taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 15 Sep 2026 12:57:42
Mwanamume ashtakiwa kumtapeli mwanamke Sh1,860 za meko ya Sun King
MWANAMUME anayeshutumiwa kwa kujipatia kwa njia ya udanganyifu Sh1,860 kutoka kwa mwanamke kwa kisingizio cha kumuuzia jiko la gesi ya LPG kutoka Sun King, alifikishwa katika Mahakama ya Nyamira Jumanne. Geoffrey Bett Kiplangat alishtakiwa kwa kosa la kutapeli lakini alikana mashtaka hayo. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, mnamo Agosti 5 katika eneo dogo la Mau Summit, Kamara Location, Kaunti Ndogo ya Kuresoi Kaskazini, Kaunti ya Nakuru, Kiplangat alijipatia kwa hila Sh1,860 kutoka kwa Hellen Nyamisa Bosire kupitia muamala wa M-Pesa. "Mshtakiwa anadaiwa kumshawishi mlalamishi kutuma pesa hizo katika akaunti mbalimbali za kibinafsi kwa kisingizio cha kununua jiko la gesi ya LPG na kulipia gharama za usafirishaji, jambo ambalo alijua kuwa si la kweli," mwendesha mashtaka wa kituo cha polisi cha Nyamira, Stephen Masaki, aliiambia mahakama. Bw Masaki aliendelea kueleza mahakama kwamba mshtakiwa amekuwa akitumia majina ya chapa mbalimbali halali kuwalaghai wateja wasio na taarifa za kutosha katika kaunti mbalimbali. Aliiomba mahakama kumzuilia mshukiwa kwa siku saba ili kuruhusu afisa wa probeshoni kuandaa na kuwasilisha ripoti kuhusu historia yake na kufaa kwake kuachiliwa kwa dhamana. "Mheshimiwa, tunaomba mshtakiwa azuiliwe kwa siku saba kusubiri kuwasilishwa kwa ripoti ya probeshoni. Hii itasaidia mahakama kuamua masharti yanayofaa ya dhamana," Masaki aliwasilisha ombi. Ombi hilo lilikubaliwa. Hakimu aliamuru Kiplangat azuiliwe katika Gereza la Nyamira GK hadi Septemba 23, 2026, kesi hiyo itakapotajwa kwa maelekezo zaidi na kuzingatiwa kwa masharti ya dhamana. Kesi hiyo inajiri wakati ambapo visa vya kujifanya wawakilishi wa chapa mbalimbali vimekuwa vikiongezeka, huku walaghai wakitumia majina ya kampuni zinazotegemewa za nishati ya jua na vifaa vya kielektroniki kuwalaghai wananchi. Akizungumza nje ya mahakama, Bi Lavender Atieno, mchambuzi wa masuala ya ulaghai kutoka Sun King, kampuni inayoongoza katika bidhaa za nishati ya jua ambayo chapa yake ilidaiwa kutumiwa na mshukiwa, aliwaonya wananchi kuwa waangalifu. Alisema chapa yao, pamoja na chapa nyingine nyingi, zimewahi kutumiwa vibaya na walaghai. "Tunawaonya watu wanaowalaghai wateja kwa kutumia majina ya chapa halali kwamba mkono wa sheria utawafikia. Tumeimarisha mifumo yetu ya uthibitishaji. Wateja wanapaswa kufanya malipo kupitia nambari rasmi za Paybill za Sun King pekee," Atieno alisema. "Usitume pesa kwa nambari za kibinafsi. Ikiwa mtu anadai kuwa anatoka Sun King au kampuni nyingine halali na kukuomba utume pesa kwenye akaunti ya kibinafsi kwa ajili ya jiko la gesi au bidhaa ya nishati ya jua, huyo ni tapeli," aliongeza. Bi Atieno alisema kampuni hiyo inashirikiana kwa karibu na Kurugenzi ya Upelelezi wa Jinai (DCI) pamoja na polisi wa maeneo mbalimbali kuwafuatilia na kuwafikisha mahakamani watu wote wanaojifanya kuwa wafanyakazi wao. Aliwahimiza waathiriwa wa ulaghai wa aina hiyo kuripoti mara moja katika kituo cha polisi kilicho karibu au kupitia njia rasmi za huduma kwa wateja za Sun King ili kupata msaada.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 15 Sep 2026 14:29:30
Takwimu za CBK zaonyesha Wakenya wanakopa sana kumudu mahitaji ya kila siku
HALI ngumu ya maisha imesukuma mamilioni ya Wakenya kutafuta mikopo ya kidijitali ili kukidhi mahitaji ya kila siku, huku zaidi ya akaunti milioni nane zikikopa zaidi ya Sh150 bilioni. Takwimu za Benki Kuu ya Kenya (CBK) zinaonyesha kuwa mikopo hiyo mingi haitumiki kuanzisha biashara au kuwekeza, bali kugharamia matumizi na mahitaji ya kimsingi ya maisha. Mkurugenzi Mkuu wa Metropol Credit Reference Bureau, Gideon Kipyakwai, alisema Wakenya wanakopa kwa viwango vya juu kutokana na ukosefu wa imani unaowazuia wengi kupata mikopo kutoka taasisi rasmi za kifedha. Alisema hali hiyo imewasukuma wengi kugeukia wakopeshaji wa kidijitali baada ya kufungiwa nje ya mifumo ya kawaida ya benki na taasisi nyingine za mikopo. "Taasisi za mikopo ya kidijitali zimeziba pengo la upatikanaji wa mikopo lililoachwa na mifumo ya jadi, huku Wakenya wakikopa mabilioni kwa kubofya kitufe kwenye simu zao," alisema Kipyakwai. Akizungumza pembezoni mwa Kongamano la Tatu la Kitaifa la Soko la Mikopo lililofanyika Naivasha, Kipyakwai alisema CBK imeidhinisha taasisi 300 za ukopeshaji, huku mamia ya zingine zikisubiri idhini. Alizitaka taasisi hizo kutumia data na teknolojia za kisasa kutathmini uwezo wa