kenyans.co.ke
@kenyans Thu, 12 Nov 2026 04:15:02
Nairobi Water Announces Emergency Shutdown Affecting Over 40 Areas
The disruption has also affected major installations and institutions such as the Kenyatta National Hospital, Nairobi Hospital, and Forces Memorial Hospital, among others, with residents advised to use water sparingly.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 12 Nov 2026 04:02:11
Worker dies after stepping on live wire at Mombasa warehouse
A 44-year-old worker has died after being electrocuted inside a warehouse at Mitchell Cotts Company in Shimanzi, Mombasa County. The deceased, identified as Khasim Salim, was reportedly working inside the company's godown when the incident occurred on Tuesday, November 10, 2026, at around 5.20pm. According to police, Salim, was electrocuted after stepping on a bare [...] The post Worker dies after stepping on live wire at Mombasa warehouse appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 12 Nov 2026 04:05:19
Sh950,000 stolen from parked Prado in Ridgeways after bank withdrawal
Police are investigating an incident in which Sh950,000 was stolen from a vehicle parked outside a car garage in Ridgeways, Nairobi. The money belonged to a resident of Kiambu, who had withdrawn the cash from DTB Bank's TRM Mall branch on Tuesday, November 10, 2026. The man withdrew the money at around 3pm before placing [...] The post Sh950,000 stolen from parked Prado in Ridgeways after bank withdrawal appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 12 Nov 2026 04:07:50
ODPP registers 71 money laundering cases in grey list exit push
The Office of the Director of Public Prosecutions (ODPP) registered 71 money laundering cases between July and October 2026 as Kenya intensifies efforts to address deficiencies identified by the Financial Action Task Force (FATF). Director of Public Prosecutions Renson Ingonga disclosed the figures during a breakfast meeting with principals of key law enforcement agencies law [...] The post ODPP registers 71 money laundering cases in grey list exit push appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 12 Nov 2026 03:49:07
Democrat Scott Colom seals historic win in Mississippi Senate race
Democrat Scott Colom has won the US Senate race in Mississippi, delivering a shock victory for the party in a deeply conservative state that has elected Republicans for decades. Coloms victory makes him the first black person from Mississippi to be elected to the US Senate in more than 140 years. Fewer than five thousand [...] The post Democrat Scott Colom seals historic win in Mississippi Senate race appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 12 Nov 2026 03:51:58
Hegseth and team reprimanded by Army guard at solemn war memorial
US Defence Secretary Pete Hegseth and members of his team were admonished by an Army guard at the Arlington National Cemetery after he and his entourage appeared to violate the solemn war memorials rules for decorum. A video of the Veterans Day observance event shows Hegseth, his wife and senior advisers laughing and talking while [...] The post Hegseth and team reprimanded by Army guard at solemn war memorial appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 12 Nov 2026 03:54:52
Clashes erupt in Barcelona after thousands join Spain general strike
Clashes have broken out between groups of masked men and police in Barcelona after tens of thousands of people took part in Spains first general strike for 14 years, called by the countrys main unions over housing and the high cost of living. Some 120,000 people joined a demonstration in the capital Madrid and more [...] The post Clashes erupt in Barcelona after thousands join Spain general strike appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Thu, 12 Nov 2026 03:59:43
