taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 26 Oct 2026 04:55:38
Wanafunzi 261,000 hawajulikani walipo mitihani ya kitaifa ikianza rasmi
ZAIDI ya wanafunzi 261,000 waliotarajiwa kuendelea na masomo na kufanya mitihani ya kitaifa mwaka huu hawajulikani walipo, hali inayozua maswali kuhusu sera ya serikali ya kuhakikisha wanafunzi wote kutoka shule ya msingi wanajiunga na zile za sekondari. Takwimu za Baraza la Kitaifa la Mitihani Kenya (KNEC) zinaonyesha kuwa watahiniwa 1,233,852 walifanya mtihani wa KCPE mnamo 2022. Hata hivyo, ni wanafunzi 1,048,355 pekee waliojisajili kufanya mtihani wa KCSE mwaka huu, pengo la wanafunzi 185,497. Vilevile, wanafunzi 1,281,210 walifanya tathmini ya KPSEA mnamo 2023, lakini waliojisajili kufanya tathmini ya KJSEA mwaka huu ni 1,206,028. Hii ni tofauti ya wanafunzi 75,182. Kwa jumla, wanafunzi 260,679 hawapo katika makundi yaliyotarajiwa kuendelea hadi mitihani inayofuata. Hata hivyo, tofauti hiyo haimaanishi kwamba wote waliacha shule, kwani huenda baadhi walifariki, wakahamia mifumo mingine ya elimu au kuchelewa kuendelea na masomo. Waziri wa Elimu Julius Ogamba alisema sababu kadhaa zinaweza kueleza tofauti hiyo. "Baadhi ya upungufu huu unatokana na hali za kawaida, ikiwemo wanafunzi waliofariki au ambao hawawezi kuendelea na masomo. Wengine wamehamia mifumo mbadala ya elimu kama shule za kimataifa," akasema. Aliongeza kuwa baadhi ya wanafunzi huacha shule kwa muda kutokana na mimba za mapema au maradhi, lakini huruhusiwa kurejea na kuendelea na masomo. Wakati huo huo, wanafunzi wa Gredi ya Sita na Gredi ya Tisa wanaanza tathmini za kitaifa, huku mitihani ya KCSE ikiendelea kote nchini. Jumla ya watahiniwa 3,634,846 wamejisajili kwa mitihani na tathmini hizo tatu. KNEC imetuma maelfu ya wasimamizi kuhakikisha zoezi hilo linaendeshwa kwa usalama. Mkurugenzi mkuu wa baraza hilo, David Njengere, alisema simu hazitaruhusiwa wakati wa mitihani ya KCSE. "Kukiuka sheria hii kutachukuliwa kuwa udanganyifu wa mtihani kwa mujibu wa sheria na kanuni za KNEC," akasema. Baraza hilo pia zinatumia kufuli zenye nembo ya usalama kwenye kontena za kuhifadhi karatasi za mitihani ili kuimarisha usalama. Hata hivyo, mgogoro kuhusu malipo ya walimu wanaosimamia mitihani bado unaendelea. Muungano wa Walimu wa Shule za Upili na Vyuo vya Anuwai (KUPPET) ummewataka wanachama wake kujiepusha na shughuli za KNEC hadi malalamishi yao yatakapotatuliwa. Naibu katibu mkuu wa chama hicho, Moses Nthurima, alisema suala si kulipwa kwa wakati pekee, bali pia kiwango cha malipo. "Tunasisitiza kuwa walimu hawapaswi kujihusisha na shughuli za mitihani kwa sababu hiyo ni aina ya utumwa," akasema. Wakati huo huo, wakuu wa shule wameiomba Bunge kusitisha ukaguzi na ziara za maafisa wa serikali shuleni hadi mitihani imalizike, wakisema shughuli hizo zinawavurugia maandalizi. Hata hivyo, Spika Moses Wetang'ula alisema uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma hauwezi kusitishwa. "Uwajibikaji kuhusu matumizi ya rasilimali za umma si jambo la hiari. Ni wajibu wa kikatiba," akasema.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Mon, 26 Oct 2026 04:15:36
Ministry Announces New Measures Affecting Drivers After Fatal Mtito Andei Crash
The Ministry's intervention comes even as NTSA and the Motorists Association of Kenya (MAK) issued a series of demands to the government, including declaring road accidents a national disaster and fast-tracking the dualing of the Nairobi-Mombasa Highway.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 26 Oct 2026 03:55:45
Jengo la mauti Eastleigh : Sakaja awalaumu polisi