wakopaji, badala ya kutegemea mbinu zinazoweza kuongeza viwango vya kushindwa kulipa mikopo. Kipyakwai alisema zaidi ya asilimia 80 ya Wakenya watu wazima wamesajiliwa katika Credit Reference Bureau, inayotumiwa kutathmini uwezo wa mtu kukopa na kulipa. Alisema ushirikishaji wa kifedha nchini umefikia asilimia 84, huku mikopo kwa biashara ndogo na za kati ikiwa asilimia 30. Hata hivyo, aliyekuwa Katibu wa Wizara ya ICT, Dkt Bitange Ndemo, alisema ukweli kwamba Wakenya wengi wanakopa kwa matumizi badala ya uwekezaji ni ishara ya hali ngumu ya uchumi. Ndemo alitaka udhibiti uimarishwe ili kukabiliana na wakopeshaji haramu wanaotumia mbinu zisizo za kimaadili na kuwanyanyasa wateja. Alisisitiza pia umuhimu wa matumizi ya Akili Unde (AI) na data kubwa katika kutathmini uwezo wa wakopaji, huku akionya kuwa ulinzi wa data ni muhimu katika ukuaji wa sekta hiyo. Mkurugenzi Mkuu wa Financial Sector Deepening Kenya (FSD Kenya), Rashmi Pillai, alisema sekta hiyo inahitaji huduma zinazoaminika zaidi na zinazokidhi mahitaji ya wateja. Kwa mujibu wa kanuni zilizopitishwa, wakopeshaji wote wenye leseni wanapaswa kuzingatia sheria za ulinzi wa data, kutoa maelezo kamili kuhusu gharama za mikopo na kutumia mbinu za haki katika kukusanya madeni.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 15 Sep 2026 17:39:53
Man Utd wana kazi dhidi ya Brighton
MANCHESTER, Uingereza: MANCHESTER United itakuwa na kibarua kingine kigumu Jumatano usiku itakapomenyana na Brighton katika raundi ya tatu ya Kombe la Carabao ugani Old Trafford. Manchester United chini ya Michael Carrick inaingia katika pambano hilo baada ya kulazwa na Manchester City 1-0 katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo Jumapili. Mshambuliaji Erling Haaland alifunga bao la ushindi kipindi cha pili, lakini United ililalamikia uamuzi wa kulikubali bao hilo baada ya kiungo wa City Enzo Fernandez kuhusika katika tukio hilo akiwa ameotea. Kikosi hicho kimeshinda mechi moja pekee kati ya nne za kwanza za EPL, kikitoka sare moja na kupoteza mbili. Pia kimeruhusu mabao saba katika mechi nne. Kabla ya kuzuru Fulham kwa mechi ya EPL mnamo Jumapili, United itatumia mechi ya Brighton kujaribu kurekebisha makosa yake. United imeshinda Carabao mara sita, huku taji lake la mwisho likija msimu wa 2022/23. Hii itakuwa mechi yake ya kwanza katika mashindano hayo msimu huu baada ya kubanduliwa katika michuano hii mapema msimu uliopita na Grimsby Town ya daraja ya nne. United pia ina kumbukumbu mbaya dhidi ya Brighton katika mashindano ya vikombe baada ya kufungwa 2-1 nyumbani katika raundi ya tatu ya Kombe la FA mnamo Januari. Hata hivyo, ililipiza kisasi kwa kuichapa Brighton 3-0 katika mechi ya mwisho ya EPL mnamo Mei msimu uliopita. Tofauti na United, Brighton imeanza msimu kwa kishindo na inashikilia nafasi ya nne kwenye msimamo wa EPL ikiwa na pointi saba kutokana na mechi nne. Brighton imefunga mabao 13 katika mechi hizo, idadi kubwa zaidi katika ligi hadi sasa. Kikosi hicho kilionyesha makali Jumapili kilipoichapa Coventry City 5-0 ugenini, huku wachezaji watano tofauti wakifunga. Hata hivyo, Brighton ina rekodi mbaya katika Carabao, ikiwa imefika robo-fainali mara moja pekee, msimu wa 1978/79. Licha ya hayo, inaweza kujipa matumaini kutokana na rekodi yake ya hivi karibuni dhidi ya United. Brighton imeshinda mechi saba kati ya 11 zilizopita dhidi ya United katika mashindano yote, ikipoteza nne. Ushindi mara nne kati saba umepatikana Old Trafford. United haitakuwa na Matthijs de Ligt, Manuel Ugarte, Amad Diallo, Tom Heaton na Carlos Baleba kutokana na majeraha. Luke Shaw bado ni shaka. Carrick anatarajiwa kufanya mabadiliko kadhaa, huku Benjamin Sesko akiwa katika nafasi nzuri ya kuanza mbele badala ya Matheus Cunha. Brighton nayo itawakosa Yankuba Minteh, Kaoru Mitoma, Jack Hinshelwood, Zadok Yohanna, Mats Wieffer, Stefanos Tzimas na Evan Ferguson. Pascal Gross, aliyefunga bao moja na kutoa pasi mbili za mabao dhidi ya Coventry, anaweza kuanza tena. Gross amefunga mabao saba dhidi ya Manchester United, idadi kubwa kuliko dhidi ya timu nyingine yoyote. Kwa kuzingatia kiwango cha sasa, Brighton inaonekana kuwa na nafasi nzuri ya kuendeleza ubabe wake dhidi ya United na kuitoa mapema tena katika Carabao. Katika mechi zingine, Everton itawaalika Wolves, Fleetwood ya Ligi ya Daraja la Tatu Uingereza itamenyana na Sheffield United nao Coventry watatoana kijasho na Aston Villa. RATIBA: Everton vs Wolves (9:45pm), Fleetwood vs Sheffield United (9:45pm), Coventry vs Aston Villa (10:00pm), Manchester United vs Brighton (10:00pm).
