na zenye kuheshimu utu wake," alisema Rais. Alizungumza wakati wa Kongamano la kwanza la Kitaifa la Afya nchini Kenya lililoandaliwa na Wizara ya Afya chini ya kaulimbiu "Mageuzi yamewasilishwa, Afya ni Haki", ambalo linalenga kujadili changamoto na mafanikio ya sekta hiyo. Rais alisema alipoingia mamlakani, mojawapo ya vipaumbele vyake vilikuwa kufufua mpango wa Huduma ya Afya kwa Wote (UHC), ambao alihisi ulikuwa umedorora. Hivyo, UHC ikawa moja ya nguzo tano za Ajenda ya Mabadiliko ya Kiuchumi kutoka Chini kwenda Juu. Kwa mujibu wake, maradhi yanaweza kufilisi familia na kuwafanya wananchi kuingia katika umaskini, jambo lililomsukuma kutunga sheria nne mpya za afya mwaka 2023 zilizozaa Mamlaka ya Afya ya Jamii (SHA). Kati ya Wakenya milioni 32.3 waliosajiliwa chini ya SHA, zaidi ya milioni nane wamepokea huduma za matibabu. Idadi hiyo inajumuisha akina mama milioni 1.2 waliosaidika kujifungua salama na zaidi ya 500, 000 kwa upasuaji tangu mpango huo uanzishwe. Rais alipuuziliaa mbali madai kwamba ameacha ajenda ya "hasla", akisema ana ushahidi kuwa wananchi wa kipato cha chini ndio wanufaika wakubwa wa SHA. "Haya si mageuzi ya siku moja. Ni safari endelevu ya kupunguza pengo kati ya ahadi tulizotoa na huduma anayopokea kila Mkenya," alisema. Hata hivyo, wadau wa afya walihoji kuwa licha ya maendeleo yaliyopatikana katika sera, changamoto kubwa bado ipo katika utekelezaji. Mkurugenzi Mkuu wa Reproductive Health Network Kenya, Bi Nelly Munyasia, alisema Kenya imepiga hatua katika sera za afya ya uzazi, lakini huduma hizo hazijafikishwa kikamilifu kwa wananchi. "Baadhi ya sera bora zaidi zinasalia kwenye makaratasi kwa sababu rasilimali hazijaelekezwa ipasavyo ili kuzitekeleza," alisema. Alisisitiza umuhimu wa ufadhili endelevu, miundombinu ya kutosha, wafanyakazi wenye ujuzi na mifumo bora ya rufaa za wagonjwa. Kwa upande wake, Patrick Oyaro wa mradi wa Liverpool VCT and Research Kenya (LVCT), alisema huduma za watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi zinapaswa kujumuishwa kikamilifu chini ya SHA. "Kwa muda mrefu huduma za Ukimwi zimefadhiliwa na wafadhili. Tunahitaji kubadili hali hiyo na kuhakikisha zinaingizwa kwenye SHA," alisema. Kongamano hilo linafanyika wakati ambapo nchi inashuhudia mgomo wa wahudumu wa afya wa UHC na wauguzi. Mwenyekiti wa Muungano wa Maafisa wa Utabibu Kenya, Peterson Wachira, alisema Kenya bado iko mbali na malengo ya Ruwaza ya 2030 ya kuwa kitovu cha utalii wa matibabu barani Afrika. Aliongeza kuwa nchi pia haijafikia Azimio la Abuja linalotaka asilimia 15 ya bajeti ya taifa kutengewa sekta ya afya. "Mfumo wa usimamizi wa wahudumu katika afya umegawanyika mno. Upendeleo na ufisadi zimekithiri na wafanyakazi wengi wa afya wanateseka kutokana na uchovu na msongo wa mawazo," alisema. Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Madaktari, Wafamasia na Madaktari wa Meno (KMPDU), Dkt Dennis Miskella, alisema changamoto kubwa inayopuuzwa ni masuala ya wafanyakazi wa afya. "Kaunti zaidi ya 40 bado hazijalipa mishahara ya madaktari. Tunahitaji mjadala wa kina kuhusu uongozi na usimamizi wa sekta hii," alisema. Alipendekeza kuwa magavana washughulikie huduma za msingi za afya huku serikali kuu ikisimamia huduma za matibabu ya kiwango cha juu ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 19 Aug 2026 12:34:06
