taifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 14 Sep 2026 15:13:51
Ukuta waangukia nyumba na kuua wanafamilia wawili baada ya mvua kubwa Mombasa
WATU wawili walifariki baada ya ukuta kuangukia nyumba katika eneo la Jomvu, Kaunti ya Mombasa, usiku wa kuamkia jana. Bi Clemence Saru, aliyepoteza mume na mtoto wake katika kisa hicho, alieleza kwamba alikuwa katika kanisa la Anointed Rock Ministry kwa maombi wakati aliposikia kishindo kikubwa. Alitoka kanisani ili kujua kilichokuwa kimetokea kisha akasikia kilio cha mumewe na watoto wao wakimwomba msaada. Dakika chache baadaye, vilio hivyo vilikoma, hali iliyothibitisha hofu yake kubwa zaidi. Ukuta wa uzio wa kampuni ya Cevas Logistics uliangukia nyumba yake katika kijiji cha Cambodia, Jomvu, na kumuua mumewe pamoja na mwanao walipokuwa wamelala majira ya saa tano na dakika 20 usiku. Mtoto wao mwingine alinusurika lakini alijeruhiwa na kupelekwa katika Hospitali ya Mikindani Medical na majirani. Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Mombasa, Bi Stella Cherono, alithibitisha kisa hicho. Janga hilo limeibua upya wasiwasi miongoni mwa wakazi wanaoishi karibu na kituo cha kuhifadhi na kusafirisha makontena (CFS), ambao wanasema sehemu za ukuta wake wa uzio zimeanguka mara kadhaa hapo awali. Wakazi walisema mvua kubwa iliyonyesha katika eneo la Pwani wiki iliyopita huenda ilidhoofisha zaidi ukuta huo. Bw Peter Ulinda, mkazi, alisema alikuwa amelala aliposikia kishindo. "Nilitoka mbio na kumwona jirani yangu akilia akiomba msaada baada ya ukuta kuangukia nyumba yake. Mama alikuwa kanisani akiomba wakati ukuta ulipoanguka juu ya nyumba yake, na kumuua mumewe pamoja na mtoto mmoja. Inasikitisha sana," alisema Bw Ulinda. Alisema majirani walikimbilia kuwaokoa waathiriwa na kuwapeleka hospitalini, lakini wawili walikuwa tayari wamefariki. "Polisi walifika saa tatu baadaye baada ya sisi kufanya kila kitu," alisema. Bw Ulinda alisema wakazi walikuwa wameibua wasiwasi kuhusu ukuta huo. "Hii ni mara ya nne kwa ukuta huu kuanguka na hatujawahi kufidiwa licha ya watu wetu kujeruhiwa. Tuna ushahidi. Katika tukio la mwisho, jirani yetu alijeruhiwa na hadi leo hajawahi kuwa kama alivyokuwa awali," alisema. Bw Ulinda pia aliachwa bila makao baada ya ukuta huo kuharibu nyumba yake. Mkazi mwingine, Bi Chenda Baya, alisema mwanawe alijeruhiwa wakati ukuta huo ulipoanguka mwaka jana lakini familia hiyo haikuwahi kufidiwa. Wasiwasi wa wakazi hao umejitokeza wakati nchi ikijiandaa kukabiliana na mvua kubwa zinazohusishwa na hali ya El Niño, hali inayozua hofu kuhusu usalama wa majengo katika maeneo ambayo tayari yanachukuliwa kuwa hatarini kukumbwa na mafuriko na hatari nyingine zinazohusiana na hali ya hewa. Viongozi wa eneo hilo wakiongozwa na Bw Beuta Mogaka waliitaka Serikali ya Kaunti ya Mombasa kukagua majengo na kuta katika kaunti nzima ili kuhakikisha zinakidhi viwango vya usalama. Bw Mogaka alisema mazingira yaliyopelekea ukuta huo kuanguka yanapaswa kuchunguzwa na hatua kuchukuliwa dhidi ya waliohusika iwapo itabainika kuwa kulikuwa na makosa. Mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu, Bw Mathias Shipeta pia alitaka uwajibikaji, akihoji iwapo kanuni za ujenzi zilifuatwa. Mzee wa kijiji, Bi Sally Wawuda, aliwataka wakazi wanaoishi karibu na kituo hicho cha mizigo kuzingatia kuhama eneo hilo kutokana na kile alichokielezea kuwa ni hatari inayokaribia. Kanisa la Anointed Rock Ministry lililokuwa karibu, pia liliathiriwa ambapo sehemu ya ukuta wa kanisa iliharibiwa.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Mon, 14 Sep 2026 14:20:23
Farmers count losses as Swine Flu outbreak kills pigs in seven counties