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Tue, 15 Sep 2026 19:01:20
Uboreshaji soko la avokado kupitia chama cha ushirika
KILICHOANZA kama mazungumzo yasiyo rasmi kati ya viongozi wa wakulima waliokuwa wamechoshwa na kero za mabroka na mawakala kwenye uuzaji wa avokado Murang'a, sasa kimegeuka kuwa jukwaa linalowapa wakulima haswa wa mashamba madogo afueni kimapato. Wakulima wa matunda hayo ambayo pia yanajulikana kama maparachichi, wanaweza kuwahi soko la nje lenye faida bora. Hii ndiyo hadithi ya Murang'a Avocado Farmers' Co-operative Union Limited, ambayo kulingana na Meneja wake wa Miradi na Uhamasishaji wa Raslimali, John Ruoho Wangechi, chama hicho cha ushirika kilianzishwa kutokana na changamoto zilizokuwa zikikabili wakulima. Kwa miaka mingi, wakulima walipunjwa na madalali, udanganyifu wa mazao shambani na masoko yasiyotabirika. "Mabroka wakija shambani, kando na kupunja mkulima kipesa na kisoko, walikuwa wakipakia avokado kupita kiasi au kiwango wanachokubaliana," anaelezea. Ruoho anasema wakati wazo la kuunda chama hicho lilipoibuka, maparachichi yakuwa yakiuzwa kwa bei ya Sh2 hadi Sh10 kwa kila tunda, bila kujali ukubwa au ubora. Mfumo huo uliwaacha wakulima bila kujitetea kupata malipo bora. Hata hivyo, kuanzishwa kwa Murang'a Avocado Farmers' Co-operative Union Limited kumeleta mabadiliko makubwa, hasa baada ya kuhamia mfumo wa malipo kwa njia ya kilo badala ya kuhesabu matunda. "Sasa tunatumia mfumo wa kilo. Shamba likisimamiwa vizuri na kutoa mazao bora, mkulima hulipwa vyema na zaidi," anasema. [caption id="attachment_192191" align="aligncenter" width="300"] Avokado za Murang'a Avocado Farmers' Co-operative Union Limited wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirika la Wakulima Duniani (WFO) uliofanyika Nairobi, Juni 8, 2026. Picha|Sammy Waweru[/caption] Chama hicho cha ushirika na kilichosajiliwa rasmi Januari 2020, kilianza na vyama vidogo vinane lakini sasa vimefika 22, huku vikihudumia takriban wakulima 8,700 wanaoleta mazao bila kukosa. Kina zaidi ya wanachama 15,000 waliosajiliwa na zaidi ya wakulima 50,000 wa avokado, kulingana na rejista. Hutoa huduma za kitaalamu, ikiwemo mafunzo ya usimamizi wa mashamba, kilimo bora na matumizi ya miche iliyoidhinishwa. "Mazao hukusanywa kwa pamoja na kuuzwa kupitia wauzaji na waagizaji wa nje wanaokidhi viwango vya kimataifa kama vile GlobalGAP," Ruoho akaambia 'Akilimali' kwenye mahojiano ya kipekee. Ulaya na Nchi za Milki ya Kiarabu haswa Mashariki ya Kati ndizo masoko makuu ya maparachichi ya Kenya, huku China ikiwa soko lenye uwezo mkubwa lakini lenye masharti makali ya udhibiti. Msimu uliopita, chama kilikusanya karibu kilo 574,000 za avokado. Hata hivyo, kiasi hicho kilikuwa chini ya matarajio kwa sababu ya kuchelewa kwa vibali vya udhibiti na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyosababisha matunda kukomaa mapema. Ruoho anasema wakulima kwa sasa hupata kati ya Sh80 na Sh90 kwa kilo katika soko la ndani kwa ndani, huku bei ikibadilika kulingana na mahitaji na ubora. Murang'a Avocado Farmers' Co-operative Union Limited ilikuwa kati ya washirika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirika la Wakulima Duniani (WFO) wa mwaka huu, 2026, uliofanyika Nairobi kati ya Juni 8 na 11, ambapo cham hicho cha ushirika kilionyesha bidhaa zake, avokado. Kongamano hillo lilihudhuriwa na viongozi na wadauhusika wa kilimo nchini na pia kutoka sehemu mbalimbali duniani. Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi, Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo Mutahi Kagwe alisisitiza umuhimu wa wakulima kujipanga kwenye mashirika ili kubadilisha sekta ya kilimo. "Wakulima wa mashamba madogo ndio uti wa mgongo kuboresha mifumo yetu ya chakula. Wapojipanga, hupata sauti ya majadiliano, kuimarisha sera na kupata heshima katika uzalishaji, kilele chake kikiwa kupata soko bora," Waziri Kagwe alisema. [caption id="attachment_192192" align="aligncenter" width="300"] John Ruoho Wangechi, Meneja wa Miradi na Uhamasishaji wa Raslimali Murang'a Avocado Farmers' Co-operative Union Limited, aaelezea kuhusu juhudi za chama hicho cha ushirika kusaidia wakulima kupata masoko ya nje ya nchi ya parachichi wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirika la Wakulima Duniani (WFO) uliofanyika Nairobi, Juni 8, 2026. Picha|Sammy Waweru[/caption] Kaulimbiu ya kongamano hilo lililoandaliwa na Shirikisho la Kitaifa la Wakulima wa Kenya (KENAFF) kwa ushirikiano na Shirika la Wakulima Duniani (WFO), ilikuwa "Future Fields: Investing in Farmers' Organisations and Empowering Communities for Sustainable Agriculture." Kilimo cha maparachichi