taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 05 Oct 2026 14:57:39
WANTAM: Seneta amshinda Rais wa Brazil katika duru ya kwanza ya uchaguzi, waelekea duru ya 2
SENETA Flavio Bolsonaro amefuzu kwa raundi ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Brazil baada ya kumpiku kwa tofauti ndogo Rais wa sasa Luiz Inacio Lula da Silva katika uchaguzi mkuu. Bolsonaro, mwanawe rais wa zamani, Jair Bolsonaro, alipata asilimia 47 ya kura dhidi ya asilimia 45 za Lula. Matokeo hayo yalikuwa kinyume na utabiri wa kura za maoni, ambazo zilitarajia Lula kuongoza kwa tofauti ya karibu asilimia tatu. Sasa wawili hao watamenyana katika uchaguzi wa mwisho utakaofanyika Oktoba 25. Baada ya matokeo, Flavio alisema raia wa Brazil wanataka mabadiliko na kutangaza kile alichokiita mwisho wa enzi ya chama cha Lula cha Workers' Party. Lula, ambaye alitarajia kushinda katika raundi ya kwanza, aliwaambia wafuasi wake kuwa kampeni mpya inaanza mara moja na akaahidi kuwaeleza wapigakura mafanikio ya serikali yake. Uchaguzi huo ulitawaliwa zaidi na masuala ya gharama ya maisha, ukosefu wa usalama na ufisadi. Licha ya kupungua kwa tatizo la uhaba wa ajira na tofauti za kimapato, Lula amekabiliwa na changamoto ya kuwashawishi wananchi wanaolalamikia gharama kubwa za maisha, madeni ya kifamilia na ongezeko la shughuli za magenge. Flavio ametumia hali hiyo kuomba kura za mabadiliko, huku Lula akipanua mipango ya ustawi wa jamii na kupendekeza msamaha wa baadhi ya madeni ya familia. Uchumi pia ulikuwa suala muhimu, huku matumizi ya serikali yakiongezeka na deni la umma kufikia zaidi ya asilimia 82 ya pato la taifa. Serikali pia ilipunguza utabiri wa ukuaji wa uchumi wa Brazil mwaka huu hadi asilimia mbili. Uchaguzi huo pia ulikumbwa na mijadala kuhusu ufisadi na madai ya kuingiliwa kutoka nje. Jair Bolsonaro, baba yake Flavio, anatumikia kifungo cha miaka 27 kwa kupanga mapinduzi baada ya kushindwa uchaguzi wa 2022. Flavio sasa anajaribu kutumia urithi wa kisiasa wa baba yake kumpinga Lula. Ingawa Rais wa Amerika, Donald Trump hajamtangaza rasmi mgombeaji anayemuunga mkono, amekuwa akimsifu Flavio na kumkaribisha Ikulu ya White House. Kwenye raundi ya pili, Brazil sasa inakabiliwa na ushindani mkali kati ya mrengo wa kushoto unaoongozwa na Lula na mrengo wa kulia unaowakilishwa na Bolsonaro. Matokeo hayo pia yanaonyesha mgawanyiko mkubwa wa kisiasa nchini Brazil, huku Flavio akifanya vizuri zaidi katika maeneo ya Kusini, Kusini-Mashariki na Kati-Magharibi, wakati Lula aliongoza katika ngome zake za Kaskazini-Mashariki pamoja na baadhi ya majimbo ya Kaskazini. Kwa upande mwingine, wapigakura waliowaunga mkono wagombeaji wengine sasa wanakuwa muhimu katika raundi ya pili. Augusto Cury alipata karibu asilimia 2.9, Renan Santos asilimia 2.2 na Ronaldo Caiado asilimia 2.2, huku wagombeaji wengine wakigawana sehemu ndogo ya kura. Ushiriki wa wapigakura pia ulikuwa suala muhimu, kwani takriban asilimia 21 ya wapigakura waliojiandikisha hawakupiga kura. Asilimia 2.93 ya kura ziliharibika na asilimia 1.84 zikawa "nyeupe" (mpigakura kutochagua mwaniaji yeyote), hali inayomaanisha kuwa sehemu kubwa ya wapigakura ambao hawakuwachagua wagombea hao wawili bado inaweza kuwa muhimu katika raundi ya mwisho. Kwa Flavio, ushindi huo wa raundi ya kwanza umempa nafasi ya kuendeleza urithi wa kisiasa wa familia ya Bolsonaro, huku Lula akilenga kuunganisha wafuasi wake na kupata kura za wagombea walioshindwa. Kwa kuwa tofauti kati yao ilikuwa chini ya asilimia mbili, kampeni ya kuelekea Oktoba 25 inatarajiwa kulenga zaidi masuala ya uchumi, usalama, ustawi wa jamii na mwelekeo wa kisiasa wa Brazil.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Mon, 05 Oct 2026 14:14:37
SHA gives counties 30 days to secure health facility contracts
MOH, CoG and SHA agree on county facility contracts, 90-day payment for clean claims and a 30-day moratorium on five compliance documents as new contracting starts Monday.