Co-op Bank's Q3 profit rises 19.6pc to Sh35.9 billion, declares higher interim dividend
Co-operative Bank of Kenya reported a 19.6 per cent growth in profit before tax to Sh35.9 billion for the nine months ended September 30, 2026, up from Sh30 billion recorded during a similar period last year. The lender's profit after tax increased by 27.2 per cent to Sh27.4 billion from Sh21.6 billion, reflecting improved earnings [...] The post Co-op Bank's Q3 profit rises 19.6pc to Sh35.9 billion, declares higher interim dividend appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Thu, 12 Nov 2026 03:55:50
Sifuna kuanza ziara ya Amerika kutafuta uungwaji wa Wakenya walio ughaibuni
KIONGOZI wa Linda Mwananchi, Seneta Edwin Sifuna anatarajiwa kuanza ziara ya wiki mbili nchini Amerika ili kuwavutia wapigakura ughaibuni na kuchangisha fedha za kugharimia azma yake ya urais. Seneta huyo wa Nairobi pamoja na wandani wake wanatarajiwa kuanza ziara hiyo Novemba 20, ambapo watakutana na Wakenya wanaoishi katika miji mbalimbali ya Amerika. Miongoni mwa viongozi wakuu wa chama hicho wanaotarajiwa kuandamana naye ni mwenyekiti na Senata wa Vihiga Godfrey Osotsi, Mwekahazina Richard Onyonka na naibu kiongozi wa chama Faith Odhiambo. Mkuu wa mawasiliano wa Linda Mwananchi Pauline Njoroge aliiambia Taifa Leo kuwa chama hicho kilikuwa kikikamilisha ratiba ya ziara kabla ya kuitangaza rasmi kwa umma. "Kuna mambo mengi yanayohusika na tukikamilisha maandalizi, tutatangaza ratiba kamili pamoja na maelezo yote," akasema. Hata hivyo, ratiba iliyochapishwa katika mtandao wa chama hicho inaonyesha kuwa Bw Sifuna atazuru AllenTown kuanzia Novemba 20 hadi 22. Kisha atasafiri hadi sehemu ya jiji kuu Washington (DMV) kati ya Novemba 23 na 24, Dallas mnamo Novemba 27 na 28, Houston mnamo Novemba 29 na 30, kabla ya kuhitimisha ziara yake kwa kutembelea Seattle na California kati ya Desemba 1 na 4. Ziara hiyo inajiri miezi kadhaa baada ya Kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua kuzuru miji kadhaa Amerika kati ya Agosti 26 na Oktoba 20 katika juhudi za kuwafikia Wakenya wanaoishi ughaibuni. Ratiba ya Bw Gachagua ilijumuisha Oregon, Kansas, Dallas, Boston, Massachusetts na Spokane katika jimbo la Washington. Seneta wa Kakamega, Dkt Boni Khalwale alisema ziara hiyo itampa Bw Sifuna fursa ya kukutana na Wakenya wanaoishi ughaibuni, kuwaeleza ajenda yake ya kisiasa na kutangaza azma yake uongozi wa nchi. "Ziara hii ni nzuri kwani itamsaidia kiongozi wetu wa chama kuungana na Wakenya wanaoishi ughaibuni, kuwaeleza mipango yake kwa taifa na pia kutangaza azma yake ya kuwania urais. Kumbuka Amerika ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya Wakenya, hivyo hii ni fursa ya kuwafikia na kuwaeleza mipango yake kwa Kenya," akasema Dkt Khalwale. Seneta huyo, ambaye ni mmoja wa washirika wa karibu wa kisiasa wa Bw Sifuna, alisema kiongozi huyo wa Linda Mwananchi anazidi kupata umaarufu miongoni mwa vijana kutoka mirengo mbalimbali ya kisiasa. Aliongeza kuwa kukutana na Wakenya na wanaoishi ughaibuni kutawapa fursa ya kueleza changamoto zao na kutoa mapendekezo kuhusu uongozi na maendeleo ya nchi. "Kama kiongozi, ni lazima usikilize wananchi na kutekeleza matakwa yao. Hii itakuwa kampeni ambayo Wakenya wanaoishi ughaibuni watapata jukwaa la kueleza masuala yanayowakabili," akasema. Dkt Khalwale, ambaye ni mbunge wa zamani wa Ikolomani, alifananisha azma ya Bw Sifuna ya kuwania urais na