taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 14 Sep 2026 04:55:09
Polisi wapiga kambi katika boma la mbunge kuhusiana na ghasia za Embu
MAAFISA wa polisi waliojihami kwa silaha jana walizingira makazi ya Mbunge wa Manyatta Gitonga Mukunji huko Mutunduri, siku moja baada ya vijana wenye hasira kujaribu kuvuruga mkutano wa Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki. Baadhi ya maafisa hao walikuwa wamevalia nguo za kiraia na walikuwa wamejipanga kimkakati nje ya makazi ya mbunge huyo, wakidaiwa kusubiri kumkamata kufuatia ghasia zilizozuka wakati wa mkutano wa naibu rais katika Uwanja wa Nembure Jumamosi. Maafisa hao walifika karibu saa 12 asubuhi na kuzingira makazi hayo, hali iliyozua hofu katika boma hilo. Walikaa hapo kwa saa kadhaa huku wakijaribu kubaini iwapo mbunge huyo alikuwa ndani. Kufikia adhuhuri, maafisa hao walikuwa bado hawajaondoka. Juhudi za kumpata mbunge huyo ili kutoa maoni yake hazikufaulu kwani simu yake ilikuwa imezimwa. Wakati wa ghasia za Jumamosi katika Uwanja wa Nembure, mtu mmoja alipigwa risasi na kuuawa na polisi huku magari sita yakichomwa. Vijana walikuwa wakali baada ya polisi kuwazuia kuingia kwa nguvu uwanjani, ambako Profesa Kindiki alikuwa akihutubia maafisa wa UDA. Kuzingirwa kwa makazi ya mbunge huyo kulitokea baada ya Profesa Kindiki kulaani vikali ghasia zilizovuruga mkutano wake. Alisema UDA ilijutia vifo na uharibifu uliosababishwa na watu waliowapanga vijana kuvuruga mkutano huo. "Ninalaani ghasia na kutaka vyombo vya usalama kuchukua hatua kali dhidi ya wote waliohusika kuchochea vurugu za kisiasa," akasema. Alisisitiza kuwa UDA inaunga mkono siasa zinazozingatia masuala na ushindani kuhusu ni chama gani kina rekodi bora ya maendeleo na sera nzuri kwa mustakabali wa Kenya, badala ya kulazimisha watu kuunga mkono kwa kutumia uongo, ghasia na kauli mbiu zisizo na maana. "Uongozi wa chama chetu Embu umepewa jukumu la kuthibitisha hasara na uharibifu uliotokea, na kuratibu hatua za kuhakikisha tunasimama pamoja na wote walioathirika kwa njia moja au nyingine," akasema. Gavana wa Embu Cecily Mbarire alishutumu upinzani kwa kuhisi umeshindwa kuelekea uchaguzi wa 2027. "Upinzani unajaribu kutuuzia hofu baada ya kutambua kuwa utashindwa katika uchaguzi wa 2027. Hatutanunua hofu hiyo," Bi Mbarire alisema huku akimhusisha Bw Mukunji kupanga ghasia hizo. Hata hivyo, mbunge huyo alijitetea akisema serikali inamtumia kama kafara. "Haiwezekani kila mara wanilaumu kwa kupanga ghasia. Sijahusika kwa njia yoyote," Bw Mukunji aliwaambia wanahabari mjini Embu Jumamosi. Kwa upande mwingine, wanahabari wa Embu walilaani ghasia hizo ambapo magari mawili yaliyokuwa yakitumiwa na wanahabari yalichomwa. Wanahabari hao, wakiongozwa na mwenyekiti wa Muungano wa Wanahabari Embu Brian Malila, walisema usalama wa wanahabari lazima ulindwe katika kila mkutano wa hadhara au wa kisiasa. "Muungano huu umeshtushwa na ghasia na uharibifu ulioshuhudiwa katika Uwanja wa Nembure wakati wa mkutano wa wajumbe wa UDA," akasema Bw Malila.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 14 Sep 2026 03:55:58
Ruto atuliza ODM, aahidi kudumisha falsafa ya uongozi wa Raila Odinga
RAIS William Ruto jana alionekana kupunguza mvutano wa kisiasa kati ya ODM na UDA, akisema vyama hivyo ni washirika katika Serikali Jumuishi akiahidi kulinda urithi wa kisiasa wa marehemu Raila Odinga. Akizungumza jijini Kisumu, Rais Ruto alisema atashirikiana na ODM kuhakikisha maono na ndoto ya marehemu Raila kuhusu Kenya yanatimia. "Nataka kuwahakikishia kama kiongozi wa taifa na kama mwanafunzi wa marehemu Raila Odinga kwamba tutatembea pamoja. ODM na UDA si washindani bali ni washirika katika Serikali Jumuishi," akasema Dkt Ruto. Alisema atahakikisha mchango wa Bw Odinga kwa Kenya unaendelea kukumbukwa, akimtaja aliyekuwa Waziri Mkuu kama mzalendo ambaye maono yake ya kisiasa yalikuwa si Nyanza pekee bali taifa zima. "Kwa heshima ya ndugu yangu Raila Odinga, nitafanya kuwa jukumu