kahawatungu.com
@kahawatungu Wed, 12 Aug 2026 21:44:57
Thousands of Canadians call for US ambassador's expulsion
More than 60,000 Canadians have signed a petition calling for the US ambassador in Ottawa to be expelled for undermining diplomatic relations between the two neighbours. The online petition accuses Pete Hoekstra of making repeated interventions in Canadian political discourse and of having normalised the Trump administrations threats to annex Canada as the 51st state' [...] The post Thousands of Canadians call for US ambassadors expulsion appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Wed, 12 Aug 2026 21:46:43
Messi unsure he will play 'much longer' after father's death
Lionel Messi said he is unsure how much longer he will continue playing football as he posted an emotional tribute after his fathers death. Messis father Jorge was 68 when he died last week following a long illness. Jorge had been the Argentina forwards agent since he was 14 and watched him become one of [...] The post Messi unsure he will play much longer after fathers death appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 12 Aug 2026 07:30:59
Wanafunzi kupata mafunzo kuhusu usafi
WANAFUNZI 2,400 kutoka eneo la Bisil, Kaunti ya Kajiado, watanufaika na vifaa vya usafi na elimu kuhusu afya kupitia mpango mpya unaolenga kuboresha usafi shuleni. Mpango huo, unaojulikana kama Clean Futures Alliance, umeanzishwa na Federal Express Corporation (FedEx) kwa ushirikiano na Feed the Children, huku ukilenga kuwasaidia watoto na vijana kujenga uzoefu wa kudumisha usafi kwa lengo la kuwalinda dhidi ya magonjwa. Kupitia mpango huo, wanafunzi wa shule za msingi watapokea vifaa vya usafi binafsi na kushiriki katika mafunzo yanayowafundisha umuhimu wa kunawa mikono, kudumisha usafi wa mwili na kuzingatia mazingira safi. Shughuli za kwanza za elimu kuhusu maji, usafi na usafi wa mazingira (WASH) zilifanyika katika Shule za Msingi za Inkati na Noontoto, Bisil. Kwa watoto wanaotumia muda mwingi shuleni, usafi ni sehemu muhimu ya maisha yao ya kila siku. Ukosefu wa vifaa au maarifa kuhusu usafi unaweza kuwaweka katika hatari ya kupata magonjwa na pia kuathiri masomo yao. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo, Mkurugenzi Mkuu wa Operesheni za FedEx katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Nelson Teixeira, alisema kampuni hiyo inalenga Kumari Sha usafi katika jamii. "Tunataka kusaidia watoto na familia kujenga maisha yenye afya na kuleta mabadiliko katika jamii tunamoishi na kufanya kazi," alisema. Kwa upande wake, Rais na Afisa Mkuu Mtendaji wa Feed the Children, Emily Callahan, alisema usafi huwasaidia watoto kuwa na afya bora, kujiamini na kuendelea kushiriki katika masomo. Ushirikiano huo unatekelezwa kupitia mpango wa FedEx Cares, ambao huwahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo katika shughuli za kujitolea na miradi inayolenga kushughulikia mahitaji ya jamii. Mbali na kutoa vifaa, wafanyakazi wa FedEx walishiriki katika kuandaa na kusambaza vifaa vya usafi kwa wanafunzi. Mpango huo unatarajiwa kuendeleza ushirikiano wa muda mrefu kati ya FedEx na Feed the Children katika kusaidia jamii kupata mahitaji muhimu na kujenga mazingira bora kwa watoto kukua na kusoma.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 12 Aug 2026 17:39:32
Wagonjwa waendelea kuteseka mgomo wa wauguzi ukikosa suluhu mpaka sasa
WAGONJWA kote nchini wanaendelea kuteseka huku mgomo wa wahudumu wa afya ukiendelea bila suluhu, hali ambayo imelemaza utoaji huduma katika hospitali nyingi za umma. Baraza la Magavana (CoG) linasisitiza kuwa wahudumu hao wanapaswa kurejea kazini kwa kuwa mchakato wa kushughulikia malalamishi yao tayari umeanza. Hata hivyo, viongozi wa vyama vya wafanyakazi wa sekta ya afya wanashikilia kuwa mgomo huo hautasitishwa hadi matakwa yao yote yatimizwe kikamilifu. Akizungumza katika mdahalo wa vyombo vya habari Jumanne, Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Magavana Mary Mwiti alisema mzozo huo unatarajiwa kutatuliwa kabla ya mwisho wa wiki. "Ni sehemu tu ya wahudumu wa afya walio katika mgomo. Tukilinganisha hali ilivyo sasa na kabla ya ugatuzi, tuko katika nafasi bora zaidi," alisema. Aliongeza kuwa migogoro ya wafanyakazi wa afya imepungua kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka saba iliyopita. Ingawa Bi Mwiti alisema ni makundi mawili pekee ya wahudumu yaliyo katika mgomo, imebainika kuwa makundi mengine kadhaa pia yamesusia kazi, yakiwemo maafisa wa afya ya umma, wauguzi, maafisa wa utabibu, wafamasia na maafisa wa maabara. Kuhusu maafisa