taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 07 Oct 2026 07:55:29
Vijana zaidi ya 50 watoweka, waaminika kuvuka kujiunga na al-shabaab
IDARA ya usalama katika Kaunti ya Lamu inachunguza kutoweka kwa zaidi ya vijana 50 wanaoaminika kuvuka hadi nchi jirani ya Somalia kujiunga na kundi la kigaidi la Al-Shabaab. Kamishna wa Kaunti ya Lamu, Bw Stephen Sangolo, alithibitisha kutoweka ghafla kwa vijana hao mapema mwezi uliopita. Ripoti za kutoweka kwao zilianza kuibuka siku chache kabla na baada ya sherehe za awamu ya 137 za Maulid kisiwani Lamu. Sherehe hizo zilifanyika Septemba 9 hadi 12.Baadhi ya vijana waliotoweka walikuwa miongoni mwa waliosafiri kutoka visiwa mbalimbali vya Lamu kufika kwenye mji wa kale wa Lamu kuhudhuria tamasha hizo za kila mwaka. Vijiji ambapo vijana wameripotiwa kutoweka kwa wingi ni vile vya kisiwa cha Pate, kaunti ndogo ya Lamu Mashariki, ikiwemo Siyu, Shanga-Rubu, Faza, Kizingitini, Tchundwa, Mbwajumwali na Myabogi. "Tuko na ripoti za ujasusi kuwahusu vijana wapatao 50 wa Lamu waliovuka kisiri kuingia nchini Somalia. Baadhi ya wanafamilia tayari wamefika kwenye vituo vyetu vya polisi kupiga ripoti kuhusu watu wao kutoweka. Usalama umeimarishwa kila upande, ikiwemo sehemu za mpakani kama vile Kiunga wakati tukiwatafuta waliotoweka," akasema Bw Sangolo. Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Lamu, Bw Shadrack Ruto, pia alithibitisha kutoweka ghafla kwa vijana hao karibu mwezi mmoja uliopita sasa. Bw Ruto alionya kuhusu kuwepo kwa maajenti wa makundi ya kigaidi ambao wamekuwa wakiendeleza usajili wa vijana kujiunga na Al-Shabaab maeneo ya Lamu. Maajenti hao wamekuwa wakitumia njia za kijanja kuwasajili vijana, ikiwemo kuwaahidi kazi na mishahara mikubwa, ambazo Bw Ruto alizitaja kuwa za uongo.Pia aliionya jamii dhidi ya kuwaamini baadhi ya wanaowaendea na kutangamana nao kwa kujidai kuwa wanachama wa mashirika ya wahisani yanayotiliwa shaka."Kuna watu wanaojidai kuleta misaada na fedha za kusaidia jamii. Baadaye wananyemelea vijana wasiokuwa na ajira. Wanawatenga na kuwaahidi kazi, vyeo vikubwa na mishahara minono. Wanawapokeza vijana hao mafundisho ya itikadi kali kabla ya kuwavukisha Somalia. Tuko macho kukabili uozo huo," akasema Bw Ruto.Wakuu hao wa usalama waliwashauri wazazi kufuatilia kwa karibu mienendo ya watoto wao na kuchunguza kazi wanazoahidiwa ili kuepusha vijana wasijipate mtegoni.Kutoweka kwa vijana 50 katika hali tatanishi kunajiri wakati ambapo Lamu imeshuhudia kuimarika kwa usalama kufuatia kuzinduliwa kwa oparesheni inayoendelea msituni Boni mnamo Septemba 2015. Oparesheni hiyo iliyoanzishwa na serikali kuu, inadhamiria kuwasaka na kuwamaliza magaidi wa Al-Shabaab wanaoaminika kujificha ndani ya msitu mkuu wa Boni.Juni 2014, magaidi wa Al-Shabaab kutoka Somalia, wakiwa wamejihami kwa silaha hatari, walivamia mji wa Mpeketoni na viunga vyake, ambapo waliua watu zaidi ya 90, wengi wao wakiwa ni wanaume kwa usiku mmoja.Magari na nyumba kadhaa ziliteketezwa kwenye uvamizi huo ambao hadi leo unazingatiwa kuwa miongoni mwa mashambulio mabaya zaidi ya kigaidi kuwahi kushuhudiwa nchini.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 07 Oct 2026 07:55:38
Mke akamatwa baada ya kuripoti mauaji ya mumewe