Pig farmers in the country are calling for urgent measures to address the swine flu outbreak that has ravaged their stocks and left farmers counting losses running into millions of shillings.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 14 Sep 2026 14:02:43
EPRA Retains September-October Fuel Prices
The Energy and Petroleum Regulatory Authority (EPRA) has retained the maximum retail prices of Super Petrol, Diesel and Kerosene for the September-October pricing cycle. The prices will remain unchanged from September 15 to October 14, 2026, meaning motorists will continue to pay Sh214.03 per litre for Super Petrol, Sh217.86 for Diesel and Sh191.38 for Kerosene [...] The post EPRA Retains September-October Fuel Prices appeared first on Kahawatungu.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Mon, 14 Sep 2026 13:34:13
Sakaja Reveals Churches Among Institutions Owing Nairobi Ksh2.7B
In education, digital systems are increasingly being used for learner and school services, while the health sector has expanded digital records and platforms for managing healthcare services.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 14 Sep 2026 13:48:56
MAONI: Yaliyompata Kindiki yanaonesha uhuni wa kisiasa hauna mipaka
GHASIA ambazo zilishuhudiwa katika mkutano wa Naibu wa Rais Prof Kithure Kindiki katika Kaunti ya Embu zinaonyesha kuwa kiongozi yeyote awe serikalini au upinzani anaweza kuathiriwa na tabia hii mbovu ambapo mara nyingi vijana hutumiwa. Kuna huu mtindo ambao umekuwa ukishuhudiwa ambapo baadhi ya wafuasi wa mirengo mbalimbali hufurahishwa uhuni unapokabili upande wasiounga kisiasa. Wakati ambapo viongozi wa Linda Mwananchi walivamiwa Homa Bay mwezi uliopita, baadhi ya wafuasi wa Serikali Jumuishi walisherehekea na hata kuwarejelea baadhi ya viongozi ambao walitajwa kuhusika. Kiongozi mmoja hata alirejelewa kama Ayatollah, jina la kiongozi wa kiimani wa Iran, linalotumiwa kuashiria utawala wa kiimla. Hii ni kutokana na upangaji wa ghasia zilizozuka Homa Bay ambazo kiongozi huyo anahusishwa nazo. Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen naye alizua kejeli kwa kushangaa kwa nini viongozi wa Linda Mwananchi walikuwa wakienda mahali ambapo walikuwa tayari wameambiwa kuna wahuni au megenge ya kisiasa. Yaliyomkumba Prof Kindiki katika Kaunti ya Embu yanastahili kukemewa kwa kinywa kipana na walioratibu au kuwatumia vijana wanastahili kuchukuliwa hatua za kisheria. Inasikitisha kuwa mtu mmoja aliaga dunia, wengine kujeruhiwa na hata magari kuteketezwa yakiwemo magari mawili ya wanahabari. Kama mkutano wa mtu wa hadhi ya naibu rais unaweza kutibuliwa, sasa itakuwaje kwa mwaniaji wa kawaida ama kiongozi wa ngazi ya chini? Hili jinamizi la uhuni halina mipaka na linaweza kuathiri kiongozi yeyote wala halifai kushabikiwa na upande mmoja linapokabili upande mwingine. Jinsi viongozi wa Linda Mwananchi walivyohisi uchungu Homa Bay huku majeruhi na kifo kikiripotiwa ndivyo pia upande wa Prof Kindiki ulihisi uchungu na kuumia baada ya mkutano wao kuingiliwa. Ingawa hivyo, tatizo katika suala hili lote ni wanasiasa na vijana na iwapo watajirekebisha na kuthamini demokrasia basi hivi visa vya ghasia havingekuwa vikiripotiwa. Kupiga kura ni haki ya kila Mkenya na ni Mkenya huyo atakayeamua jinsi atakavyotekeleza wajibu huo iwe kiongozi ameandaa mkutano eneo lake au la. Iwapo unahisi kwamba unaona humhitaji kiongozi, basi hakuna haja ya kuenda kwa mkutano wa mwanasiasa huyo na kuuvuruga. Kufanya hivyo ndiko huzua makabiliano na maafisa wa usalama ambao vifo huishia kuripotiwa pamoja na majeraha. Ndiyo, jinsi hali ilivyo vijana wengi hawana ajira ila