wa utabibu, alisema Baraza la Magavana tayari limekubaliana kuhusu Mkataba wa Pamoja (CBA) na kuutia saini. Pia alisema mfumo wa kurejea kazini umekamilishwa, lakini utekelezaji wake unahitaji kufuata taratibu fulani. Alifafanua kwamba baada ya CBA na makubaliano ya kurejea kazini kutiwa saini, Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC) lazima ithibitishe mishahara na marupurupu mapya ili viwango viwe sawa katika makundi mbalimbali ya watumishi. Bi Mwiti alisema magavana walikutana Alhamisi iliyopita kujadili masuala yanayowahusu wauguzi na kukubaliana kuhusu hatua mbalimbali za kuwawezesha kurejea kazini. Aliongeza kuwa kutakuwa na mkutano mwingine wa kukamilisha mazungumzo hayo. "Tunangoja kupokea barua rasmi na Baraza la Magavana liko tayari kushiriki mazungumzo ili kurejesha kikamilifu huduma kwa wananchi," alisema. Serikali pia inatarajiwa kufanya Mkutano Mkuu wa Kitaifa wa Afya wa siku mbili wiki ijayo ambapo suala la wahudumu katika sekta ya afya litajadiliwa. "Ninaamini kabla ya mwisho wa wiki tutakuwa tumekubaliana. Kufikia wakati wa mkutano huo, migomo yote itakuwa imekwisha," alisema. Hata hivyo, mwenyekiti wa chama cha maafisa wa utabibu Kenya Peterson Wachira alisema SRC tayari imetekeleza wajibu wake kwa kutoa mwongozo wa utekelezaji wa mishahara mipya. "Sasa tunasubiri Baraza la Magavana kufanya marekebisho ya mishahara katika mfumo wa malipo. Wanapaswa kuwasiliana na Wizara ya Utumishi wa Umma ili hatua hiyo ikamilike," alisema. Wachira alisema kumekuwa na maendeleo katika kutiwa saini kwa makubaliano ya kurejea kazini katika kaunti nyingi, lakini kaunti 18 bado hazijakamilisha mchakato huo. Kaunti hizo ni pamoja na Kisumu, Kakamega, Busia, Kajiado, Uasin Gishu, Nyandarua, Embu, Kiambu, Nyeri na Murang'a. "Natarajia kukamilisha hatua zote wiki ijayo. Kufikia sasa hakuna jambo la msingi lililotoka kwenye mikutano tuliyofanya. Tutakutana tena na Baraza la Magavana Alhamisi kujadili masuala yetu," alisema. Katibu Mkuu wa Muungano wa Wataalamu wa Afya ya Mazingira na Afya ya Umma Kenya (KEHPHPU), Brown Ashira, alisema hakuna hata takwa moja la wanachama wao ambalo limetekelezwa. "Magavana bado wanataka turejee kazini bila makubaliano yoyote," alisema. Aliongeza kuwa huduma muhimu kama chanjo zimeathirika huku kukiwa na ongezeko la magonjwa yanayosababishwa na chakula na maji yasiyo salama. Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Muungano wa Kitaifa wa Wauguzi Kenya Lucy Mburu, alisema bado hawajafikia muafaka katika mazungumzo yao na Baraza la Magavana. "Tumekutana na mpatanishi kutoka Wizara ya Kazi lakini bado hakuna makubaliano. Tutakuwa na mkutano mwingine wiki ijayo," alisema.
read morekenyanews.go.ke
@kna Wed, 12 Aug 2026 14:53:57
High transport costs drive potato prices higher in Murang'a
Residents of Murang'a County are feeling the pressure of rising food prices, with the cost of potatoes increasing significantly amid higher fuel and transportation costs. A spot check at Mukuyu Market in Murang'a town on Wednesday established that a kilogramme of potatoes is retailing at about Sh170, up from Sh100 two months ago. Vegetable traders...
read morekenyanews.go.ke
@kna Wed, 12 Aug 2026 14:55:11
Al Shifaa edge Azzam United, book place in Cup Final
Al Shifaa Media FC have booked their place in the Sisi Ni Dola Cup 2026 final after edging Azzam United 1-0 in the second semi-final played at Mombasa Sports Club. Swaleh Kenrod scored the decisive goal in the 44th minute to send Al Shifaa through to Friday's grand final, where they will face Green Eagles...
read morekenyanews.go.ke
@kna Wed, 12 Aug 2026 14:56:53
Kutus town set for major facelift with World Bank support
The Kirinyaga County Government has rolled out a Sh33 million modernization project to give Kutus town a major facelift and create a more conducive environment for businesses, residents and visitors. The project, funded through the World Bank-supported Kenya Urban Support Program (KUSP), will involve installation of 2,500 square metres of cabro paving, construction of pedestrian...
read morekenyanews.go.ke
@kna Wed, 12 Aug 2026 14:59:38
Machakos Assembly passes half of Sh17.7 billion budget amid finance row
The Machakos County Assembly has approved Sh8.9 billion, about 50% of the county's Sh17.7 billion budget, to cover essential services and salaries as a standoff between the Executive and the Assembly continues. The partial approval was necessitated by delays linked to a dispute over the Finance docket. County Assembly members impeached CECM for Finance Catherine...
read moreRight Column Content