kahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 25 Aug 2026 06:10:57
Two men drown while swimming in Twiga Dam in Juja
Two men drowned while swimming in Twiga Dam in Murera, Juja Sub-County, Kiambu County, on Monday afternoon. The incident was reported on August 24, 2026, police said. Upon arrival, the police officers found two mountain bikes, a tablet and other personal belongings, including clothes and mobile phones, lying on the shore. The bodies could not [...] The post Two men drown while swimming in Twiga Dam in Juja appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 25 Aug 2026 06:14:00
Boy drowns in family farm dam in Makueni
A two-and-a-half-year-old boy drowned in a dam within his family farm in Illingoni village, Mavindini Location, Makueni County. The incident was reported on Monday, August 24, 2026. The deceased child was reportedly fetching water from the dam when he fell into the water. His mother managed to rescue him and rushed him to Mavindini Level [...] The post Boy drowns in family farm dam in Makueni appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 25 Aug 2026 06:18:35
Lawyer Angela Mulwa re-arrested, to face murder charge alongside her mother, brother
Nairobi lawyer Angela Mulwa was re-arrested on Monday at the Milimani Law Courts and is expected to be charged with the murder of Dr Victoria Thunya Mutiso alongside her mother and her brother. Dr Mutiso was a psychiatrist and former Director of the African Institute of Mental and Brain Health. According to a charge sheet, [...] The post Lawyer Angela Mulwa re-arrested, to face murder charge alongside her mother, brother appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 25 Aug 2026 06:25:06
Sonko vows to appeal Sh385 million tax dispute in High Court
Former Nairobi Governor Mike Sonko has vowed to move to the High Court after losing a Sh385 million tax dispute with the Kenya Revenue Authority (KRA). This will escalate his long-running legal battle with the taxman. Sonko is expected to challenge a decision by the Tax Appeals Tribunal, which dismissed his appeal against a tax [...] The post Sonko vows to appeal Sh385 million tax dispute in High Court appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 25 Aug 2026 05:55:40
Kauli ya Wetang'ula kwamba ajira za TSC hugawiwa wabunge Ikulu yachemsha vyama
VYAMA vya walimu vimekasirishwa na matamshi ya Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang'ula kwamba baadhi ya wabunge hupewa barua za ajira za Tume ya Kuwaajiri Walimu (TSC) katika Ikulu. Chama cha Walimu Nchini (KNUT), Muungano wa Walimu wa Shule za Upili na Vyuo vya Anuwai (KUPPET) na Muungano wa Walimu wanaofundisha maeneo kame (KETHAWA), wote wamesema kauli hiyo imeibua upya madai ya mapendeleo ya kisiasa katika kuwaajiri walimu. Bw Wetang'ula alisema mwishoni mwa wiki kwamba baadhi ya wabunge huandamana naye hadi Ikulu na kupewa hadi barua 10 za ajira za walimu, lakini baadaye huziuza kwa Sh400,000 kwa kila mzazi. "Baadhi ya wabunge ninaowapeleka kwa Rais hupewa hadi barua 10 za ajira za walimu. Lakini baadaye unasikia wamekuwa wakiziuza," akasema Bw Wetangúla. Alisema kitendo hicho si cha kimaadili, hasa kwa wazazi maskini wanaolazimika kutafuta fedha nyingi ili watoto wao wapate ajira. Kauli hiyo imezua wasiwasi wakati TSC imechapisha nafasi 20,000 za ajira za walimu wa shule za sekondari za chini. Naibu Katibu Mkuu wa Kuppet Moses Nthurima alisema madai hayo ni ya kusikitisha na yanalemaza uhuru wa TSC, ambayo ni tume huru ya kikatiba. Alisema walimu waliohitimu miaka mingi iliyopita na kupata alama za juu katika mahojiano wanafaa kupewa kipaumbele badala ya nafasi kupewa watu wenye uhusiano na wanasiasa. "TSC ina