Makosa ya kudondosha viambishi vya idadi ya nomino katika wingi
KATIKA Kiswahili, upatanisho wa kisarufi ni muhimu tunapotaja idadi. Mojawapo ya makosa yaliyozoeleka ni kuhesabu miezi bila kutumia kiambishi cha nomino ambacho ni mi-. Ni kawaida kukutana na sentensi kama vile: *Msimu huo mvua ilinyesha kwa mwezi tatu. Sentensi hii si sahihi. Nomino mwezi inamaanisha kipindi cha siku ishirini na nane hadi thelathini na moja. Kwa hivyo katika wingi itakuwa miezi. Vilevile, kivumishi cha idadi tatu kinafaa kichukue kiambishi mi-. Ili kuisahihisha tutasema: Msimu huo mvua ilinyesha kwa miezi mitatu. Makosa mengine yaliyozoeleka katika kuhesabu nomino ni kuvipa vivumishi tasa viambishi vya idadi: sita, saba, tisa na kumi. Kila mara utakumbana na sentensi kama vile: Nilipofika darasani niliwapata wanafunzi *wasita. Vikombe *visaba vimeoshwa na mpishi. Magari *matisa yameegeshwa. Miti *mikumi ilipandwa jana. Sentensi hizi si sahihi kwani zimetumia viambishi vya nomino mwanzoni mwa vivumishi sita, saba, tisa na kumi. Tunafaa kuzisahihisha kwa kusema: Nilipofika darasani niliwapata wanafunzi sita. Vikombe saba vimeoshwa na mpishi. Magari tisa yameegeshwa. Miti kumi ilipandwa jana. Kosa jingine la kawaida tunapohesabu nomino ni kukosa kutumia viambishi vya nomino tunapotaja vivumishi vya idadi vinavyobadilika katika wingi. Aghalabu utakumbana na sentensi kama: *Nilinunua vitabu kumi na moja. *Wageni tano wamewasili kwetu. Tunafaa kusema: Nilinunua vitabu kumi na kimoja. Wageni watano wamewasili kwetu. Mwanafunzi mwenye changamoto ya kuhesabu nomino kwa usahihi, afanye mazoezi ya kuhesabu nomino ainati katika umoja na wingi.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 19 Aug 2026 12:55:42
Msichana ahadithia jinsi baba humdhalilisha kingono kabla kumpa mahitaji ya shule
MAHAKAMA ya Eldoret ilipigwa na butwaa Jumatatu wakati msichana mwenye umri wa miaka 16 alipoeleza jinsi baba yake mzazi alivyomdhulumu kingono mara kwa mara kila alipokuwa akimuuliza mahitaji ya shule. Msichana huyo, aliyetambuliwa kwa jina la siri A.W., alisimulia masaibu yake kwa majonzi kwa kukariri madhila aliyopitia mikononi mwa babake mzazi A. W wakati wa kusikizwa kwa kesi hiyo mahakamani. Akiwasilisha ushahidi wake mbele ya hakimu mkuu mkaazi Keyne Gweno, alieleza kuwa baada ya mama yake kufariki dunia na kuwaacha mabinti wanne akiwemo yeye, waliendelea kuishi chini ya uangalizi wa baba yao. "Wakati wowote mwalimu wangu aliponiambia nilete kitabu na kalamu, kadri nilipomwomba baba yangu aninunulie vitu hivyo ndivyo alinilazimu kushiriki naye tendo la ngono kabla ya kuninunulia vitu husika," alisimulia. Mahakama ilielezwa kuwa licha ya kutishiwa maisha iwapo angefichua unyama huo, hatimaye msichana huyo aliamua kumweleza mmoja wa walimu wake kuhusu unyanyasaji aliokuwa akifanyiwa. Walimu kutoka shule hiyo walichukua jukumu la kutoa ripoti kwa polisi ambapo mshukiwa alikamatwa na maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Langas na kufikishwa katika mahakama ya Eldoret. Mwanaume huyo alifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kosa la kufanya tendo la ngono na mtu wa familia ya karibu yaani kujamiiana, kinyume na Kifungu cha 20 (1) cha Sheria ya Makosa ya Kijinsia Nambari 3 ya mwaka 2006. Hati ya mashtaka inaeleza kuwa katika tarehe mbalimbali kati ya Januari 16, 2026, na Februari 6, 2026, katika eneo la Lemmok katika Kaunti Ndogo ya Kapseret, Kaunti ya Uasin Gishu, alimdhulumu kimapenzi binti yake mwenye umri wa miaka 16 kwa makusudi na kinyume cha sheria. Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashtaka hayo kabla ya kuamrishwa kuwachiliwa kwa dhamana ya Sh300,000 au dhamana mbadala ya pesa taslimu kiasi cha Sh100,000. Tangu wakati huo, mshtakiwa ambaye alishindwa kupata pesa taslimu za dhamana au dhamana ambapo amezuiliwa katika rumande ya Gereza la Eldoret GK akisubiri kesi kusikilizwa kikamilifu na kuamuliwa. Ombil la kutaka kupunguziwa dhamana ya pesa taslimu kutoka Sh100,000 hadi Sh50,000 lilikataliwa mahakamani. "Sitapunguza zaidi kiasi hicho cha dhamana ya pesa taslimu cha Sh100,000 kwa sababu najua kuwa mara tu utakapopata uhuru wako, hutawahi kurejea mahakamani hapa," aliamuru Hakimu. Akitoa ushahidi kuhusu suala hilo, Dkt Irene Simiyu, daktari katika Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Moi (MTRH), alithibitisha kuwa binti huyo alikuwa amedhulumiwa kingono. Upande wa mashtaka umepanga kuwasislihsa mashahidi watano muhimu, akiwemo afisa upelelezi kutoka Kituo cha Polisi cha Langas. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Septemba 8, 2026.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 19 Aug 2026 13:26:41
Vijana 122,000 walionufaika na pesa za NYOTA sasa kupokea mafunzo ya kukuza biashara
ZAIDI ya vijana 122,000 waliopokea mtaji wa kuanzisha biashara kupitia mradi wa National Youth Opportunities Towards Advancement (NYOTA) wataanza mpango unaolenga kuimarisha biashara zao na kuongeza nafasi za kuzikuza kwa muda mrefu. Mpango huo ulianza Jumatatu, huku washauri wa biashara zaidi ya 4,879 wakiajiriwa kote nchini kuwasaidia vijana hao. Katibu katika Idara ya Maendeleo ya Biashara Ndogo na za Kati, Susan Mang'eni, alisema kila mnufaika atapangiwa mshauri mwenye uzoefu wa biashara. Kila mshauri atahudumia vijana wasiozidi 20. Mpango huo utahusisha ziara za biashara, ushauri kati ya wafanyabiashara wenzao, uzoefu wa biashara, mafunzo, ushauri na kuwaunganisha na masoko. Mpango huo ni sehemu ya juhudi za serikali kuwawezesha vijana kujiajiri kupitia mafunzo ya ujuzi na kupata mtaji wa kuanzisha biashara. Mradi wa NYOTA ulizinduliwa Machi 2025 na hutumia teknolojia ya kidijitali kuwawezesha vijana kupata fursa katika maeneo mbalimbali nchini. Mnamo Julai 10, 2026, serikali ilitoa mtaji kwa zaidi ya vijana 122,000 walionufaika na mpango wa kusaidia biashara ili waanzishe au kupanua shughuli zao. Mradi huo unawahusisha vijana kutoka wadi zote 1,450 nchini, hasa wale walio katika viwango vya chini vya kiuchumi. Serikali pia inaandaa njia mpya za ufadhili zitakazowawezesha wanufaika kupata fedha zaidi kupitia hazina za serikali. Hatua hiyo inafuatia agizo la Rais William Ruto la kupanua upatikanaji wa fedha kwa vijana wa NYOTA. Idara hiyo pia inashirikiana na serikali za kaunti kuandaa mfumo wa kuwaondolea wanufaika wa NYOTA baadhi ya ada za leseni za biashara ili kuwawezesha kupata masoko na maeneo bora ya kufanyia biashara. Mafunzo ya Access to Government Procurement Opportunities (AGPO) yanatarajiwa kuanza mwezi ujao na yanalenga zaidi ya vijana 600,000. Mafunzo hayo yatawapa ujuzi wa kushiriki katika zabuni za serikali. Wakati huo huo, mpango wa On-the-Job Experience (OJE) unaendelea katika kaunti 18, ambako vijana wanapitia mafunzo ya kukuza ujuzi wa kijamii na kihisia. BI Mang'eni aliwataka vijana kushiriki kikamilifu katika mafunzo hayo, akisema kukamilisha mpango huo ni sharti la kuendelea kupata msaada katika hatua inayofuata. Lengo ni kuwapa vijana zaidi ya fedha za kuanzisha biashara, na pia maarifa, mitandao na mwongozo wa kuwasaidia kujenga biashara endelevu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 19 Aug 2026 13:34:33
