taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Thu, 09 Jul 2026 11:55:29
Majonzi mtoto akifa baada ya kugongwa na basi alipowasili shuleni
FAMILIA moja katika eneo la Naromoru, Kaunti ya Nyeri, imeachwa katika majonzi makubwa baada ya mwana wao wa miaka miwili na miezi tisa kufariki dunia kutokana na tukio lililotajwa kuwa kugongwa na basi la shule dakika chache baada ya kuwasili shuleni. Carlos Brown Mukere, mwanafunzi wa Shalom Schools, alifariki Jumatano asubuhi katika eneo la maegesho ya shule. Babake, Baptista Mukere, alisema alipokea simu akiwa kazini Mukurweini akiarifiwa na mwalimu wa mwanawe kwamba mtoto alikuwa amepata dharura na alihitajika kufika haraka Hospitali ya Naromoru Level Four. Kwa kuwa alikuwa umbali wa zaidi ya kilomita 80, alimwelekeza mkewe, Caroline Wambui, kwenda hospitalini. Alipowasili, alimkuta mfanyakazi wa shule pamoja na basi la shule nje ya hospitali, lakini alisema hakuna aliyekuwa tayari kumweleza kilichotokea. "Baada ya kuuliza mara kadhaa, wauguzi pamoja na mke wa mkurugenzi wa shule walinieleza kuwa mwanangu alikuwa amefariki. Nilihisi dunia imeporomoka," alisema Bi Wambui. Kwa mujibu wa maelezo aliyodai kupewa na shule, Carlos alishuka salama kutoka kwenye basi la shule na kutembea nyuma yake. Dereva alipokuwa akirudisha gari nyuma, inadaiwa hakumwona mtoto huyo na akamgonga. Mtoto alikimbizwa hospitalini akiwa hai lakini baadaye akafariki kutokana na majeraha aliyopata. Hata hivyo, polisi walitoa simulizi tofauti. Bi Wambui alisema maafisa wa Kituo cha Polisi cha Naromoru walimweleza kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha mtoto aliingia mbele ya basi baada ya kushuka ndipo akagongwa na gurudumu la mbele. Aidha, alisema polisi walimweleza kuwa watoto waliokuwa ndani ya basi walipiga mayowe mara baada ya ajali, lakini dereva aliendelea kuendesha gari hadi ndani ya uwanja wa shule kabla ya kusimama. Bi Wambui alisema aliporejea eneo la maegesho ya shule alikuta mkoba wa mwanawe ukiwa wazi, huku vitafunwa alivyokuwa amemfungia vikiwa bado ndani. Kamanda wa Polisi wa Kieni Mashariki David Kabuthia, alithibitisha kuwa dereva aliachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu ya Sh50,000 huku uchunguzi ukiendelea. Alisema polisi wataandika taarifa kutoka kwa uongozi wa shule, wafanyakazi na mashahidi wengine ili kubaini kilichotokea. Bw Kabuthia alisema dereva anatarajiwa kufikishwa mahakamani Julai 11, akikabiliwa na shtaka la kusababisha kifo kwa kuendesha gari bila umakini. Pia alisema upasuaji wa mwili wa mtoto utafanywa ili kusaidia kukamilisha uchunguzi.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Thu, 09 Jul 2026 10:30:35
Police Give New Details on Deceased KFS Senior Manager After Failed Autopsy
Missing Kenya Forest Service (KFS) Legal Services Manager, Esther Wairimu Keige, was found dead inside a coffee plantation in Juja farm after going missing fo weeks.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Thu, 09 Jul 2026 09:55:58
Wanne wanyakwa kwa kuiba mchele wa pishori wa Sh2 bilioni siku ya Saba Saba
