kahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 17 Aug 2026 07:05:48
Kang'ata condemns violence against Linda Mwananchi in Homa Bay, demands action
Murang'a Governor Irungu Kang'ata Monday condemned violence reported during a Linda Mwananchi mobilisation in Homa Bay, accusing authorities of allowing political goons to attack citizens exercising their constitutional rights. Kang'ata said the reported violence amounted to a violation of the rights to peaceful assembly and personal security, warning the government against reverting to tactics associated [...] The post Kang'ata condemns violence against Linda Mwananchi in Homa Bay, demands action appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 17 Aug 2026 06:55:19
Kitany arai viongozi Bondeni wachape kazi hata wakiimba TuTam
MBUNGE wa Aldai, Marianne Kitany amewataka viongozi wa UDA Bonde la Ufa kukosa kulumbana huku akisisitiza yupo tayari kumenyana na mgombeaji yeyote anayesaka ubunge. Bi Keitany amesema kuwa rekodi yake ya maendeleo iko wazi na kwamba yupo tayari kumenyana na kiongozi yeyote lakini akasisitiza ubabe unaoendelea bondeni utatatiza kuchaguliwa kwa Rais William Ruto. "Siasa haihusu tena kulumbana na kutusiana, inahusu kazi ambayo umefanya. Mimi naamini kwamba nitachaguliwa tena Aldai kwa sababu ya kazi ambayo nimefanya na inaonekana," akasema Bi Kitany. Mbunge huyo alisema yupo tayari kuwania mchujo wa UDA na mgombeaji yeyote ambaye anamezea mate kiti chake kupitia chama hicho. "Saa hii wapinzani wangu wametoroka wote. Gavana wa sasa na mbunge wa zamani walikuwa wamesema watanipinga lakini sasa wamehepa hawana nia ya kuwania kiti hiki tena," akasema Bi Kitany. "Mimi niko UDA na siendi mahali popote na iwapo wanata kurudi kuwania basi niko tayari kupambana nao. Nikishindwa kwenye mchujo, sitaenda mahali popote, nitasalia tu UDA," akaongeza. Bi Keitany aliorodheshwa na TIFA kama mbunge ambaye ana utendakazi bora zaidi kati ya wabunge wanawake baada ya Naisula Lesuda wa Samburu Magharibi. Bw Sang' wiki jana alitangaza kuwa amejiondoa katika kiny'anganyiro cha ubunge baada ya kushauriana na Rais William Ruto na akimaliza muhula wake wa pili kama gavana, atakwea ngazi na kushiriki siasa za kitaifa. Mbunge huyo anayehudumu muhula wa kwanza alimkashifu Bw Sang' akisema utendakazi wake ni duni na hata iwapo angewania kiti hicho, hangeenda mahala popote. "Hospitali kadhaa hazifanyi kazi, hatuna mochari ya umma inayofanya kazi. Gavana mwenyewe ana shule za chekechea ambazo bado zimejengwa kwa udongo na hata bado tunayachota maji mtoni," akasema. "Mengi ambayo yametimizwa yanatokana na miradi ambayo imeanzishwa na serikali kuu. Hata sasa tunakuza miwa na kuwasilisha kiwanda cha Kibos," akasema. Gavana Sang' alisema kuwa hana nia ya kuwania kiti hicho cha ubunge na atamakinikia siasa za kitaifa. "Nina hiari kuwania cheo cha kisiasa na nilikuwa niwanie useneta au niwanie ubunge Aldai. Hiari hizi ni muhimu lakini baada ya kushauriana na Rais aliniambia nimakinikie kuchaguliwa kwake 2027. Kwa hivyo, nitakuwa nashiriki siasa za kitaifa wala sitagombea cheo chochote cha kisiasa," akasema Bw Sang'. Mwaka jana, Bw Sang alitangaza kuwa ifikiapo 2027 atakuwa na umri wa miaka 42 ambayo ni ya chini zaidi kwa mwanasiasa kustaafu. Hii ndiyo maana sasa alikuwa akilenga kiti cha ubunge wa Aldai. Bi Kitany alitaja kuwekwa lami kwa baadhi ya barabara, kuimarisha taasisi za elimu na kujengwa kwa masoko ya kisasa ambayo yamesaidia kuimarisha biashara katika eneobunge hilo.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 17 Aug 2026 05:48:53
