taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Fri, 28 Aug 2026 05:55:10
Hofu Ziwa Bogoria likikaribia kuungana na Ziwa Baringo
KUNA uwezekano wa Ziwa Bogoria na Ziwa Baringo kuungana hivi karibuni huku umbali kati yao ukipungua hadi chini ya kilomita tatu kutoka kilomita 20. Hali hiyo imezua hofu ya janga la kimazingira kwa kuwa maziwa hayo mawili yana sifa tofauti. Ziwa Baringo lina maji yasiyo na chumvi, huku Bogoria likiwa na maji yenye chumvi. Kwa zaidi ya muongo mmoja, wakazi wa Loboi, Baringo Kusini, wamekuwa wakishuhudia Ziwa Bogoria likipanuka na kuelekea kwenye makazi, mashamba na biashara zao. Maji hayo tayari yamemeza nyumba, kituo cha afya, maeneo ya malisho na maelfu ya ekari za mashamba. Wataalamu wanaonya kuwa iwapo maziwa hayo yataungana, mfumo wa ikolojia wa Baringo unaweza kuathirika pakubwa. Samaki, viboko, mamba na jamii zinazotegemea maji ya Baringo zinaweza kuwa miongoni mwa waathiriwa. Serikali sasa inapanga kujenga bwawa na mitaro ya kuzuia maji ya Bogoria kuelekea Baringo. Mpango huo unajumuisha ujenzi wa tuta la kilomita tano huko Sandai, bwawa katika Mto Waseges na mtaro wa takriban kilomita 40. Mtaro huo utatumika kuondoa maji mengi kutoka Baringo kuelekea Chemolingot na hatimaye Bonde la Suguta. Timu ya mashirika mbalimbali, ikiwemo Idara ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi, Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF), Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya, imekuwa ikichunguza eneo hilo. Gavana wa Baringo, Benjamin Cheboi, alisema mafuriko hayo yamezidi uwezo wa serikali ya Kaunti. "Mafuriko haya ni makubwa sana na kama serikali ya kaunti hatuwezi kuyakabili peke yetu. Ndiyo maana tumeomba usaidizi kutoka kwa serikali ya kitaifa na washirika wengine," alisema. Wakazi wanasema Bogoria ilianza kupanuka kwa kasi mwaka 2010, hali iliyoongezeka mwaka 2013. Bw Bismark Kibet alisema zaidi ya vijiji sita, kikiwemo Chepng'erechi na Kaprong'uno, vimeathirika huku Bw Jonathan Tireito akisema wakazi walidhani maji yangepungua baada ya muda. "Tulidhani yangepungua lakini hayajapungua. Yamefunika nyumba, maeneo ya malisho, mashamba na hata zahanati yetu," alisema Bw Tireito. Msimamizi Mkuu wa Hifadhi ya Bogoria James Kimaru, alisema eneo la ziwa limeongezeka kutoka takriban kilomita 34 za mraba mwaka 2013 hadi karibu kilomita 45 kwa sasa. Barabara na miundombinu mingine katika hifadhi hiyo imehamishwa, huku chemchemi za maji moto na maeneo yaliyokuwa yakivutia watalii kutazama flamingo yakizama. Profesa Simon Onywere, mtaalamu wa mipango ya mazingira na jiolojia, alisema umbali kati ya maziwa hayo ulipungua kutoka zaidi ya kilomita 20 hapo awali hadi kilomita saba mwaka 2020 na sasa ni chini ya kilomita tatu. "Kuungana kwa maziwa haya kumekaribia na ni suala la muda tu," alisema. Alisema maji mengi kutoka Mto Waseges yanaendelea kuingia Bogoria, hivyo kuongeza uwezekano wa maji yenye chumvi kuelekea Baringo. "Ikiendelea hivi, Ziwa Baringo linaweza kuwa na maji ya chumvi na kuhatarisha samaki, viboko, mamba na jamii zinazolitegemea," alisema. Serikali pia inapanga kutumia maji hayo kwa unyunyizaji, huku mpango mpana ukilenga angalau ekari 100,000 katika Baringo na Turkana. Wakati huo huo, Ziwa Baringo lenyewe limepanuka kutoka kilomita 178 za mraba hadi zaidi ya 260. Afisa Mkuu wa Hifadhi, Bw Jackson Komen, alisema nyumba, shule, biashara na hoteli zimeathirika.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 28 Aug 2026 05:16:35
Mali music star Salif Keïta cancels South African concerts over 'xenophobic violence'
The decision by world-famous Malian musician Salif Keïta to stop touring in South Africa over what he called xenophobic violence has been met with disappointment by the province hosting a festival he was due to perform at next month. South Africa has been hit by a wave of protests demanding that undocumented migrants leave the [...] The post Mali music star Salif Keïta cancels South African concerts over xenophobic violence appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 28 Aug 2026 05:27:18
