taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 24 Aug 2026 04:55:02
Gachagua asema hatafika mbele ya Tume ya NCIC kama alivyoamrishwa
ALIYEKUWA Naibu Rais, Rigathi Gachagua amesema hatafika mbele ya Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) Agosti 27 kama alivyoamrishwa. NCIC ilimtaka kiongozi huyo wa DCP kufika saa nane alasiri kujibu madai ya kutoa matamshi yanayoweza kuchochea chuki za kikabila katika maeneo ya Vihiga, Kisii na Meru. Tume ilionya kuwa kutofika kunaweza kusababisha hati ya kukamatwa kutolewa. Hata hivyo, mawakili wa Gachagua wameiambia NCIC kuwa mteja wao atakuwa nje ya nchi kati ya Agosti 26 na Oktoba 20 kwa safari iliyopangwa kabla ya kuitwa. Mawakili hao pia wamelalamikia kutowasilishwa kwa ushahidi kamili, wakitaka rekodi halisi za video na sauti pamoja na tafsiri rasmi za baadhi ya matamshi yaliyotolewa kwa Sheng na Gikuyu. Wanadai matamshi hayo yamechukuliwa nje ya muktadha na hayakuwa na nia ya kuchochea chuki za kikabila. NCIC bado haijajibu barua hiyo. Wafuasi wa Bw Gachagua wamekosoa wito huo wakisema tume inatumiwa kisiasa dhidi ya upinzani.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Mon, 24 Aug 2026 05:00:00
From fraud to audit obstruction: Why eCitizen empire is under scrutiny
The World Banks five-year ban on Webmasters Kenya and founder James Ayugi over alleged fraud in Somalia has raised concerns about the companys role in Kenyas eCitizen platform.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 24 Aug 2026 03:14:26
Burnham to visit Kyiv on first foreign trip and reaffirm UK support for Ukraine
Andy Burnham will mark his first foreign visit as prime minister with a trip to Kyiv on Monday to reiterate the UKs support for Ukraine and honour the countrys independence day. The prime minister will chair his first meeting of the coalition of the willing, set up by the UK and France under his predecessor, [...] The post Burnham to visit Kyiv on first foreign trip and reaffirm UK support for Ukraine appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 24 Aug 2026 03:17:49
New Tata boss to face formidable challenges
The shock resignation of Tata Sons chairman N Chandrasekaran earlier this month has left corporate Indias top job vacant. But finding his successor will be no easy task for the countrys most revered conglomerate, whose sprawling $300bn empire spans Jaguar Land Rover and Air India as well as manufacturing iPhones for Apple. Chandrasekaran resigned amid [...] The post New Tata boss to face formidable challenges appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 24 Aug 2026 03:20:18
Guinea rubbish landfill collapse kills 30
At least 30 people have been killed after a mound of rubbish at a major waste site collapsed on to nearby homes in Guineas capital Conakry, the government has said. Another 22 people were injured, including six seriously, in the citys Dar-es-Salam area. Significant resources and personnel including the military have been deployed [...] The post Guinea rubbish landfill collapse kills 30 appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 24 Aug 2026 04:11:34
Ruto says not scared, trusts the judgement of Kenyans
President William Ruto says he is confident Kenyan voters will distinguish between political rhetoric and credible plans ahead of the upcoming general elections. He also dismissed his political rivals. Ruto said in an interview he was "not scared" of his competitors and expressed confidence in the judgement of the Kenyan people. "I am not scared [...] The post Ruto says not scared, trusts the judgement of Kenyans appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 24 Aug 2026 03:55:41
