taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Fri, 14 Aug 2026 04:25:17
Gachagua awekea mtego wanaohama UDA wakitaka kujiunga na DCP
WANASIASA waliochaguliwa katika eneo la Mlima Kenya wanaoanza kujitenga na Chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Rais William Ruto na kujiunga na Democracy for Citizens Party (DCP) wanakabiliwa na mtihani mpya wa kisiasa. DCP, chini ya aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua, kimeweka wazi kuwa kujiunga na chama hicho hakumaanishi mwanasiasa atapewa tiketi moja kwa moja kugombea katika Uchaguzi Mkuu wa 2027. Onyo hilo linajiri baada ya ushindi wa DCP katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa Ol Kalou mnamo Julai 16, ambapo mgombea wa chama hicho Kamau Ngotho alimshinda Muchina Nyaga wa UDA kwa zaidi ya kura 30,000. Ushindi huo umechochea kuhama kwa baadhi ya wanasiasa kutoka UDA na vyama vingine, huku Jubilee na The Service Party cha Mbunge wa Laikipia East Mwangi Kiunjuri pia vikikumbwa na misukosuko hiyo ya kisiasa. Hata hivyo, Kaimu Katibu Mkuu wa DCP John Methu amesema chama hicho kitakuwa makini katika kuwapokea wanasiasa wanaotafuta hifadhi ya kisiasa ndani yake. "Ikiwa ulipigia UDA kampeni Ol Kalou na ulikuwepo katika eneo bunge hilo siku ya kupiga kura, tafadhali usijaribu hata kukaribia DCP," alisema Bw Methu. Pia aliwaonya viongozi ambao walinyamaza wakati wakazi wa Mlima Kenya walidaiwa kutukanwa katika mikutano ya kisiasa. "Ikiwa ulihudhuria mikutano ambako watu wa Mlima Kenya walidhalilishwa na kutukanwa na hukupaza sauti kupinga, jichukulie kuwa hutakiwi DCP," alisema. Bw Methu alisema wale waliounga mkono kuondolewa kwa Bw Gachagua katika wadhifa wa Naibu Rais mnamo 2024 hawataadhibiwa moja kwa moja, akisema kiongozi huyo amewasamehe. Hata hivyo, aliongeza kuwa baadhi ya wanasiasa wanaotaka kujiunga na DCP watalazimika kupigania tiketi za chama hicho kupitia kura za mchujo badala ya kupewa tiketi moja kwa moja. Kwa sasa, Gavana wa Nyandarua Kiarie Badilisha ndiye kiongozi mashuhuri zaidi aliyepokelewa rasmi na DCP. Gavana wa Murang'a Irungu Kang'ata pia ameonyesha anaelekea DCP, ingawa wakati huo huo anajihusisha na kundi la Linda Mwananchi linaloongozwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna. Mchanganuzi wa siasa Malila Munywoki, hata hivyo, amewatahadharisha wanasiasa wanaohama UDA dhidi ya kudhani kuwa DCP itawapa usalama wa kisiasa. "Nchini Kenya, vyama vya kisiasa vinamilikiwa na watu na kujiunga navyo si haki bali ni fursa unayopewa," alisema. Alisema DCP ilianzishwa kwa msingi wa upinzani dhidi ya Bw Ruto na kwamba, wafuasi wake huenda wasikubali kwa urahisi viongozi wanaohusishwa na utawala wa Kenya Kwanza. Seneta wa Murang'a Joe Nyutu alithibitisha kuwa baadhi ya maafisa wakuu serikalini kutoka Mlima Kenya, Nairobi na Bonde la Ufa wameonyesha nia ya kujiunga na DCP. "Tusubiri kiongozi wa chama chetu atangaze majina makubwa kwa wakati wake," alisema. Bw Kiunjuri, hata hivyo, alikanusha madai kwamba maafisa wakuu serikalini wanajiandaa kuhamia DCP, akimtaja Bw Gachagua kama mwanasiasa mwenye ujuzi mkubwa wa propaganda. Bw Gachagua ameendelea kusisitiza kuwa juhudi zake za kuunganisha Mlima Kenya dhidi ya Bw Ruto zinaendelea vizuri. Alisema baadhi ya maafisa wakuu serikalini wanabaki humo kwa sababu za riziki huku kwa siri wakiunga mkono mipango yake ya kisiasa kuelekea 2027. "Tumekubaliana wabaki serikalini kwa sababu ya kujitafutia unga. Lakini wataendelea kutusaidia kutekeleza ajenda yetu ya 2027," alisema. Alisema upinzani hatimaye utakubaliana kuhusu mgombea mmoja wa urais wa kukabiliana na Bw Ruto.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Fri, 14 Aug 2026 04:55:02