sera ya kuajiri. Waliohitimu mapema na kupata alama za juu katika mahojiano wanapaswa kuwa na nafasi kubwa ya kuajiriwa," akasema. Katibu wa Kitaifa wa Kethawa Ndung'u Wangenye alisema kauli ya Spika imethibitisha madai ya muda mrefu kwamba wanasiasa huingilia mchakato wa kuwaajiri walimu. Mwenyekiti wa Kitaifa wa Kuppet Omboko Milemba alisema walimu lazima waajiriwe kupitia TSC pekee, kwa kuwa hiyo ndiyo taasisi iliyopewa jukumu hilo kikatiba. Naibu Katibu Mkuu wa Knut Hesbon Otieno alisema baadhi ya walimu wameomba ajira mara nyingi bila mafanikio huku wengine wakipata nafasi kupitia uhusiano wa kisiasa. Hata hivyo, TSC imepuuza madai hayo na kusisitiza kuwa mchakato wake wa kuwaajiri walimu hufanywa kwa haki na ushindani kwa mujibu wa Katiba na sheria. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TSC Evaleen Mitei alisema ajira hufanywa katika ngazi ya kaunti ndogo baada ya nafasi kutangazwa rasmi na miongozo ya uteuzi kuchapishwa. Waziri wa Elimu Julius Migos Ogamba alisema serikali itashirikiana na TSC kukabiliana na uuzaji wa nafasi za ajira, akisema ni uhalifu unaopaswa kukomeshwa.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 25 Aug 2026 06:55:41
Ruto azungumzia siku za mwisho na Raila akisema alimwambia alishatoka hospitali
RAIS William Ruto ameeleza jinsi alivyopokea taarifa ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, mauti ambayo yalizua wingu la huzuni na kutumbukiza taifa kwenye wimbi la maombolezo. Kwenye mahojiano na Taifa Leo, Rais Ruto alisema alikuwa akielekea afisini mwake mwendo wa saa 12:30 asubuhi Oktoba 15, 2025, simu yake ilipokereza. Simu hiyo ilipigwa na Seneta wa Siaya Dkt Oburu Oginga, kakake mkubwa wa Bw Odinga. "Kuna tatizo, 'kiongozi wa vijana' (Oburu) aliniambia. Nadhani nimempoteza kaka yangu," Rais Ruto alikumbuka Dkt Oburu akisema. Dkt Oburu hujiita "kiongozi wa vijana" licha ya umri wake pevu wa miaka 83. Raila alikuwa amefariki India, ambako alikuwa ameenda kutibiwa akiwa na matumaini ya kupona na kurejea nchini. Rais Ruto, alisema alikuwa amezungumza na Raila siku chache kabla ya kifo chake na akaambiwa alikuwa ametoka hospitalini na alikuwa akienda kupumzika. Muda mfupi baadaye, dadake Raila, Ruth Odinga, pia alimpigia simu Rais Ruto simu. Familia ilimweleza kuwa Raila alikuwa ameamka asubuhi hiyo, akafanya mazoezi kabla hali yake kuzorota ghafla. "Maisha yake hayakuweza kuokolewa," Rais Ruto akasema akikumbuka kauli ya Ruth Odinga. Rais Ruto na Raila walikuwa wamefahamiana kwa miongo kadhaa, wakati mmoja wakishirikiana kisiasa na mara nyingine wakitofautiana vikali na kila mmoja kuchukua mwelekeo wake. "Tulianza tukiwa pande tofauti tulipokuwa Kanu, wao wakiwa Ford na wengine. Tulikutana ODM, tukaijenga pamoja. Nilijitahidi kumuunga mkono na alikuwa kiongozi mzuri wa kikosi chetu, kisha tukatengana tena," akasema Rais Ruto. Wawili hao walikabiliana katika uchaguzi wa urais wa 2022, ambapo Rais Ruto alishinda kwa kura 7,176,141 dhidi ya 6,942,930 za Raila. Hata hivyo, maandamano ya 2024 yalibadilisha mazingira ya kisiasa na hatimaye makundi yao yakashirikiana katika Serikali Jumuishi, Raila akiwa sehemu ya serikali hiyo. Rais Ruto alisema katika wiki za mwisho za maisha ya Raila, uhusiano wao ulikuwa umeimarika sana. Walipigiana simu, kukutana na hata kula chakula cha jioni nyumbani kwa Raila. Aidha Rais Ruto alisema Raila alikuwa amepiga simu akisema hakuwa akijihisi vizuri na alitaka kumwona. Raila alimtembelea Rais katika Ikulu ya Nairobi na kujadili masuala mbalimbali kuhusu mustakabali wa nchi. Baadaye, Rais Ruto alimtembelea Raila nyumbani kwake baada ya kuambiwa alikuwa amerejea Nairobi. Walikula chakula cha jioni pamoja na Raila kumweleza kuwa alitaka kupata maoni