kahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 15 Nov 2026 06:25:29
Man stabbed to death by robbers in Nyeri, wife injured
Police in Kieni East, Nyeri County, are investigating the killing of a 90-year-old man who was stabbed by two armed assailants who raided his homestead in Gatuamba Village. The deceased, identified as Edward Kamau Mukiha, was attacked on November 14, while basking in the sun outside his house. The deceased's 70-year-old wife told investigators that [...] The post Man stabbed to death by robbers in Nyeri, wife injured appeared first on Kahawatungu.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Sun, 15 Nov 2026 05:57:42
Relief for Kenyans as Govt Introduces New Rules for Saudi Arabia Jobs
The new rules affect recruitment costs and other expenses incurred by Kenyans during the process of securing visas and securing employment in the Middle Eastern country.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 15 Nov 2026 05:55:04
Washirika wa Ruto wapanga kumuokolea asilimia 40 ya kura Mlimani
Washirika wa Rais William Ruto katika eneo la Mlima Kenya wameanzisha mkakati mpya wa kisiasa unaolenga kumrejeshea angalau asilimia 40 ya kura za eneo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa 2027, licha ya kuongezeka kwa ushawishi wa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua. Mpango huo unaoitwa Diehard Movement unaongozwa na Mbunge wa Laikipia Mashariki Mwangi Kiunjuri na mwenzake wa Ndia, George Kariuki. Unalenga kujenga mtandao wa wafuasi wa Ruto katika ngazi za mashinani badala ya kutegemea mikutano mikubwa ya kisiasa. Kiunjuri alisema lengo lao ni kuthibitisha kuwa bado kuna wakazi wa Mlima Kenya wanaomuunga mkono Rais na walio tayari kufanya kampeni kuhakikisha anapata angalau asilimia 40 ya kura za eneo hilo. Alisema harakati hizo zitajikita katika kaunti za Meru, Tharaka Nithi, Embu, Nyeri, Murang'a, Kirinyaga, Nyandarua, Laikipia, Nakuru, Nairobi, Kiambu na Lamu. Mpango huo unajumuisha mikutano ya wananchi, mashindano ya kandanda kwa vijana na kuunda mitandao ya viongozi wa mashinani watakaohamasisha wapiga kura. Kariuki alisema washirika hao hawana muda wa kukaa kwenye mikutano ya ndani, bali wanataka kuzungumza moja kwa moja na wananchi na kuwaeleza kuhusu miradi ya maendeleo ya serikali, hasa barabara. Hata hivyo, alikiri kuwa bado hawajafikia kiwango wanachotaka, akisema serikali imekosa kiongozi mwenye ushawishi wa kuwaunganisha viongozi wa eneo hilo tangu Gachagua alipoondolewa mamlakani. Harakati hizo zinajitokeza huku Gachagua na rais mstaafu Uhuru Kenyatta wakionekana kuwa na ushawishi mkubwa miongoni mwa sehemu ya wakazi wa Mlima Kenya. Gachagua amekuwa akisema eneo hilo lilisalitiwa na Ruto na linapaswa kumwadhibu katika uchaguzi ujao. Gachagua alitumia ushindi wa chama chake cha DCP katika uchaguzi mdogo wa Ol Kalou kama ishara ya kile anachotarajia kufanikisha mwaka 2027, akisema ushindi huo wa asilimia 85 aliopata Ruto mwaka 2022 utakuwa mdogo ikilinganishwa na atakachomfanyia. Akijibu, Kiunjuri alisema Diehard haitategemea mikutano mikubwa pekee, bali kujenga mtandao wa watu wanaoweza kushawishi wapiga kura katika kila eneo. Alisema kila kaunti itakuwa na angalau watu 20 watakaoratibu shughuli za kisiasa, huku wale watakaoshindwa kutimiza malengo wakibadilishwa. Mchambuzi wa siasa John Okumu alisema Ruto hawezi kukaa kimya akitazama eneo hilo likigeuka dhidi yake. Alisema kupata asilimia 40 ya kura za Mlima Kenya kunaweza kuwa muhimu kwa ushindi kitaifa, kwani Rais hahitaji tena kupata ushindi mkubwa kama ule wa 2022, bali kubaki na uungwaji mkono wa kutosha. Mlezi wa baraza la wazee la Kiama Kia Ma, Kung'u Muigai, alisema hasira za kisiasa hazipaswi kuwa msingi wa maamuzi ya eneo hilo. Alionya kuwa kumuondoa Ruto bila kuwa na mbadala kunaweza kuwa hatari kwa mustakabali wa Mlima Kenya. Naye Naibu Spika wa Seneti Kathuri Murungi alisema washirika wa Ruto hawalengi kurejesha uungwaji mkono wa kila mtu, bali kupata kura za kutosha kumwezesha kushindana. Mbunge wa Maragua Mary Wamaua alisema mkakati huo unalenga kuunganisha wafuasi wa Ruto katika familia za kisiasa za eneo hilo. Kiunjuri alisema Mlima Kenya haupaswi kuingia uchaguzi wa 2027 ukiwa na lengo la kulipiza kisasi, bali unahitaji mazungumzo na mpango utakaohakikisha unaendelea kushiriki katika uongozi wa kitaifa. Hata hivyo, mafanikio ya Diehard yatategemea iwapo washirika wa Ruto wataweza kubadilisha mikakati yao kuwa kura halisi, katika eneo ambalo upinzani unaendelea kuimarisha ushawishi wake.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 15 Nov 2026 05:18:52