GAVANA wa Nairobi Johnson Sakaja amelaumu polisi kwa kuwaachilia washukiwa waliohusishwa na ujenzi wa jengo lililoporomoka Eastleigh. Bw Sakaja amewataka maafisa wa usalama waeleze kwa nini watu waliokamatwa kwa kukiuka sheria za mipango ya miji waliachiliwa kwa dhamana ya Sh50,000 bila kufikishwa mahakamani. Gavana huyo alisema maafisa wa kaunti walikagua eneo hilo na kubaini kuwa ruhusa ya kubadilisha matumizi ya ardhi ilikuwa imetolewa, lakini mipango ya usanifu iliyohitajika kuidhinisha ujenzi haikuwa imeidhinishwa. Alisema kaunti iliwakamata washukiwa na kuwakabidhi katika Kituo cha Polisi cha Kamukunji, lakini baadaye baadhi yao wakaachiliwa. "Tulitekeleza sheria na kuwakamata waliohusika na kwa kuwa hatuna mamlaka ya kuendesha mashtaka, washukiwa walikabidhiwa polisi. Inaripotiwa kuwa waliachiliwa kwa dhamana ya Sh50,000 bila kufikishwa mahakamani," akasema. Rekodi za polisi zinaonyesha washukiwa 14 waliwekwa kizuizini Juni 17, 2026, kwa makosa yanayohusiana na ukiukaji wa sheria za mipango miji. Hata hivyo, rekodi nyingine zinaonyesha washukiwa 10 waliachiliwa kwa dhamana kwa maagizo ya mkuu wa kituo hicho, hali inayozua maswali kuhusu kilichowapata wengine. Wakati viongozi wakilaumiana, familia za watu waliopotea katika mkasa huo zinaendelea kusubiri habari za wapendwa wao. Kufikia Jumapili adhuhuri, familia 47 zilikuwa zimeripoti ndugu zao kutoweka, ingawa tisa zilikuwa zimeunganishwa tena na jamaa zao, kulingana na Katibu wa Wizara Susan Mang'eni. Dina Mueni amekuwa katika eneo la mkasa tangu Ijumaa akimtafuta dada yake, Eunice Mwikali, 41, aliyekuwa akifanya kazi ya ushonaji katika jengo hilo. "Kama anaweza kupatikana, nitashukuru sana. Si rahisi kumtafuta mtu bila kujua kama yu hai au amefariki," akasema Bi Dina. Hata hivyo, manusura Victor Onyango amewapa familia hizo matumaini. Fundi huyo wa ushonaji alinaswa chini ya vifusi Ijumaa, lakini akaokolewa Jumamosi akiwa na majeraha madogo. "Ninamshukuru Mungu sana," alisema. Hata hivyo, mashine zake tatu za kushona na biashara yake zilibaki chini ya vifusi.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Mon, 26 Oct 2026 03:00:00
Sakaja's fatal failures exposed as City Hall remains dogged by corruption, cartels
Nairobis Eastleigh building collapse exposes persistent failures in construction oversight, enforcement and accountability despite repeated warnings and previous tragedies.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 26 Oct 2026 02:20:48
Lula wins fourth term in Brazil but faces hostile Congress and divided country
Brazils veteran left-wing president, Luiz Inácio Lula da Silva, has been re-elected after a bitterly fought campaign, beating his right-wing rival Flávio Bolsonaro. It is Lulas fourth win in a presidential election, having served two terms as president from January 2003 to December 2010, and again from January 2023. But the road to his win [...] The post Lula wins fourth term in Brazil but faces hostile Congress and divided country appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 26 Oct 2026 02:23:41
Elation across Serbia after veteran ruler Vučić concedes to student-led protest movement
Serbias long-standing leader Aleksandar Vučić has admitted defeat to the student-led protest movement in snap parliamentary elections. We still do not have final results it is clear that we have lost these elections, the right-wing populist leader said as he conceded late on Sunday. Preliminary figures from Serbias election commission indicated a record high turnout, [...] The post Elation across Serbia after veteran ruler Vučić concedes to student-led protest movement appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 26 Oct 2026 02:32:16