kimekuwa chanzo cha utajiri maeneo ya mashambani, kikisaidia familia kugharamia elimu, kuboresha maisha na uchumi. Hata hivyo, sekta hii inakabiliwa na changamoto za hasara hasa baada ya mavuno, zinazokadiriwa kufikia asilimia 60–65, pamoja na ushindani kutoka kwa wachakataji wa mafuta ya maparachichi. Wasindikaji wa mafuta hulipa wakulima kati ya Sh18–20 kwa kilo, ikilinganishwa na zaidi ya Sh80 kwa kilo katika soko la nje. Ruoho anasema tofauti hiyo ya bei inawashawishi baadhi ya wakulima kuvuna mapema na kuelekeza mazao yao kwenye viwanda vya mafuta, jambo linalopunguza uuzaji wa avokado kwenye masoko ya nje. Kwa upande mwingine, teknolojia imekuwa nguzo muhimu katika shughuli za Murang'a Avocado Farmers' Co-operative Union Limited, huku malipo yakifanywa kwa njia ya simu, utunzaji wa kumbukumbu kidijitali na majukwaa ya mitandao ya kijamii yakisaidia kuboresha mawasiliano na masoko. Chama hicho cha ushirika kimekuwa kikipigwa jeki na shirika la We Effect, hasa katika uimarishaji wa masuala ya uongozi, uwekezaji wa fedha, kuhamasisha usawa wa kijinsia na matumizi ya teknolojia.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 16 Sep 2026 02:55:23
Pigo kuu korti ikiagiza serikali irejeshe hisa za Safaricom ilizouzia kampuni ya Afrika Kusini
MAHAKAMA Kuu imebatilisha uuzaji wa asilimia 15 ya hisa za Serikali ya Kenya katika kampuni ya Safaricom kwa Vodacom Group, ikisema shughuli hiyo ilifanyika kinyume na Katiba na sheria za nchi. Jopo la majaji watatu liliamuru hisa hizo zirudishwe serikalini, likibaini kuwa mchakato wa uuzaji ulikumbwa na dosari nyingi ikiwemo ukosefu wa ushiriki wa kutosha wa umma, kufichwa kwa taarifa muhimu, uwekaji wa bei usio na msingi wa wazi na kutoshughulikiwa kwa masuala ya usalama wa taifa yaliyotokana na kuhamishwa kwa udhibiti wa kampuni hiyo kwa wawekezaji wa kigeni. "Kwa kuzingatia hitimisho letu, tunashikilia kuwa hakukuwa na ushiriki wa umma wa maana na wa kutosha kuhusu uuzaji huo. Hivyo basi, Kifungu cha 10 na 118 cha Katiba kilikiukwa," walisema Majaji Francis Gikonyo, Roselyne Aburili na Tabitha Ouya. Uamuzi huo ni pigo kubwa kwa mpango wa serikali wa kukusanya fedha za Hazina ya Kitaifa ya Miundombinu kupitia uuzaji wa mali ya umma. Serikali iliuza hisa hizo kwa Sh204.3 bilioni kwa bei ya Sh34 kwa kila hisa. Aidha, ilipata takriban Sh40.7 bilioni kutokana na kuuza haki zake za kupata mgao baadaye kutoka kwa asilimia 20 ya hisa ilizobaki. Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na mwanaharakati Tony Gachoka pamoja na wengine waliopinga uuzaji huo, wakisema Safaricom ni rasilimali muhimu ya kitaifa. Mahakama ilikataa hoja ya Vodacom Group kwamba, kesi hiyo ilikuwa imepitwa na wakati baada ya Bunge kuidhinisha muamala huo Machi 31, 2026. Majaji walisema kesi hizo zilipinga msingi wa kikatiba wa muamala wenyewe na kwamba, idhini ya baadaye ya Bunge isingeondoa ukiukaji uliodaiwa. Mahakama ilisema kuwa ingawa Bunge lilifanya mikutano ya ushirikishaji katika kaunti 30, stakabadhi muhimu kama mkataba wa ununuzi wa hisa na makubaliano kuhusu haki za mgao wa baadaye hazikuwekwa wazi kwa umma. "Tunakubaliana na walalamishi kwamba, taarifa na stakabadhi muhimu zilifichwa umma, Baraza la Mawaziri na Bunge la Taifa," majaji walisema. Mahakama ilisisitiza kuwa ushiriki wa umma si suala la kufanya mikutano pekee bali lazima uwe wa kweli, wa wazi, wa maana na unaowezesha wananchi kushawishi maamuzi yanayofanywa. Majaji pia walibaini kuwa serikali iliwasilisha mpango huo kama uuzaji wa sehemu ya hisa, ilhali kwa hakika ulikuwa ni mchakato mpana zaidi wa marekebisho ya umiliki ambao ungeipa Vodacom udhibiti halisi wa Safaricom. Chini ya mpango huo, hisa za Vodafone Kenya katika Safaricom zingepanda kutoka asilimia 39.9 hadi asilimia 55, huku Vodacom Group ikimiliki kikamilifu Vodafone Kenya. Kwa mujibu wa mahakama, hatua hiyo ilifanana zaidi na unyakuzi wa kampuni kuliko uuzaji wa kawaida wa hisa za serikali. Mahakama pia ilikosoa serikali kwa kutofungua uwekezaji huo kupitia mchakato wa wazi wa kuchagua mwekezaji wa kimkakati. Kuhusu bei ya Sh34 kwa kila hisa, majaji walikubaliana kuwa mchakato uliotumika haukuwa wa kimantiki na ulikuwa wa kiholela. Zaidi, mahakama ilieleza kuwa muamala huo ulizua masuala mazito ya usalama wa taifa kwa kuwa Safaricom inaendesha miundombinu muhimu inayotumika katika uchaguzi, mifumo ya malipo ya serikali, huduma za fedha za simu na kuhifadhi data binafsi za mamilioni ya Wakenya. Majaji walisema kuhamisha udhibiti wa miundombinu hiyo kwa kampuni ya kigeni bila tathmini ya awali ya usalama wa taifa kulikiuka wajibu wa serikali wa kulinda maslahi ya nchi. Hivyo, mahakama ilitangaza uuzaji huo kuwa batili, ikafutilia mbali uamuzi wa Bunge uliouidhinisha pamoja na idhini yenyewe, mikataba na hatua zote zilizohusiana nao. Mahakama iliamuru asilimia 15 ya hisa za Safaricom zirudishwe chini ya umiliki wa Serikali ya Kenya kwa niaba ya wananchi. Pia ilikataa kusimamisha utekelezaji wa hukumu hiyo ili kuruhusu rufaa, na kuwaelekeza wahusika kuwasilisha ombi rasmi la kusitisha utekelezaji iwapo wanataka kufanya hivyo.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 16 Sep 2026 03:55:36
