taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 20 Jul 2026 05:24:18
Makosa ya kutumia kihusishi 'ndani ya' na kiambishi 'ni' katika sentensi
SILABI 'ni' hutumiwa kwa kuwasilisha dhana mbalimbali katika maneno kama vile kutoa amri au rai kwa watu wengi. Mfano: Someni hadithi hiyo. Pia kiambishi ni hutumiwa katika ukanusho wa kitenzi kilicho katika kauli ya kutendana. Mfano: Siku hizi hatupigiani simu na shangazi yangu. Vilevile, kiambishi tamati ni, hutumiwa kama kiwakilishi cha nafsi ya kwanza katika sentensi. Mfano: Ninaenda shuleni. Isitoshe kiambishi ni kinapotumiwa mwishoni mwa nomino ya kawaida hubadilisha nomino hiyo kuwa mahali. Mfano: Nomino ya kawaida darasa hupatikana katika ngeli ya LI-YA. Hata hivyo, nomino hiyo inapoambishwa silabi ni mwishoni hubadilika kuwa nomino ya mahali kwa mfano darasani ambayo huwa katika ngeli ya PA-KU-MU. Baadhi ya wanafunzi wana mazoea ya kufanya makosa ya kawaida ya kutumia kiambishi ni mwishoni mwa nomino pamoja na kihusishi 'ndani ya' katika sentensi moja. Aghalabu utapata sentensi kama vile: *Siafu wameingia ndani ya sebuleni. *Wanafunzi wanakula kishuka ndani ya bwaloni. Mifano hii ya sentensi si sahihi. Kila sentensi imetumia kihusishi ndani ya pamoja na kiambishi ni mwishoni mwa nomino. Ili kuzisahihisha sentensi hizo tunafaa kusema: Siafu wameingia ndani ya sebule ama Siafu wameingia sebuleni. Vilevile tunafaa kusema: Wanafunzi wanakula kishuka ndani ya bwalo au Wanafunzi wanakula kishuka bwaloni. Tuendelee kujifunza kutunga sentensi sahihi ili kuimarisha mawasioliano yetu.
read morekenyanews.go.ke
@kna Mon, 20 Jul 2026 04:52:06
Free skills training transforms lives of Murang'a youth
As unemployment continues to pose a major challenge for thousands of young Kenyans, a vocational training initiative in Mathioya, Muranga County, is equipping youth with practical skills that are enabling them to secure employment, establish businesses and build sustainable livelihoods. The 360 Climate Institute is offering free vocational training to young people who were unable...
read morekenyanews.go.ke
@kna Mon, 20 Jul 2026 05:00:11
Run 4 Seniors attracts 1,000 participants supporting Kenya's older persons
More than 1,000 registered participants converged at Karura Forest for the second edition of the Run 4 Seniors charity event, highlighting growing national commitment to improving the welfare, dignity and wellbeing of older persons across Kenya. The annual event, organised by Mama Ibado Charity, brought together individuals, families, corporate organisations, fitness enthusiasts and community groups...
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 20 Jul 2026 05:19:36
Vijay Singh Net Worth
Vijay Singh is a Fijian professional golfer with an estimated net worth of $75 million. Known as The Big Fijian, Singh is one of the most accomplished golfers in PGA Tour history. During a remarkable professional career, he won 34 PGA Tour events, captured three major championships, reached World No. 1, and became one of [...] The post Vijay Singh Net Worth appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 20 Jul 2026 05:02:20
Mwalimu anayebadilisha mtazamo wa wanafunzi wasiopenda Ushairi na Sarufi
KATIKA kipindi ambapo jamii nyingi zinakabiliwa na changamoto za malezi, nidhamu na maadili, bado wapo walimu wanaosimama imara kama nguzo za matumaini. Wao hawafundishi darasani pekee, bali huishi maisha yanayowapa wanafunzi mfano wa kuigwa. Kupitia juhudi zao, wanafunzi wengi hupata mwelekeo sahihi na kuhamasika kufikia ndoto zao. Miongoni mwa walimu hao ni Bi Valentine Nayaku, mwalimu wa Kiswahili katika Shule ya Upili ya Itabua, Kaunti ya Embu. Safari yake ya mafanikio ni ushahidi kwamba bidii, nidhamu na uongozi bora vinaweza kumwezesha mtu kufikia kilele cha ufanisi. Nayaku alizaliwa na kulelewa katika eneo la Malava, Kaunti ya Kakamega. Yeye ndiye mwanambee katika familia ya watoto wanane ya Bw Antony Inyanje na Bi Linet Lelei. Tangu akiwa mtoto, alionyesha ari kubwa ya kujifunza na kujituma katika masomo yake. Safari yake ya elimu ilianzia katika Shule ya Msingi ya Lugusi kabla ya kupitia katika Shule ya Upili ya Kongoni. Akiwa mwanafunzi, alivutiwa sana na uigizaji pamoja na ughani wa mashairi aliyoyasikia redioni na runingani. Hata hivyo, mapenzi yake makubwa yalikuwa kwa somo la Kiswahili. "Walimu wangu kama Bw Lumasai, Edward Barasa, Seth Ambei na Makhanu walinilea na kuninoa katika Kiswahili. Aidha, walimu wangu wa darasa, Bw Kelvin Mutali na Bw Daniel Wemanya, walinishauri nichague taaluma ya ualimu wa Kiswahili ili niendelee kung'ara katika lugha hii," anasimulia. Uongozi wake ulianza kujidhihirisha akiwa shuleni alipoteuliwa kuwa kiranja tangu kidato cha pili. Nafasi hiyo ilimjenga kuwa kiongozi