kahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 18 Aug 2026 05:45:47
Lawyer Kinyanjui demands Sh50 million in damages over alleged post on Sh25 million claims
Nairobi lawyer Harrison Kinyanjui has demanded Sh50 million in damages from businessman Michael Makarina who allegedly linked him to a Sh25.4 million bribery scheme involving former Deputy President Rigathi Gachagua. Through his lawyers, Mbichire Co. Advocates, Kinyanjui has issued a demand notice to Makarina, who operates the X account @michaelmakarina under the name "Hon. [...] The post Lawyer Kinyanjui demands Sh50 million in damages over alleged post on Sh25 million claims appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 18 Aug 2026 04:55:52
Ghasia za Homa Bay zazua kumbukumbu ya ubabe wa Raila-Orengo miaka ya 90's
VURUGU zilizoshuhudiwa katika mikutano ya Linda Mwananchi Homa Bay mwishoni mwa wiki zimeibua tena kumbukumbu za migogoro mikali ya kisiasa iliyotikisa Luo Nyanza baada ya kifo cha Jaramogi Oginga Odinga, mwanasiasa mashuhuri wa eneo hilo. Kwa sasa, viongozi wa Linda Mwananchi, kundi lililojitenga na ODM, wanakabiliana vikali na mrengo unaoongozwa na Seneta wa Siaya Dkt Oburu Oginga. Linda Mwananchi inaongozwa na Gavana wa Siaya James Orengo, Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na Mbunge wa Embakasi East Babu Owino. Kiini cha mzozo huo ni msimamo kuhusu uchaguzi wa 2027. Mrengo wa Dkt Oburu unaunga mkono kuchaguliwa tena kwa Rais William Ruto, huku upande wa Bw Orengo ukitaka ODM kusimamisha mgombea wake wa urais. Bw Orengo na washirika wake pia wanamlaumu Rais Ruto kwa kuchangia migawanyiko ndani ya ODM. Kifo cha Raila Odinga kimeacha pengo kubwa la kisiasa Nyanza, huku makundi mbalimbali yakijitokeza kuwania ushawishi katika eneo hilo. Vurugu za Homa Bay zimewakumbusha wengi tukio la Aprili 24, 1999, wakati uhasama kati ya Raila na Orengo ulifikia kilele katika harambee Ugunja, wakati huo ikiwa sehemu ya eneobunge la Ugenya. Raila, aliyekuwa akiongoza NDP, na Orengo, aliyekuwa mbunge wa Ugenya, walikuwa wameingia katika mzozo mkali wa kisiasa. Raila aliwasili kwenye harambee akiwa amevalia agbada ya Nigeria na kuandamana na vijana waliokuwa wakimshangilia kwa kaulimbiu yake ya kampeni "Amollo Tinga". Bw Orengo naye aliwasili na kundi la vijana, hali iliyosababisha makabiliano na hatimaye vurugu. Polisi walilazimika kutumia vitoa machozi na mbwa wa kunusa kuwatenganisha vijana hao. Bw Orengo alilazimika kukimbilia katika shamba la miti ambako alimshambulia Raila kwa madai ya kuwaleta watu kutoka nje ya Ugenya. "Magari mengi yalikuja Ugenya, malori yaliyojaa, matatu na watu hao hawatoki Ugenya," akasema. Raila naye alijibu kwa kuuliza ni nani aliyemwalika Bw Orengo katika hafla hiyo. "Ni nani aliyesema naye na kumwalika katika hafla hii? Aliulizwa kama jina lake lingewekwa kwenye kadi ya mwaliko lakini akasema atafikiria," alisema Raila. Mwaka huo huo, Raila pia alikabiliwa na upinzani mkali Kisumu kutoka kwa aliyekuwa Meya Akinyi Oile, mshirika wa kisiasa wa Rais wa zamani Daniel Moi. Uhasama wa Mabw Orengo na Raila ulianza baada ya kifo cha Jaramogi mwaka 1994 wakati wa uchaguzi wa naibu mwenyekiti wa Ford Kenya. Bw Orengo alishinda kwa kura moja, hatua iliyomkasirisha Raila na kumfanya kumpinga katika kinyang'anyiro cha uongozi wa chama. Mnamo Machi 18, 1995, uchaguzi wa uongozi wa