kuhatarisha maisha kwa sababu ya mwanasiasa kisha ujeruhiwe au kuuawa si suluhu kwa tatizo hili ambalo limekuwepo miaka nenda miaka rudi. Kinachoudhi ni kwamba viongozi huwapa vijana kati ya Sh500 na Sh2,000 ili kuenda kuzua ghasia kwenye mkutano wa kiongozi pinzani ilhali fedha hizo ni ndogo na hata haziwezi kuyabadilisha maisha yao. Nguvu na haki ya kuwachagua viongozi iko katika kupiga kura wala si vurugu za kuzuia upande mmoja kuandaa mkutano wa kisiasa. Mikutano ya Linda Mwananchi Nairobi na Rais William Ruto iliyofanyika jijini Kisumu kwa amani inastahili kutumiwa kama mfano kwa wanasiasa. Viongozi wa Linda Mwananchi walihutubia mikutano mingi jijini na wakaenda zao naye Rais Ruto bado anaendelea na ziara yake Nyanza. Ushindani wa kisiasa si uadui na kila mwanasiasa anastahili kuruhusiwa auze sera yake kisha wananchi waachwe waamue.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 14 Sep 2026 12:47:08
Arsenal yatangaza haitacheka na mtu baada ya kutolewa kijasho chembamba EPL
LONDON, Uingereza: ARSENAL iliendelea na msururu wa matokeo mazuri katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) baada ya kuvuna ushindi wa 2-0 dhidi ya Sunderland Jumamosi usiku katika Uwanja wa Stadium of Light. Mlinda lango David Raya alikuwa shujaa wa Arsenal baada ya kuokoa penalti ya Enzo Le Fee dakika ya 55, kabla ya Bruno Guimaraes kufungua ukurasa wa mabao kwa Wanabunduki dakika mbili baadaye. Guimaraes, aliyekuwa ameanza kipindi cha pili baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba, alifunga kwa shuti maridadi kutoka takriban mita 18. Mkwaju huo ulilogonga mwamba kabla ya kuingia wavuni. Lilikuwa bao lake la kwanza tangu ajiunge na Arsenal na lilikuwa na umuhimu zaidi kwa sababu alifunga dhidi ya Sunderland, mahasimu wa zamani wa klabu yake ya Newcastle United. Arsenal walifunga bao la pili mwishoni mwa mchezo kupitia Bukayo Saka, aliyefunga kwa njia ya penalti baada ya kufanyiwa madhambi na Reinildo Mandava. Beki huyo wa Sunderland alionyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa uwanjani. Ushindi huo uliifanya Arsenal kufikisha ushindi wake wa sita katika mechi zote msimu huu, huku ikiwa haijapoteza mchezo wowote wa ligi. Licha ya kumiliki mpira kwa asilimia 66 katika kipindi cha kwanza, Arsenal ilitatizwa na ulinzi thabiti wa Sunderland. Kai Havertz alipoteza nafasi nzuri kabla ya shuti lake jingine kuokolewa na kipa Robin Roefs. Sunderland pia walikaribia kufunga kupitia Granit Xhaka, ambaye aliendelea kuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa wenyeji dhidi ya timu yake ya zamani. Hata hivyo, Arsenal walitumia uzoefu wao kuhakikisha wanapata pointi tatu. Kwa upande mwingine, Chelsea ilishindwa kuendeleza ushindi baada ya kulazimishiwa sare ya 2-2 na Hull City nyumbani. Morgan Rogers aliipa Chelsea uongozi dakika ya saba, lakini Mohamed Belloumi alifunga mabao mawili na kuifanya Hull kuenda mapumziko ikiwa mbele 2-1. Joao Pedro aliisawazishia Chelsea dakika ya 66 kwa shuti lililoenda moja kwa moja kwenye kona ya juu ya lango baada ya kupokea pasi kutoka kwa Cole Palmer. Chelsea walitafuta bao la ushindi katika dakika za mwisho, lakini kipa wa Hull, Konstantinos Tzolakis, alifanya kazi nzuri kuwalinda wageni. Katika mechi nyingine za Jumamosi, Liverpool ilishindwa kupata ushindi nyumbani baada ya kutoka sare ya 0-0 na Fulham, huku Tottenham Hotspur pia ikitoka sare kama hiyo dhidi ya Everton. Nottingham Forest iliishinda Aston Villa mabao 2-1, huku Ipswich Town ikiichapa Crystal Palace 3-2 katika mchezo ambao ulikuwa na mabao mengi. Nao Bournemouth na Brentford walitoka sare ya 2-2.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 14 Sep 2026 12:02:41