Death toll in Nigeria village raided by gunmen rises to 48, police say
The death toll from Fridays attack on a remote village in the north-eastern Nigerian state of Taraba has risen to at least 48, police have told the BBC. The police had initially reported 10 deaths after unidentified gunmen on motorcycles raided the village of Binnari, looting shops and setting houses ablaze. More bodies were discovered [...] The post Death toll in Nigeria village raided by gunmen rises to 48, police say appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 26 Oct 2026 02:36:16
Rapper Nicki Minaj joins Trump onstage at Michigan rally
Rapper Nicki Minaj said US President Donald Trump has changed the energy of the country as she joined him at a Michigan rally to stump for Republicans ahead of the nationwide midterm elections. Hes given us a future to look forward to, she said, after Trump praised her figure and called her on stage to [...] The post Rapper Nicki Minaj joins Trump onstage at Michigan rally appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 26 Oct 2026 02:55:26
Pepo la mauti laangamizi waumini wengine 25
SAFARI ya kurudi Mombasa baada ya mazishi ya askofu mwenzao iligeuka kuwa janga kwa wachungaji na familia zao baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana ana kwa ana na lori katika eneo la Kanga, karibu na Mtito Andei, barabara kuu ya Mombasa-Nairobi. Watu 25 waliaga dunia katika ajali hiyo ya saa mbili kasorobo asubuhi, huku manusura wakisimulia matukio ya mwisho, juhudi za kuokoa wenzao na maumivu ya kutofahamu hatima ya jamaa zao waliokuwa safarini. Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa dereva wa basi hilo lenye uwezo wa kubeba abiria 52 alikuwa ameliendesha kwa zaidi ya saa 16 bila msaada wa dereva mwingine, jambo lililozua wasiwasi kuhusu uchovu na usalama barabarani. "Dereva aliendesha gari kutoka Lugari, Kaunti ya Kakamega, hadi hapa. Hakuwa na mtu mwengine wa kumsaidia. Lazima alikuwa amechoka," akasema Mchungaji Cosmas Nyangweso, mmoja wa manusura. Alisema aliona basi likianza kuyumba barabarani kabla ya kugongana na lori lililokuwa likitoka upande wa pili. Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, basi hilo lilikuwa likijaribu kuyapita magari mengine lilipopoteza mwelekeo. Kamishna wa Kaunti ya Makueni, Abdullahi Khalif, alisema basi liliteleza na kuingia upande wa pili wa barabara kabla ya kugongana na lori, na kusababisha sehemu kubwa ya paa lake kung'oka. Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama Barabarani (NTSA) ilisema ripoti za awali zinaashiria kuwa magari hayo yaligongana ana kwa ana na huenda kuyapita magari mengine isivyofaa kulichangia ajali hiyo. Basi hilo lilikuwa likirejea Mombasa baada ya abiria kuhudhuria mazishi ya Askofu Isaiah Kiganane katika kijiji cha Marakusi, Kakamega mnamo Jumamosi. Askofu Zachariah Mwagandi, mkuu wa Kanisa la Glorious River International, alisema wachungaji walijadiliana iwapo warudi Mombasa siku hiyo hiyo baada ya mazishi. Hatimaye waliamua kuondoka saa kumi jioni na kusafiri usiku kucha. "Tulikuwa na furaha tulipoondoka Mtito Andei baada ya kupata kifungua kinywa mwendo wa saa moja asubuhi. Tulikubaliana kuenda moja kwa moja nyumbani kwa askofu marehemu, ambako safari yetu ilianzia Alhamisi," akasema. Hata hivyo, furaha hiyo ilikatizwa na ajali iliyotokea dakika 15 tu baada ya kuondoka Mtito Andei. Mchungaji Spenza Mdave wa Kanisa la Voice of Faith, Malindi, alisema manusura walilazimika kushirikiana na dereva kuwatoa wenzao kwenye mabaki ya basi, huku baadhi ya madereva waliopita wakipuuza kilio chao cha kuomba msaada. "Tulishirikiana