kahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 18 Sep 2026 03:44:18
White House withdraws Trump's ICE nominee as Republican senator objects
The White House has withdrawn President Donald Trumps nominee to lead Immigration and Customs Enforcement (ICE) after a Republican senator joined Democrats in opposing his confirmation. Richard Schroyer was serving as a senior aide to the secretary of Homeland Security when Trump picked him to lead the immigration enforcement agency in June. The White House [...] The post White House withdraws Trumps ICE nominee as Republican senator objects appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 18 Sep 2026 03:47:22
Court issues warrant to recover nearly Sh2.9 billion from Bank of Baroda
Bank of Baroda (Kenya) Limited could have its movable assets attached and auctioned after the High Court issued a warrant to recover nearly Sh2.9 billion owed to Infinity Industrial Park Limited. The warrant, issued on September 15, 2026, directs Moran Auctioneers to attach the bank's movable and attachable property until the outstanding amount of Sh2,996,003,000 [...] The post Court issues warrant to recover nearly Sh2.9 billion from Bank of Baroda appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 18 Sep 2026 03:50:40
Court quashes IRA notice cancelling Trident, Corporate Insurance policies
The High Court has drawn a legal line around the powers of the Insurance Regulatory Authority (IRA), ruling that the regulator cannot invalidate existing insurance policies merely because an insurer has been placed under statutory management. The court found that the Commissioner of Insurance acted beyond the powers granted by the Insurance Act when the [...] The post Court quashes IRA notice cancelling Trident, Corporate Insurance policies appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 18 Sep 2026 03:53:01
Judge orders Trump to give 30 days' notice before any 'demolition' at Kennedy Center
A US federal judge ruled the Trump administration must give 30 days notice before any demolition occurs to the Kennedy Center, as President Donald Trump warned the Washington DC performing arts venue could be ripped down. The order comes after Trump was photographed onboard Air Force One looking at a poster with a headline that [...] The post Judge orders Trump to give 30 days notice before any demolition at Kennedy Center appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Fri, 18 Sep 2026 03:56:51
At least two killed, 10 evacuated after petrol tanker fire along Eldoret-Bungoma Highway
At least two people were killed and 10 evacuated to various hospitals following a petrol tanker fire near Paul Boit Secondary School along the Eldoret-Turbo road in Uasin Gishu County. Police said they collected two bodies from the scene on Friday dawn following the fire. Rift Valley police boss Samuel Ndanyi said they had collected [...] The post At least two killed, 10 evacuated after petrol tanker fire along Eldoret-Bungoma Highway appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Fri, 18 Sep 2026 03:55:41
Mwanamume amshtaki Sifuna akitaka kujua alivyotumia Sh55 alizomchangia