School night watchman found dead in store in Machakos
Police are investigating an incident where a 30-year-old school night watchman was found dead inside a store at Kivingoni Secondary School in Matuu, Machakos County. The deceased, identified as Jackson Kioko Nyamai, was reportedly on duty alongside a fellow watchman when he went into the store to rest. According to police, the body was discovered [...] The post School night watchman found dead in store in Machakos appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 17 Aug 2026 05:53:18
Man dies after fight at Kisumu motel
A 26-year-old man died after he was allegedly stabbed during a fight at a motel in Kombedu, Kisumu West Sub-County. Police said the incident occurred at Chadwicks Motel at about 10pm on Sunday, August 16, 2026, following a disagreement between the deceased, identified as Shawn Omondi Otiendo, and a 36-year-old man. The two men got [...] The post Man dies after fight at Kisumu motel appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 17 Aug 2026 05:56:02
US commander says mental health a 'priority' on USS Lincoln
The top US military commander in the Middle East has said mental health is a priority on the warship USS Lincoln, following reports of difficult conditions on board the long-deployed ship. After visiting the vessel on Saturday, Adm Brad Cooper said it had among the lowest number of cases related to mental health out of [...] The post US commander says mental health a priority on USS Lincoln appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 17 Aug 2026 05:55:49
Kagwe asema nchi haitalemewa na njaa licha ya mabadiliko ya tabianchi
SERIKALI inapanga mikakati ya kuwasaidia wakulima kukabiliana na athari za ukame huku kipindi kirefu cha kukosekana kwa mvua kikitishia uzalishaji wa mahindi katika baadhi ya maeneo nchini. Waziri wa Kilimo, Mutahi Kagwe alisema serikali itawasaidia wakulima walioathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa na kuweka mikakati ya kuhakikisha usalama wa chakula nchini. Bw Kagwe alisema hayo baada ya kutembelea na kutathmini hali ya kilimo katika kaunti za Eldoret, Nandi na Trans Nzoia, ambako alitambua athari za ukame kwa uzalishaji wa mahindi. Aliwahakikishia Wakenya kuwa nchi haitakabiliwa na uhaba wa chakula licha ya changamoto zinazowakumba wakulima. "Hatutaruhusu Wakenya kuteseka na kulemewa na njaa kutokana na hali ya hewa iliyopo sasa," akasema. Waziri huyo pia alionya dhidi ya biashara ya mbegu bandia akisema inazorotesha uzalishaji wa kilimo na kusababisha wakulima kupata hasara. Alisema baadhi ya wakulima hugundua kuwa walinunua mbegu bandia miezi mitano hadi sita baada ya kupanda, wakati mimea yao inaposhindwa kustawi. Aliagiza vyombo vya usalama kuongeza juhudi za kukabiliana na wafanyabiashara wa mbegu hizo na akawataka wabunge kuunga mkono sheria itakayofanya uuzaji wa mbegu bandia kuwa uhalifu wa kiuchumi. Wakulima walishauriwa kununua mbegu zilizoidhinishwa kutoka taasisi zinazotambulika kama Kampuni ya Mbegu (KSC) na Kampuni inayohusika na Utafiti kuhusu Mbegu za Kisasa (KALRO). Mkurugenzi Mkuu wa KSC Sammy Chepsiror alisema kuna akiba ya kutosha ya mbegu nchini. Alisema mavuno ya mahindi mwaka jana yalifikia karibu magunia milioni 70 ya kilo 90.
read moreRight Column Content