WASHUKIWA wanne wamezuiliwa kwa siku 14 huku polisi wakiendelea na uchunguzi kuhusu wizi wa magunia ya mchele wa Pishori kutoka kwa shehena yenye thamani ya Sh2 bilioni iliyokuwa imehifadhiwa katika ghala moja mjini Mombasa. Wizi huo ulisemekana kutokea Julai 7, wakati sehemu nyingi za nchi zilikuwa zikikumbwa na wasiwasi kuhusu maandamano ya kuadhimisha siku ya Saba Saba. Washukiwa hao, Collins Wanjala Wafula, David Isata Asembo, Daniel Mwendwa Muthoka na Omar Adede Onduto walifikishwa mbele ya Mahakama ya Mombasa Jumatano, ambapo maafisa wa upelelezi walipata kibali cha kuwazuia kwa muda wa siku 14 ili kukamilisha uchunguzi. Kwa mujibu wa hati ya kiapo iliyowasilishwa na afisa anayechunguza kesi hiyo, Bw Feisal Omar, uchunguzi unahusu kosa la kuvamia jengo na kutekeleza uhalifu, kinyume na sheria. Kisa hicho kiliripotiwa na Bw Yusuf Swalleh Juma, Mkuu wa Idara ya Usalama katika Kampuni ya FOCUS Container Freight Station, katika Kituo cha Polisi cha Changamwe. Wapelelezi waliiambia mahakama kuwa watu wasiojulikana walivunja ghala la kampuni hiyo na kuiba idadi ambayo haijabainishwa ya magunia ya kilo 25 ya mchele aina ya Marai Premium Pishori kutoka kwa shehena ya awali ya magunia 800,000 yenye thamani ya Sh2 bilioni. Uchunguzi pia unaonyesha kuwa, wahusika walivamia chumba cha mfumo wa kamera za usalama (CCTV), wakaharibu kabisa mfumo huo na kuondoka na kifaa cha kuhifadhi kumbukumbu za video (DVR) zilizofaa kunaswa. Aidha, sehemu kuu ya kuwasha na kuzima umeme iliharibiwa, jambo ambalo polisi wanaamini lililenga kuzima mfumo wa usalama kabisa kabla ya wizi kutekelezwa. Afisa anayechunguza kesi hiyo alisema wanahitaji muda zaidi kupata rekodi za kamera za usalama kutoka kampuni na maghala jirani ili kusaidia kubaini waliohusika na wizi huo. Polisi pia waliieleza mahakama kuwa zoezi la kuhesabu upya shehena yote bado linaendelea kutokana na ukubwa wa mzigo uliokuwa umehifadhiwa, ili kubainisha kiwango halisi cha magunia yaliyodaiwa kuibiwa. Kwa mujibu wa hati ya kiapo, zaidi ya washukiwa 30 bado hawajakamatwa. "Washukiwa hawa wanne wakiachiliwa wanaweza kutatiza juhudi za kuwakamata washukiwa wengine kwa kuwa wanaweza kuwasiliana nao." Wapelelezi waliongeza kuwa kuachiliwa kwa washukiwa kunaweza kuathiri juhudi za kurejesha vielelezo na mali zilizoibwa, pamoja na kuwakamata washirika wengine wanaoshukiwa kuhusika katika uhalifu huo. Polisi pia walisema wanakusudia kufanya gwaride la utambuzi kwa kutumia mashahidi waliojitokeza kusaidia kubaini washukiwa na nafasi aliyotekeleza kila mmoja katika kutekeleza uhalifu huo. Mahakama ilielezwa kuwa amri ya kuwazuilia washukiwa ni muhimu ili kuwapa wapelelezi nafasi ya kukamilisha uchunguzi kabla ya kuamua iwapo watafunguliwa mashtaka ya jinai.
read morekenyanews.go.ke
@kna Thu, 09 Jul 2026 09:51:13
Relief food must reach the vulnerable, Marsabit County Commissioner vows
The government has committed to strict accountability in the distribution of relief food and nutrition supplies to ensure humanitarian assistance reaches vulnerable families affected by food insecurity in Marsabit County. Marsabit County Commissioner Stanley Kamande said relief food is intended to save lives and restore the dignity of people facing hunger and must never be...
read moreRight Column Content