read morekenyanews.go.ke
@kna Mon, 05 Oct 2026 14:18:12
Coffee farmers reap from subsidized seedlings, diversification projects
Coffee farmers in Kirinyaga are benefiting from improved access to high-yielding coffee seedlings and alternative income-generating enterprises as cooperatives and development partners step up efforts to strengthen livelihoods in the sector. The initiatives, being implemented through the Rainforest Alliance-led Bringing the Future of Coffee to Stay project, are aimed at improving coffee production while helping...
read morekenyanews.go.ke
@kna Mon, 05 Oct 2026 14:21:23
Keep politics out of Lamu Refinery, Lusaka
Bungoma Governor Kenneth Lusaka has called on leaders in the United Opposition to stop politicizing the Lamu Refinery Project, saying the investment was set to create jobs, spur economic growth and improve livelihoods. He urged political leaders to put national interests above partisan politics, arguing that strategic investments should be embraced as catalysts for economic...
read morekenyanews.go.ke
@kna Mon, 05 Oct 2026 14:25:15
'Onset of short rains expected from Thursday', says weatherman
The much awaited El Nino rains are expected to commence as early as Thursday this week in several parts of Nyeri County. Nyeri County Kenya Meteorological Services Authority (KMSA) Director Peter Wambugu told KNA there is a high likelihood of the county experiencing the first showers of the rains towards the end of this week...
read morekenyanews.go.ke
@kna Mon, 05 Oct 2026 14:29:18
Nakuru own source revenue jumps by 47.7 percent as County strengthens reforms
Nakuru's Own Source Revenue (OSR) grew by Sh1.75 billion in the last financial year marking a 47.7 percent increase from 2024/2025. Governor Susan Kihika said OSR has risen steadily over the past few years rising from Sh3.65 billion in 2023/2024 to Sh5.4 billion in 2024/2025 reflecting a tremendous increase above the target her administration had...
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 05 Oct 2026 14:03:58
Sh234m land dream turns into nightmare as Borabu victims turn on lawyer
A land-buying venture that promised hundreds of families in Borabu, Nyamira County, a fresh start has turned into a bitter dispute, with victims claiming they lost a combined Sh234 million in a deal involving the acquisition of Kimintet farm in Trans Mara, Narok County. The aggrieved residents, accompanied by human rights activists, staged protests on [...] The post Sh234m land dream turns into nightmare as Borabu victims turn on lawyer appeared first on Kahawatungu.
read morekenyanews.go.ke
@kna Mon, 05 Oct 2026 12:35:37
ORPP North Rift Launches Customer Service Week 2026
The Office of Registrar of Political Parties (ORPP) in the North rift Region has launched the customer service week 2026 to appreciate its clients, showcasing achievements and increasing awareness of the office's mandate. The event held at ORPP North rift Office in Eldoret brought onboard representatives from Uasin Gishu Civil Society Organizations (CSOs) Network, political...
read morekenyanews.go.ke
@kna Mon, 05 Oct 2026 12:13:29
Lake Turkana under-used, costing county millions in revenue, says deputy governor Dr. John Erus
Turkana County is losing millions of shillings in own-source revenue because Lake Turkana is not being fully exploited deputy Governor Dr John Erus has said. Speaking in Lodwar at a stakeholders forum supported by the World Food Programme (WFP), Dr Erus said current approaches cannot unlock the lakes potential because sustainable, locally led solutions have...
read morekenyanews.go.ke
@kna Mon, 05 Oct 2026 12:16:33
Mutula calls for dualling of Mombasa Highway after fatal pilgrims' crash
Makueni County Governor Mutula Kilonzo Jr. has sent heartfelt message of condolence to the families of the 17 Catholic pilgrims who died in a road crash at Salama along the Mombasa–Nairobi Highway at Mlima Kiu in Mukaa Subcounty on Saturday morning. While renewing his call on the national government to dual the busy highway to...
read morekenyanews.go.ke
@kna Mon, 05 Oct 2026 12:21:54
County moves to map focal persons, tighten partner coordination
Turkana Countys Resource Mobilisation, Partnerships and Donor Coordination (RMPDC) Directorate has convened coordinators and focal persons from county departments and partner organisations to strengthen how development partners are managed and aligned with county priorities. The meeting aimed to ensure focal persons are properly mapped within their departments, improving accountability, information sharing, planning and resource allocation....
read morekenyanews.go.ke
@kna Mon, 05 Oct 2026 12:27:00
Over 300 patients benefit from free eye camp at Lodwar Referral Hospital
More than 300 patients have received specialised eye care after a five-day free medical camp at Lodwar County Referral Hospital (LCRH), as the County Government works to improve access to prevention and treatment and raise the countys cataract surgical rate. Services included eye examinations, diagnosis, treatment, cataract surgeries, corrective reading glasses and health education. An...
read moreRight Column Content