Uhuru: Ruto au kiongozi yeyote hafai kujilazimisha kwa Wakenya
RAIS Mstaafu Uhuru Kenyatta na Rais William Ruto wameendeleza mvutano wao wa kisiasa huku wakitofautiana kuhusu uchaguzi wa 2027, nafasi ya upinzani na maendeleo ya serikali. Akizungumza Jumapili katika maadhimisho ya miaka 23 ya kifo cha aliyekuwa Makamu wa Rais Michael Kijana Wamalwa, Milimani, Trans Nzoia, Bw Kenyatta alisema hana nia ya kurejea mamlakani baada ya kuhudumu kama rais kwa miaka 10. Alisema Wakenya ndio wataamua atakayekuwa rais 2027 na hakuna kiongozi anayepaswa kuwalazimisha kumuunga mkono. "Wakenya wataamua wanayemtaka kuwa Rais 2027. Hakuna mtu atakayewalazimisha kumuunga mkono upande wake. Tutafute kura kwa amani na uadilifu," akasema. Bw Kenyatta pia alitetea uhuru wa kisiasa na haki ya viongozi wa upinzani kufanya mikutano ya kisiasa, akilaani vurugu zilizotokea Homa Bay wakati wa mikutano ya viongozi wa Linda Mwananchi. Aliwataja Kalonzo Musyoka, Fred Matiang'i, Edwin Sifuna na Rais Ruto kama baadhi ya viongozi ambao Wakenya wanaweza kuchagua kati yao katika uchaguzi ujao. Viongozi wa upinzani waliohudhuria hafla hiyo, akiwemo Bw Musyoka, Dkt Matiang'i, Martha Karua, Charity Ngilu na Justin Muturi, walisema wako tayari kuunda muungano wenye nguvu wa kumng'oa Ruto madarakani. Bw Musyoka alisema upinzani unafanya mipango ya kuunda muungano utakaomfanya Ruto kuwa rais wa muhula mmoja. Kwa upande wake, Dkt Ruto aliwashutumu viongozi wa upinzani kwa kutumwa kupinga miradi yote ya serikali badala ya kutoa sera mbadala. Alisema wapinzani wanapiga kelele kuhusu "must go", "one term" na "Kasongo", lakini hawana ajenda ya maendeleo. Rais alisema serikali yake inapaswa kuhukumiwa kwa miradi na huduma inazowaletea Wakenya, badala ya misingi ya ukabila. Akiongea katika Kaunti ya Taita Taveta, Rais Ruto alisema serikali imetenga Sh10 bilioni kushughulikia changamoto za ardhi na kuwaondoa maskwota Pwani. Pia alitaja ukarabati wa reli ya Voi-Taveta yenye urefu wa kilomita 129 kama mradi unaolenga kukuza biashara, utalii na ajira. Kule Kitale, Bw Kenyatta alimsifu marehemu Bw Wamalwa kama kiongozi mzalendo aliyependa maslahi ya taifa kuliko siasa za chuki. Aliyekuwa waziri Musikari Kombo alisema Bw Wamalwa alikuwa kiongozi mwadilifu aliyekufa bila utajiri wa kutatanisha. Aliyekuwa waziri Noah Wekesa alijitolea kuongoza jopo litakalosaidia upinzani kuunda muungano wa pamoja, akisema bila mgombea mmoja itakuwa vigumu kumshinda Ruto 2027.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 24 Aug 2026 02:55:29
Ruto asema walimalizana na Gachagua akimtaja kama mchochezi na mkabila
RAIS William Ruto ameweka wazi tofauti kati ya viongozi wa upinzani ambao yuko tayari kufanya nao kazi huku akiweza kuwa hawezi kushirikiana kisiasa tena na Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua. Katika mahojiano na Taifa Dijitali katika Ikulu ya Nairobi, Rais Ruto alisema yuko tayari kushirikiana na viongozi kutoka pande zote za kisiasa, lakini akasema hawezi kufanya kazi na kiongozi anayechochea ukabila, anayetoa matamshi ya kugawanya Wakenya au kuwatusi raia wengine. "Ninaamini katika demokrasia na hapa Kenya watu hufanya kazi na kila mtu. Hata hivyo, sitakuwa tayari