Mrengo mpya sasa waibuka Mlimani kumuunga mkono Ruto
HUKU vita vya kisiasa kudhibiti kura za eneo la Mlima Kenya vikizidi kushika kasi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027, mrengo wa tatu wa kisiasa unaohusishwa na Rais William Ruto umeibuka. Mbunge wa Ndia George Kariuki, mshirika wa karibu wa Rais Ruto, ameanzisha kile anachokiita "vikao vya mashauriano" nyumbani kwake Gacharu. Baada ya Rigathi Gachagua kung'olewa kutoka wadhifa wa Naibu Rais mnamo Oktoba 2024, alianza kampeni kali dhidi ya aliyekuwa bosi wake, akimlaumu kwa usaliti wa kisiasa. Kupitia chama chake cha Democracy for Citizens Party (DCP), Bw Gachagua amekuwa akiendesha mikutano na kampeni katika kaunti mbalimbali za Mlima Kenya, hali ambayo karibu imefungia nje chama cha United Democratic Alliance (UDA). Ushindi wa DCP katika uchaguzi mdogo wa ubunge wa Ol-Kalou, ambapo mgombea wake Kamau Ngotho alimshinda Muchina Nyaga wa UDA kwa zaidi ya kura 30,000, umempa nguvu zaidi Bw Gachagua, ambaye anadai ushindi huo ulikuwa kura ya kuamua kukataa Rais Ruto. Mwezi Julai, Bw Gachagua alitangaza kujifungia kwa siku 45 katika makazi yake ya Wamunyoro, ambako amekuwa akipokea jumbe na viongozi kutoka maeneo mbalimbali ya Mlima Kenya, Nairobi na Bonde la Ufa. Hali hiyo imefanya Wamunyoro kuwa kitovu kikuu cha maamuzi ya kisiasa. Kwa upande mwingine, Naibu Rais Kithure Kindiki pia amekuwa akitumia nyumbani kwake Irunduni kupokea viongozi kutoka eneo hilo kwa lengo la kupunguza ushawishi wa Bw Gachagua na kuimarisha uungwaji mkono wake. Bw Kariuki amesema kwa siku 90 zijazo ataalika wakazi wa Mlima Kenya pamoja na maeneo mengine ya nchi kujadili mustakabali wa kisiasa wa eneo hilo kabla ya kutoa tamko ambalo ameliita "Azimio la Gacharu." Kauli zake alipokutana na viongozi wa wanawake kutoka eneo la Othaya Jumatatu zilitoa dalili za hatua zake za baadaye. Wachambuzi wa siasa wanaamini kuwa mbunge huyo anaandaliwa kuwa kiongozi wa kisiasa katika Mlima Kenya Magharibi na huenda akazingatiwa kama mgombea mwenza wa Rais Ruto mwaka wa 2027. "Mwaka ujao nitakuwa nimetumikia wananchi wa Ndia kwa miaka kumi. Je, sifai kushikilia wadhifa mkubwa zaidi? Siwezi kushiriki siasa za kitaifa?" alihoji Bw Kariuki. Aliwasihi wananchi kutochagua viongozi kwa misingi ya vyama vya kisiasa pekee bali kwa uwezo na kujitolea kwao kuhudumia wananchi. Pia kuna madai kuwa anapigiwa upatu kuchukua nafasi ya mgombea mwenza wa Rais iwapo itaonekana ana uwezo mkubwa zaidi wa kuunganisha kura za Mlima Kenya kuliko Profesa Kindiki. Alipoulizwa iwapo analenga wadhifa wa juu zaidi wa kisiasa, Bw Kariuki alikataa kuthibitisha azma yoyote ya kuwa Naibu Rais, akisema atatangaza msimamo wake baada ya kukamilisha mashauriano hayo. Katika siku za hivi majuzi amekuwa akiongea kwa sauti kuhusu uongozi wa eneo hilo akisisitiza kuwa "Mlima Kenya unahitaji viongozi imara", kauli ambayo wengi wametafsiri kuwa kukosoa Prof Kindiki ambaye bado hajafanikiwa kupunguza ushawishi wa Bw Gachagua. Wakati huo huo, baadhi ya viongozi kutoka Mlima Kenya Mashariki, wakiongozwa na Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku, wamekuwa wakishinikiza eneo hilo lichukue mkondo wake wa kisiasa tofauti na Mlima Kenya Magharibi. Prof Kindiki amejipata katika hali ngumu kutokana na msimamo huo, huku akiendelea kutetea umoja wa eneo lote la Mlima Kenya. Mlima Kenya Mashariki unajumuisha kaunti za Embu, Meru na Tharaka Nithi ambako Prof Kindiki anatoka, huku Kirinyaga, Nyeri, Murang'a, Nyandarua na sehemu za Laikipia zikihesabiwa kuwa Mlima Kenya Magharibi. Bw Ruku anasema upinzani mkubwa dhidi ya Rais Ruto unatoka Mlima Kenya Magharibi na ameshutumu eneo hilo kwa kile anachokiita usaliti wa kisiasa. Jumanne, Bw Ruku aliambia Taifa Leo kuwa yeye na Mbunge Kariuki wana mpango mkubwa wa kumsaidia Rais Ruto kupata takriban kura milioni tatu katika eneo la Mlima Kenya.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Fri, 14 Aug 2026 03:55:55