langu kuhakikisha urithi wake, chama chake na yale aliyoyaamini yanaendelea tunaposhirikiana kujenga taifa," akasema. Dkt Ruto alikuwa akizungumza katika Kanisa la Voice of Salvation and Healing jijini Kisumu, mwanzoni mwa ziara yake ya Nyanza. Alikuwa ameandamana na Gavana wa Kisumu Anyang' Nyong'o, Gladys Wanga (Homa Bay) , Ochilo Ayacko (Migori) na viongozi wengine wanaounga mkono serikali. Kiongozi wa ODM Oburu Oginga hakuhudhuria, kwa sababu yuko Uingereza anakoendelea kupokea matibabu. Rais alieleza uhusiano wake na Bw Odinga kuwa ulijengwa juu ya maono ya pamoja ya maendeleo, akitaja reli ya kisasa ya SGR, nyumba za gharama nafuu na ajira kama baadhi ya miradi waliyoibuni walipokuwa pamoja katika ODM. "Nasimama hapa Kisumu, jiji la ndugu yangu marehemu Raila Amolo Odinga, ambaye najua angependa kuwa hapa Kisumu leo, mtu ambaye nilishirikiana naye kutekeleza maono makubwa ya Kenya," akasema. Dkt Ruto alisema SGR ni miongoni mwa miradi ambayo Bw Odinga angejivunia kuona ikiendelea. Alisema upanuzi wa reli kutoka Narok hadi Kisumu hatimaye utatimiza mojawapo ya malengo muhimu ya maendeleo ya Bw Odinga. Gavana Wanga alisema Nyanza inashuhudia maendeleo makubwa chini ya serikali hiyo. "Leo tunashuhudia maendeleo katika eneo hili kwa kiwango ambacho hatujawahi kuona," akasema. Alikosoa kundi la Linda Mwananchi, akisema ODM imechagua kushirikiana na serikali ya Ruto ili kupata maendeleo kwa wakazi wa Nyanza. "Wapo watu ambao kazi yao pekee ni kutoka hoteli moja hadi nyingine ilhali hawana mgombea wala sera. Sisi katika serikali ya muungano mpana tuna mgombea," alisema.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 14 Sep 2026 03:17:55
Amazon pauses operations with cargo carrier after fatal Miami crash
E-commerce giant Amazon says it is suspending work with the firm that operated a cargo plane that was involved in a fatal crash in Miami this month. After the tragic incident last weekend, weve spent time supporting the investigation and reviewing some of the surrounding circumstances, and weve decided to pause our operations with 21 [...] The post Amazon pauses operations with cargo carrier after fatal Miami crash appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 14 Sep 2026 03:20:27
Carney gambles on the world's biggest investors betting on Canada
Its been a little over 18 months since Canadian Prime Minister Mark Carney said his countrys relationship with the United States, based on over a century of tight economic and military cooperation, was over. Trade talks collapsing, tit-for-tat tariffs, and Donald Trumps talk of making Canada a 51st state have all fuelled this bitter feud [...] The post Carney gambles on the worlds biggest investors betting on Canada appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 14 Sep 2026 03:23:20
Russia hits Ukrainian train shortly after Boris Johnson and top European officials leave station
A Russian drone hit a train near the Ukraine-Poland border shortly after former UK Prime Minister Boris Johnson and top European security officials had passed through. No casualties were reported after the strike at Yahodyn, which hit the trains engine. All the passengers had been evacuated, Ukrainian authorities said. Johnson and other European national security [...] The post Russia hits Ukrainian train shortly after Boris Johnson and top European officials leave station appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 14 Sep 2026 02:55:01
Kauli mbiu ya Wantam yatawala Nairobi Sifuna akitamba jijini