Ford Kenya katika Uwanja wa Thika uligeuka kuwa vurugu, huku jaribio la kutaka kumuua Raila likiripotiwa. Leo, historia hiyo inaonekana kujirudia, lakini mara hii bila Raila. Bw Orengo anakabiliana na Dkt Oburu katika vita vya kuwania ushawishi wa kisiasa wa jamii ya Luo. Upande wa Orengo unaungwa mkono na Babu Owino na Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi, huku Dkt Oburu akiungwa mkono na Gavana wa Homa Bay Gladys Wanga na Mawaziri Opiyo Wandayi na John Mbadi. Mbunge wa Suba Kaskazini Millie Odhiambo na Mbunge Mwakilishi wa Kike wa Kisumu Ruth Odinga nao wana msimamo vuguvugu na hawajaonyesha upande wanaounga mkono.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 18 Aug 2026 03:55:20
'Afghanistan' ya Kaunti ya Homa Bay yaanikwa kwa kusheheni vumbi na uchakavu
MKUTANO wa kisiasa wa Linda Mwananchi uliofanyika Homa Bay Jumapili ulifichua upande wa kaunti hiyo ambao Wakenya wengi huwa hawauoni. Picha za Homa Bay zinapowekwa mtandaoni, mara nyingi huonyesha fukwe za mchanga, vilima vya kijani, Ziwa Victoria na wanyamapori katika Mbuga ya Kitaifa ya Ruma. Lakini mbali na mandhari hayo kuna Homa Bay nyingine ambayo wakazi wanaijua vyema na hii ni barabara inayounganisha Kituo cha Biashara cha Kiabuya na ufuo wa Nyandiwa. Wakenya walipokuwa wakifuatilia mkutano huo kupitia simu, hawakusikiliza hotuba pekee bali pia walitazama mandhari katika maeneo yaliyotembelewa na Gavana James Orengo, Seneta Edwin Sifuna na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino. Barabara ya Nyandiwa, ambako mkutano wa kwanza ulifanyika, ilivutia zaidi kutokana na hali yake ya vumbi na uchakavu. Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii waliifananisha kwa kejeli na Afghanistan na Gaza. Picha kutoka video za moja kwa moja zilionyesha barabara za Suba Kusini ikiwa katika hali mbaya, huku baadhi ya maeneo yakiwa bila nguzo za umeme. Vilevile, picha moja ilionyesha Ziwa Victoria kwa mbali, huku mandhari yakiwa kame na bila miti mingi. Baadhi ya watumiaji waliita eneo hilo kwa mzaha "Mwanzo wa Hormuz". Hata hivyo, wengine walisema hali ya barabara ni ushahidi wa miaka mingi ya kutengwa kwa eneo hilo na serikali zilizopita. Mbunge wa Suba Kaskazini, Millie Odhiambo, alikiri kuwa barabara nyingi eneo la Suba Kaskazini na Suba Kusini ziko katika hali mbaya. Bi Odhiambo alisema serikali ya Rais William Ruto imeweka lami kwenye Barabara ya Mzunguko ya Rusinga na kufungua Barabara ya Mzunguko ya Mfangano, huku Sindo-Mbito ikiwa miongoni mwa barabara nyingine zilizopangiwa kufanyiwa kazi. Gavana Gladys Wanga alisema kutengwa kwa eneo hilo kwa kiasi fulani kulitokana na ODM kuwa chama cha upinzani kwa miaka mingi. "Tuache kuwapotosha watu kwa kusema hizi ni barabara za mashambani na kwamba barabara kuu zilikuwa zimezuiwa. Unachoona hapa, isipokuwa barabara ya Homa Bay hadi Mbita na Barabara ya Mzunguko ya Rusinga, ni barabara kuu. Rais Kibaki na Waziri Mkuu Raila waliweka lami barabara ya Homa Bay hadi Mbita. Rais Uhuru Kenyatta alijenga daraja la Mbita," akaandika kwenye ukurasa wa Facebook. Aliahidi barabara hiyo ingekarabatiwa. "Sasa tuko ndani ya Serikali Jumuishi, na barabara ya Suba itakarabatiwa chini ya mradi wa Barabara ya Mzunguko ya Ziwa Victoria. Waziri Mbadi ametia saini ili kuhakikisha inaboreshwa," akasema. Bw Sifuna alishangaa kwa nini barabara hiyo ilikuwa katika hali