taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 17 Aug 2026 04:55:18
'Sultan' Joho aponyoka kesi ya maadili
WAZIRI wa Madini, Hassan Ali Joho amepata afueni baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali ombi la kutaka atangazwe kuwa hafai kushikilia wadhifa wa umma kutokana na madai ya kutotii amri ya mahakama alipokuwa Gavana wa Mombasa. Kesi hiyo iliwasilishwa na wafanyabiashara Ashok Labshanker Doshi na Pratibha Ashok Doshi baada ya Bw Joho kupatikana na hatia ya kudharau amri ya mahakama na kuhukumiwa mwaka 2021. Doshi walitaka mahakama itamke kuwa Bw Joho alikiuka masharti ya Katiba kuhusu uongozi na uadilifu na kumzuia kabisa kushikilia wadhifa wowote wa umma au Serikali. Mzozo huo ulitokana na kesi ya ardhi kuhusu kipande cha ardhi cha ekari mbili huko Changamwe. Mnamo Mei 2019, maafisa wa Kaunti ya Mombasa wakiongozwa na Bw Joho walibomoa ukuta wa uzio uliokuwa kwenye ardhi hiyo iliyokuwa na mgogoro. Serikali ya Kaunti ilidai kuwa ardhi hiyo ilikuwa mali ya shule ya eneo hilo, huku akina Doshi wakisisitiza kuwa ilikuwa mali yao binafsi na ilikuwa imelindwa na amri ya mahakama. Ubomoaji huo ulizua mzozo , ambapo Mahakama ya Mazingira na Ardhi mnamo Februari 12, 2020, ilimpata Bw Joho na hatia ya kutotii amri ya mahakama.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 17 Aug 2026 03:55:27
Kalonzo ataka Omollo ajiuzulu, adai ameshindwa kuzima uhuni
KIONGOZI wa Wiper, Kalonzo Musyoka amemtaka Katibu katika Wizara ya Usalama wa Ndani, Dkt Raymond Omollo kujiuzulu, akishutumu serikali kwa kushindwa kudhibiti uhuni wa kisiasa. Bw Musyoka pia alidai kuwa ukosefu wa usalama unaoshuhudiwa katika maeneo mbalimbali ni sehemu ya mpango wa kuunda mazingira yatakayotumiwa kuahirisha Uchaguzi Mkuu wa mwaka ujao. "Wahuni wanaeneza hofu na hatuwezi kufuata mkondo huo. Katibu Omollo lazima ajiuzulu kwa sababu mkuu wake amekataa kumtimua ilhali kuna visa vya ukosefu wa usalama kila mahali," akasema Bw Musyoka alipokuwa akizungumza katika Kanisa la Reedemed Gospel Kithimani, Kaunti ya Machakos. Alishangaa kwa nini vitendo vya kihuni vinaendelea licha ya Rais William Ruto kutoa hakikisho hapo awali kwamba serikali ilikuwa imemaliza tatizo hilo. Bw Musyoka alitaja ghasia zilizoshuhudiwa Homa Bay Jumapili, ambapo waandishi wawili wa habari walijeruhiwa na biashara kufungwa kuelekea mkutano wa Linda Mwananchi. Pia alirejelea vurugu zilizotokea katika eneobunge la Rongai Kaunti ya Nakuru Jumamosi, ambapo msafara wa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua ulipigwa mawe na mikutano ya kisiasa kuvurugwa. Bw Musyoka pia alielekeza lawama zake kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), akisema Wakenya wanafuatilia kwa karibu kila hatua inayochukuliwa katika maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2027. "IEBC inapaswa kuwaruhusu Wakenya kuwachagua viongozi ambao hawajatwaliwa na serikali. Tulisema hatuwezi kuelekea katika uchaguzi ujao tukiwa na Smartmatic kama kampuni inayotoa programu ya uchaguzi, na tunajua michezo hii na lazima ikome," alisema. Bw Musyoka aliandamana na Gavana wa Machakos Wavinya Ndeti, Mwenyekiti wa Wiper na aliyekuwa Mbunge wa Kigumo Jamleck Kamau, Seneta wa Machakos Agnes Kavindu na Naibu Gavana Francis Mwangangi. Bw Kamau alimuunga mkono Bw Musyoka katika azma yake ya kuwania urais 2027, akisema ana ushawishi wa kitaifa nje ya Ukambani. "Kalonzo si mwanasiasa