taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Thu, 27 Aug 2026 16:59:38
Ruto: Serikali lazima ipewe nafasi kutekeleza ahadi zake
RAIS William Ruto ameibua mjadala kuhusu nafasi ya Serikali iliyochaguliwa kutekeleza manifesto yake bila kuingiliwa na mahakama. Akizungumza wakati wa maadhimisho ya 16 ya Katiba ya 2010 jijini Nairobi, Rais Ruto aliuliza ni kiasi gani cha nafasi Katiba inapaswa kupatia serikali iliyochaguliwa kutekeleza mpango ambao uliifanya ishinde uchaguzi. "Serikali iliyochaguliwa inapaswa kuwa na nafasi ya kikatiba kiasi gani kutekeleza mpango ambao ilichaguliwa kuutekeleza?" Rais aliuliza. Alisema changamoto hujitokeza wakati mipango ya Serikali inapopingwa mahakamani, akitaka kuwe na tofauti kati ya mahakama kuchunguza uhalali wa hatua za Serikali na kufanya maamuzi ya sera ambayo ni jukumu la taasisi zilizochaguliwa. Hata hivyo, Rais alisema uhuru wa Mahakama haupaswi kuhojiwa. "Mahakama lazima ibaki huru kutafsiri Katiba, kulinda haki na kubatilisha hatua zisizo halali," alisema. Aliongeza kuwa Serikali inapokiuka sheria, inapaswa kuheshimu maagizo ya mahakama na kurekebisha mwenendo wake. Lakini alisema sera halali zinazotekelezwa ndani ya mamlaka ya taasisi zilizochaguliwa zinapaswa kuheshimiwa. "Kura hutoa mwelekeo. Katiba huweka mipaka. Taasisi za umma huhakikisha mambo hayo mawili yanaheshimiwa," alisema. Kauli hiyo inajiri huku baadhi ya miradi mikuu ya Kenya Kwanza ikikumbwa na changamoto za kisheria, hasa kuhusu haki za wananchi, matumizi ya fedha za umma na mipaka ya mamlaka ya Serikali. Rais alitaja huduma ya afya kwa wote, nyumba za bei nafuu, utoshelevu wa chakula, elimu na ulinzi wa kijamii kuwa nguzo za ajenda yake ya mabadiliko ya kiuchumi. Aliuliza iwapo uchunguzi wa mahakama unaweza wakati mwingine kusababisha utekelezaji wa sera halali za Serikali kucheleweshwa. "Tunawezaje kulinda uchunguzi wa mahakama bila kuzorotesha utekelezaji halali wa Serikali? Tunawezaje kuhakikisha mfumo wa kuangalia na kusawazisha mamlaka unabaki kuwa chombo cha uwajibikaji badala ya kusababisha taasisi kukwama?" aliuliza. Rais pia alizungumzia maandamano ya Gen Z ya 2024, akisema vijana walikuwa wakitumia haki zao za kikatiba na walitaka kusikilizwa. Alisema vijana walitumia haki za kuzungumza, kukusanyika, kuandamana na kuwasilisha malalamiko kwa serikali. "Ujumbe wao ulikuwa wazi: walitaka kusikilizwa. Walitaka uwajibikaji zaidi, serikali bora na nafasi ya maana katika kuamua mustakabali wa taifa lao," alisema. Kauli hiyo ni tofauti na ile aliyotoa Juni 25, 2024, alipotaja maandamano hayo kuwa "uhaini". Rais pia alikiri madai ya ukiukaji wa haki za binadamu wakati wa maandamano hayo, yakiwemo kukamatwa kiholela, watu kutoweka na matumizi ya nguvu kupita kiasi. Alisema kila madai ya ukiukaji wa haki yanayoweza kuthibitishwa yanapaswa kuchunguzwa kwa kina na kwa uwazi, na waliohusika wawajibishwe. Hata hivyo, alisisitiza kuwa haki ya kuandamana haijumuishi vurugu, uporaji au uharibifu wa mali. Naibu Rais Kithure Kindiki alisema maadhimisho hayo yalikuwa fursa ya kutafakari hatua ambazo Kenya imepiga katika kudumisha umoja na kuvumiliana. Kwa upande wake, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka alisema kutoheshimiwa kwa maagizo ya mahakama ni tishio kwa utawala wa sheria. Alisema pia ukiukaji wa haki za waandamanaji na kutotekelezwa kwa Sura ya Sita kuhusu uongozi na uadilifu kunaweza kudhoofisha Katiba. Alionya kuwa uchaguzi ukisimamiwa vibaya au matokeo yake kuibwa, suala hilo linaweza kubadilika kutoka tatizo la kisheria na kuwa la kiusalama na kibinadamu. "Hatupaswi kurudi huko tena," alisema.