MWANAMKE mmoja katika Kaunti ya Homa Bay alikamatwa na kuzuiliwa na polisi baada ya uchunguzi kumhusisha na mauaji ya mumewe ambayo awali alikuwa ameenda kuripoti katika kituo cha polisi. Rose Akoth alifika katika Kituo cha Polisi cha Ndiru Jumatatu akidai kuwa mumewe, John Okoko, alikuwa ameuawa na watu wasiojulikana. Hata hivyo, maelezo aliyotoa yaliibua maswali na kuwafanya maafisa wa usalama kuanza kumchunguza kwa kina. Mwili wa Okoko, mwenye umri wa miaka 42, ulipatikana ukiwa umetupwa kwenye kichaka katika Kijiji cha Kadibuoro, Kaunti ya Homa Bay, Jumapili. Polisi wanasema uchunguzi wao ulionyesha kuwa mauaji hayo yalifanyika nyumbani kwake kabla ya mwili kuhamishwa na kutupwa eneo ulikopatikana. Kwa mujibu wa polisi, Okoko aliuawa akiwa amelala ndani ya nyumba yake baada ya kupigwa kwa kifaa kizito. Baada ya mauaji hayo, washukiwa walioshiriki walidaiwa kuusafisha mwili huo bafuni, kumvisha nguo nyingine na baadaye kuubeba umbali wa takriban kilomita moja hadi kichakani. Kamanda wa Polisi wa Rangwe, Magdalene Chebet, alisema Akoth awali alidai kuwa mumewe alikuwa ameenda kukutana na mkulima aliyekuwa amemwahidi miche ya mpunga kabla ya kuuawa na mtu asiyejulikana. Alipoulizwa maswali zaidi na kuombwa kuwaongoza maafisa hadi nyumbani kwake, polisi waligundua ushahidi uliobadilisha mwelekeo wa uchunguzi. Madoa ya damu yalipatikana kwenye kuta za chumba cha kulala na kwenye kitanda cha wanandoa hao. "Ushahidi huo ulitosha kuonyesha kuwa marehemu aliuawa ndani ya nyumba," alisema Chebet. Baada ya kuhojiwa zaidi, Akoth alidaiwa kuwahusisha mwanawe mwenye umri wa miaka 24 na mwanaume mwingine mwenye umri wa miaka 36 kuwa washirika katika mauaji hayo. Habari za kukamatwa kwa washukiwa hao ziliwashtua wakazi wa eneo hilo ambao hapo awali walidhani Okoko alikuwa ameuawa na watu wasiojulikana. Wakazi wenye hasira walimvamia mshukiwa huyo wa miaka 36 kabla ya polisi kuingilia kati na kumuokoa. Polisi wamesema bado hawajabaini sababu ya mauaji hayo. Washukiwa wote watatu wanazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Ndiru wakisubiri kufikishwa mahakamani, huku mwili wa Okoko ukihifadhiwa katika mochari ya Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Homa Bay kwa uchunguzi wa maiti
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Wed, 07 Oct 2026 06:45:08
Four miners killed in gold mine collapse in West Pokot
At least four artisanal miners died after a gold mine collapsed at Kambi Karaya mining site in Pokot Central, West Pokot County. This is the latest such incident to happen in the area. A similar incident happened there last week where five miners were killed. According to the police, the incident was reported at about [...] The post Four miners killed in gold mine collapse in West Pokot appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 07 Oct 2026 06:55:46
Hofu magenge yakitinga 109 uchaguzi ukinukia
WASHUKIWA 1,827 wamekamatwa nchini kwa tuhuma za kuhusika katika uhalifu wa magenge kati ya Januari na Agosti mwaka huu, huku 729 wakipatikana na hatia. Kati ya kesi hizo, 716 bado ziko mahakamani huku serikali ikiongeza msako dhidi ya makundi hayo kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.Idara ya Serikali ya Usalama wa Ndani na Utawala wa Kitaifa, imetambua magenge na makundi 109 ya wahalifu nchini, idadi ambayo imeongezeka kutoka 89 yaliyotangazwa kuwa haramu kupitia Gazeti la Serikali Nambari 10427 la mwaka 2016.Katibu wa