Beth Mooney Siblings: Meet Tom and Gabrielle Mooney
Bethany Louise Mooney, commonly known as Beth Mooney, is an Australian professional cricketer born on 14 January 1994 in Shepparton, Victoria. A left-handed batter and skilled wicket-keeper, she has represented the Australian national team across all three formats of the game since her international debut in 2016. At the domestic level, she has played for [...] The post Beth Mooney Siblings: Meet Tom and Gabrielle Mooney appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 14 Sep 2026 12:04:13
Alyssa Healy Siblings: Getting to Know Kareen Healy
Alyssa Jean Healy, born on 24 March 1990 on the Gold Coast in Queensland, Australia, is a former professional cricketer who played as a right-handed wicketkeeper-batter for the Australian women's national team. Known by the nickname Midge, she is the daughter of Greg Healy, a former Queensland squad member, and Sandy Healy. Her uncle Ian [...] The post Alyssa Healy Siblings: Getting to Know Kareen Healy appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 14 Sep 2026 12:08:30
Meta Partners with This Is Digital to Launch AI Academy Kenya
Meta has partnered with African AI accelerator This Is Digital to launch AI Academy Kenya, a flagship capacity-building programme aimed at equipping Kenyan students, developers, startups, small business owners and career professionals with practical artificial intelligence skills. The initiative, officially launched on September 11, 2026, brings together Meta's AI tools and This Is Digital's expertise [...] The post Meta Partners with This Is Digital to Launch AI Academy Kenya appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 14 Sep 2026 12:26:05
MAONI: Rais Ruto alifanya vyema kufafanua binafsi suala la wageni nchini
UFAFANUZI wa Rais William Ruto kwamba raia wa mataifa ya Afrika wako huru kuwekeza na kufanya kazi nchini Kenya kwa kuzingatia sheria inastahili. Hii ilifuatia mjadala kuhusu wafanyabiashara wa kigeni nchini uliozua taharuki kubwa miongoni mwa wananchi na wageni wanaoishi hapa. Wengine walifAsiri matamshi ya awali ya rais kuwa mwito wa kuwatenga au hata kuwafukuza wageni wanaojihusisha na biashara ndogo ndogo. Fasiri hiyo ilisababisha hofu na hata visa vya vurugu katika baadhi ya maeneo. Kwa kufafanua msimamo wake, Rais Ruto ameonyesha kwamba Kenya bado ni taifa linaloheshimu sheria, ushirikiano wa kikanda na misingi ya biashara huru. Ukweli ni kwamba Kenya imefaidika kwa miaka mingi kutokana na uwekezaji kutoka mataifa jirani na sehemu nyingine za Afrika. Wawekezaji hao wamechangia katika ukuaji wa uchumi, kuunda nafasi za ajira na kuimarisha mahusiano ya kibiashara katika ukanda huu. Hata hivyo, ufafanuzi wa rais hauondoi haja ya serikali kushughulikia malalamishi halali ya wafanyabiashara wa humu nchini. Wakenya wengi wamekuwa wakihisi kushinikizwa na ushindani kutoka kwa baadhi ya wageni wanaofanya biashara katika sekta ambazo kwa kawaida zimekuwa zikitegemewa na wananchi wa kipato cha chini. Suluhisho la changamoto hiyo halipaswi kuwa chuki au mashambulizi dhidi ya wageni, bali kuwepo kwa sera wazi na utekelezaji wa sheria kwa haki kwa wote. Ni muhimu kukumbuka kwamba Muungano wa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Comesa na Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) vinategemea ushirikiano na uhuru wa wananchi kufanya biashara na kuwekeza katika mataifa mbalimbali. Kenya haiwezi kunufaika na masoko ya mataifa mengine huku ikifunga milango kwa raia wa nchi hizo. Kwa hivyo, hatua ya Rais Ruto ya kusisitiza kuwa wageni wanaofuata sheria wanakaribishwa nchini ni ya busara. Wakati huo huo, serikali inapaswa kuhakikisha sheria za biashara, uhamiaji na ajira zinatekelezwa sawasawa bila ubaguzi. Kenya imejijengea jina kama taifa la ukarimu, biashara na uwekezaji. Sifa hizo zinapaswa kulindwa. Ufafanuzi wa rais umesaidia kupunguza mvutano uliokuwa umeanza kujitokeza na kutoa mwelekeo unaohitajika katika mjadala huu muhimu wa kitaifa.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 14 Sep 2026 10:41:39
