taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 12 Jul 2026 03:55:21
Mwanajeshi apatikana na hatia ya kuua mkewe na wanawe kambini
BAADA ya takriban miaka saba ya kusubiri haki, Mahakama Kuu jijini Nairobi Ijumaa ilihitimisha moja ya kesi zilizotikisa taifa kwa kumpata aliyekuwa Meja wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF), Peter Mugure Mwaura, na hatia ya kumuua mkewe Joyce Syombua pamoja na watoto wao wawili. Jaji Martin Muya alisema upande wa mashtaka ulithibitisha bila shaka yoyote kwamba Mugure alipanga mauaji hayo kwa umakini, akayatekeleza ndani ya Kambi ya Jeshi la Anga ya Nanyuki, kisha akashirikiana na mtu mwingine kuficha miili ya marehemu kwa kuizika eneo la Thigithu, Kaunti ya Laikipia. Kulingana na ushahidi uliowasilishwa mahakamani, Joyce, mwenye umri wa miaka 31, alisafiri kutoka Nairobi hadi Nanyuki Oktoba 25, 2019 akiwa na watoto wake Shanice Maua, 10, na Prince Michael, 5, baada ya Mugure kuwaalika kwa kile kilichoonekana kuwa mkutano wa kifamilia. Siku iliyofuata walionekana wakiondoka kambini pamoja kabla ya kula chakula cha mchana katika Hoteli ya Kilimara Springs. Huo ndio ulikuwa mwisho wao kuonekana wakiwa hai. Jaji Muya alisema baada ya kurejea kambini, Mugure aliwaua watatu hao, akaweka miili yao kwenye mifuko maalumu ya kuhifadhia maiti na kuificha kwenye buti la gari lake kabla ya kwenda kuizika kwa siri Thigithu. Mahakama ilisema mauaji hayo hayakuwa ya ghafla. Ushahidi ulionyesha kuwa siku tatu kabla ya tukio, Mugure alikuwa ametembelea eneo hilo akiwa na afisa mwingine, hatua ambayo ilimshawishi jaji kuwa tayari alikuwa amechagua mahali pa kuficha miili kabla ya kutekeleza mpango wake. Shahidi muhimu katika kesi hiyo alikuwa Collins Pamba, aliyekiri kusaidia kuondoa miili. Alieleza kuwa alipofika nyumbani kwa Mugure alikuta mwili wa Joyce ukiwa ndani ya mfuko wa maiti huku miili ya watoto ikiwa kwenye bafu. Alisema walifunga miili kwa kamba, wakaiweka ndani ya buti la gari baada ya kuondoa tairi la akiba ili kupata nafasi zaidi, kisha wakaitoa kambini na kuizika. Ingawa alikiri kushiriki kuficha ushahidi, Pamba alifanya makubaliano na upande wa mashtaka, akakiri kosa dogo na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano gerezani. Jaji alisema ushahidi wake uliungwa mkono na ushahidi wa kisayansi. Uchunguzi wa DNA uliofanywa na Mkemia Mkuu wa Serikali ulithibitisha kuwa mabaki yaliyopatikana kaburini yalikuwa ya Joyce, Shanice na Prince Michael. Aidha, vipimo vilionyesha kwa uwezekano wa asilimia 99.9 kwamba Mugure alikuwa baba wa watoto hao wawili. Ripoti ya uchunguzi wa maiti ilionyesha Joyce alifariki kutokana na majeraha makubwa ya kupigwa, huku watoto wote wawili wakinyongwa. Mahakama pia ilibaini kuwa kulikuwa na sababu ya kifedha nyuma ya mauaji hayo. Joyce alikuwa amepata amri ya mahakama iliyomtaka Mugure kulipa Sh25,000 kila mwezi kama matunzo ya watoto, lakini alilipa mara moja pekee kabla ya kumshawishi asafiri hadi Nanyuki. Jaji Muya alitupilia mbali utetezi wa Mugure kwamba aliwaacha watoto kwa rafiki wa Joyce, akisema hakuna ushahidi uliounga mkono na kwamba familia hiyo haikuwahi kutoka kambini ikiwa hai. Kwa msingi huo, mahakama ilimpata Mugure na hatia katika mashtaka yote matatu ya mauaji, ikisema upande wa mashtaka ulithibitisha kesi yake bila shaka yoyote. Atahukumiwa Julai 14, 2026.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 12 Jul 2026 03:13:23
Body of unidentified man retrieved from Thika River
Police have launched investigations after the body of an unidentified man was retrieved from the Thika River in Kiambu County on Saturday evening. Police officers who responded to the scene found the body of an unidentified African male, believed to be about 35 years old, floating in the middle of the river. The Kiambu County [...] The post Body of unidentified man retrieved from Thika River appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 12 Jul 2026 03:19:26
US Senator Lindsey Graham dies after 'brief and sudden illness', his office says
US Republican Senator Lindsey Graham has died following a brief and sudden illness. His office has released a statement saying he died on Saturday evening. Senator Grahams family appreciates prayers at this time and asks for privacy during this incredibly difficult period. Elected to the Senate in 2002, the South Carolina politician was one of [...] The post US Senator Lindsey Graham dies after brief and sudden illness, his office says appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 12 Jul 2026 03:03:37
Boyfriend arrested after woman dies in fall from fifth floor in Kayole
Police in Nairobi's Kayole area are investigating the death of a 19-year-old woman who fell from the fifth floor of a residential apartment building following an alleged argument with her boyfriend. A team responded to the scene after a resident reported hearing a loud bang at about 5.40pm on July 11. The witness initially believed [...] The post Boyfriend arrested after woman dies in fall from fifth floor in Kayole appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 12 Jul 2026 03:06:36
Man fatally stabbed in Trans Nzoia land dispute, suspect on the run
Police in Trans Nzoia County launched a manhunt for a suspect accused of fatally stabbing a 28-year-old man during a dispute over a land boundary in Kwanza Sub-County. Witnesses said Brian Wekesa was attacked on July 11 after intervening in an altercation between his mother and their neighbour. Preliminary investigations indicate that the suspect, allegedly [...] The post Man fatally stabbed in Trans Nzoia land dispute, suspect on the run appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content