Mkenya apokea Sh103m Amerika kukuza 'managu'
ARI ya Dkt Truphena Choti, Mkenya anayeishi Amerika, ya kulima mboga za kienyeji za Kiafrika imepigwa jeki baada ya mradi wake kupata ufadhili wa Sh103 milioni. Fedha hizo zitatumika kukuza biashara yake ya kulima na kusambaza mboga kama kunde, managu, terere, mchicha na mrenda kwa watumiaji nchini Amerika, wengi wao wakiwa Waafrika wanaoishi ughaibuni. Seneta wa Maryland Chris Van Hollen alimkabidhi Dkt Choti hundi hiyo rasmi Jumatatu, ishara ya kuungwa mkono kwa mradi wake unaolenga kuboresha lishe na upatikanaji wa chakula salama. Dkt Choti, ambaye ana taaluma ya sheria, alianza kupenda maisha yenye afya na lishe bora kupitia shughuli za kijamii. Bustani yake ya jamii ilianza kwa kulima vyakula alivyozoea nchini Kenya, ikiwemo viazi vitamu na Sukuma wiki. Mradi huo, unaojulikana kama AfriThrive Community Food Center, ulianza baada ya Waafrika wengi kuonyesha kuvutiwa na bustani yake. Kwa sasa unahudumia takriban watu 20,000 kila mwaka. Dkt Choti alisema malezi yake nchini Kenya, hasa Kisii, yalichangia pakubwa kuibua shauku ya kulima vyakula alivyokua akila. "Kwetu, utoshelevu wa chakula si kuwapa watu kitu cha kula pekee. Tunataka familia zipate vyakula wanavyojua, wanavyofurahia na vinavyowakumbusha nyumbani," alisema. Alisema alipohamia Amerika alikosa mboga alizokua akila Kenya, hasa managu na saga. "Nilipata kipande kidogo cha ardhi karibu na nyumbani kwangu, ndipo upande wa Kisii ndani yangu ukajiuliza, 'Kwa nini usilime saga yako mwenyewe?' Nilifanya hivyo," alisema. Dkt Choti ana uzoefu wa karibu miongo miwili katika maendeleo ya kimataifa. Anasema uzoefu huo ulimsaidia kuona kilimo cha mboga hizo kama zaidi ya kutafuta ladha ya nyumbani. "Bustani nilipanda mbegu, lakini uzoefu wangu wa maendeleo ulinisaidia kuona picha kubwa. Bustani hiyo ndogo hatimaye ikawa AfriThrive," alisema. Ufadhili huo utatumika kwanza kukarabati na kuendeleza kituo cha AfriThrive huko Essex. Kituo hicho kitawekwa vifaa vya kuhifadhi chakula kwa baridi, maeneo ya kuandaa chakula na vifaa vingine vya kuhifadhi na kusambaza chakula salama. Dkt Choti anasema hatua hiyo itawezesha mradi kutoa huduma mwaka mzima. Kwa malengo ya muda mrefu, anataka mradi huo kusaidia jamii kuelewa umuhimu wa lishe bora na kuzuia magonjwa yanayohusishwa na lishe duni. Anasema elimu ya lishe pekee haitoshi ikiwa vyakula bora havipatikani au wengi hawamudu gharama yake. "Watu wanahitaji maarifa na chakula mezani," alisema. Kwa Dkt Choti, mboga za kienyeji pia ni alama ya utamaduni. "Nilikulia maeneo ya mashambani Kisii, Kenya, ambako tulilima vyakula vingi tulivyokula. Kilimo kimekuwa sehemu ya maisha yangu," alisema. Leo, anaongoza AfriThrive kama mkurugenzi mkuu, lakini Jumapili bado ni siku yake ya shamba. Akiangalia zaidi ya ekari tano zilizo chini ya kilimo cha managu na saga, anasema anakumbushwa utoto wake, familia na mila. "Haijalishi niko mbali kiasi gani kutoka Kisii, udongo bado hunirudisha nyumbani," alisema. Dkt Choti anasema lengo lake ni kuona AfriThrive ikiwa zaidi ya kituo cha kusambaza chakula. Anataka kuanzisha mipango inayohusisha chakula kama tiba, elimu ya lishe, kusaidia wakulima wa eneo hilo, vijana na familia, huku akiimarisha uhusiano kati ya chakula na afya. Kilichoanza na mama mmoja aliyetafuta saga, sasa kimekua kuwa mradi unaolenga kuwafikia maelfu ya familia. "Tunajenga mahali ambapo maelfu ya familia zinaweza kupata chakula bora, heshima na ladha kidogo ya nyumbani," alisema.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 14 Aug 2026 03:15:15