Ruto amshambulia Orengo, amtaka aache kuwa 'kibaraka wa Uhuru', ajiunge na serikali
KATIKA siku yake ya tatu ya ziara ya Nyanza, Rais William Ruto alipeleka mapambano yake ya kisiasa dhidi ya vuguvugu la Linda Mwananchi hadi Siaya, ngome ya Gavana James Orengo, akiwataka wapigakura kukataa vyama vipya ambavyo alisema havijathibitisha uwezo wao wa kuongoza nchi. Rais Ruto aliwataka wakazi kuunga mkono vyama vilivyo katika serikali jumuishi, akipuuza vyama vipya ambavyo bado havijasajiliwa rasmi. Alisema vyama hivyo havina uzoefu, mtandao wa kitaifa wala mipango thabiti ya kuongoza Kenya. Ziara yake Siaya ilikuwa na umuhimu wa kisiasa, hasa kwa kuwa viongozi wa Linda Mwananchi wanatarajiwa kuzuru eneo hilo siku chache zijazo. Rais Ruto pia alimshambulia Gavana Orengo kwa kuhusishwa na vuguvugu hilo, akimtaka badala yake kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo Siaya. "Namwambia Orengo aache kundi hilo linaloitwa Linda Sponsors au Linda Sponyo na ajiunge nami katika safari hii ya maendeleo na kujenga hospitali. Je, ninyi watu mlimchagua ajiunge na Linda Sponsors? Kwa nini anaruhusu kuwa kibaraka wa kisiasa na kutumiwa na rais mstaafu?" Rais Ruto alisema. Pia alimshambulia Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, akimlaumu kwa kuacha jukumu la kuwa kiongozi mstaafu na kuingia katika siasa za upinzani dhidi ya serikali yake. Rais Ruto alisema Bw Kenyatta alikuwa akiwafadhili wanasiasa wanaompinga baada ya kushindwa kutekeleza baadhi ya mipango aliyokuwa nayo katika sekta ya elimu na afya. Akizungumza alipokuwa akikagua ujenzi wa Daraja la Dhogoye, Siaya, Rais Ruto aliunganisha ujumbe wa maendeleo na siasa, akisema serikali jumuishi imefungua ukurasa mpya wa maendeleo katika Nyanza. "Serikali jumuishi ndiyo muungano pekee wenye uwezo wa kuunganisha taifa letu. Ndiyo yenye historia ya utekelezaji, maono ya kuaminika ya siku zijazo na mpango wa kushughulikia changamoto zinazokabili taifa," alisema. Alionya wapigakura dhidi ya kuunga mkono vyama vipya, akisema Kenya haiwezi "kujaribu" viongozi wasio na historia ya utekelezaji. "Taifa letu halitajaribu watu wanaofanya majaribio. Msicheze kamari na watu ambao hawana mpango au historia ya wazi ya kuwafanyia kazi wananchi," alisema. Rais Ruto pia alimwalika Mbunge wa Ugenya David Ochieng, ambaye anaongoza chama cha Movement for Democracy and Growth (MDG), kujiunga na serikali jumuishi. Bw Ochieng alikubali ombi hilo, lakini akaomba Rais Ruto kumuunga mkono katika azma yake ya kumrithi Bw Orengo kama Gavana wa Siaya. Aliahidi kumpa Rais Ruto asilimia 99.9 ya kura za Ugenya katika uchaguzi wa 2027 iwapo atapata uungwaji mkono huo. "Nimefurahia kufanya kazi nawe, Mheshimiwa Rais, kwa sababu umekuwa rafiki mzuri. Umetusaidia kuendeleza Ugenya... ndiyo maana tutakupa asilimia 99.9 ya kura zetu," alisema Bw Ochieng. Viongozi walioandamana na Rais Ruto walitumia ziara hiyo kumshambulia Gavana Orengo, ambaye hakuwa kwenye ziara hiyo. Waziri wa Kawi na Petroli Opiyo Wandayi alisema viongozi wengi wa Siaya wameungana isipokuwa mmoja, akimtaja Bw Orengo. "Rais Ruto, tuachie Orengo sisi. Tutahakikisha anaenda nyumbani," alisema Bw Wandayi. Gavana wa Homa Bay na Mwenyekiti wa ODM Gladys Wanga pia alimshambulia Bw Orengo, akimtaka aache kupotosha jamii ya Luo. Naibu Gavana wa Siaya William Oduol alijitangaza kuwa kaimu gavana kutokana na kutohudhuria kwa Bw Orengo. Rais Ruto alitaja miradi kadhaa ya maendeleo ambayo serikali imepanga kutekeleza Siaya. Alisema ujenzi wa barabara ya kilomita 500 inayozunguka Ziwa Victoria utaanza Novemba 2026, baada ya kusubiriwa kwa zaidi ya miaka 15. Barabara hiyo itaunganisha Busia na Muhuru Bay kaunti ya Migori kupitia Siaya, Kisumu na Homa Bay. Aidha, Sh32 bilioni zitatumika kujenga kilomita 400 za barabara mpya Siaya. Rais Ruto pia alisema Sh10 bilioni zimetengwa kwa uchumi wa baharini, ikiwemo utafiti na teknolojia ya uzalishaji wa samaki wachanga, gati nne, huduma za feri na vituo vya uokoaji.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 16 Sep 2026 04:55:52
NI HISTORIA: Sababu za Kenya kutuzwa uandalizi wa mbio kubwa zaidi duniani