Atafanikiwa kuingia kwenye rekodi ya Guinness kwa kufuga mamilioni ya kuku halisi wa kienyeji?
KILOMITA chache kutoka barabara kuu ya Nairobi-Mombasa, katika shamba la Nick Mwendwa eneo la Makindu, Kaunti ya Makueni, unapolizuru utakaribishwa na milio ya maelfu ya kuku halisi wa kienyeji. Shamba hilo la ekari 100, ambapo ni ekari 10 pekee zimetumika kwa sasa, lina zaidi ya kuku 150,000 wa kienyeji wa umri tofauti. Kila siku, karibu mayai 2,500 hukusanywa na kuwekwa kwenye mashine za kuatamia mayai na kuangua vifaranga (incubators). "Kila baada ya siku 21, vifaranga huanguliwa ili kupanua mpango wa uzalishaji unaolenga kuongeza idadi ya kuku," anasema. Mwendwa, ambaye wengi wanamfahamu kutokana na uongozi wake wa zamani katika Shirikisho la Soka Kenya (FKF), alianza mradi huo miaka mitatu iliyopita akiwa na kuku saba tu wa mama yake. "Nilitenga kuku hao saba na nikaapa kwamba kuanzia siku hiyo tutakuwa tukizalisha kutoka kwao pekee," anafichua. [caption id="attachment_191336" align="aligncenter" width="300"] Nick Mwendwa akikagua kuku wake. Anahoji analenga kufikisha idadi ya kuku milioni moja hivi karibuni. Picha|Sammy Waweru[/caption] Awali, alilenga kuongeza kundi hilo hadi kuku kati ya 7,000 na 15,000. Mama yake alicheka, akimwambia hakuna aliyekuwa na kuku 5,000 wa kienyeji halisi nchini. Hata hivyo, baada ya kutambua jinsi walivyohitajika sokoni, alibadilisha lengo na kulenga kuku milioni moja. "Baba yangu aliposikia mazungumzo hayo kati yangu na mama, alisema Nairobi imenigeuza kuwa wazimu," anakumbuka huku akicheka. Hii leo, Mwendwa ana zaidi ya kuku 150,000 na lengo lake ni kuwahi milioni moja. "Licha ya shabaha hiyo kuonekana kuwa mbali, ninaamini itawezekana," anaiambia 'Akilimali Dijitali'. Kulingana naye, anapanga kufikisha idadi ya kuku 400,000 kufikia Desemba mwaka huu. Endapo katika miaka ijayo atagonga ndipo, kufikisha idadi ya zaidi ya kuku milioni moja, ataingia kwenye rekodi ya kumbukumbu za Guiness? Guiness World Record, kama inavyofahamika kwa Kiingereza, hata hivyo, haijawahi kuangazia mkulima au mfugaji mwenye idadi ya juu ya kuku. [caption id="attachment_191337" align="aligncenter" width="300"] Nick Mwendwa akikagua mayai kwenye kiangulio. Picha|Sammy Waweru[/caption] Kuku mkubwa anayeishi na yai kubwa, ndio pekee imeangaziwa na Guiness World Record. Mwendwa, anasema angetamana sana kuingia kwenye kumbukumbu hiyo ya dunia haswa kwa kufuga idadi ya juu ya kuku halisi wa kienyeji. "Kenya na Afrika kwa jumla, sidhani kunaye (mfugaji) aliyefikisha idadi ya kuku 150,000 ninaofuga kwa sasa," anahoji. Rais huyu wa zamani wa FKF alianza ufugaji baada ya kugundua pengo kubwa katika soko la kuku na mayai ya kienyeji. Mwendwa anasema alikuwa akipenda kula kuku wa kienyeji, lakini mara nyingi hakuwa akiwapata kwenye maduka ya kijumla. Utafiti wake ulionyesha kuwa maduka hayo, maarufu kama supamaketi, yanahitaji kuku halisi wa kienyeji kwa wingi lakini wakulima wengi hawana uwezo wa usambazaji wa kudumu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 19 Aug 2026 13:55:02