MWANAMUME anayedai alichangia Sh55 kwa kampeni ya Linda Mwananchi, amewasilisha kesi katika Mahakama Kuu akiomba itoe amri kumlazimisha Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna, na vuguvugu hilo kutoa hesabu ya fedha zilizochangwa kwa mradi huo wa kisiasa. Bw Alan Masakhalia anataka mahakama iamuru Bw Sifuna na viongozi wa Linda Mwananchi kutoa taarifa kamili ya michango yote iliyotumwa kupitia nambari ya Paybill 3033049 pamoja na njia nyingine zozote zilizotumika kukusanya fedha. Bw Masakhalia anasema kuwa wananchi waliochanga fedha kwa hiari yao baada ya kualikwa hadharani kufanya hivyo wana haki ya kufahamu jinsi fedha hizo zinavyohifadhiwa, kusimamiwa na kutumiwa. Aidha, anataka mahakama kubaini ni hatua gani za kisheria zinazoweza kuchukuliwa iwapo mradi huo wa kisiasa utaachwa, kubadilishwa mwelekeo, kuhamishwa kwa mtu mwingine au kufanyiwa mabadiliko makubwa yanayokwenda kinyume na maelezo yaliyotolewa wakati fedha zilipoombwa. Bw Masakhalia anasema kuwa kesi hiyo haisukumi ajenda ya kibinafsi ya kisiasa kwamba Bw Sifuna anapaswa kugombea urais. Badala yake, anasema inalenga kupata ufafanuzi kuhusu wajibu wa kisheria unaohusishwa na fedha zinazochangwa na umma kwa madhumuni mahsusi ya kisiasa. Kulingana naye, baada ya kukusanya kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa Wakenya, Bw Sifuna anaweza kuamua kutowania urais, kuunga mgombea mwingine na kumhamishia miundombinu iliyoanzishwa kupitia mradi huo, au kutumia fedha hizo kwa madhumuni tofauti na yale yaliyoelezwa kwa waliochangia. "Hali kama hiyo itazua swali muhimu iwapo wananchi waliochangia fedha zao wana maslahi ya kikatiba na kisheria yanayoweza kutekelezwa kuhusu uhifadhi, uwajibikaji na matumizi halali ya fedha pamoja na mradi wa kisiasa waliofadhili," alisema. Anataka mahakama kubaini iwapo Bw Sifuna anaweza kukusanya fedha kutoka kwa wananchi kwa ajili ya azma ya urais, kisha baadaye kuachana na azma hiyo au kumuunga mkono mgombea mwingine baada ya fedha hizo kupatikana. Bw Masakhalia alikumbusha kuwa mnamo Julai 21, 2026, Bw Sifuna alizindua hadharani Paybill nambari 3033049 na kuwaalika Wakenya kutoa michango ya kifedha kusaidia vuguvugu la Linda Mwananchi. Anadai kuwa waandalizi walitangaza hadharani kwamba, watu 9,419 walichanga takriban Sh519,144 katika siku ya kwanza ya shughuli hiyo ya kuchangisha fedha. "Ndani ya takriban saa 36, jumla ya pesa zilizoripotiwa hadharani iliongezeka hadi karibu Sh2,210,836.82," alisema. Mlalamishi huyo anasema kuwa sehemu kubwa ya michango ilikuwa ni michango midogo, mingine ikiwa ya chini hadi Sh10, jambo linaloonyesha kuwa mpango huo uliwasilishwa kama mradi wa kisiasa unaofadhiliwa na wananchi badala ya shughuli binafsi ya kifedha. Anasema kuwa alitoa mchango wake kwa hiari na kwa kutegemea maelezo yaliyotolewa hadharani kuhusu malengo ya mradi huo na sababu zilizowafanya wananchi waombwe kuchangia. "Sikutoa mchango huo kama zawadi binafsi kwa mshtakiwa wa Kwanza kwa matumizi yake mwenyewe. Wala sikuwa nikichangia harambee ya matibabu au elimu. Mchango wangu ulikuwa wazi kwa ajili ya hazina ya kampeni ya urais ya Mheshimiwa Sifuna," alisema. Bw Masakhalia aliongeza kuwa ombi hilo la kuchangisha fedha lilivutia michango kutoka kwa Wakenya wengi wengine. Baadhi ya michango hiyo, alisema, ilikusanywa kupitia ndoo zilizowekwa katika masoko ya Naitiri, Butula, Kakamega na Kabuchai zikiwa na mabango ya Bw Sifuna ambayo waliochangia waliamini yalihusishwa na kampeni ya urais. "Ninaamini kuwa uhuru wa kikatiba wa kiongozi wa kisiasa kufanya maamuzi ya kisiasa hauondoi, kwa wenyewe, wajibu wa kisheria kuhusu fedha zilizoombwa na kupokelewa kutoka kwa wananchi kwa madhumuni ya kisiasa yaliyowasilishwa hadharani," alisema. Mlalamishi huyo anataka mahakama ibaini iwapo wananchi waliochangia kifedha katika mradi huo wa kisiasa uliotangazwa hadharani walipata haki za kikatiba na kisheria zinazoweza kutekelezwa kuhusu matumizi, uwajibikaji na ufichuzi wa michango yao. Miongoni mwa maagizo anayotaka ni amri itakayomlazimisha Bw Sifuna na vuguvugu la Linda Mwananchi kutoa hesabu kamili na zilizothibitishwa za fedha zote zilizopokelewa kupitia Paybill nambari 3033049 pamoja na njia nyingine zozote. Pia anataka mahakama kuwaamuru washtakiwa kufichua matumizi yote ya fedha hizo, ikiwemo stakabadhi za malipo, kumbukumbu za malipo na stakabadhi nyingine zozote zinazothibitisha matumizi hayo.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Fri, 18 Sep 2026 03:15:00