mwajibikaji mwenye nidhamu ya hali ya juu. Walimu wake, akiwemo Bw Nyabera na Bi Sheila Sifuna, walimpa mwongozo ulioimarisha uwezo wake wa kuongoza hadi alipokamilisha masomo ya shule ya sekondari. Baada ya kuhitimu, alijiunga na Chuo Kikuu cha Embu kusomea shahada ya ualimu (Kiswahili/Historia). Huko, hakujitokeza tu kuwa mwanafunzi mahiri, bali pia kiongozi mashuhuri. Alichaguliwa kuwa mwakilishi wa wanafunzi wa Kiswahili kwa miaka minne na akawa mwanachama hai wa Chama cha Kiswahili cha Embu (CHAKIE). Uwezo wake wa uongozi ulimwezesha kupanda ngazi kutoka Katibu Mkuu hadi Mwenyekiti wa chama hicho. Umahiri wake ulivuka mipaka ya chuo na kumfikisha katika Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili katika Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (CHAWAKAMA–KENYA), ambapo alihudumu akiwa Katibu Mtendaji na baadaye Afisa wa Nidhamu. Bi Nayaku anawashukuru sana Dkt Timothy Kinoti na Dkt Wanyama kwa mchango wao mkubwa katika kumkuza kitaaluma hadi alipohitimu mwaka wa 2023. Pia anawakumbuka Bw Oscar na Bi Florence, viongozi wa dini waliomkaribisha na kumwelekeza vyema alipokuwa chuoni. Baada ya kuhitimu, alifundisha katika Shule ya Upili ya Kongoni kwa miaka miwili kabla ya kuhamia Shule ya Upili ya Itabua. Leo, anaendelea kutekeleza ndoto yake ya kutumia Kiswahili kubadilisha maisha ya wanafunzi. "Nilitamani kuwa mwalimu wa Kiswahili ili nibadilishe mtazamo wa wanafunzi wasiopenda ushairi na sarufi, kisha niwasaidie kuwa wataalamu na viongozi bora wa baadaye," anasema kwa tabasamu. Kupitia moyo wake wa kujitolea, mapenzi kwa Kiswahili na uongozi wa kuigwa, Bi Nayaku anaendelea kuwasha taa ya matumaini kwa kizazi cha sasa na kijacho.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 20 Jul 2026 03:55:00
Walimu wapokea mafunzo ya kugundua dalili za itikadi za ugaidi mapema
WALIMU kadha katika eneo la Pwani wamepokea mafunzo kuhusu jinsi ya kukabili itikadi kali. Mafunzo hayo yanayotolewa na Wizara ya Elimu na Kituo cha Kitaifa cha Kuzuia Ugaidi (NCTC) yalihusisha walimu karibu 40 kutoka shule mbalimbali za umma ili waweze kutambua mapema na kuepusha dalili za uenezaji itikadi kali shuleni, ambazo husababisha vijana kusajiliwa katika makundi ya kigaidi. Mkuu wa Mawasiliano katika NCTC, Bw Charles Opiyo, alisema ni muhimu walimu kupokea mafunzo hayo kwa sababu wana uhusiano wa moja kwa moja na wanafunzi. "Walimu ndio walezi wa vijana hawa na wao huwa na uhusiano wa karibu zaidi na wanafunzi kuliko mtu yeyote mwingine katika mfumo wa elimu. Kutokana na kuwa vijana wadogo ndio hulengwa zaidi na makundi ya kigaidi, kuwapa walimu ujuzi huu kutawawezesha kutambua mabadiliko ya tabia mapema na huenda wakafanikiwa kuokoa maisha," akasema Bw Opiyo.
read morekenyanews.go.ke
@kna Mon, 20 Jul 2026 03:26:42
Government to spend Sh10 million to desilt Kosowe Earth dam
The National Government through National Drought Management Autbority (NDMA) will spend Sh10 million to desilt Kosowe Earth Dam in Nzaui Subcounty with a view to increase its water capacity to 30,000 cubic meters, Makueni County Drought Co-ordinator (CDC) Alice Munyao has disclosed. Munyao made the disclosure in a County Steering Group meeting held at the...
read morekenyanews.go.ke
@kna Mon, 20 Jul 2026 03:32:50
Maalim urges Northern Kenya residents to register as voters
Mandera Deputy Governor Dr. Ali Maalim has called on residents of Northern Kenya to register as voters, saying higher voter registration will strengthen the regions political influence ahead of the 2027 General Election. Speaking during an Annual General Meeting (AGM) of a school in Mandera, Dr. Maalim urged all eligible residents to take advantage of...
read morekenyanews.go.ke
@kna Mon, 20 Jul 2026 03:45:25
Nandi upscales coffee processing to maximize profits
The Nandi Coffee Farmers' Cooperative Union milling plant at Chebonet in Songhor-Soba Ward has emerged as the centerpiece of the coffee revival programme in Nandi County. It is transforming the fortunes of thousands of smallholder farmers through value addition, improved marketing and cooperative development. Standing strategically in Tinderet Sub County, the modern milling facility has...
read morekenyanews.go.ke
@kna Mon, 20 Jul 2026 03:02:16
Turkana pastoralists welcome mass livestock vaccination drive to Combat Diseases
Livestock keepers in Elelea Ward, Turkana East Sub-County, have welcomed a mass livestock vaccination and supportive treatment campaign aimed at improving animal health, controlling diseases and expanding access to domestic and international livestock markets. The 10-day exercise, being implemented through a partnership between the Turkana County Government and GENCO Livestock and Fresh Meat Export Ltd,...
read moreRight Column Content