taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 06 Oct 2026 04:55:35
Dai huenda Ruto akamtema Kindiki kabla ya 2027
NAIBU Rais Profesa Kithure Kindiki huenda asiwe mgombea mwenza wa Rais William Ruto katika uchaguzi mkuu wa 2027, Mbunge wa Ndia George Kariuki amedai. Bw Kariuki, ambaye ni mshirika wa karibu wa Rais Ruto, alisema Profesa Kindiki kwa sasa anashikilia wadhifa huo lakini anaweza kubadilishwa kabla ya uchaguzi. Akizungumza na redio ya Kameme, mbunge huyo alipinga madai kwamba Chama cha ODM ndicho kitatoa mgombea mwenza wa Rais Ruto. Alisema nafasi hiyo bado itaenda kwa mtu kutoka eneo la Mlima Kenya, ingawa huenda asiwe Profesa Kindiki. "ODM haitahitajika kutoa mgombea mwenza. Suala hilo litajadiliwa ili kubaini anayefaa zaidi kutoka eneo hili lenye kura nyingi," akasema. Bw Kariuki pia alisisitiza umuhimu wa wakazi wa Mlima Kenya kubaki na umoja na kukataa mipango ya kugawanya kura za eneo hilo. Majuzi, Bw Kariuki alimvamia Profesa Kindiki akisema ameshindwa kuwatetea wakazi wa Mlima Kenya. Pia aliwakosoa Profesa Kindiki na kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua kwa kushambuliana kisiasa na kugawanya eneo hilo.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 06 Oct 2026 04:55:47
Huzuni na hasira mwanafunzi wa kidato cha nne akiuawa kwa kukatwa kichwa
HUZUNI imetanda Kiambaa, katika kijiji cha Moto, Molo, Kaunti ya Nakuru, baada ya mwanafunzi wa Kidato cha Nne kupatikana ameuawa kikatili nyumbani kwao. Joy Wangui, 18, mwanafunzi wa Shule ya Upili ya Molo, alipatikana Jumapili akiwa amelala na kulowa damu kwenye jikoni, huku kichwa chake kilichokatwa kikapatikana karibu na bafu. Polisi wameanzisha msako wa mshukiwa anayefahamika kwa familia na wakazi wa eneo hilo, ambaye alitoroka baada ya mauaji. Kamanda wa Polisi wa Molo Justus Katana alisema polisi walipokea taarifa kutoka kwa wananchi mwendo wa saa nane Jumapili kuhusu mauaji hayo. Jirani Paul Muraguri Mwangi alisema tukio hilo limewaacha wakazi wakiwa na hofu. Alisema shoka, panga na kisu, zote zilipatikana katika eneo la tukio na huenda zilitumika katika mauaji. Jirani mwengine, Charles Njenga Matendo, alisema kaka mdogo wa Wangui ndiye aliyegundua mwili wake baada ya kurejea kutoka kwa duka la familia lililokuwa karibu. Wakazi wanahofia kuwa mauaji hayo huenda yalihusiana na mzozo wa kimapenzi, ingawa polisi bado hawajathibitisha nia ya mshukiwa. Maafisa wa Idara ya Upelelezi Nchini (DCI) waliendesha uchunguzi wa kitaalamu katika eneo la tukio huku damu ikiwa bado imeonekana jikoni. Askofu Joram Nderu alimtaja Bi Wangui kama msichana mnyenyekevu, mwenye heshima na furaha aliyekuwa na matarajio mengi mema maishani.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 06 Oct 2026 04:32:30
Police officer found dead in river in Nandi County
A police officer is feared to have drowned after his body was found floating in River Abundas in Tinderet Sub-County, Nandi County. The body, believed to be that of Police Constable Obadiah Nyametia, was discovered at around 2pm on October 5, 2026, in Chepsweta Sub-Location, Chemase Location, police said. According to police, Nyametia had not [...] The post Police officer found dead in river in Nandi County appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content