kahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 18 Aug 2026 06:20:02
Missing Vihiga man found dead in water pit at primary school
A 47-year-old man who had been reported missing has been found dead in a water pit within the compound of Khwiliba Primary School in Luanda Sub-County, Vihiga County. The body of Laban Zafania Ongombe, a resident of Khwiliba Village in Mukhalahala Sub-location, was discovered on Monday evening. Police established that the body belonged to Ongombe, [...] The post Missing Vihiga man found dead in water pit at primary school appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 18 Aug 2026 07:10:04
Zambia President Hichilema has been reelected for a second term
Zambian President Hakainde Hichilema has been reelected for a second five-year term, the Electoral Commission of Zambia announced early Tuesday. He was declared the outright winner of last Thursday's presidential election without the need for a run-off, having secured 61.4% of the 5 million votes cast. According to the commission, Hichilema won with 2,965,326 votes [...] The post Zambia President Hichilema has been reelected for a second term appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 18 Aug 2026 05:55:09
Eti sijui kusoma? Wewe ndio ulikuwa unanililia ulipopokonywa Wizara ya Ulinzi, Jumwa ajibu Duale
ALIYEKUWA Waziri wa Utumishi wa Umma Aisha Jumwa wikendi alimjibu vikali Waziri wa Afya Aden Duale baada ya kutoa madai ya kutokuwa na uwezo wa kusoma na kuelewa stakabadhi za Baraza la Mawaziri walipokuwa serikalini. Bi Jumwa alimshutumu Bw Duale kwa unafiki na kusema matamshi yake yalilenga kumdhalilisha kisiasa. Alisisitiza kuwa alikuwa na uwezo kamili wa kuelewa shughuli za Baraza la Mawaziri. "Nilikaa nawe katika Baraza la Mawaziri na hakuna siku yoyote ulizungumza nami isipokuwa siku moja," akasema Bi Jumwa. Alidai Bw Duale alimkasirikia baada ya kumpeleka mmoja wa magavana wa zamani kumwona Rais William Ruto. "Siku hiyo ulipozungumza nami ulikuwa na hasira kubwa, ukiniuliza kwa nini nilimpeleka gavana huyo kwa Ruto," akasema. Bw Duale alikuwa amemshambulia Bi Jumwa Jumamosi jijini Mombasa, akidai wakati walipokuwa Barazani alikuwa akimsaidia kusoma na kuelewa baadhi ya stakabadhi za serikali. Alisema mara kadhaa Bi Jumwa alishindwa kueleza baadhi ya masuala yaliyokuwa kwenye hati hizo, hivyo akalazimika kumsaidia. Bw Duale alitoa matamshi hayo alipokuwa akikosoa uhusiano wa Jumwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua pamoja na kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka. Hata hivyo, Bi Jumwa alimtaka Bw Duale kuacha kujaribu kuamulia Pwani upande wa kisiasa wa kuunga mkono. "Hutatuamulia Pwani mahali pa kupigia kura. Pwani ina viongozi wake na ikiwa unafikiri Pwani haina kiongozi, mimi niko hapa kwao," alisema. Mbunge wa EALA Falhada Iman Dekow pia alilaani matamshi ya Bw Duale, akisema tofauti za kisiasa hazifai kugeuka kuwa vita vya kibinafsi dhidi ya viongozi wanawake. Alisema kila kiongozi ana haki ya kidemokrasia kuchagua upande wa kisiasa anaounga mkono.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 18 Aug 2026 06:55:46
Mkuu wa kuwalinda mashahidi aagizwa afike mahakamani leo
MAHAKAMA Kuu jana ilimwaamuru Mkurugenzi wa Mamlaka ya Kuwalinda Mashahidi (WPA) kufika kortini leo, kueleza hatua zilizochukuliwa kuwalinda mashahidi katika kesi ya kutoweka kwa wanaharakati wanne wa Mathare. Jaji Alexander Muteti alimwamuru mkurugenzi huyo kufika binafsi kortini Agosti 18, 2026, ili kutoa maelezo kuhusu ulinzi wa mashahidi wanaohusishwa na kesi hiyo. Wanaharakati hao, Abdul Aziz Zizu, MacMillan Kiarie, Michael Oloo na Evans Oloo, walitekwa nyara Juni 20 na wanaume waliokuwa wamevalia barakoa na kuficha nyuso zao. Mawakili Abner Mango, Noordeen Khagai na Pius Oyoo waliambia mahakama kuwa walifika katika afisi za WPA lakini hawakupewa taarifa kuhusu mashahidi waliowasilisha majina yao. "Tulienda kwa afisi za WPA lakini hatukupata msaada wowote. Hatukuelezwa ikiwa mashahidi hao wamehojiwa na kuwekwa mahali salama ili wasitishwe na maafisa wa usalama," alisema Mango. Jaji Muteti aliamuru WPA kuwalinda mashahidi na kuhakikisha wanatoa ushahidi bila kuhofia usalama wao. Mahakama pia iliagiza maafisa Brenda Akoth Opondo, Waceke Macharia na Jane Nyambura Njoroge kufika kutoa ushahidi kuhusu kutoweka kwa wanaharakati hao. Afisa wa polisi Humphrey Kaimenyi aliagizwa kuwasilisha kanda za CCTV zinazoonyesha matukio yaliyopelekea kutoweka kwao. Awali, Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja na Mkurugenzi wa DCI Mohamed Amin waliambia mahakama kuwa wanaharakati hao "hawako mikononi mwa polisi." Jaji Muteti alisema mahakama ina jukumu la kuhakikisha ukweli unapatikana na haki inatendeka kwa mujibu wa Katiba.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 18 Aug 2026 05:31:07
Human remains of missing man found in Kwale forest
Police in Kwale recovered human remains believed to belong to a 39-year-old man who went missing about two weeks ago. The remains were discovered on Monday morning in a forested area in Kasemeni Sub-location, Mwereni Location, Lungalunga Sub-County. According to police, locals reported the discovery at about 7:40am, prompting officers to visit the scene. Police [...] The post Human remains of missing man found in Kwale forest appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content