taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 30 Sep 2026 02:55:20
Historia Kenya ikizundua ujenzi wa kiwanda cha mafuta kitakachogharimu Sh2 trilioni
KENYA leo inaingia katika hatua muhimu ya sekta ya kawi huku ikianza rasmi ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kusafisha mafuta kinachotarajiwa kugharimu takriban Sh2 trilioni. Mradi huo unaopangwa kujengwa katika Bandari ya Lamu unatajwa kuwa mkubwa zaidi wa aina yake Afrika Mashariki na unatarajiwa kubadilisha sekta ya mafuta nchini na kufanya Kenya kuwa kitovu cha kawi katika eneo hili. Gharama ya mradi huo ni sawa na takriban asilimia 12 ya Pato la Taifa la Kenya la mwaka 2025, lililofikia Sh17.58 trilioni, kwa mujibu wa Shirika la Kitaifa kuhusu Takwimu Kenya (KNBS). Kiwanda hicho kinatarajiwa kuwa na uwezo wa kusafisha mapipa 700,000 ya mafuta ghafi kwa siku, kiwango sawa na uwezo wa kiwanda cha Dangote kilichoko Lagos, Nigeria. Wiki iliyopita, Rais William Ruto alitembelea kiwanda hicho cha Dangote nchini Nigeria kabla ya hafla ya kuanza ujenzi wa mradi wa Lamu. Kiwanda cha Dangote, ambacho ni kikubwa zaidi Afrika kwa kutumia mfumo mmoja wa kusafisha mafuta, kimegeuka kuwa kituo kikubwa cha viwanda kinachozalisha petroli, dizeli na mafuta ya ndege kwa soko la Nigeria na mataifa mengine. Baada ya ziara hiyo, Rais Ruto alisema kiwanda cha Nigeria kina uwezo wa kusafisha mapipa 700,000 ya mafuta ghafi kwa siku na kuzalisha zaidi ya lita 100 milioni za petroli, dizeli na mafuta ya ndege kila siku. Alisema mradi huo pia umejengwa ukiwa na miundombinu mikubwa, ikiwemo kilomita 120 za mabomba ya chini ya bahari yanayotumika kusafirisha mafuta ghafi kutoka kwenye meli hadi kiwandani. Mradi wa Lamu unalenga kutumia mfano huo kuimarisha uzalishaji wa mafuta nchini na kupunguza kutegemea bidhaa za petroli kutoka nje. Kiwanda hicho kinatarajiwa kuhudumia Kenya pamoja na nchi jirani kama Ethiopia, Uganda, Tanzania, Sudan Kusini na Burundi. Aidha, waendelezaji wa mradi huo wanatarajia kutumia mafuta ghafi yanayochimbwa nchini Kenya pamoja na kutoka mataifa jirani, yakiwemo Sudan Kusini. Mradi huo pia unatarajiwa kutoa ajira nyingi. Rais Ruto amesema unaweza kuzalisha hadi ajira 60,000 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja wakati wa ujenzi na kikianza kufanya kazi. Mbali na mafuta, kiwanda hicho kinatarajiwa kuchochea viwanda vingine, vikiwemo vya kemikali na mbolea "Mradi huu utabadilisha sekta ya mafuta nchini na katika eneo hili, kuhakikisha upatikanaji wa mafuta, kuimarisha usalama wa kawi, kuongeza uzalishaji viwandani na kuunda ajira 60,000," Rais Ruto alisema. Maandalizi ya ujenzi tayari yameanza. Mwishoni mwa wiki, meli MV Da Yang Bai He ilitia nanga katika Bandari ya Lamu ikiwa na zaidi ya tani 2,900 za vifaa vya ujenzi na mizigo ya mradi. Ujenzi wa kiwanda hicho unatarajiwa kuchukua kati ya miezi 30 na miaka minne baada ya uzinduzi. Kampuni ya Engineers India Limited (EIL) kutoka India, ambayo ilihusika katika ujenzi wa kiwanda cha Dangote nchini Nigeria, imepewa mkataba wa karibu Sh58 bilioni, kuwa mshauri mkuu wa usimamizi wa mradi wa Lamu. EIL ilisema kiwanda hicho kitakuwa cha kisasa na kitasaidia kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya mafuta katika Afrika Mashariki. Kampuni hiyo pia ilisema mradi huo utasaidia kupunguza kutengemea bidhaa za mafuta kutoka nje na kuimarisha usalama wa kawi katika ukanda huu. Kiwanda cha Dangote nchini Nigeria kiligharimu karibu Sh2.6 trilioni, na sasa kinafanya kazi kikamilifu. Dangote pia amepanga kuongeza uwezo wake wa kusafisha mafuta hadi mapipa 1.4 milioni kwa siku ifikapo 2029. Kwa Kenya, mradi wa Lamu unalenga kuiga mafanikio hayo katika pwani ya Afrika Mashariki, huku ukifungua nafasi kwa shughuli zaidi za viwanda na biashara zinazohusiana na mafuta. Iwapo utakamilika kama ulivyopangwa, kiwanda hicho kitakuwa mojawapo ya miradi mikubwa zaidi ya uwekezaji binafsi kuwahi kufanywa Afrika Mashariki.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Wed, 30 Sep 2026 02:23:49