Degree in the dock: Fresh storm over Barasa academic profile as JKUAT disowns him
Kimilili MP Didmus Barasa finds himself in the court of public opinion and deep in the throes of a credibility question, thanks to a damning revelation by the JKUAT.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Fri, 18 Sep 2026 02:55:42
Mikutano ya kisiasa yaendelea kuandamana na majonzi, 11 wakiangamia
TAKRIBAN watu 11 wamepoteza maisha katika ghasia na matukio mengine yanayohusishwa na mikutano ya kisiasa nchini tangu Februari, huku mikutano iliyokusudiwa kurai wapigakura ikigeuka kuwa hatari Kenya inapokaribia Uchaguzi Mkuu wa Agosti 10, 2027. Vifo hivyo vimetokea Nairobi, Homa Bay, Kisumu, Kisii, Vihiga, Kajiado na Embu, ambapo waathiriwa waliuawa au kujeruhiwa vibaya katika visa vya kupigwa risasi, kudungwa visu, kushambuliwa na makundi ya watu na mapigano kati ya polisi na raia. Mikutano ya kisiasa imezidi kuandamana na mapigano, uharibifu wa mali na madai ya kuwepo kwa vijana wanaotumiwa kufanya vurugu. Katika Kaunti ya Nairobi, miili mitatu ambayo haikuwa imetambuliwa awali ilipelekwa Nairobi Funeral Home na polisi baada ya mkutano wa Linda Mwananchi wa Jumapili iliyopita ulioanzia katikati ya jiji na kumalizikia Jacaranda Grounds. Familia za waathiriwa zimekanusha madai yaliyoenezwa mitandaoni kwamba waliuawa baada ya kukamatwa wakiiba simu katika Barabara ya Jogoo. "Kaka yangu, Joseph Omondi Shikuku, hajawahi kumwibia mtu yeyote. Yeye ni mtu mwema aliyekuwa akiendesha biashara ya kuuza nguo za mitumba Umoja 2. Kila kinachosemwa kwenye mitandao ya kijamii si kweli kabisa na sisi kama familia tumeumia," alisema dadake, Mercy Awino Shikhukhu. Uchunguzi wa baada ya kifo ulionyesha kuwa Omondi alifariki kutokana na majeraha kwenye fuvu la kichwa. Familia inashuku huenda alisukumwa kutoka kwenye daraja la waenda kwa miguu na watu ambao hawakutambuliwa. Brandon Ong'or, 19, pia alifariki Jumapili. Mama yake, Hellen Ong'or, alisema mwanawe hakuwahi kuiba bali alituhumiwa kuwa mwizi na mfuasi wa kundi pinzani la kisiasa. Mkuu wa Polisi wa Buruburu, Boniface Lomuk, alithibitisha kupatikana kwa miili hiyo na kusema waathiriwa walidaiwa kushambuliwa na wakazi waliowalaumu kwa kuiba simu za waliohudhuria mkutano. Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino, alilaani ghasia hizo na kusema siasa hazipaswi kuwa sababu ya watu kupoteza maisha. Vifo hivyo vilitokea siku chache baada ya watu wawili, Mike Macharia, 23, na Moses Munene, 30, kupigwa risasi wakati wa mapigano katika mkutano uliohutubiwa na Naibu Rais Kithure Kindiki katika Uwanja wa Nembure, Embu. Vijana waliokuwa nje ya uwanja walirusha mawe huku polisi wa kukabiliana na ghasia wakiwatawanya. Mapigano hayo yalidumu kwa saa kadhaa na magari sita yakachomwa moto. Kaunti ya Homa Bay pia ilirekodi vifo viwili Agosti 16 wakati wa ghasia zilizohusishwa na mkutano wa Linda Mwananchi. Konstebo Jim Richardson Onkundi, 36, alipigwa kichwani kwa jiwe, na gari lake likagonga jengo. Norine Nalangwa aligongwa na gari lililokuwa likienda kwa kasi alipokuwa akivuka barabara. Na Kaunti ya Kisumu, Dickson Oduor alifariki Julai 12 baada ya kudungwa visu wakati wa makabiliano kati ya wafuasi wa Linda Mwananchi na wanaounga mkono serikali. Katika kaunti ya Kisii, Vincent Osiemo, maarufu Mapinduzi, alifariki Julai 3 baada ya kuanguka kutoka kwa gari lililokuwa likitoroka mawe wakati wa mapigano. Katika kisa kingine huko Vihiga, mwendesha boda boda George Otobe aliuawa na kundi la watu Februari 21, huku