Sh60 Million Bhang Plantation Discovered in Mwingi
Security officers have uncovered a three-acre bhang plantation estimated to be worth Sh60 million in Mwingi Central, Kitui County. The plantation was discovered along the Tana River in Kiomo Kyethani Ward following an intelligence-led operation involving officers from the National Police Service (NPS) and National Government Administration Officers (NGAO). According to police, the officers acted [...] The post Sh60 Million Bhang Plantation Discovered in Mwingi appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Mon, 14 Sep 2026 11:12:35
Jhanda ajitetea, adai ni haki yake 'kuwaosha' wafuasi wake na pesa
MBUNGE wa Nyaribari Chache, Zaheer Jhanda, ametetea tabia yake ya kutoa fedha kwa wakazi wanaohudhuria mikutano yake ya kisiasa, akisema kuwa fedha hizo ni za kuwasaidia wananchi wanaosafiri umbali mrefu kufika kwenye shughuli zake za kisiasa. Akizungumza katika mahojiano ya televisheni Alhamisi, Jhanda alisema kuwa ana uwezo wa kutoa msaada huo kutokana na mshahara wake wa ubunge pamoja na mapato anayopata kupitia biashara zake. Kulingana naye, wananchi wengi wanahitaji maendeleo lakini pia wanahitaji fedha za kujikimu katika maisha yao ya kila siku. Mbunge huyo alieleza kuwa si haki kwa wakazi kutoka maeneo mbalimbali kusafiri kwa gharama zao wenyewe, kuhudhuria mkutano na kisha kurejea nyumbani bila msaada wowote wa kifedha. Alisema fedha hizo zinakusudiwa kufidia gharama za usafiri na changamoto nyingine wanazokumbana nazo wananchi wanaposhiriki mikutano hiyo. Jhanda alihoji jinsi wazee, vijana na watu wengine kutoka sehemu za mbali wanavyoweza kuhudhuria mikutano na kurejea nyumbani bila msaada wa kifedha. Kwa mtazamo wake, hali hiyo ni kutowatendea haki wananchi wanaojitolea kushiriki shughuli za viongozi wao. Kauli zake zimeibua mjadala mpya kuhusu desturi ya wanasiasa kutoa fedha, chakula au bidhaa mbalimbali kwa wananchi wanaohudhuria mikutano na mikusanyiko ya kisiasa. Wanasiasa wengi wamekuwa wakitaja misaada hiyo kama njia ya kuwawezesha wananchi au kuwashukuru kwa ushiriki wao. Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wa masuala ya utawala bora na uchumi wamekosoa utamaduni huo wakisema vita dhidi ya umaskini haviwezi kushindwa kwa kugawa fedha au vifaa kwa lengo lakupata sifa za kisiasa. Huku maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2027 yakianza kushika kasi, mjadala kuhusu nafasi ya fedha katika uhamasishaji wa kisiasa unaendelea kugawa maoni kati ya wanaounga mkono na wanaopinga mtindo huo.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Mon, 14 Sep 2026 10:09:26
Lodwar set for historic national grid connection after independence
Lodwar town and its environs are set to receive electricity from Kenya's national power grid for the first time since independence, marking a historic milestone in the development of Turkana County. Kenya Power is nearing completion of two government-funded projects designed to connect the commercial hub to the national grid: a 66/11kV Lodwar substation and [...] The post Lodwar set for historic national grid connection after independence appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content