Caleb Flynn, former 'American Idol' contestant, found guilty of murdering his wife
Caleb Flynn, a former worship leader and "American Idol" contestant, was found guilty of murdering his wife, Ashley Flynn, and all other charges Tuesday after prosecutors argued he fatally shot her and staged the scene to look like an intruder did it. The jury found Flynn, 40, guilty of all nine charges, including aggravated murder, [...] The post Caleb Flynn, former 'American Idol' contestant, found guilty of murdering his wife appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Wed, 30 Sep 2026 02:26:49
South Africa to clean up high-risk areas after 12 women killed
South Africas President Cyril Ramaphosa on Tuesday announced a clean-up of high-risk areas across the country, after the bodies of 12 women were discovered in an area east of Johannesburg in just two months. The deaths sparked a national outcry about the scale of violence against women in South Africa, which has one of the [...] The post South Africa to clean up high-risk areas after 12 women killed appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Wed, 30 Sep 2026 02:31:08
US Supreme Court denies Christa Pike's last-ditch bid to halt execution
The US Supreme Court declined to stop the execution of Tennessee inmate Christa Pike on the eve of the date appointed for her death by lethal injection. Pike, 50, has been awaiting execution since she was convicted and sentenced to death in 1996 for the murder of a teenage classmate. Hoping for a last-minute reprieve, [...] The post US Supreme Court denies Christa Pikes last-ditch bid to halt execution appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 29 Sep 2026 21:51:30
First female prime minister named in Morocco after winning elections
Fatima Zahra El Mansouri has been named Moroccos first female prime minister, after her centrist Authenticity and Modernity Party (Pam) won the most seats in last weeks parliamentary elections. Her appointment makes her only the second woman to lead a government in the Arab world, after Tunisias Najla Bouden. She was named by King Mohammed [...] The post First female prime minister named in Morocco after winning elections appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 29 Sep 2026 21:40:24
Centralise Compliance, Localise Decisions: Gene Grand's Operating Model for East African Growth
Companies expanding across East Africa face a recurring structural question: which decisions belong at headquarters, and which belong with the team on the ground. Gene Grand argues that most operators get this balance wrong in a specific and predictable way, centralising the decisions that should be local and localising the ones that should not be. [...] The post Centralise Compliance, Localise Decisions: Gene Grands Operating Model for East African Growth appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 29 Sep 2026 18:04:38
Manchester City Found Guilty of Premier League Financial Breaches
The Premier League has confirmed that an independent Commission has found Manchester City guilty of all charges related to serious breaches of the Premier Leagues financial rules over a nine-season period, and the majority of charges in relation to its failure to cooperate with the Leagues investigation. The club has the right to appeal the [...] The post Manchester City Found Guilty of Premier League Financial Breaches appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 29 Sep 2026 17:47:13
Murkomen declares one-month amnesty for surrender of illicit firearms
Interior and National Administration Cabinet Secretary Kipchumba Murkomen has declared a one-month amnesty for individuals holding illicit firearms, ammunition and other small arms and light weapons to voluntarily surrender them to the authorities. The amnesty was announced on Tuesday during the launch of Africa Amnesty Month 2026 at the Kenya School of Government in Nairobi. [...] The post Murkomen declares one-month amnesty for surrender of illicit firearms appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content