Vincent Ayomo akipigwa risasi na kufariki Kitengela mwezi huo huo. Ghasia hizo zimeibua wasiwasi kuhusu usalama kuelekea uchaguzi wa 2027. Rais William Ruto, mwezi uliopita alikosoa washukiwa wa vurugu za kisiasa wanavyoshughulikiwa, akisema baadhi hupewa dhamana ndogo na kurejea kwenye mikutano. IEBC imesema itachukua hatua dhidi ya wanaokiuka sheria za uchaguzi. Mwenyekiti wake Erastus Ethekon, amesema tume hiyo, haina mamlaka ya kutekeleza usalama na inategemea idara za usalama. Kipindi rasmi cha kampeni kitaanza Mei 29, 2027 na kumalizika Agosti 7. Hata hivyo, miezi kadhaa kabla ya kampeni kuanza rasmi, mikutano ya kisiasa tayari imehusishwa na vifo.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 17 Sep 2026 21:59:42
Ninth woman's body found as South African police investigate string of deaths
Police in South Africa have confirmed the discovery of a ninth womans body in just two months, amid growing concern over a string of unexplained deaths east of Johannesburg. The latest victim was found half-naked and wrapped in a sheet on the side of a road in Dawn Park on Thursday morning, police said. Her [...] The post Ninth womans body found as South African police investigate string of deaths appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 17 Sep 2026 22:04:02
NCIA receives 16-classroom training block built with AFRICOM support
The National Criminal Investigations Academy (NCIA) has received a newly constructed 16-classroom training block aimed at enhancing the capacity of the National Police Service (NPS) to deliver specialised and professional criminal investigations training. The facility was constructed with support from the United States Africa Command (AFRICOM), through its Counter Drug Element (AFCE), and the Drug [...] The post NCIA receives 16-classroom training block built with AFRICOM support appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 17 Sep 2026 22:07:24
Former US Sen. Jon Kyl of Arizona, a 'workhorse' who shaped water policy, dies at 84
Former U.S. Sen. Jon Kyl, a longtime Republican lawmaker from Arizona who shaped landmark water policies in the U.S. West and guided the confirmation of Supreme Court Justice Brett Kavanaugh, has died. He was 84. Kyl died Wednesday night from a neurological disorder, said Gordon James, a communications professional who is a longtime friend of [...] The post Former US Sen. Jon Kyl of Arizona, a 'workhorse' who shaped water policy, dies at 84 appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 17 Sep 2026 22:10:52
Duale rejects Maraga coalition's interpretation of Bomas Tallying Centre
Health Cabinet Secretary Aden Duale has dismissed assertions by a coalition led by former Chief Justice David Maraga questioning the legal basis of Bomas of Kenya as the national tallying centre. Duale argued that the coalitions interpretation of the Constitution amounted to "pure sophistry" and selectively relied on constitutional provisions while disregarding the Elections Act, [...] The post Duale rejects Maraga coalitions interpretation of Bomas Tallying Centre appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 17 Sep 2026 22:13:42
MP Didmus Barasa fights back ghosts of fake against papers
Kiminini MP Didmus Wekesa Barasa Thursday hit back at allegations questioning his academic credentials. The legislator declared that he had attained a PhD and challenged his critics to undertake their own research rather than engage in what he termed political gossip. In a strongly worded response directed at an activist Stephen Mutoro and others who [...] The post MP Didmus Barasa fights back ghosts of fake against papers appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content