HISTORIA pevu ya Kenya katika riadha, ongezeko kubwa la mashabiki wa mchezo huo, ukarabati kabambe wa miundomsingi ya michezo na ufadhili thabiti wa serikali umeiwezesha Nairobi kushinda zabuni ya kuandaa Riadha za Dunia za mwaka 2029. Tunu hiyo pia imetokana na mafunzo muhimu yaliyopatikana baada ya Nairobi kushindwa katika zabuni ya kuandaa Riadha za Dunia za 2025, ambazo zilipewa Tokyo, Japan. Nairobi ilirekebisha kasoro zilizojitokeza katika uwaniaji huo na kuboresha mipango yake ili kulishawishi Baraza la Riadha Duniani mara hii. Rais wa Riadha Duniani, Sebastian Coe, alisema Nairobi iliweka rekodi nzuri zaidi baada ya kurejea na pendekezo imara la kuandaa mashindano ya 2029, ikitumia tajriba ya karibu muongo mmoja ya kuandaa mashindano makubwa ya kimataifa ya riadha. Coe alisema Nairobi ilianza kujijengea sifa kwa kuandaa Riadha za Dunia za Wasiozidi miaka 18 (Under-18) mnamo 2017, Under-20 mwaka 2021 na Kip Keino Classic, mashindano ya World Athletics Continental Tour Gold yaliyoanzishwa mwaka wa 2020. "Riadha za Under-18 ya 2017 zilidhihirisha hamu kubwa ya Wakenya katika riadha, huku umati mkubwa ukijaza uwanja wa Kasarani katika kipindi chote cha mashindano. "Tangu wakati huo, Nairobi imeifanya Kip Keino Classic kuwa mojawapo ya mashindano makubwa ya siku moja barani Afrika, huku mashindano hayo yakiwa sehemu ya World Athletics Continental Tour Gold," alisema Coe. Aliongeza kuwa tajriba hiyo iliweka msingi imara wa zabuni ya 2029 iliyojumuisha mipango madhubuti ya uendeshaji pamoja na dhamana za kifedha. Uwanja wa Kasarani, ambao unafanyiwa ukarabati mkubwa kabla ya kuandaa Kombe la Afrika (AFCON) 2027, miaka miwili kabla ya Riadha za Dunia, ni sehemu muhimu ya maono ya kuandaa Riadha za Dunia kwa mara ya kwanza barani Afrika. Kiongozi huyo wa riadha duniani alisema Nairobi imeonyesha wazi kuwa wakati umefika wa kuharakisha maendeleo ya riadha nchini Kenya na barani Afrika, huku ikiweka urithi utakaolihamasisha bara hilo na dunia nzima. Nguvu ya uhusiano wa Kenya na riadha pia imeonekana katika utafiti wa World Athletics kuhusu mashabiki, ambao umeonyesha kiwango cha kipekee cha ushiriki wao. Asilimia 68 ya Wakenya waliohojiwa walisema wana hamu kubwa ya kufuatilia riadha, ikilinganishwa na wastani wa kimataifa wa asilimia 39. Hii inaifanya Kenya kuwa soko lenye hamu kubwa zaidi ya riadha miongoni mwa masoko yaliyofanyiwa utafiti. "Kenya ina alama ya juu zaidi ya net promoter score kuliko soko lolote, na riadha ndiyo mchezo wa pili unaofuatiliwa zaidi nchini, baada ya soka pekee," alisema Coe. Aliongeza kuwa Kenya ni nchi ya nne duniani kwa idadi ya wafuasi wa kurasa za Riadha Duniani katika mitandao ya kijamii. Kenya ni nchi ya pili yenye mafanikio makubwa zaidi katika historia ya Mashindano ya Dunia ya Riadha, ikiwa nyuma ya Marekani katika orodha ya medali. Kenya imeshinda jumla ya medali 182 — dhahabu 72, fedha 60 na shaba 50 — tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo mjini Helsinki, Finland, mwaka 1983. Marekani ina medali 649, zikiwemo dhahabu 211, fedha 139 na shaba 119. Katika Mashindano ya Dunia ya Riadha yaliyofanyika Tokyo mwaka uliopita, Kenya ilishinda medali saba za dhahabu na 11 kwa jumla. Wanariadha wa Kenya walinyakua mataji yote ya wanawake katika mbio za masafa ya kati hadi marefu uwanjani na mbio za marathoni. Coe alisema Nairobi iliwasilisha zabuni iliyokuwa na ushindani mkubwa na iliyogusa hisia, akieleza jiji hilo kuwa kitovu kinachokua kwa kasi, chenye nguvu na cha kisasa katika huduma, uchumi, utamaduni na siasa za Afrika Mashariki. "Kupeleka Mashindano ya Dunia ya Riadha barani Afrika kwa mara ya kwanza kutakuwa jambo la kihistoria. Ilikuwa muhimu mashindano hayo yaje Afrika wakati tunapokuwa na mwenyeji anayefaa, zabuni inayofaa na mazingira yanayofaa. Nairobi imeonyesha wazi kuwa wakati wake umefika," alisema Coe. Alisema riadha imejikita katika maisha ya Wakenya na imekuwa chimbuko la wanariadha waliounda historia ya mchezo huo duniani, wakiwemo mabingwa wa dunia Faith Kipyegon, Vivian Cheruiyot, Eliud Kipchoge, Hellen Obiri na David Rudisha. Wengine ni bingwa wa Olimpiki mara mbili Kip Keino, bingwa mara kadhaa wa dunia wa mbio za nyika Paul Tergat na bingwa mara kadhaa wa dunia wa nusu marathoni Tegla Loroupe.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 16 Sep 2026 05:55:28
Waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran walemea Saudi Arabia kwa makombora