wa Wakamba pekee, yeye ndiye rais wa sita wa Kenya. Kuanzia wikendi ijayo tutaanza ziara zetu za kisiasa na haki itakuwa msingi katika chama hiki," alisema Bw Kamau. "Kalonzo ni mtu wa amani na 2007, kama hangeungana na Mwai Kibaki, nchi isingekuwa na amani. Amejitolea kwa dhati kwa Raila na sasa ni zamu yake. Hana doa. Ikiwa tunataka kiongozi mwenye amani, basi huyo ni Kalonzo Musyoka," akaongeza Bw Kamau. Bw Musyoka pia alizungumzia utata wa bajeti katika Bunge la Kaunti ya Machakos, akiwataka MCA kuidhinisha bajeti hiyo ili serikali ya kaunti iweze kuendelea kutoa huduma kwa wananchi. "Bajeti si pesa za kibinafsi za gavana, kwa hivyo tushirikiane na tusonge mbele," akasema kiongozi huyo wa Wiper. Gavana Ndeti alimtaka Rais Ruto na vyombo vya usalama kuchukua hatua madhubuti dhidi ya vitendo vya kihuni na kurejesha usalama nchini. Pia alimuunga mkono Bw Musyoka kuwania urais 2027, huku akiwakosoa madiwani kwa kuidhinisha nusu tu ya bajeti ya kaunti, ambayo alisema inaweza kugharamia mishahara pekee. "Bila bajeti hatuwezi kutoa huduma ambazo wananchi wetu wanahitaji. Nimewaita madiwani ili tukae pamoja kwa sababu ni sisi tutakaoipeleka kaunti hii mbele," alisema Bi Ndeti.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 17 Aug 2026 02:55:38
Sifuna avamia ngome ya Raila
MAKABILIANO makali ya kisiasa yaliyoshuhudiwa Jumapili katika Kaunti ya Homa Bay yamefichua vita vinavyozidi kushika kasi vya kutaka kudhibiti ngome ya kisiasa ya marehemu Raila Odinga, huku makundi hasimu yakijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa 2027. Linda Mwananchi, inayoongozwa na Gavana wa Siaya James Orengo na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna, ilikaidi vizuizi vya barabarani, uvamizi na na hatimaye kuandaa mikutano Nyandiwa, Sindo na Homa Bay mjini. Kuingia kwao katika eneo hilo kulionyesha wazi mtihani mkubwa kwa juhudi za Rais William Ruto na washirika wake kuendeleza ushawishi katika eneo la Luo Nyanza. Eneo hilo lilimkataa katika uchaguzi wa 2022 na kumpigia kura mwanao marehemu Raila. Kwa sasa eneo hilo linangáng'aniwa na makundi mbalimbali ya kisiasa. Upande mmoja ni kundi la ODM linalopinga kuchaguliwa tena kwa Rais Ruto na sasa linaendesha shughuli zake chini ya vuguvugu la Linda Mwananchi. Mrengo mwingine ni kambi inayounga mkono serikali, ambayo imekuwa ikitumia miradi ya maendeleo na teuzi serikalini kujipigia debe. Homa Bay kwa miaka mingi imekuwa ngome kuu ya kisiasa ya Bw Odinga lakini sasa ni kitovu kinachongángániwa na mirengo hii miwili Kufuatia kifo cha Bw Odinga mwaka jana, kilichoacha pengo kubwa la kisiasa, Homa Bay imekuwa eneo muhimu la kupimia ni nani atakayerithi ushawishi wake kisiasa. Gavana Gladys Wanga, ambaye ametajwa kama mmoja wa viongozi wanaoweza kuchaguliwa kuwa mgombea mwenza wa Rais Ruto mnamo 2027, anakabiliwa na changamoto ya kulinda ngome ya jadi ya ODM. Ana kibarua kuonyesha kuwa ushirikiano wa chama hicho na serikali ya Kenya Kwanza umeleta manufaa kwa eneo hilo. Tangu aingie mamlakani, Rais Ruto ameongeza ushawishi wake wa kisiasa na miradi ya maendeleo katika Nyanza ya Waluo. Serikali imetaja miradi kama kukamilishwa kwa Uwanja wa Raila Odinga, Gati ya Homa Bay, Soko la Samaki la Koginga, Ikulu ndogo , nyumba za gharama nafuu, Barabara ya Mzunguko ya Mfangano-Rusinga, ukarabati wa Chuo Kikuu cha Tom Mboya pamoja na ujenzi na uwekaji wa lami katika barabara