ya pili ya madaktari kwa sababu afya yake haikuwa ikiimarika. Raila baadaye alisafiri hadi India akiwa na binti yake, madaktari na wengine. Wawili hao waliendelea kuwasiliana kwa simu. Rais Ruto alisema Raila mwanzoni alikuwa na matumaini, akimweleza kuwa madaktari kadhaa walikuwa wamemchunguza na kuamini wamepata matibabu yaliyofaa. Lakini siku chache baadaye, Rais alipokea habari kwamba Raila alikuwa ametoka hospitalini na alikuwa akipanga kupumzika. Hiyo ndiyo ilikuwa taarifa ya mwisho aliyopokea Rais Ruto kabla ya simu ya Dkt Oburu kumjulisha kuhusu kifo cha Raila. Baadaye Ruto alishiriki katika mipango ya kurejesha mwili wa Raila nchini, akiwemo kuwasiliana na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, ambaye alisema alimfahamu Raila binafsi. Kwa Rais Ruto, sehemu ngumu zaidi ilikuwa jinsi kifo hicho kilivyotokea ghafla, kwani siku chache tu kabla walikuwa wakijadili mustakabali wa Kenya.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 25 Aug 2026 04:55:17
Atwoli: Wakati wetu tukiwa Azimio kumfikia Uhuru ilikuwa ngumu, wala hakufanya mengi
KATIBU Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi (COTU), Francis Atwoli, sasa anadai ilikuwa vigumu kumfikia Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, akidai kwamba mara nyingi alisita kushirikiana na mawaziri na viongozi wa kisiasa kuhusu masuala muhimu ya kitaifa. Akizungumza Khwisero, Kaunti ya Kakamega, jana Bw Atwoli alisema Bw Kenyatta alikuwa mgumu kufikiwa ikilinganishwa na marais wengine aliowahi kufanya nao kazi. "Nimefanya kazi na marais wote na namjua Uhuru Kenyatta. Kama si juhudi za Naibu Rais wa wakati huo William Ruto, hata kuwafanya wabunge wakutane na Rais haikuwa rahisi," akasema. Kauli hii inajiri wakati uhusiano kati ya Bw Kenyatta na Rais Ruto ukiwa na mashaka. Mnamo Disemba 9, 2024, Rais Ruto alimtembelea Bw Kenyatta nyumbani kwake Ichaweri, Gatundu, katika juhudi za kurejesha uhusiano wao baada ya miaka kadhaa ya tofauti kali za kisiasa. Katika mahojiano ya hivi majuzi na Taifa Leo, Rais Ruto alisema pia alikuwa amemtembelea Kenyatta katika afisi yake karibu na Ikulu ili kumshawishi kuunga mkono ajenda ya kitaifa. "Nilienda kumuona Ichaweri na pia katika afisi yake iliyo hapa karibu (na Ikulu) na nikajaribu kumshawishi kwamba kama kiongozi wa zamani wa nchi, na ndiye pekee aliye hai sasa, ilikuwa bora atusaidie kujenga nchi, lakini alisita. Hakuwa na uhakika kama alitaka kufanya hivyo na hayo ni maamuzi ambayo watu hufanya. Alichagua kushirikiana na upinzani, akiwafadhili," akasema Rais. Rais Ruto alisema wazo la viongozi hao kushirikiana lilitokana na mazungumzo yake na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, aliyefariki Oktoba 2025. "Sasa sisi ndio wazee. Sisi ndio viongozi wa taifa hili. Kwa nini tusishirikiane, tujenge taifa ambalo tunaweza kulikabidhi kwa kizazi kijacho cha viongozi?" akasema Rais Ruto. Bw Atwoli pia aliwaonya wakazi wa Magharibi dhidi ya kugawanywa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027, akionekana kumlenga Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna. "Jamii ya Waluhya ni rahisi kudanganywa lakini nataka muwe macho," alisema. Alisema pia urais hauwezi kupatikana kupitia michango midogo ya wananchi. "Njia ya kuelekea urais si rahisi. Huwezi kutembea na ndoo sokoni ukikusanya Sh50 kutoka kwa mama mboga. Hizo haziwezi kukufanya uwe rais," akaongeza. Bw Atwoli pia alimtaka Bw Kenyatta kumruhusu Rais Ruto kukamilisha muhula wake bila kuingiliwa. "Tayari alihudumu mihula yake miwili bila chochote cha maana cha kuonyesha. Kwa nini sasa asikae chini na kumruhusu Rais Ruto kuwahudumia Wakenya?" akauliza. Kiongozi huyo wa COTU pia alimkosoa Seneta wa Kakamega Boni Khalwale kwa kugeuza mazishi ya mkewe marehemu, Gloria Khalwale, kuwa jukwaa la kisiasa.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Tue, 25 Aug 2026 04:50:00