mbaya ilhali iko karibu na nyumbani kwa Waziri wa Fedha John Mbadi. "Juzi tuliambiwa kwamba kwa sababu mnaunga mkono Serikali Jumuishi, barabara zote zimewekewa lami. Leo tumekula vumbi. Tumekula vumbi sawasawa," akasema. Alisema kwamba wakazi wa Homa Bay bado hawajanufaika kikamilifu na miradi ya serikali kuu. "Hakuna tofauti kati yenu na sisi Magharibi. Bado mnasafiri kwenye barabara za vumbi kama sisi," alisema. Baadhi ya picha zilizotengenezwa kwa AI pia zilisambaa mtandaoni, lakini Taifa Leo ilithibitisha kuwa barabara iliyoonyeshwa ni njia inayotumiwa kwa kawaida na wenye magari kutoka Kiabuya hadi Nyandiwa. Katika sehemu moja, magari hulazimika kuvuka kijito, huku magari yenye injini dhaifu yakitatizika kupanda mteremko mara baada ya kuvuka.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 18 Aug 2026 03:20:16
Roads in ruins: Masaba South in fury over shoddy county works
Poor workmanship on roads undertaken by the Kisii County Government in Masaba South Sub-County has sparked anger among residents, with a local MCA questioning the quality of projects being implemented using public funds. Residents have raised concerns that some roads deteriorate shortly after rehabilitation, putting the spotlight on the supervision of contractors and the county's [...] The post Roads in ruins: Masaba South in fury over shoddy county works appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 18 Aug 2026 03:22:54
Tupac murder trial: 'All hell broke loose' night of rapper's shooting, witness says
In the opening day of Tupac Shakurs murder trial, prosecutors painted former gang leader Duane Keffe D Davis as someone seeking revenge before masterminding the drive-by shooting that killed the iconic rapper. Witnesses took a Las Vegas jury back in time three decades ago to the night Shakur was shot, when gangs had a hold [...] The post Tupac murder trial: All hell broke loose night of rappers shooting, witness says appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 18 Aug 2026 03:24:57
US-Canada trade talks 'intense' as new tariff deadline looms
Intense trade talks are going down to the wire as Canada seeks to avoid a fresh round of tariffs from the Trump administration due to come into effect in less than 48 hours. Canadian negotiators have been camped out in Washington for a week, trying to pin down some agreement before new 50% tariffs on [...] The post US-Canada trade talks intense as new tariff deadline looms appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Tue, 18 Aug 2026 03:27:17
Russia warns UK over supplying drones to Ukraine
Russia has accused the UK of deliberately opting for an escalation of the Ukraine crisis following confirmation that British-made drones had been used in strikes on targets in Russia. In doing so, the United Kingdom is acting as an accomplice and co-perpetrator of the bloody crimes and terrorist attacks, the Russian Embassy to the UK [...] The post Russia warns UK over supplying drones to Ukraine appeared first on Kahawatungu.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Tue, 18 Aug 2026 03:30:00
Security failure: Kenya on edge of lawlessness as citizens call for Ruto's action
Kenyas security agencies are under scrutiny over their alleged failure to prevent and effectively respond to the deadly political violence witnessed during the Linda Mwananchi tour of Homa Bay.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 18 Aug 2026 02:55:42