SENETA wa Nairobi, Edwin Sifuna na viongozi wa Linda Mwananchi jana walitikisa Jiji Kuu la Nairobi kupitia misururu ya mikutano mikubwa iliyovumisha ujumbe wa kumbandua Rais William Ruto madarakani mnamo 2027. Ziara hiyo ilitumiwa kama ratili ya kuonyesha ushawishi wa kisiasa wa Bw Sifuna jijini, huku idadi kubwa ya waliojitokeza ikiashiria kuunga mkono vuguvugu hilo. Tofauti na mikutano ya awali ya kundi hilo Homa Bay na Kisumu, ambako kulishuhudiwa vurugu, mkutano wa Nairobi ulikuwa wa amani polisi wakitoa usalama. Bw Sifuna aliandamana na Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino, Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi na Gavana wa Siaya James Orengo, Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya miongoni mwa viongozi wengine. Viongozi hao walianza ziara yao kwa kuhudhuria ibada katika Kanisa la All Saints Cathedral kabla ya kupitia masoko ya Marikiti na Gikomba hadi Uwanja wa Jacaranda. Wakiwa Gikomba, waliwataka wapiga kura kumng'oa Rais Ruto madarakani katika uchaguzi wa 2027, wakishutumu serikali yake kwa udikteta na kutowajali wananchi wa kawaida. Bw Sifuna alisema mapokezi waliyopata Nairobi ni ishara kwamba Wakenya wamekerwa na uongozi wa Kenya Kwanza. "Ruto hajafahamu ujumbe wetu. Mitaa ya mabanda Nairobi si tatizo la nyumba bali ni tatizo la mapato. SHA haifanyi kazi na ndiyo maana hata Rais bado anatoa pesa katika michango ya harambee, jambo ambalo aliahidi wakati wa kampeni kulikomesha," akasema Bw Sifuna. Seneta huyo alisema anahitaji uungwaji mkono wa wakazi wa Nairobi katika azma yake ya kuwania urais, lakini akasisitiza kuwa kumng'oa Dkt Ruto kutahitaji nguvu za pamoja za viongozi wa upinzani. Alitaja kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua, Kalonzo Musyoka wa Wiper Patriotic Front na naibu kiongozi wa Jubilee Fred Matiang'i miongoni mwa viongozi ambao wanapaswa kuungana. "Watu katika maeneo mengine ya nchi wanataka kunipeleka kwenye kazi fulani. Je, nyinyi pia mnataka niende kwenye kazi hiyo? Haitakuwa rahisi. Lazima tutembee pamoja na Kalonzo Musyoka, Rigathi Gachagua na viongozi wengine wote wa upinzani," akasema Nairobi ina maeneobunge 17, wadi 85 na zaidi ya wapiga kura milioni 2.7 waliosajiliwa. Idadi hiyo inatarajiwa kufikia milioni 3.1 katika uchaguzi wa 2027, hivyo kuifanya Nairobi kuwa muhimu kwa yeyote anayelenga kuingia Ikulu. Bw Sifuna pia alieleza sababu ya kutofautiana kwake na Kiongozi wa ODM Dkt Oburu Oginga, akisema hawezi kukubali kumuunga mkono Dkt Ruto kutokana na kile alichodai kuwa ni kuongezeka kwa gharama ya maisha. Linda Mwananchi inalenga kurithi maeneo ya uungwaji mkono ya marehemu Raila Odinga, ikidai kundi la Dkt Oginga limeharibu falsafa ya uongozi wa mwanasiasa huyo mkongwe wa upinzani. Kwa miongo kadhaa, Bw Odinga alikuwa na ushawishi mkubwa Nairobi, jiji ambalo lilikuwa nguzo muhimu ya miungano yake ya kitaifa. Katika mkutano wa jana, viongozi wa Linda Mwananchi pia walionya kuwa hawatasita kupinga matokeo ya uchaguzi katika Mahakama ya Juu iwapo yatachakachuliwa. Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya alidai Mahakama ya Juu iliwahi kutumiwa kumnyima Bw Odinga ushindi wa urais. Bw Odinga alipinga matokeo ya uchaguzi wa 2013, 2017 na 2022. Mnamo 2017, Mahakama ya Juu chini ya aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga ilibatilisha ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta na kuamuru uchaguzi mpya. Katika Uwanja wa Jacaranda, viongozi hao pia walimpigia debe Bw Babu Owino kuwania ugavana wa Nairobi. Walimshtumu Gavana Johnson Sakaja kwa kushindwa kutatua matatizo ya wakazi wa Nairobi licha ya kaunti hiyo kupokea mgao mkubwa zaidi wa fedha kutoka kwa serikali kuu. Bw Owino alisema Bw Sakaja amelemewa na majukumu na akadai kuwa makubaliano ya Sh80 bilioni kati ya kaunti na serikali kuu yalilenga kuficha uzembe wa utawala wake. "Wakazi wa Nairobi huamka kila siku na kukabili jiji chafu kwa sababu Sakaja hawezi kulisafisha jiji. Hilo litakuwa jambo la zamani chini ya uongozi wangu," akasema Bw Owino. Viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo, Seneta wa Kakamega Boni Khalwale, Seneta Crystal Asige, aliyekuwa Gavana wa Meru Kawira Mwangaza, aliyekuwa Rais wa LSK Faith Odhiambo na Wakili Laureen Mogotsi ambaye analenga kiti cha Ubunge Ikolomani Kaunti ya Kakamega.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 14 Sep 2026 02:55:38

read moreRight Column Content