Conditions on US aircraft carrier at sea for more than 250 days raise alarms
Thousands of US military members who have lived aboard an aircraft carrier for more than 250 days are reportedly contending with food shortages, broken plumbing and exhaustion, leading lawmakers to demand answers from the Pentagon and pressuring the Trump administration over the Iran war. Military news outlets reported that some USS Abraham Lincoln sailors have [...] The post Conditions on US aircraft carrier at sea for more than 250 days raise alarms appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 14 Aug 2026 03:18:39
Done in a weekend – the $12.5bn LA Lakers sale that shocked the NBA
It was a move that has left the NBA world in shock. And the deal was done astonishing quickly. The Los Angeles Lakers record $12.5bn (£9.3bn) sale was agreed in the space of a weekend. News broke on Wednesday that Josh Kushner, the brother of US President Donald Trumps son-in-law Jared, and former Disney chief [...] The post Done in a weekend the $12.5bn LA Lakers sale that shocked the NBA appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 14 Aug 2026 03:22:01
Who could replace Karoline Leavitt as White House press secretary?
It's become Washington's hottest new parlor game: Who will be Karoline Leavitt's successor? Names started circulating at dinner tables and over text chains after President Donald Trump announced on Wednesday his press secretary's plans to depart at the end of the month to spend more time with her young family, upending his press operation with [...] The post Who could replace Karoline Leavitt as White House press secretary? appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 14 Aug 2026 03:26:03
Palestinians told to leave homes in village where Israeli settlers besieged houses
About a dozen Palestinian households in a village in the occupied West Bank were told to leave their properties during an Israeli military operation to remove Israeli settlers. The settlers had besieged residents in three homes in the area since Sunday, cutting off their power and water supplies. Qusra Mayor, Abdel Azim Wadi, told the [...] The post Palestinians told to leave homes in village where Israeli settlers besieged houses appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Fri, 14 Aug 2026 02:55:33
Maoni mseto yazuka kuhusu Ruwaza 2060 wengi wakihoji utekelezaji wa ile ya 2030
HATUA ya Rais William Ruto kuanzisha mpango mpya wa maendeleo ya muda mrefu imeibua mjadala mkali wa kisiasa huku wakosoaji wakihoji kwa nini Kenya inapanga hadi mwaka 2060 kabla ya kutoa tathmini kamili ya yaliyofanyika chini ya Ruwaza ya 2030. Mzozo huo umeibuka baada ya kuzinduliwa kwa Mazungumzo ya Kitaifa kuhusu Mustakabali wa Kenya baada ya Ruwaza ya 2030, yanayolenga kuwashirikisha Wakenya katika kuamua vipaumbele vya maendeleo baada ya mpango huo wa sasa kufikia mwisho wake. Viongozi wa Kenya Kwanza wanatetea mpango huo wakisema unalenga kuhakikisha maendeleo ya nchi hayaongozwi na vipindi vya uchaguzi bali mipango ya muda mrefu inayoweza kuendelezwa