ile ya aliyekuwa Rais wa Amerika Barack Obama, miaka ya 47. Bw Sifuna atakuwa na umri wa miaka 45 iwapo atachaguliwa kuwa Rais katika uchaguzi mkuu wa 2027. "Wale ambao wamekuwa wakimwambia Sifuna asubiri kwa sababu bado ni kijana wanapaswa kujua kuwa Obama pia alichukua uongozi wa Amerika akiwa miaka ya 40. Jambo muhimu ni kile unachowafanyia Wakenya na namna unavyoboresha maisha yao," akasema. Akiwa Amerika Bw Gachagua alikiri kuongezeka kwa ushawishi wa kisiasa wa Bw Sifuna, baada ya kutangaza kuwa yuko tayari kumuunga mkono iwapo atabainika kuwa mgombea anayefaa zaidi kumshinda Rais William Ruto katika uchaguzi wa 2027. "Hakuna tatizo kwa sababu hata Riggy G anaweza kuwa naibu wa Sifuna. Kuna ubaya gani?" akauliza alipokuwa akiwahutubia Wakenya mjini Spokane, katika jimbo la Washington. "Ikiwa tutafanya hesabu na kubaini kuwa mtu anayefaa zaidi kumwondoa Rais Ruto mamlakani mapema ni Edwin Sifuna, basi iwe hivyo. Tutaunda timu ya uongozi ambayo mtaipenda. Tutaunganisha nguvu za vijana na uzoefu," akaongeza Bw Gachagua. Hata hivyo, mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Javas Bigambo alisema kufanya kampeni Amerika hakumaanishi kuwa wagombea urais watarejea na kiasi kikubwa cha fedha. Alisema huenda baadhi ya watu wachache matajiri wakachangia fedha nyingi, hasa iwapo wagombea wana marafiki na mitandao ya watu wenye ushawishi nchini humo, kama alivyokuwa nao aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga. "Kuna wale wanaoalikwa na makundi ya kisiasa pamoja na Wakenya wanaoishi ughaibuni. Mtu mmoja au wawili wanaweza kuwaunganisha na watu wenye uwezo wa kuchangia fedha. Mara nyingi huwa hawakutani na wafadhili wakuu wa vyama vya Republican na Democrat kwa sababu hawana maslahi makubwa katika siasa za Kenya," akasema, Bigambo. Kwa mujibu wa sajili ya wapiga kura ya Tume ya Uchaguzi (IEBC) ya mwaka 2022, Kenya ilikuwa na wapigakura 2,959 waliosajiliwa ughaibuni, ambapo 590 walikuwa Wakenya wanaoishi Amerika.
read morestandardmedia.co.ke
@standard Thu, 12 Nov 2026 03:30:00
Bare-knuckled: Ruto-Gachagua toxicity turns into accusations of extortion, murder, tribal jibes and body shaming
President Ruto and his former deputy Rigathi Gachagua have renewed a bitter public war of words, drawing condemnation from the clergy who warn that the inflammatory rhetoric threatens peace.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Thu, 12 Nov 2026 03:25:12
Hata mkiungana muwe 1,000 nitawashinda nyote, Ruto amjibu Uhuru
RAIS William Ruto amemshambulia mtangulizi wake Uhuru Kenyatta, akimtaja kama dalali wa kisiasa anayepoteza muda kuwaunganisha viongozi wa upinzani badala ya kushughulikia changamoto zinazowakabili Wakenya. Ruto alisema Uhuru ameachana wajibu wake kama kiongozi wa kitaifa na sasa anashughulika kutafuta mgombea mmoja wa upinzani kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Alikuwa akizungumza jana alipohitimisha ziara yake ya siku nne katika eneo la Gusii, iliyohusisha kaunti za Kisii na Nyamira. "Nimesikia kuhusu huyo sponza, rafiki yangu. Je, hamumjui? Ameacha kuwa kiongozi wa kitaifa na sasa amekuwa dalali. Anajaribu kuunganisha huyu na yule. Namwambia aharakishe kazi yake ya udalali na atafute mtu anayemtafuta," alisema Ruto. Rais alidhihaki juhudi za upinzani kupata mgombea wa pamoja, akisema viongozi hao wamekuwa wakizunguka hoteli, nyumba za watu na mazishi kwa mwaka mmoja na nusu bila kufikia makubaliano. Alisema ikiwa viongozi hao wanachukua muda mrefu kukubaliana kuhusu mgombea mmoja, itakuwa vigumu kwao kupanga masuala ya nchi yenye watu milioni 60. "Wamekuwa kwa mwaka mmoja na nusu wakimtaja huyu au yule