Kampeni zaanza Nigeria Tinubu akikabiliwa na ushindani mkali anaposaka 'Tu Tam'
ABUJA, Nigeria: KAMPENI za uchaguzi wa Januari 2027 Nigeria zilianza Jumatano huku Rais Bola Tinubu akikabiliwa na swali gumu anapowania muhula wa pili hasa kuhusu utendakazi wake. Wengi wanajiuliza iwapo wananchi wa Nigeria wanaishi maisha bora baada ya zaidi ya mwongo mmoja wa utawala wa chama cha All Progressives Congress (APC). Tinubu yupo katika kinyang'anyiro dhidi ya aliyekuwa Makamu wa Rais Atiku Abubakar na Peter Obi, ambao wamekita kampeni zao katika masuala ambayo wananchi wanalalamikia hasa ugumu wa maisha na ukosefu wa usalama. Wapinzani wanadai kuwa miaka karibu 12 ya APC madarakani imeiacha Nigeria, taifa lenye watu wengi zaidi Afrika, likiwa maskini zaidi, lenye madeni mengi na lisilo salama kuliko 2015. Hali ni mbaya zaidi ikilinganishwa na chama hicho kilipoingia mamlakani chini ya aliyekuwa Rais Muhammadu Buhari. Kwa Tinubu, ambaye baadhi ya wananchi humwita "T-Pain" kutokana na gharama ya juu ya maisha, uchaguzi huo utakuwa kipimo cha iwapo wapiga kura wako tayari kuvumilia maumivu ya muda mfupi kwa matumaini ya kupata nafuu ya muda mrefu. Asilimia 80 ya raia wa Nigeria wanaamini nchi yao inaongozwa vibaya, huku asilimia 45 wakitaja ugumu wa kiuchumi na ukosefu wa usalama kuwa changamoto zao kuu. Tinubu amefanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi tangu aingie madarakani. Alifuta ruzuku ya mafuta iliyokuwa ikigharimu serikali fedha nyingi na kushusha thamani ya naira mara mbili. Hatua hizo zimepongezwa na wawekezaji na wakopeshaji wa kimataifa, lakini pia zimesababisha athari za kiuchumi kwa familia na kuchochea maandamano kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha. Serikali ya Tinubu inasema mageuzi hayo yameimarisha mapato ya serikali na kuongeza imani ya wawekezaji. Hata hivyo, wananchi wengi hupima hali ya uchumi kwa uwezo wao wa kununua chakula na kugharamia mahitaji ya familia. Mfanyabiashara wa nyama Abdullahi Sani alisema zamani alikuwa akiuza mbuzi sita kwa siku, lakini sasa anahangaika kuuza hata wawili. Mizigo ya madeni pia imeongezeka. Usalama nao ni changamoto kubwa kwa Tinubu. Ingawa serikali inasema operesheni za kijeshi zimepunguza mashambulizi na kuwezesha wakulima kurejea mashambani, ghasia, utekaji nyara na ujambazi bado umeenea. Wapinzani sasa wanatumia hali hiyo kumshambulia Tinubu, wakisema baada ya zaidi ya miaka 10 ya APC madarakani, wananchi wanataka kuona matokeo, si ahadi. Kwa wapiga kura wengi, uchaguzi huo utahusu maisha, usalama na chakula. Hata hivyo, mgawanyiko katika upinzani unaweza kumpa Tinubu nafasi ya kubaki madarakani licha ya changamoto zinazokabili uongozi wake.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 18 Aug 2026 21:36:31
Kanye West announces tour dates in Russia
Ye, the rapper formerly known as Kanye West, is to play two shows in St Petersburg, Russia, this October becoming the biggest Western star to play in the country since its invasion of Ukraine four years ago. Tickets for the shows at the 70,000-capacity Gazprom Arena sold out within hours of the announcement on [...] The post Kanye West announces tour dates in Russia appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 18 Aug 2026 21:43:03