RIYADH, Saudi Arabia WAASI wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran wameanzisha wimbi jipya la mashambulizi dhidi ya Saudi Arabia, hatua ambayo imeongeza wasiwasi kuhusu usalama wa usafirishaji wa mafuta katika Mashariki ya Kati. Serikali ya Yemen ilisema kuwa Wahouthi wapo pwani ya magharibi ya Yemen, kando ya Bahari ya Shamu ambapo wamenogesha mikakati ya kushambulia Saudi Arabia. Wahouthi wenyewe walisema walirusha makombora kadhaa na ndege zisizo na rubani katika kituo cha kijeshi cha Khamis Mushait kusini mwa Saudi Arabia. Walisema walilenga ndege, uwanja wa ndege na maghala ya risasi, kulipiza kisasi mashambulizi ya anga ya Saudi Arabia nchini Yemen. Serikali ya Saudi Arabia imetoa tahadhari kwa wanaopanga kuzuru miji minne ya kusini. Saudi Arabia ilisema raia 13 walijeruhiwa katika mashambulizi hayo ya Wahouthi. Mashambulizi hayo yameongeza shinikizo kwa usafirishaji wa mafuta wa Saudi Arabia baada ya shambulizi la anga Alhamisi kusababisha bomba la mafuta linalounganisha mashariki na magharibi mwa nchi hiyo kusitisha shughuli. Saudia ililaumu wanamgambo hao wanaoungwa mkono na Iran kutokana na shambulizi hilo. Wafanyabiashara wa mafuta walisema kufungwa kwa muda mrefu kwa bomba hilo kunaweza kuathiri hadi asilimia nne ya usambazaji wa mafuta duniani, hasa wakati Mkondo wa kupitisha mafuta wa Hormuz ukiwa bado umefungwa na Iran. Wakati huo huo, matumaini ya diplomasia yalipungua baada ya nchi za Ghuba kuahirisha mazungumzo yaliyopangwa na Iran kuhusu kufunguliwa tena kwa Mlango wa Hormuz. Kabla ya vita kati ya Amerika-Israel dhidi ya Iran, Strait of Hormuz ilikuwa ikipitisha asilimia 20 ya mafuta yanayouzwa duniani. Oman, iliyokuwa imepanga kuandaa mkutano huo, ilitangaza kuwa umeahirishwa. Iran ilisema Saudi Arabia ndiyo iliyoomba kuahirishwa. Rais wa Amerika Donald Trump alisema Iran ilikuwa tayari kufanya makubaliano, lakini Mohsen Rezaei, katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, alikataa kauli hiyo na kusema hakuna mazungumzo hadi masharti ya Iran yatimizwe. Saudi Arabia imekuwa ikiongoza vita dhidi ya Wahouthi tangu 2015. Ingawa mapigano yalipungua baada ya pande zote kuafikia makubaliano ya kusitisha mapigano, vita vilianza tena mwezi huu. Kuendelea kwa mapigano na tishio kwa Mlango wa Hormuz kunazua hofu zaidi kwamba usambazaji wa mafuta duniani unaweza kuvurugika, hali ambayo huenda ikaendelea kuweka shinikizo la kupanda kwa bei ya mafuta.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 16 Sep 2026 06:55:33
Wakenya mpakani Tanzania wadumisha ushirikiano licha ya agizo tata lililohusu wageni
WAKAZI katika mipaka ya Kenya na Tanzania, maeneo ya Taveta na Lunga Lunga wamedumisha ushirikiano wao licha ya matukio ya hivi majuzi nchini yaliyotishia usalama wa wafanyabiashara wadogo ambao ni raia wa kigeni. Kwa miongo mingi, raia wa nchi hizo mbili wamekuwa wakifanya biashara pamoja, kuoana, kuvuka mipaka kutafuta elimu bora, matibabu, na hata kushiriki pamoja kwa tamaduni zao. Ushirikiano huo wa karibu ulijaribiwa kufuatia hatua za Kenya za kutekeleza kanuni za uhamiaji na biashara dhidi ya wafanyabiashara wa kigeni wasio na hati halali. Wakati mjadala kuhusu wafanyabiashara wa kigeni ukiendelea kitaifa, shughuli za biashara katika maeneo mawili ya mpakani Pwani zinaendelea kwa kiasi kikubwa kama kawaida. Wakazi wa Lunga Lunga, Kaunti ya Kwale, wanasema mpaka huo haujawahi kuwa kikwazo kikubwa kwa uwiano wao. "Tunasoma na kuona kwenye vyombo vya habari kuhusu wageni wanaoondoka nchini, lakini katika eneo letu hatuwezi kuwabagua kwa sababu ni sehemu ya familia. Tunavua katika bahari moja, tumeoana na tunashiriki utamaduni mmoja," alisema mkazi, Bw Juma Mwaguza. Kulingana nao, mtu aliyezaliwa upande mmoja wa mpakani anaweza kuwa na ndugu, mwenzi wa ndoa au washirika wa biashara upande mwingine. Familia huvuka mpaka mara kwa mara kwa ajili ya harusi, mazishi, shughuli za kidini, elimu na matibabu. Vilevile, wakazi wanasema baadhi ya wafanyabiashara wa Tanzania hutumia marafiki au jamaa zao wanaoaminika nchini Kenya kupata huduma za pesa kwa njia ya simu na kusajili laini za simu, huku Wakenya wanaoishi karibu na mpaka wakiwa na mipango kama hiyo upande wa Tanzania. Wanasema desturi hizo kwa kiasi kikubwa zinatokana na uaminifu uliojengwa kwa miongo mingi, wala si kwa nia ya kukwepa sheria za kitaifa. Mpakani Taveta, utegemezi wa kiuchumi kwa Tanzania ni mkubwa zaidi hasa kwa bidhaa za kilimo. "Jamii zimeungana na hatujaathiriwa na agizo hilo kwa sababu tunafanya biashara ya kuvuka mpaka. Lakini ikiwa agizo hilo litatulazimisha kubaki katika nchi zetu, Wakenya watateseka kwa sababu zaidi ya asilimia 60 ya bidhaa zinazouzwa katika soko la Taveta hutoka Tanzania," alisema mfanyabiashara wa Tanzania, Bw Allen Kubo. Soko la Kisasa la Taveta liko umbali wa takriban kilomita tatu pekee