Tate brothers blast US jail conditions as they seek bail in UK extradition fight
Andrew and Tristan Tate have told a Florida court they should be released from jail so they can fight extradition to the UK on charges of rape and trafficking. Wearing tan jail uniforms, the brothers maintained they did not commit the alleged crimes as they slammed conditions in US custody. Government lawyers argued that the [...] The post Tate brothers blast US jail conditions as they seek bail in UK extradition fight appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 28 Aug 2026 05:29:37
Colombia's new president approves extradition of rebel leaders to US
Colombias new right-wing president, Abelardo de la Espriella, has approved the extradition of five rebel armed group members who are wanted in the US on drug-related charges. The move is a step towards ending a plan by his left-wing predecessor Gustavo Petro who tried to end the violence that has plagued Colombia for decades by [...] The post Colombias new president approves extradition of rebel leaders to US appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 28 Aug 2026 05:31:43
Trump signs order to rename Lake Ontario as Lake America
US President Donald Trump has signed an executive order seeking to change the name of Lake Ontario to Lake America. The move comes after trade talks between the US and Canada collapsed late last week, and the US imposed new 50% tariffs on $20bn (C$28bn) worth of Canadian goods. Canada will implement dollar for dollar [...] The post Trump signs order to rename Lake Ontario as Lake America appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 28 Aug 2026 05:34:20
Decomposed body of woman recovered from River Awach in Homa Bay
Police in Rachuonyo East, Homa Bay County, are investigating an incident where the decomposing body of an unidentified woman was recovered from River Awach. The body, believed to be that of a woman aged about 32, was discovered floating in the river in the Nyawangi area on Thursday morning. Police officers visited the scene and [...] The post Decomposed body of woman recovered from River Awach in Homa Bay appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 28 Aug 2026 05:38:13
Man dies days after assault in land dispute in Nyamira
Police in Masaba North, Nyamira County, arrested two family members after a 38-year-old man was found dead inside his house days after he was allegedly assaulted following a land dispute. The body of Evans Mogere Nyakundi was discovered at his home in Nyasore Village, Nyasore Sub-location, on Thursday morning. A team of police officers visited [...] The post Man dies days after assault in land dispute in Nyamira appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Fri, 28 Aug 2026 04:55:40
Vinara wa Upinzani wakosa kutoa majibu kuhusu atakayebeba bendera 2027
KIKAO cha vinara wa upinzani kilichotarajiwa kutoa mwelekeo mpya wa kisiasa kuelekea uchaguzi wa 2027 kilimalizika Kiambu Jumatatu bila kutatua baadhi ya masuala muhimu yanayotishia juhudi za kuunda muungano mmoja wa kisiasa. Kikao hicho kilichopangwa kufanyika kwa siku mbili, Agosti 24 na 25, kilimalizika baada ya siku moja. Muungano huo unahusishwa na kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka, naibu kiongozi wa Jubilee Fred Matiang'i, kiongozi wa PLP Martha Karua, kiongozi wa Democratic Party Justin Muturi, Eugene Wamalwa wa DAP-Kenya na Peter Munya wa PNU. Viongozi hao walitia saini ahadi ya umoja na kukubaliana kumuunga mkono atakayeteuliwa kuwa mgombea wao wa urais. Hata hivyo, maswali muhimu kuhusu muungano huo bado hayajajibiwa. Yanahusu nani atakayeongoza muungano, afisi ya usimamizi itaundwaje, maamuzi yatafanywa kwa njia gani na mgombea wa urais atachaguliwa vipi. Hakukuwa na mwafaka kuhusu kubadilisha jina la