na dereva kuwaokoa manusura. Wengi wa waliofariki walikuwa wameketi nyuma ya basi," alisema akiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mtito Andei. Hata hivyo, Bw Mdave alikuwa na wasiwasi kuhusu watoto wake wanne waliokuwa safarini. Alisema alianza safari akiwa na watoto wake watano, lakini mmoja alishuka Nairobi huku wengine wakisisitiza kuendelea hadi Malindi kumwona mama yao. Violet Mwandonyi, jamaa wa askofu marehemu, pia hakuwa na taarifa kuhusu watoto wake wawili waliokuwa kwenye basi hilo. Katika Kaunti ya Mombasa, habari za vifo ziliwaacha waumini na familia katika majonzi. Mchungaji Joseph Vura wa Kanisa la Campaign for Salvation and Healing alikuwa amempigia msaidizi wake saa 6:45 asubuhi akimwambia atachelewa kufika kwenye ibada. "Wakati wa simu alikuwa na furaha sana na aliniambia kuhusu safari na wachungaji aliokuwa nao. Sikujua alikuwa akinitumia ujumbe wa mwisho," akasema Mchungaji Andrew Mjomba. Baadaye, Bw Mjomba alipata habari kwamba Vura alikuwa miongoni mwa waliofariki. Mchungaji Isaac Juma wa Kanisa la Grace Healing Centre pia aliaga dunia. Mchungaji Isaac Wangila wa Kanisa la Glory Worship Centre alisema zaidi ya wachungaji 30 waliondoka Mombasa kuenda Kakamega kuhudhuria mazishi hayo. Alisema Mchungaji Stephen Ouma alikuwa amejeruhiwa kifuani na kichwani, huku wachungaji watatu kutoka Bangladesh wakiripotiwa kufariki. Jukwaa la Wahubiri Mombasa limeiomba serikali kuwasafirisha kwa ndege manusura wanaohitaji matibabu maalumu, kuondoa au kulipia bili za hospitali na kusaidia familia kugharamia mazishi. Ajali hiyo imezua tena wito wa kupanuliwa kwa barabara ya Mombasa-Nairobi, wiki tatu tu baada ya mahujaji 17 Wakatoliki kufariki katika ajali nyingine karibu na Salama. Mkurugenzi mkuu wa NTSA, Nashon Kondiwa, alisema ajali za barabarani zimefikia kiwango cha dharura kitaifa, huku watu 5,000 wakipoteza maisha kila mwaka. Alisema kutangaza ajali za barabarani kuwa janga la kitaifa kungewezesha serikali kuunganisha juhudi za usalama, kuongeza ufadhili na kuweka malengo yanayopimika ya kupunguza vifo.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Sun, 25 Oct 2026 21:00:00
Deadly cost of enforcement failures as City Hall shifts blame
Nairobis Eastleigh building collapse exposes persistent failures in construction oversight, enforcement and accountability despite repeated warnings and previous tragedies.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 25 Oct 2026 20:26:23
Venezuelan opposition leader María Machado returns after months in exile
Venezuelan opposition leader María Corina Machado has returned home to a fraught political landscape after over 10 months in exile. I am here. With you, Machado wrote on X on Sunday. Her ally, former presidential candidate Edmundo González Urrutia, confirmed the news minutes later, writing: I am thrilled to announce to you that our leader, [...] The post Venezuelan opposition leader María Machado returns after months in exile appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 25 Oct 2026 20:29:22
Police officer shot dead by colleague at Kitui Training Camp, suspect flees
A police constable undergoing induction training was shot dead at the Wikithuki BPU Training Camp in Tseikuru, Kitui County, on Sunday afternoon. He was shot at close range by a colleague who escaped after dropping his official killer weapon, police authorities said. The motive was not immediately known. The deceased, identified as police constable Raphael [...] The post Police officer shot dead by colleague at Kitui Training Camp, suspect flees appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content