kuwa mgombea wao. Wanazunguka kutoka hoteli moja hadi nyingine na nyumba moja hadi nyingine. Ikiwa wanachukua muda wote huo kupata mgombea mmoja, watawezaje kupanga mambo ya watu milioni 60?" aliuliza. Aliongeza kuwa yuko tayari kukabiliana na upinzani bila kujali iwapo utawasilisha mgombea mmoja, kumi au hata 1,000. Ruto pia alikosoa madai ya Uhuru kwamba amekuwa akizungumza na wananchi wa kawaida anapokwenda kununua uji, akisema Rais mstaafu huyo anapaswa kutafuta maoni kutoka kwa wakulima, wafanyabiashara na walimu badala ya watu anaokutana nao kwenye baa. Alimshauri Uhuru kutafuta ushauri kutoka kwa watu anaowataja kuwa wenye busara na wanaofanya kazi, akidai kuwa taarifa anazopata kutoka kwa watu wanaokunywa pombe hazionyeshi hali halisi ya nchi. Uhuru alikuwa amezungumza katika ibada ya kumuaga binamu yake Beatrice Wambui Muturi katika Kanisa la PCEA Nairobi West, Lang'ata. Aliwataka viongozi wa upinzani kuweka kando tofauti zao na kuungana kuelekea uchaguzi wa 2027. Ibada hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa upinzani akiwemo aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka na Eugene Wamalwa wa DAP-K. Ruto pia alimshambulia Gachagua, akimuonya dhidi ya kile alichokitaja kuwa siasa za uchochezi na ukabila. Alimtaja kama kiongozi aliyeshindwa katika nyadhifa mbalimbali, ikiwemo kazi ya utumishi wa umma, ubunge na unaibu wa rais. Alidai kuwa Gachagua hana mamlaka ya kimaadili ya kuwahubiria wengine, huku akimlaumu kwa kuhusika na matumizi mabaya ya chakula cha msaada alipokuwa afisa wa utawala katika miaka ya 1980 na 1990. "Wakenya hawana muda na watu wanaochochea chuki, ubaguzi na ukabila," alisema. Rais aliongeza kuwa hataruhusu Gachagua kusababisha machafuko au kugawanya wananchi kwa misingi ya makabila kabla ya uchaguzi. Katika ziara hiyo ya Gusii, Ruto alizindua ujenzi wa barabara ya Keroka-Ibacho-Kiamokama, mradi wa kusambaza umeme katika maeneo ya mashambani na chuo cha mafunzo ya matibabu (KMTC)_ 0Ibeno.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Thu, 12 Nov 2026 02:55:40
Uhuru ashauri vigogo kuweka tamaa kando na kusimamisha mwaniaji mmoja
RAIS Mstaafu Uhuru Kenyatta amewataka viongozi wa upinzani kuweka kando tamaa zao za kibinafsi za kuwania urais na kuungana nyuma ya mgombea mmoja, akisema Wakenya tayari wameamua kumwondoa Rais William Ruto mamlakani katika uchaguzi mkuu wa Agosti 2027. Bw Uhuru alisema changamoto kubwa inayokabili upinzani si ukosefu wa wananchi wanaotaka mabadiliko, bali viongozi wake kukosa kukubaliana kuhusu mwelekeo mmoja wa kisiasa. Alionya kuwa ushindani wa viongozi kutaka kuwania urais unaweza kuvuruga juhudi za kuunda muungano ulio na msimamo mmoja dhidi ya utawala wa Kenya Kwanza. Alitaja kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka, aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na kiongozi wa DAP-K Eugene Wamalwa, akiwakumbusha kuwa kiti cha urais kinaweza kushikiliwa na mtu mmoja pekee kwa wakati mmoja. "Tunapaswa kuwa na wasiwasi kuhusu mustakabali wa nchi yetu, wala si yaliyopita. Ninawaambia ndugu zangu Kalonzo, Rigathi Gachagua na Eugene kwamba mtu mmoja pekee ndiye anaweza kukalia kiti hicho kwa wakati mmoja," alisema. Alikuwa akizungumza jana wakati wa ibada ya mazishi ya binamu yake Beatrice Wambui Muturi katika Kanisa la PCEA Nairobi West, Lang'ata, Nairobi. Bw Kenyatta alisema mazungumzo yake na Wakenya wa kawaida, hata anapokwenda "kununua uji", yamemshawishi kuwa wananchi wanataka mabadiliko ya uongozi. Hata hivyo, alisema wanataka kwanza kuona viongozi wa upinzani wakimaliza tofauti zao. "Ingawa nimestaafu, masikio yangu hayajafungwa. Ninazungumza