read morekenyanews.go.ke
@kna Thu, 27 Aug 2026 14:50:33
Uasin Gishu strengthens Ebola preparedness amid high population movement
The Uasin Gishu County Department of Health Services has conducted a training for health workers to strengthen preparedness against and response to a possible Ebola Virus Disease (EVD) outbreak, with emphasis on surveillance, infection prevention and control, case investigation and coordination. Speaking during the training, Director of Preventive and Promotive Services Laban Kiprop said the...
read morekenyanews.go.ke
@kna Thu, 27 Aug 2026 14:56:57
Elgeyo Marakwet enrolls record 46 referees to tackle deficit
A 16-year-old boy from Kibendo Junior Secondary School is among a cohort of 46 football referees currently undergoing a four-day intensive training by the Football Kenya Federation (FKF) in Elgeyo Marakwet County. FKF Elgeyo Marakwet Branch Vice Chairperson Dominic Otieno highly praised Ezra Kipruto, the grade nine (9) student whom he discovered on social media...
read morekenyanews.go.ke
@kna Thu, 27 Aug 2026 15:01:09
Africa urged to shape communication narrative
African countries have been urged to take greater ownership of the continent's global narrative and leverage reputation, culture and strategic communication to drive economic growth and enhance international influence. Speaking during the opening of the second Africa Global Public Relations Week (AGPRW) 2026 in Nairobi, the high commissioner of the Republic of South Africa to...
read morekenyanews.go.ke
@kna Thu, 27 Aug 2026 15:07:42
Murang'a DCC cautions chiefs against arbitrating defilement cases
Murang'a East Deputy County Commissioner Charles Muriithi has warned chiefs and other community leaders against attempting to settle cases of child defilement, including sodomy, outside the justice system. The DCC stated that such matters must be reported to security agencies and prosecuted through the courts. Muriithi said government administrators, community leaders, and other persons entrusted...
read morekenyans.co.ke
@kenyans Thu, 27 Aug 2026 14:18:49
Oburu Odinga Addresses Targeting Linda Mwananchi Rallies in ODM 'Strongholds'
His remarks come weeks after violence disrupted the Linda Mwananchi rally in Homa Bay, when Nairobi Senator Edwin Sifuna led the faction in a rally in the county.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Thu, 27 Aug 2026 13:45:00
Of Sakaja and 'el chapo' promise: Chapati making machine finally lands in Nairobi
More than a year after President Rutos chapati machine pledge made him the butt of jokes, Nairobi schools have started getting chapati, from a machine making 2,000 an hour.
read morekenyanews.go.ke
@kna Thu, 27 Aug 2026 13:54:47
Kiambu steps up in preparation for El Nino
Kiambu County has rallied water companies to help clear drainage systems and reduce flood risks ahead of the anticipated El Nino rains. The move comes after Governor Kimani Wamatangi met with the managing directors of water companies in the county to work on modalities of cleaning drainage channels to avert expected floods during the heavy...
read morekenyanews.go.ke
@kna Thu, 27 Aug 2026 14:02:20
First Lady calls for urgent action to protect children from 'Tiple Threat'
Leaders have called for renewed and coordinated efforts to protect children and adolescents from the Triple Threat" of HIV infections, teenage pregnancies, and sexual and gender-based violence (SGBV). The First Lady, Rachel Ruto, warned that young people continue to bear the burden of serious encounters they did not create, particularly the challenges of the Triple...
read morekenyanews.go.ke
@kna Thu, 27 Aug 2026 14:04:08
Refugee inclusion programmes a success, needs to be sustained
Tukana Deputy Governor Dr. John Erus has stressed the need to safeguard successes realised from implementing refugee inclusion programmes over the years, lauding UNHCR and development partners for their support. Dr. Erus made the remarks when he hosted a UNHCR team, led by the Country Representative, Fatima Mohammed-Cole, at the county headquarters on Thursday. The meeting discussed...
read morekenyanews.go.ke
@kna Thu, 27 Aug 2026 14:08:14
Govt trains women's groups on livestock production in Homa Bay
Over 80 womens groups in Homa Bay County have benefited from an empowerment program rolled out by the government through the State Department for Livestock Development. The program encompasses training on modern livestock production practices, as well as financial literacy targeting women to boost sustainable livelihoods. The womens groups are among 2,300 groups identified from...
read moreRight Column Content