Usalama wa Ndani, Dkt Raymond Omollo, alisema serikali haitawalenga watu wanaotekeleza uhalifu pekee, bali pia viongozi, wafadhili na wanaoendesha shughuli za makundi hayo.Trans Nzoia inaongoza kwa idadi ya washukiwa waliokamatwa ikiwa na 491, ikifuatiwa na maeneo mengine yaliyoathiriwa na vitendo vya magenge. Kwa mujibu wa serikali, magenge hayo yanaweza kutumiwa wakati wa uchaguzi kuvuruga mikutano, kuwatisha wapinzani, kushambulia na kusababisha ghasia.Katibu wa Usalama wa Ndani, Raymond Omollo, alisema serikali haitawalenga watu wanaotekeleza uhalifu pekee, bali pia viongozi, wafadhili na wanaoendesha shughuli za makundi hayo."Wale wanaoajiri, kufadhili au kuongoza makundi hayo watawajibishwa pamoja na wanaotekeleza ghasia," alisema.
read morekenyanews.go.ke
@kna Wed, 07 Oct 2026 06:15:54
Lands CS Wahome commends staff for sustained excellence in service delivery
Cabinet Secretary for Lands, Public Works, Housing and Urban Development Alice Wahome has praised staff at the State Department for Lands and Physical Planning for their sustained excellence in service delivery, saying the SD's growing list of national accolades is a testament to its strong performance. Speaking during the official launch of the departments 2026...
read morekenyanews.go.ke
@kna Wed, 07 Oct 2026 06:19:03
Police holding 23-year-old man over murder of student
Police in Nakuru are holding a 23-year-old man in connection with last month's murder of an 18-year-old Form Four student in Molo sub-county. The suspect, who detectives say has been on the run since early September, has been identified as Walter Kipkoech and was traced to a hideout in Lagwenda Village, within Kuresoi North Sub-County....
read morekenyanews.go.ke
@kna Wed, 07 Oct 2026 06:19:40
Vihiga commissions water project to serve 140 households
Vihiga Governor Dr Wilber Ottichilo has commissioned the M'mbworo Water Supply and Catchment Conservation Project in Lugaga-Wamuluma Ward, which is expected to improve access to clean water for 140 households and several institutions. The project was implemented under the Financing Locally-Led Climate Action (FLLoCA) programme through the Vihiga County Climate Change Fund, with support from...
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Wed, 07 Oct 2026 05:45:58
How to Stay Safe From Ebola
Ebola is a serious viral disease that can spread through direct contact with the blood or body fluids of an infected person or through contaminated materials. Knowing how to stay safe from Ebola is especially important during an outbreak or after possible exposure. Good hygiene, avoiding risky contact and following public health guidance can help [...] The post How to Stay Safe From Ebola appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Wed, 07 Oct 2026 05:49:18
How Ebola Outbreak Affects Social Life
An Ebola outbreak can affect much more than peoples physical health. Because the disease can create fear of infection and require strict public health measures, it can change how people interact, work, study, travel and participate in community activities. Understanding how Ebola outbreak affects social life helps communities prepare for these challenges while reducing fear, [...] The post How Ebola Outbreak Affects Social Life appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content