UK 'supports Ukraine 100%', Burnham says, after Russia's drone warning
UK Prime Minister Andy Burnham has said the UK will continue to support Ukraine 100%, after Moscow warned of consequences following confirmation that British-made drones were used in recent Ukrainian strikes in Russia. We are not fair-weather friends, we will be there in Ukraines hour of need and that wont change, said Burnham. The Russian [...] The post UK supports Ukraine 100%, Burnham says, after Russias drone warning appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 18 Aug 2026 21:47:47
Maraga gives Ruto seven-day ultimatum to publish police reforms report
Former Chief Justice David Maraga has given President William Ruto seven days to publish the full report of the National Taskforce on Police Reforms, warning that he will release the document himself if the President fails to do so. Maraga, who chaired the taskforce, said the report was submitted to President Ruto on November 16, [...] The post Maraga gives Ruto seven-day ultimatum to publish police reforms report appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 18 Aug 2026 21:55:13
Brazil's President Lula hails oil discovery near Amazon river
Brazilian President Luiz Inácio Lula da Silva has hailed the discovery of oil near the mouth of the Amazon river. Speaking after the find was announced by Brazils state-run oil company Petrobras, he said it could be a passport to the countrys future. His decision to allow exploratory drilling in the area known as the [...] The post Brazils President Lula hails oil discovery near Amazon river appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 18 Aug 2026 22:00:27
KNCHR warns Kenya risks 'precipice' as political violence, goonism escalate
The Kenya National Commission on Human Rights (KNCHR) warned Tuesday that escalating political intolerance, violence, incitement and the alleged use of organised groups to intimidate opponents are threatening Kenya's democratic space ahead of the 2027 General Election. The commission said it had documented a worrying pattern of political-related violence between June and August 2026, including [...] The post KNCHR warns Kenya risks 'precipice' as political violence, goonism escalate appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 18 Aug 2026 22:08:16
Kisii on the edge: lawlessness, goons and the dark battle for succession
Kisii is entering the 2027 election season under a cloud of political tension, with succession battles, youth mobilisation and allegations of organised violence threatening to overshadow the region's traditionally vibrant political contests. What was once largely a battle of speeches, rallies and political persuasion is increasingly being accompanied by allegations of intimidation, threats and physical [...] The post Kisii on the edge: lawlessness, goons and the dark battle for succession appeared first on Kahawatungu.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Tue, 18 Aug 2026 21:00:00
Inside Homa Bay political gang and its reign of terror on the opposition
Their language is one-fear and violence against anyone opposing the push for President William Rutos reelection and that of senior ODM politicians bankrolling their activities.
read moreRight Column Content