na serikali zinazofuata. Hata hivyo, wapinzani wanasema Serikali inapaswa kwanza kuwaeleza Wakenya kilichofanikiwa, kilichoshindikana na kilichosalia chini ya Ruwaza 2030. Naibu mwenyekiti wa Wiper Patriotic Front na Gavana wa Makueni Mutula Kilonzo Junior, alihoji muda wa kuanzishwa kwa mpango huo akisema mamilioni ya Wakenya wanakabiliwa na matatizo ya kiuchumi ya kila siku. "Hatutaki mpango wa 2060. Wakenya wengi hawajui watakula nini kesho, na vijana wengi wamepoteza matumaini. Hatuwezi kuwa tunazungumzia Ruwaza ya 2060 katika hali kama hii," alisema Bw Kilonzo. Mbunge wa Tetu, Bw Geoffrey Wandeto, alisema Serikali lazima kwanza ikabiliane na ufisadi ambao unaweza kuharibu mpango wowote wa maendeleo. "Tusiposhughulikia hatari kuu, yaani ufisadi, utakula Ruwaza ya 2030, Ruwaza ya 2060 na Ruwaza ya 2100 kama kiamsha kinywa," alisema Bw Wandeto. Mbunge huyo pia alihoji iwapo Serikali imefanya tathmini ya kina ya Ruwaza ya 2030 ili kubaini yaliyofanikiwa na yaliyoshindikana. "Bado sijaona tathmini yoyote kubwa ya Ruwaza ya 2030. Nini kilifanyika vizuri? Nini kilikwenda vibaya? Nini kinaweza kuboreshwa? Tunaweza kuokoa nini?" aliuliza. Mwanasheria Harrison Kinyanjui, pia ameibua maswali kuhusu kwa nini mpango huo umepewa jina la Ruwaza ya 2060 badala ya Ruwaza ya 2050. Amedai huenda muda huo ukawa umechaguliwa kwa kuzingatia ajenda ya maendeleo ya Muungano wa Afrika ya mwaka 2063. Pia ameibua hofu kwamba mpango huo unaweza kutumiwa baadaye kufungua njia ya kubadilisha Katiba, ingawa hakutoa ushahidi wa kuonyesha kuwa Serikali ina mpango huo. Katibu Mkuu wa Shirikisho la Watumiaji Kenya (Cofek), Bw Stephen Mutoro, alionya dhidi ya jaribio lolote la kutumia mpango wa maendeleo kama sababu ya kubadilisha Katiba. "Wanaofikiria wanaweza kubadilisha Katiba na kuweka 'ruwaza ya lazima' wanaota ndoto za mchana," alisema Bw Mutoro. Upinzani pia umepinga wazo la kuanzisha ahadi nyingine kubwa ya maendeleo ilhali Ruwaza ya 2030 bado haijakamilika. Msemaji wa Wiper Patriotic Front, Bw Ndegwa Njiru, alisema Kenya inahitaji kwanza tathmini ya kweli ya mafanikio na kushindwa kwa Ruwaza ya 2030. "Kenya haihitaji ahadi nyingine kubwa wakati ahadi zilizotolewa kwa wananchi bado hazijatimizwa kwa kiwango kikubwa," alisema Bw Njiru. Hata hivyo, viongozi wa Kenya Kwanza wamepuuza ukosoaji huo wakisema mipango ya taifa haipaswi kuongozwa na kalenda ya uchaguzi. Seneta wa Nandi, Bw Samson Cherargei, alisema Ruwaza ya 2030 yenyewe iliandaliwa kupitia ushirikishaji wa wananchi. "Katika chama chetu, tunaangalia vizazi vitakavyokuja kesho, wala hatufikirii siasa za mwaka ujao," alisema Seneta Cherargei. Mbunge wa Aldai, Bi Marianne Kitany, pia alitetea muda wa kuanzishwa kwa mpango huo akisema kazi ya Ruwaza ya 2030 ilianza wakati wa utawala wa Rais mstaafu Mwai Kibaki. Wakati huohuo, wabunge wanaomuunga mkono aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua wameanzisha mashambulizi mapya dhidi ya Serikali ya Rais Ruto. Seneta wa Nyandarua, Bw John Methu alisema Wakenya wameonyesha kutoridhishwa na utendaji wa Serikali katika kipindi cha miaka minne. Alitaja gharama ya maisha, kodi, ukosefu wa ajira na deni la taifa kuwa miongoni mwa masuala yanayowasumbua Wakenya.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Fri, 14 Aug 2026 03:00:00
Crumbling: Leaders flee Ruto party as 2027 political storm gathers
The political class has embarked on a self-preservation journey to save themselves from the raging political waves that sweep away anyone who is not politically correct.
read moreRight Column Content