Wamunyoro's political gambit: After 55-day conclave, Gachagua declares self fit to unseat Ruto
Rigathi Gachaguas 45-day political conclave has evolved into an extended campaign of consultations aimed at uniting Kenyas opposition ahead of the 2027 General Election.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 25 Aug 2026 03:55:38
Ayacko: Hatutaki viongozi wa Linda Mwananchi Migori
GAVANA wa Migori Ochilo Ayacko amewaonya viongozi wa kundi la Linda Mwananchi dhidi ya kuzuru kaunti hiyo, akisema ziara yao iliyopangwa inaweza kuongeza joto la kisiasa na kusababisha ghasia kama zile zilizoshuhudiwa hivi karibuni katika Kaunti ya Homa Bay. Onyo hilo linatolewa wiki moja baada ya mapigano kati ya wafuasi wa ODM na kundi la Linda Mwananchi huko Homa Bay kusababisha vifo vya watu wawili na kujeruhi wengine kadhaa. Kwa siku tatu zilizopita, Bw Ayacko amekuwa akitoa tahadhari kuhusu mpango wa Gavana wa Siaya James Orengo na viongozi wengine wa Linda Mwananchi kuzuru Migori kama sehemu ya kampeni zao katika eneo la Kusini mwa Nyanza. Akizungumza wakati wa harambee katika Chuo cha Ualimu cha Migori, Gavana Ayacko alisema viongozi wa kisiasa wanafaa kushauriana na viongozi wa maeneo wanayonuia kuzuru, hasa pale ambapo kuna mvutano wa kisiasa. Alisema ziara ya awali ya Bw Orengo mjini Homa Bay bila maelewano ya kutosha na viongozi wa eneo ilichangia mazingira yaliyozaa machafuko. "Orengo alikuwa ameapa kufika Homa Bay hata iweje. Ziara yake bila mwaliko wa viongozi wa eneo na bila uungwaji mkono mashinani ndiyo chimbuko la matatizo yaliyoshuhudiwa," akasema Bw Ayacko. Gavana huyo aliwauliza waliohudhuria mkutano huo ikiwa wangependa Bw Orengo kuzuru Migori, huku wengi wakijibu kwa sauti kwamba hawamtaki. Bw Orengo, Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino ni miongoni mwa viongozi wanaohusishwa na kampeni za Linda Mwananchi. Bw Orengo ameashiria kuwa kundi hilo linapanga kuzuru maeneo mbalimbali ya Kusini mwa Nyanza, yakiwemo Migori na Homa Bay. Katika ziara yao ya mwisho Homa Bay, viongozi hao walifanikiwa kuhutubia wakazi wa Nyandiwa na Sindo katika eneo la Suba Kusini. Hata hivyo, mpango wa kufanya mkutano mjini Homa Bay ulivurugika baada ya kundi hilo kufika jioni na kukabiliwa na mapokezi baridi. Machafuko yaliyofuatia yalisababisha kifo cha afisa mmoja wa polisi na mfanyabiashara mwanamke, huku mali ikiharibiwa. "Jambo muhimu zaidi ni amani kudumu. Serikali yangu imejikita katika maendeleo, hasa kuboresha miundombinu ya barabara, na hatuwezi kuruhusu siasa kuvuruga amani," akasema Bw Ayacko. Wakati huo huo, Gavana wa Homa Bay Gladys Wanga amejitenga na madai yanayomhusisha na ghasia hizo na kutaka uchunguzi ufanywe dhidi ya wote watakaopatikana na hatia. Aliyekuwa Naibu Gavana wa Homa Bay Oyugi Magwang ameonya kuwa kuendelea kwa vurugu za kisiasa kunaweza kutatiza juhudi za maendeleo kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Viongozi mbalimbali sasa wamewataka wanasiasa kushindana kwa sera na hoja badala ya kutumia ghasia, huku hofu ikiongezeka kuwa mivutano ya Homa Bay inaweza kusambaa hadi kaunti jirani za Nyanza.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 25 Aug 2026 03:09:25
US removes Syria from list of state sponsors of terrorism
The US has removed Syria from its list of state sponsors of terrorism after 47 years, lifting what it said was the final major barriers for private sector investment in the country and its reintegration into the global economy. US Secretary Of State Marco Rubio said the move was in recognition of the Syrian governments [...] The post US removes Syria from list of state sponsors of terrorism appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 25 Aug 2026 03:12:20
