taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Thu, 20 Aug 2026 06:55:11
Benki ya Equity yaripoti kuvuna faida kemkem ikielezea kuimarika sekta ya mikopo na akiba
EQUITY Group Holdings imeripoti ongezeko la asilimia 32 la faida baada ya ushuru katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu, ikiashiria kuimarika kwa biashara yake nchini Kenya na katika matawi yake ya kikanda. Benki hiyo ilisema jana faida baada ya ushuru ilipanda hadi Sh45.5 bilioni kutoka Sh34.6 bilioni katika kipindi kama hicho mwaka jana. Faida kabla ya ushuru iliongezeka kwa asilimia 39 hadi Sh57.8 bilioni kutoka Sh41.5 bilioni. Ukuaji huo ulitokana na ongezeko la mapato yasiyotokana na riba na mchango mkubwa wa matawi yake katika nchi nyingine za Afrika. Pesa zilizowekwa na wateja ziliongezeka kwa asilimia 24, huku mikopo ikikua kwa asilimia nane. Benki hiyo pia ilirekodi ongezeko la asilimia 11 la mikopo kwa robo moja. Matawi ya kikanda pia yalifanya vizuri, yakiongozwa na Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ambapo faida baada ya ushuru iliongezeka kwa asilimia 82 na 30 mtawalia. Kwa jumla, mikopo ya kundi hilo iliongezeka kwa asilimia 19 hadi Sh981 bilioni kutoka Sh825 bilioni. Wakati huo huo, mapato yasiyotokana na riba yaliongezeka kwa asilimia 36 hadi Sh55.6 bilioni, yakichangia asilimia 44.5 ya mapato yote ya kundi hilo, kutoka asilimia 40.8 mwaka jana. Equity Insurance Group pia ilirekodi ongezeko la asilimia 24. Ubora wa mikopo uliimarika huku mikopo isiyolipwa ukishuka hadi asilimia 9.5 kutoka asilimia 13.7, huku kiwango cha kufidia mikopo hiyo kikiongezeka hadi asilimia 70 kutoka asilimia 68. Gharama ikilinganishwa na mapato pia ilishuka hadi asilimia 48.6 kutoka asilimia 51.7, ikiashiria kuimarika kwa ufanisi wa biashara.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Thu, 20 Aug 2026 05:55:03
Mwanamume kulipa mpenziwe wa zamani Sh2.5m baada picha za siri kusambaa mitandaoni
MAHAKAMA Kuu imeamuru mwanamume mmoja kumlipa Sh2.5 milioni mwanamke aliyeolewa baada ya picha zake za uchi kusambaa mtandaoni, ikisema mtu anayemiliki picha za siri za mwingine ana wajibu wa kuzilinda. Mahakama ilisema kutozuia picha hizo kusambazwa bila idhini kunaweza kumfanya mhusika kuwajibika, hata kama mwathiriwa hawezi kuonyesha moja kwa moja akaunti iliyozichapisha. Mwanamume huyo, GH, alipatikana na hatia ya kuchangia kusambaa kwa picha za DN, mpenzi wake wa zamani, kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo WhatsApp na Facebook miaka mitatu iliyopita. Ingawa DN hakuweza kuonyesha kuwa GH ndiye aliyepakia picha hizo, alithibitisha kuwa alikuwa na picha hizo zilizopigwa wakati wa uhusiano wao. Mahakama ilisema GH alichangia kusambaa kwa picha hizo moja kwa moja, kwa njia isiyo ya moja kwa moja au kwa kutokuwa mwangalifu, na hivyo kukiuka haki za faragha na utu za DN. DN, ambaye ana watoto wawili, alisema picha hizo zilitumwa kwa marafiki, jamaa na mumewe na kumfanya adharauliwe. Alisema alipokea simu na jumbe zenye picha hizo na kulazimika kufunga akaunti zake za Facebook na WhatsApp. Pia alisema alihitaji matibabu na ushauri nasaha baada ya kupata msongo mkubwa wa mawazo. Kwa mujibu wa DN, picha hizo zilipomfikia mumewe, ndoa yao ilivurugika na akalazimika kurudi kwa wazazi wake pamoja na watoto. GH alikanusha kusambaza picha hizo. Alisema alifahamu kuwa zilikuwa zikisambazwa baada ya mama yake kumjulisha Machi 23, 2023. Pia aliambia mahakama kuwa alikuwa amelazwa hospitalini kuanzia Machi 15 hadi 17 kutokana na ugonjwa na hivyo hangeweza kusambaza picha hizo. Hata hivyo, mahakama ilisema kulazwa hospitalini hakumaanishi kwamba hangeweza kutumia simu yake. Mahakama pia ilikubali picha za skrini za mitandao ya kijamii licha ya kutowasilishwa kwa cheti kinachohitajika kwa ushahidi wa kielektroniki. Ilisema ushahidi wa mashahidi, mazingira ya kesi na taarifa nyingine zilithibitisha uhalisi wa picha hizo. Picha hizo zilionekana kusambazwa kupitia ukurasa uliokuwa na jina "Leaked Videos in Kenya", lakini hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja uliomtaja GH kama chanzo. Hata hivyo, mahakama ilisema GH hakutoa maelezo ya kuaminika kuhusu namna picha alizokuwa nazo zilifika kwa umma. Jaji alisema kumiliki picha za siri kunampa mtu "wajibu mkubwa wa kuhakikisha hazisambazwi bila idhini". Mahakama pia ilimzuia GH kuchapisha au kusambaza picha hizo kwa njia yoyote.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 20 Aug 2026 05:18:11
Tanzania suspends newspaper after report alleging gov't divisions
Tanzania has suspended a weekly newspaper for six months over alleged breaches of media law, the information ministry said Wednesday, after the outlet published a story alleging government divisions. International observers have warned of narrowing civil and political rights in the country, which last year saw hundreds massacred during election unrest. The suspension of Mwanahalisi [...] The post Tanzania suspends newspaper after report alleging govt divisions appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 20 Aug 2026 05:24:11
Two in Range Rover theft case linked to Dr Mutiso murder freed on bond
Two suspects arrested in connection with the theft of a Range Rover from a disputed 21-acre parcel of land in Mlolongo, which has been linked to the murder of Dr Victoria Mutiso, have been released on bond. The suspects include a daughter to the husband of Dr Mutiso. Mavoko Senior Resident Magistrate Lilian Kwamboka on [...] The post Two in Range Rover theft case linked to Dr Mutiso murder freed on bond appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content