kufanya kazi na kiongozi ambaye haamini katika umoja wa taifa." akasema Rais Ruto. Alisisitiza kuwa hawezi kushirikiana na mtu anayehusika na "ubaguzi wa kikabila" au kutumia maneno yanayolenga jamii nyingine. Pia alisema hana muda na viongozi wanaowatusi wanawake kwa kutumia lugha chafu. Kauli hizo zinaonekana kueleza kwa nini uhusiano wake wa kisiasa na Bw Gachagua ulivunjika, licha ya wawili hao kuwa washirika wakuu katika ushindi wa Kenya Kwanza mnamo 2022. Rais Ruto alitofautisha uhusiano wake na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga marehemu, akimtaja kama "mtu wa kipekee". Alisema walifanikiwa kugeuka kuwa wapinzani hadi washirika katika serikali ya mseto kwa sababu walikuwa na maono yanayofanana kuhusu mustakabali wa Kenya na walikubaliana kuzima ukabila. Kwa hivyo, ujumbe wa Rais haukuwa kwamba hataki kufanya kazi na viongozi wa upinzani, bali kwamba ushirikiano huo lazima ujengwe kwa misingi ya umoja wa kitaifa, kuheshimu jamii zote, Katiba na kuweka maslahi ya nchi mbele ya siasa za kikabila. Hapo ndipo Bw Gachagua anakuwa tofauti, kwa mtazamo wa Rais. Kiongozi wa DCP amejijenga kisiasa kupitia kujenga himaya yake Mlima Kenya na sasa ni mmoja wa viongozi wakuu wanaopinga serikali ya Rais Ruto. Bw Gachagua, pamoja na viongozi wa upinzani akiwemo Kalonzo Musyoka wa Wiper, Dkt Fred Matiang'i wa Jubilee, Martha Karua wa PLP, Justin Muturi wa DP na Eugene Wamalwa wa DAP-Kenya, wameunda muungano wa kisiasa kwa lengo la kumng'oa Rais Ruto madarakani. Mnamo 2022, Bw Gachagua alikuwa mgombea mwenza wa Rais Ruto na alichangia pakubwa kumsaidia kupata uungwaji mkono wa Kenya Kwanza katika eneo la Mlima Kenya. Hata hivyo, uhusiano wao ulizorota baada ya kuingia serikalini, hatimaye kusababisha Bw Gachagua kuondolewa katika wadhifa wa Naibu Rais kupitia bungeni mnamo Oktoba 2024. Tangu aondoke serikalini, Bw Gachagua amejitokeza kama sauti kuu ya Mlima Kenya na mpinzani mkali wa Rais Ruto. Kauli zake zimekuwa zikilenga zaidi maslahi, malalamishi na ushawishi wa kisiasa wa eneo hilo. Rais Ruto alisema aina hiyo ya siasa ndiyo hawezi kuikubali, akiwataja viongozi wanaowagawa Wakenya kuwa wasaliti na maadui na kutumia siasa za kikabila kuwadharau wengine. Pia alitetea kuondolewa kwa Bw Gachagua kama naibu rais, akisema mchakato huo ulikuwa wa kikatiba na uliotekelezwa na wabunge. "Kutimuliwa kwake kulikuwa zoezi la kikatiba lililofanywa na wabunge," akasema Rais. Mzozo kati ya wawili hao ulikuwa umejikita katika masuala ya uteuzi wa viongozi, ugavi wa rasilimali za serikali, nafasi ya Mlima Kenya serikalini na mwelekeo wa utawala. Bw Gachagua alikuwa akiishutumu serikali kwa kupuuza Mlima Kenya, huku washirika wa Rais wakimpinga kwa kuendesha ajenda ya kieneo badala ya kuzingatia maslahi ya kitaifa. Sasa, wawili hao wako pande tofauti kuelekea 2027. Bw Gachagua anajenga muungano imara wa upinzani huku akijaribu kuimarisha ushawishi wake Mlima Kenya. Kwa upande wake, Rais Ruto anajaribu kujisawiri kama kiongozi aliye tayari kufanya kazi na yeyote anayekubali ajenda ya kitaifa, huku akimtenga Bw Gachagua kwa kucheza siasa za kikabila. Rais pia amewataka wapinzani wake wawasilishe sera mbadala kwa Wakenya badala ya kutegemea matusi, kauli za chuki na uvamizi wa kisiasa. Kauli yake inaashiria kuwa nafasi ya maridhiano ya kisiasa bado i wazi, lakini kwa masharti ushirikiano wowote hautatumika kukuza migawanyiko ya kikabila.
read moreRight Column Content