kutoka mpaka wa Kenya na Tanzania, hali inayowezesha mazao kuwafikia watumiaji haraka kupitia Kituo cha Pamoja cha Mpaka cha Taveta-Holili. Wiki iliyopita, serikali iliwapa raia wa nchi za Afrika Mashariki wasio na hati halali nchini siku 90 kurekebisha stakabadhi zao za uhamiaji na kutimiza masharti ya leseni za biashara iwapo wangependa kuendelea kuendesha biashara nchini. Agizo hilo lilizua wasiwasi miongoni mwa baadhi ya wafanyabiashara wa kigeni, huku mamia ya raia wa Burundi wakitafuta msaada katika ubalozi wao jijini Nairobi kutokana na hofu ya mashambulizi. Nchini Uganda, gazeti la Daily Monitor liliripoti kuwa wafanyabiashara wa Uganda walikuwa miongoni mwa walioondoka Kenya wakihofia kushambuliwa. "Taita Taveta ni kaunti yenye amani. Tunaishi pamoja na biashara zetu zinaendelea bila kikwazo chochote," alisema Gavana Andrew Mwadime. Jumuiya ya Afrika Mashariki inahimiza usafirishaji na uhamishaji wa watu, bidhaa na huduma miongoni mwa nchi wanachama, huku serikali za kila nchi zikipewa jukumu la kutekeleza kanuni za uhamiaji, ushuru na biashara. Rais Ruto baadaye aliwahakikishia wawekezaji na wafanyabiashara wa kigeni kwamba Kenya bado iko wazi kwa biashara na uwekezaji. Akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kwa hospitali inayojengwa na kampuni ya Tanzania, Dkt Ruto aliwaonya Wakenya dhidi ya kuwalenga raia wa kigeni wanaoendesha biashara ndogo nchini, akisema wako huru kufanya kazi nchini bora tu watii sheria za Kenya.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Wed, 16 Sep 2026 07:55:34
Maraga abuni muungano kushinikiza mageuzi IEBC, asema kuhesabu kura Bomas ni haramu
MUUNGANO unaoongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga umetaka mageuzi makubwa kufanyiwa mchakato wa uchaguzi kabla ya kura za mwaka ujao na ukatishia kuongoza Wakenya kwenye maandamano iwapo mabadiliko hayo hayatafanywa. Muungano huo, unaojulikana kama People's Coalition on Electoral Reforms, umeibua mjadala mpya kuhusu maandalizi ya uchaguzi huku ukielekeza lawama kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Bunge na serikali. Miongoni mwa mageuzi unaopendekeza ni kufutwa kwa kituo cha kitaifa cha kujumlisha kura za urais katika ukumbi wa Bomas, ukaguzi huru wa sajili ya wapigakura, kuongezwa kwa adhabu kali kwa makosa ya uchaguzi, kugatuliwa kwa matumizi ya mfumo wa teknolojia ya uchaguzi na mchakato wa wazi wa kuajiri maafisa wa IEBC. Muungano huo unawaleta pamoja Maraga, Mbunge wa Saboti Caleb Hamisi, Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi, kiongozi wa Thirdway Alliance Ekuru Aukot na aliyekuwa Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi. Akizungumza kwa niaba ya muungano huo, Maraga alisema mageuzi hayo lazima yatekelezwe kabla ya uchaguzi wa Agosti 2027 ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru, wa haki, wenye uwazi na unaoaminika. "Kenya haiwezi kumudu uchaguzi mwingine ambao uaminifu wake ni wa kutiliwa shaka. Ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007/2008 ni onyo la kitaifa ambalo hatuko tayari kulirudia," alisema Maraga. Muungano huo unasema suala la uaminifu wa uchaguzi wa 2027 si la kisiasa pekee bali ni jambo la maslahi ya taifa linalohitaji wahusika wote-wapigakura, wagombeaji, serikali, upinzani na wananchi kwa jumla. Kwa mujibu wa Caroli Omondi, muungano huo unapinga kuwepo kwa kituo cha kitaifa cha kujumlisha kura za urais, ukisema Katiba inahitaji kura zihesabiwe na kutangazwa katika vituo vya kupigia kura na katika ngazi ya eneo bunge. "Hakutakuwa na kituo cha kitaifa cha kujumlisha kura za urais kinachoendeshwa na IEBC au mwenyekiti wake katika Bomas au mahali pengine popote," alisema Omondi.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Wed, 16 Sep 2026 12:01:30
Don't punish him': Sharon's mother pleads with court to spare Obado
Melinda Auma made the emotional appeal as she addressed Justice Cecilia Githua during the mitigation and sentencing hearing following Obados conviction for the murder of her daughter.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 14 Sep 2026 21:19:34
Beyond the City Gates: What Safari Drivers Have Learned About Kenya Park Fees in 2026
If you drove through the East Gate of Nairobi National Park in early 2024, you probably remember the crawl of Land Cruisers idling while drivers argued over paper receipts. That queue is gone. The early morning air still carries the same mix of cold dew and acacia blossom, but the bottleneck has moved from the [...] The post Beyond the City Gates: What Safari Drivers Have Learned About Kenya Park Fees in 2026 appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content