How Canada could hit back to hurt the US economy – and Trump
What leverage does Canada, which sells about 70% of its goods to the US, actually have in this spiralling trade dispute with its southern neighbour, who also happens to be the worlds largest economy? Canada is the top customer for 26 US states, including Maine, Michigan, and Wisconsin. And it is in the top three [...] The post How Canada could hit back to hurt the US economy and Trump appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 25 Aug 2026 03:15:58
Burnham vows support for Ukraine despite 'outrageous threats' from Russia
Andy Burnham has promised to keep up the pressure on Russia despite Moscows outrageous threats, on his first official visit to Ukraine as UK prime minister. Burnham met Ukrainian President Volodymyr Zelensky and chaired his first meeting of the coalition of the willing, set up by the UK and France under his predecessor Sir Keir [...] The post Burnham vows support for Ukraine despite outrageous threats from Russia appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 25 Aug 2026 02:55:57
Jinsi ugomvi kuhusu mwanamke ulivyozua ghasia za kikabila mpaka wa Kisii na Narok
UGOMVI kati ya vijana wawili kuhusu mwanamke katika baa moja kwenye mpaka wa Kisii na Narok umegeuka kuwa vita vya kijamii, na kusababisha watu kujeruhiwa huku usafiri na biashara zikitatizika. Wiki mbili zilizopita, vijana hao walikuwa wakiburudika jioni katika baa inayopatikana katika kituo cha kibiashara cha Nyabitunwa walipoanza kupigana kuhusu mwanamke. Jamaa zao walijiunga, na kugeuza mzozo huo kuwa makabiliano yaliyoathiri Nyabitunwa, Kiango na Enoosaen. "Lilikuwa tukio dogo kati ya wanaume wawili ambalo lingeweza kutatuliwa hapa hapa, lakini kwa bahati mbaya lilizidi kuwa kubwa," akasema Elvis Machoka, mkazi wa Nyabitunwa. Tangu wakati huo, baadhi ya familia zimekuwa zikilala vichakani kwa hofu ya kuvamiwa usiku. "Huwezi kupita Kiango-Enoosaen bila polisi. Waendesha bodaboda wamejiondoa. Eneo hili limeachwa," alisema Peter Maisei, mkazi wa Enoosaen. Maafisa wa usalama na wazee wa jamii walisema mapigano hayo yameingia wiki ya pili, huku watu kadhaa wakitibiwa majeraha ya mishale. Barabara ya Kiango-Enoosaen sasa inaweza kutumiwa chini ya ulinzi wa polisi pekee. Naibu Kamishina wa Kaunti Ndogo ya Kenyenya, William Bett, alisema hali ya utulivu ilikuwa imeanza kurejea Jumapili asubuhi. "Tumepeleka maafisa wa kutosha wa usalama kukomesha mvutano huo. Kufikia asubuhi hii, utulivu wa kiasi umeanza kurejea. Jumapili tulifanya mkutano wa usalama katika eneo hilo kuwataka wakazi kudumisha amani kabla ya shule kufunguliwa kesho," akasema Bw Bett. "Tungependa kuwahakikishia wazazi na wanafunzi ambao wamekuwa likizoni kwamba usalama utakwepo. Hatutaondoka hadi hali ya kawaida irejee kikamilifu," akaongeza. Wakati huo huo, shughuli katika Kiwanda cha Sukari cha Transmara zimeathirika. Wafanyakazi wanaoishi upande wa Kisii wanalazimika kutumia njia ya Kisii-Kilgoris chini ya ulinzi wa polisi baada ya Kiango-Enoosaen kutopitika. "Malori yanayosafirisha sukari kuelekea Kisii na maeneo mengine hayawezi kupita Enoosaen. Hata usafirishaji wa miwa umeathirika," akasema.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Tue, 25 Aug 2026 03:00:00
Wamunyoro's political gambit: After 55-day conclave, Gachagua declares readiness for 2027 presidency
Rigathi Gachaguas 45-day political conclave has evolved into an extended campaign of consultations aimed at uniting Kenyas opposition ahead of the 2027 General Election.
read moreRight Column Content