Wahuni walilipwa Sh4,000 kwa siku, mkutano ulifanywa nyumbani kwa mwanasiasa mashuhuri -Ufichuzi
VURUGU zilizotokea Homa Bay Jumapili wakati wa mikutano ya kundi la Linda Mwananchi huenda zilipangwa siku kadhaa kabla, huku wanasiasa wakidaiwa kuwahamasisha vijana na kuunda mtandao wa kuratibu uvamizi. Duru kutoka kwa polisi na mahojiano na baadhi ya vijana waliohusika vilifichua kuwa mkutano wa kwanza ulifanyika Agosti 2 nyumbani kwa mwanasiasa mashuhuri, muda mfupi baada ya hafla ya kumkaribisha Mbunge wa Mwakilishi wa Kike wa Homa Bay, Joyce Osogo. Vijana hao walidaiwa kuagizwa kumzuia Gavana wa Siaya James Orengo pamoja na kikosi cha Linda Mwananchi, inayojumuisha Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, kufanya mikutano katika kaunti hiyo. Inadaiwa kila kijana aliyehusika katika fujo hizo alilipwa kati ya Sh2,000 na Sh4,000. Wale waliolipwa Sh4,000 walidaiwa kusafirishwa kutoka kaunti jirani ya Migori. Siku moja kabla ya mikutano hiyo, vijana walifanya mkutano mwingine katika eneo la Lo Rateng, uliokuwa umeandaliwa na Mbunge wa Homa Bay Mjini Peter Kaluma. Katika video iliyosambazwa mitandaoni, Bw Kaluma aliwataka wafuasi wake kuwafukuza wanachama wa kundi pinzani aliowatuhumu kuingilia shughuli za ODM. Alisema: "Tunatoa amri sasa kwamba yeyote anayesema muhula mmoja afukuzwe." Pia aliwataka wafuasi wake kuwatafuta wanachama wa Linda Mwananchi katika hoteli na maeneo mengine ya kulala na kuwafukuza. Muda mfupi baadaye, ripoti za uvamizi zilianza kuibuka katika maeneo mbalimbali ya Homa Bay. Vijana waliokuwa kwenye pikipiki walionekana wakiwa na panga, marungu na silaha nyingine hatari. Katika Hoteli ya Homa Bay Tourist, vijana waliingia kwa nguvu, wakawafukuza wageni na kuwashambulia wafanyakazi. Walivamia vyumba 21 na kuiba magodoro na televisheni. Pia waliharibu kanda za CCTV ili kuzuia kurekodiwa kwa matukio yaliyofuata. Baada ya hapo, vijana hao waliagizwa kukutana katika kituo cha mabasi cha Homa Bay saa 10 alfajiri Jumapili na kuweka vizuizi barabarani ili kuzuia watu wanaohusishwa na Linda Mwananchi. Mawe na vitu vingine vilitumiwa kuziba barabara, hali iliyowalazimisha wakazi kubaki nyumbani huku baadhi ya wafanyabiashara wakishindwa kufika sokoni. Mmoja wa vijana waliozungumza na Taifa Leo alisema maagizo yalipitishwa kupitia simu kutoka kwa wanasiasa na wahamasishaji wa vijana. Alidai baadhi ya vijana hutumiwa kama walinzi binafsi wa wanasiasa na hupewa silaha kabla ya maandamano. Kamishina wa Kaunti ya Homa Bay Ronald Mwiwawi alisema baadhi ya vijana walikuwa wameunganisha panga mbili kwa kuzichomelea ili kutengeneza silaha ndefu zaidi. Vurugu ziliongezeka msafara wa Bw Orengo ulipokaribia Homa Bay. Msafara huo, uliokuwa na Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, ulizuiwa Ndhiwa na mzunguko wa Kodoyo. Polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya vijana waliokuwa wamefunga barabara. Baadhi ya vijana waliokuwa katika msafara wa Linda Mwananchi pia walihusika katika kuwatawanya wapinzani. Magari kadhaa yalipigwa mawe na mengine kugongana. Baada ya mikutano ya Nyandiwa na Sindo, msafara ulipokuwa ukirejea Homa Bay Mjini, mapigano mengine yalizuka karibu na mzunguko wa Kodoyo. Mmoja wa vijana aliyeokolewa na wanahabari wa Taifa Leo alikuwa na majeraha