Judge temporarily blocks Trump from closing Washington DC golf course for renovation
A federal judge has temporarily blocked the US governments closure of a historic golf course and park in Washington DC. US District Judge Ana Reyes has been overseeing a months-long challenge to the presidents plans for East Potomac Golf Links, which he said would be closed from 15 November for extensive renovations. Reyes has said [...] The post Judge temporarily blocks Trump from closing Washington DC golf course for renovation appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 15 Nov 2026 05:26:06
Judo champion shakes up French presidential race with surprise candidacy
Apart from an overwhelming urge to pin ones opponent to the floor of the house, there is no obvious connection between politics and the world of top-level judo. That has not stopped Frances much-garlanded world heavyweight champion Teddy Riner from throwing his hat into the ring for next Aprils presidential race. The Guadeloupe-born 37-year-old may [...] The post Judo champion shakes up French presidential race with surprise candidacy appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 15 Nov 2026 05:28:28
Arrested generals and a threatened VP: President's son fuels Ugandan succession fever
In Ugandas military, even senior generals are finding that their rank offers little protection from the wrath of the countrys powerful army chief. Over the past 15 months, at least a dozen generals and senior officers have been arrested under Gen Muhoozi Kainerugaba, who is also the son of President Yoweri Museveni, in a crackdown [...] The post Arrested generals and a threatened VP: Presidents son fuels Ugandan succession fever appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 15 Nov 2026 04:55:09
Uchovu, mwendo wa kasi wahatarisha madereva katika barabara ya Mombasa-Malaba
Uchovu wa madereva, mwendo wa kasi na matumizi ya vileo na dawa za kulevya vinahatarisha maisha ya watumiaji wa barabara kuu ya Mombasa-Malaba, ambako zaidi ya maeneo 200 yametambuliwa kuwa hatari kwa ajali. Wadau wa sekta ya uchukuzi wanasema kuongezeka kwa malori yanayosafirisha bidhaa katika barabara hiyo, pamoja na msongamano na miundombinu duni, kunazidisha hatari ya ajali. Wito huo umetolewa Kenya ikijiandaa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka Waathiriwa wa Ajali za Barabarani kesho, Novemba 15, kwa kaulimbiu, "Wekeza katika Usalama, Sio Mwendo Kasi". Takwimu za Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama Barabarani (NTSA) zinaonyesha watu 5,009 walifariki katika ajali mwaka 2025, ikilinganishwa na 4,748 mwaka 2024, ongezeko la asilimia 5.5. Ajali zilizoripotiwa ziliongezeka kutoka 11,165 hadi 11,638, huku idadi ya waliojeruhiwa ikipanda kutoka 24,245 hadi 24,905. Afisa wa Polisi anayesimamia Ukanda wa Kaskazini, Beatrice Kiraguri, alisema makosa ya madereva, uchovu na matumizi ya vileo ni miongoni mwa sababu kuu za ajali. Akizungumza wakati wa kampeni ya siku tano iliyoanzia Mombasa na kuhitimishwa Malaba Ijumaa, aliwataka madereva wa malori, magari ya umma, waendesha bodaboda na watembea kwa miguu kuwajibika. Kampeni hiyo inaongozwa na Mamlaka ya Uratibu wa Usafiri na Biashara ya Ukanda wa Kaskazini (NCTTCA), kwa ushirikiano na NTSA, KeNHA, polisi na Chama cha Wasafirishaji Kenya. Katibu Mkuu wa NCTTCA John Deng alisema ajali husababisha vifo, uharibifu wa mizigo na miundombinu, uchafuzi wa mazingira na kukatiza biashara za kikanda. Wasafirishaji pia wanataka barabara hiyo ipanuliwe kuwa ya njia mbili ili kupunguza msongamano na magari kugongana. Wadau wanasema juhudi za usalama pia zinatatizwa na uhaba wa magari ya doria. Vitengo vya polisi vinavyohudumia ukanda huo vina magari matatu pekee, licha ya kuwa na vituo tisa vya polisi. Maadhimisho makuu yatafanyika katika uwanja wa Jaramogi, Kisumu, huku maeneo mengine 12 yakiandaa hafla sawia.
read moreRight Column Content