na watu na kuwasikiliza. Ninapokwenda kununua uji na kuwauliza wanataka nini, kuna jambo moja wanalosisitiza: watu wameamua. Wako tayari wakati huu, lakini tatizo pekee ni umoja wa upinzani," alisema. Aliwataka viongozi hao kutimiza matarajio ya wananchi kwa kuonyesha umoja na kuweka maslahi ya nchi mbele ya matarajio yao binafsi. Kauli yake inaongeza uzito katika mazungumzo yanayoendelea kuhusu kuunda muungano wa upinzani kabla ya uchaguzi wa 2027, huku suala la mgombea mmoja wa urais likiwa miongoni mwa masuala yanayohitaji makubaliano. Upinzani unaojumuisha DCP ya Gachagua, Wiper ya Kalonzo, DAP-K ya Wamalwa, vuguvugu la Linda Mwananchi linaloongozwa na Edwin Sifuna, Jubilee ya Fred Matiang'i na vyama vingine vinavyohusishwa na Martha Karua, Justin Muturi na aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga, bado unakabiliwa na changamoto ya kuunganisha maslahi ya kila mmoja. Ingawa viongozi wamekuwa wakiahidi kumuunga mkono atakayeteuliwa kuwa mgombea wa urais, bado kuna maswali kuhusu nani atakayeongoza muungano huo, utaratibu wa kufanya maamuzi na namna ya kumpata mgombea wa pamoja. Uhuru pia aligusia uhusiano wake na Gachagua, ambaye amekuwa akitumia makazi yake ya Wamunyoro, Kaunti ya Nyeri, kama kitovu cha shughuli zake za kisiasa na mikutano na washirika wake. Alisema atatembelea Wamunyoro wakati ufaao, akisisitiza kuwa anataka amani na umoja licha ya kujiondoa katika siasa za uchaguzi. "Nimepoteza mtu aliyekuwa muhimu sana katika kukua kwangu. Sina mengi ya kusema kwa sababu nimestaafu. Hata hivyo, nataka kusema nitakuja Wamunyoro wakati ufaao. Tunataka amani na umoja," alisema. Kwa upande wake, Gachagua, alisema jamii ya Mlima Kenya imeamua kutoruhusu tena migawanyiko ya kisiasa kuidhoofisha. Alikiri kuwa alifanya makosa wakati wa uchaguzi wa 2022 na kusema amejifunza kutokana na yaliyotokea. "Tumeamua kuwa hatutamruhusu mtu yeyote kugawanya jamii yetu. Nilifanya kosa kubwa mwaka 2022 na nimejifunza kwa njia ngumu. Ninafurahi kwamba sasa tuko pamoja kama jamii na tutaendelea mbele pamoja," alisema. Kalonzo, aliyezungumza katika hafla hiyo, aliunga mkono haki ya Uhuru kutoa maoni yake kuhusu mustakabali wa nchi. Kwingineko, Rais Ruto alimshambulia mtangulizi wake Uhuru, akimtaja kama dalali wa kisiasa anayepoteza muda kwa kujaribu kuwaunganisha viongozi wa upinzani badala ya kushughulikia changamoto zinazowakabili Wakenya. Ruto alisema Uhuru ameachana wajibu wake kama kiongozi wa kitaifa na sasa anashughulika kutafuta mgombea mmoja wa upinzani kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027. Alikuwa akizungumza jana alipohitimisha ziara yake ya siku nne katika eneo la Gusii, iliyohusisha kaunti za Kisii na Nyamira. "Nimesikia kuhusu huyo sponsa, rafiki yangu. Je, hamumjui? Ameacha kuwa kiongozi wa kitaifa na sasa amekuwa dalali. Anajaribu kuunganisha huyu na yule. Namwambia aharakishe kazi yake ya udalali na atafute mtu anayemtafuta," alisema Ruto.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Wed, 11 Nov 2026 21:54:38
Who is Alice Huang, the Chinese businesswoman tied to Nvidia's CEO?
Alice Huang built a career in Chinese finance before emerging in a very different arena: the global race for artificial-intelligence chips. Known also as Huang Le, the Chinese businesswoman held senior roles at a Shanghai investment firm before becoming the controlling shareholder of Singapore-based cloud-computing company Megaspeed International, according to more than 30 publicly available [...] The post Who is Alice Huang, the Chinese businesswoman tied to Nvidias CEO? appeared first on Kahawatungu.
read moreRight Column Content