makubwa shingoni, mkononi na mgongoni. Alidai alikuwa ndani ya gari lililochomwa moto. Mtu mmoja anayetajwa kama Abdi alidaiwa kuwa kiungo muhimu kati ya wanasiasa na vijana. Duru zilisema Abdi, anayetajwa kuwa kiongozi wa vijana wa ODM, ana ushawishi mkubwa na hujulikana kwa jina la "Kamanda." Duru ziliarifu kuwa Abdi hupokea simu kutoka kwa viongozi kabla ya kuwasiliana na vijana kutoka maeneo ya Shauri Yako, Sophia, Misita na Got Rabuor. Kwa vijana wengi wasio na ajira, ahadi ya pesa za haraka imekuwa kivutio kikubwa. Baadhi yao walidaiwa kulipwa Sh2,000 baada ya kushiriki vurugu. Vurugu hizo hata ziliingia katika Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Kaunti ya Homa Bay, ambako vijana walijaribu kuingia baada ya kusikia kuwa baadhi ya waliojeruhiwa walikuwa wakipatiwa matibabu. Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Vincent Oduor, alisema polisi waliitwa kusaidia kudhibiti hali hiyo. Wakati huo huo, ushahidi uliokusanywa ulionyesha kuwa upande wa Linda Mwananchi pia ulikuwa umejiandaa kwa uwezekano wa makabiliano. Duru kutoka kundi hilo zilisema baadhi ya wagombea waliokuwa katika msafara walikuwa na leseni za kumiliki bunduki na walikuwa wameandaa walinzi wenye silaha. Polisi walikamata watu 15 waliodaiwa kuhusishwa na Linda Mwananchi katika Kaunti ya Kisumu na kupata silaha hatari. Watu wengine wawili walikamatwa Migori na panga tano zikapatikana. Kamanda wa Polisi wa Homa Bay Lawrence Koilem alisema watu wasiopungua 22 walikamatwa kuhusiana na vurugu hizo. Polisi pia walipata bastola aina ya Ceska iliyokuwa na risasi 13. Vurugu hizo ziliacha watu wawili, akiwemo afisa wa polisi, wakiwa wamefariki, huku wengine kadhaa wakijeruhiwa. Magari sita yalichomwa moto na biashara kadhaa kuporwa.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Mon, 17 Aug 2026 22:00:00
Security failure? Interior chiefs on the spot over Homa Bay chaos
Kenyas security agencies are under scrutiny over their alleged failure to prevent and effectively respond to the deadly political violence witnessed during the Linda Mwananchi tour of Homa Bay.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 17 Aug 2026 21:27:30
A Buyer's Guide to Bidding Confidently at Vintage Guitar Auctions
Vintage guitar auctions reward patience, evidence, and a clear head. A clean finish or famous decal can draw attention, but value often sits in quieter details. Neck angle, solder joints, pot codes, bridge height, fret wear, finish history, and repair records all deserve careful review. Confident bidding starts before registration. Buyers who prepare well can [...] The post A Buyers Guide to Bidding Confidently at Vintage Guitar Auctions appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 17 Aug 2026 21:34:50
'It was a state-backed ambush,' says Linda Mwananchi over Homa Bay chaos
The Linda Mwananchi movement accused security officers and alleged state operatives of coordinating a violent attack against its leaders and supporters during its tour of Homa Bay County on Sunday, leaving two people dead and several others injured. Movement leaders described the incident as a "deliberate operation" rather than a spontaneous outbreak of political violence, [...] The post 'It was a state-backed ambush,' says Linda Mwananchi over Homa Bay chaos appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content