Azimio wala jina jipya la muungano, ingawa Komboa Kenya Coalition bado inaonekana kuwa chaguo linalopendelewa na baadhi ya viongozi wa upinzani. "Kenya kwanza. Umoja badala ya mgawanyiko. Huduma badala ya madaraka," viongozi hao walisema katika taarifa yao. Lakini kando na picha hiyo ya umoja, tofauti za kisiasa zinaendelea kujitokeza. Bw Gachagua hakuhudhuria kikao hicho na badala yake alimtuma naibu wake Cleophas Malala kumwakilisha. Duru zilisema Bw Gachagua alikerwa na matamshi ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta katika kumbukumbu za aliyekuwa Makamu wa Rais Michael Wamalwa, ambapo alimtaja Bw Musyoka, Dkt Matiang'i na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kama baadhi ya wanasiasa wanaoweza kumkabili Rais William Ruto. Bw Gachagua, kwa mujibu wa duru hizo, hakufurahishwa na kutotajwa licha ya jukumu lake kubwa katika muungano huo. Pia kulikuwa na sintofahamu kuhusu kuhudhuria kwa Bw Musyoka. Baadhi ya watu wa karibu naye walidai alifika katika kikao hicho dakika za mwisho. Muungano huo pia bado hauna afisi inayofanya kazi kikamilifu. Duru za upinzani zilisema hakuna makubaliano kuhusu namna ya kumpata mgombea wa urais kwa sababu viongozi hao bado hawajajadili ripoti ya kiufundi iliyowasilishwa mapema mwaka huu. Hilo ni suala nyeti kwa kuwa karibu viongozi wote wakuu wa muungano huo wana matamanio ya urais au wana wafuasi wanaoamini kuwa wanafaa kumkabili Rais Ruto. Bw Gachagua alisema uteuzi wa mgombeaji urais unapaswa kufanyika baadaye. "Tutazungumzia mgombeaji wetu baada ya Krismasi. Hauwezi kusukuma mgombeaji atajwe sasa ilhali hauna idadi kubwa( ya wafuasi) na haujaanza kuhamasisha watu," alisema. Bi Karua, Bw Wamalwa na Dk Matiang'i pia wanaendelea kuwa na ushawishi katika siasa za upinzani, huku umaarufu wa Bw Sifuna ukiongeza sura mpya katika mjadala wa urithi wa kisiasa. Hata hivyo, viongozi hao wanasisitiza kuwa swali la mgombea wa urais linaweza kusubiri. "Kuchagua mgombea mmoja wa urais ndilo jambo rahisi zaidi kati ya changamoto zote tulizo nazo. Tunaweza kukutana siku moja kwa chakula cha mchana na kabla ya chakula cha jioni tukawa tayari tuna mgombeaji," alisema Bw Gachagua. Lakini changamoto za muungano hazikomei kwa uteuzi wa mgombea. Viongozi wanapaswa kukubaliana kuhusu nani atafanya maamuzi, iwapo maamuzi yatafanywa kwa makubaliano au kura, nani atasimamia afisi ya usimamizi na namna mizozo itakavyotatuliwa. Muungano huo pia unakabiliwa na ushindani wa kisiasa katika Mlima Kenya, ambako DCP ya Bw Gachagua inajaribu kujijenga kama chombo kikuu cha kisiasa. Kuanzishwa kwa People's Party of Kenya na Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro baada ya kuondoka UDA ya Rais Ruto kumeongeza ushindani kuhusu chama kitakachodhibiti kura za eneo hilo. Kwa sasa, kikao cha Windsor kimezalisha tamko la umoja, lakini bado hakijaunda mfumo wa kisiasa unaoweza kudumishwa.Jaribio kubwa litakuwa wakati viongozi hao wataanza kugawana madaraka. Nani atakuwa sura ya muungano? Nani atadhibiti shughuli zake? Ni chama kipi kitapata nafasi gani? Na nini kitatokea viongozi wakuu wakitofautiana? Muhimu zaidi, ni yupi kati ya viongozi hao atakubali kumwachia mwingine azma ya kumkabili Rais Ruto mwaka 2027?
read morestandardmedia.co.ke
@standard Fri, 28 Aug 2026 05:10:00
New uniform, no reforms: Irony of misplaced priority for service plagued by corruption and brutality
President William Ruto is expected to unveil the new uniform on Friday during the pass-out parade of 6,000 recruits at the National Police Training College in Kiganjo, Nyeri County.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Fri, 28 Aug 2026 04:17:14
KRA Clarifies New Tax Rule for Traders Amid Planned Nationwide Protests
KRA's clarification comes hours after small-scale traders across the country announced plans to stage nationwide demonstrations to protest what they described as high taxation by the government.
read moreRight Column Content