mbalimbali. Hata hivyo, Linda Mwananchi inatoa hoja tofauti ikisema barabara, viwanja na miradi mingine ya maendeleo haiwezi kuchukua nafasi ya uwajibikaji, haki za kidemokrasia na kuheshimu utawala wa sheria. Bw Sifuna aliwaambia wakazi kuwa maendeleo hayafai kutumiwa kuwanyima haki za kikatiba na uongozi wenye uwajibikaji. "Baba alituambia tuweke demokrasia, uhuru na kuheshimu utawala wa sheria mbele ya kila kitu, lakini baadhi ya watu wanataka kuwahadaa kwamba maendeleo yanatosha hata kama maana yake ni kumuua Albert Ojwang," akasema, akirejelea mauaji ya mwalimu na mwanaharakati huyo kutoka Homa Bay. Alisema serikali inayoheshimu utawala wa sheria haipaswi kuwa na tatizo la kuleta maendeleo. "Kama Sifuna, kujenga barabara na viwanja si jambo gumu kwangu, lakini ninachowaahidi ni kwamba nitaheshimu utawala wa sheria, nitalinda haki zenu na sitawahi kuwaua watoto wenu," akaongeza. Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi pia alipinga hoja ya maendeleo, akisema eneo hilo halijastawi sana chini ya utawala wa sasa. Bw Omondi alidai serikali imewekeza Sh50 bilioni katika eneo hilo, kiasi ambacho alisema ni sawa na gharama ya mradi mmoja mkubwa katika Bonde la Ufa. Mbunge huyo pia aliishutumu serikali kwa kuchukua udhibiti wa kampuni za sukari katika eneo hilo, akitaja Miwani na Chemelil. Gavana Orengo naye aligeuza mkutano huo kuwa jukwaa la kueleza ni nani anayepaswa kubeba urithi wa kisiasa wa Bw Odinga. Alimshutumu Rais Ruto kwa kushindwa kushughulikia malalamishi ya muda mrefu ya Nyanza, yakiwemo mzozo wa Migingo, na kukosoa namna serikali ilivyoshughulikia maandamano na madai ya mauaji yaliyotekelezwa na polisi. Kauli iliyovutia zaidi ilitolewa alipokuwa akijitaja kama mrithi wa kisiasa wa Bw Odinga. "Hapa ndipo roho ya Raila ilipo, haikufa pamoja naye. Uongozi unachukuliwa, haupeanwi, na ndiyo maana mimi ndiye Raila aliyesalia," akasema Bw Orengo. Alitangaza kuwa Linda Mwananchi itaadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha Bw Odinga Oktoba 15, ambapo itaitaka serikali kutoa majibu kuhusu kifo chake. Mkutano wa Homa Bay pia ulihudhuriwa na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya na Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi. Bw Owino alimtaja Bw Orengo kama kiongozi anayeweza kuwa daraja kati ya viongozi wa upinzani ambao wamekuwa wakishindwa kuungana. "Huyu ndiye mtu atakayewaleta viongozi hawa wote pamoja mezani na kuamua kuhusu kiongozi mmoja," akasema. Bw Natembeya na Bw Osotsi pia waliwahakikishia wafuasi kwamba miungano mipya ya upinzani haitavuruga uhusiano wa kihistoria kati ya jamii za Luo na Luhya. Bw Natembeya alisema upinzani unahitaji kuunganisha zaidi uungwaji mkono wake Magharibi na Nyanza kuelekea uchaguzi wa 2027. RIPOTI ZA GEORGE ODIWUOR, DOMNIC OMBOK na RUSHDIE OUDIA
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 16 Aug 2026 21:02:03
1 dead in Hawaii as Lala, now a tropical storm, moves west
One person is dead and tens of thousands have lost power after Hurricane Lala lashed parts of Hawaii overnight, before weakening slightly Sunday morning to a tropical storm with 70 mph sustained winds and heavy rain. At least 126,000 customers are without power across the islands. Nearly 70% of the Big Island is without power. [...] The post 1 dead in Hawaii as Lala, now a tropical storm, moves west appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content