kahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 13 Sep 2026 07:42:46
Man killed after attempting to snatch cop's firearm outside GSU college in Embakasi
A man was shot dead after allegedly attempting to snatch a firearm from police officers at the main gate of the National Police B Campus in Embakasi, Nairobi, on Saturday morning. According to police, the incident occurred at Gate D at approximately 6:57 a.m. when an unidentified adult male approached officers manning the entrance and [...] The post Man killed after attempting to snatch cops firearm outside GSU college in Embakasi appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 13 Sep 2026 07:55:11
Ng'ombe, mbuzi na kondoo kupewa vitambulisho kudhibiti wizi
SERIKALI imeanza kutekeleza mfumo mpya wa kitaifa wa kutambua na kufuatilia mifugo unaolenga kudhibiti wizi na kuboresha biashara ya bidhaa za mifugo nchini. Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, Mutahi Kagwe, alisema kila ng'ombe nchini atakuwa na alama maalum ya manjano ya mfumo wa Animal Identification and Traceability (ANITRAC) itakayowezesha kufuatilia alikotoka, afya yake na mahali alikopitia. Akizungumza katika Maonesho ya Kilimo ya Kanda ya Kati ya Kenya mjini Nyeri, Bw Kagwe alisema mifugo itakayopatikana bila vitambulisho hivyo itazua maswali kuhusu usalama. "Katika siku zijazo kila ng'ombe atakuwa na alama maalum. Mtu akipatikana na ng'ombe asiye na alama hiyo atalazimika kueleza alikotoka," alisema. Mfumo huo pia unatarajiwa kusaidia serikali kufuatilia magonjwa ya mifugo na kuimarisha usalama wa chakula huku ukisaidia Kenya kutimiza masharti ya kimataifa ya masoko ya nje. Waziri huyo pia alitangaza hatua za kupunguza gharama ya uzalishaji kwa wafugaji wa maziwa kupitia ruzuku ya mbegu za kisasa upatikanaji wa malisho bora na vifaa vya kupooza maziwa. Aidha, alisema mageuzi katika sekta ya kahawa yanaendelea kutekelezwa kufuatia kuanza kazi kwa Bodi ya Kahawa ya Kenya. Kwa upande wa chai, ushuru mpya wa asilimia 0.8 kwa mauzo ya nje utasaidia kuboresha miundombinu na kuongeza thamani ya bidhaa hiyo. Hata hivyo, aliwaonya wakulima dhidi ya kuvuna mazao kabla ya kukomaa, akisema hali hiyo huharibu sifa ya Kenya katika masoko ya kimataifa na kupunguza mapato ya wakulima.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 13 Sep 2026 07:13:34
Police deployed in Nairobi CBD ahead of Linda Mwananchi rally
Anti-riot police officers were Sunday deployed across major streets in Nairobi's Central Business District (CBD) ahead of a planned Linda Mwananchi mobilisation rally. The officers were seen patrolling the city on foot and in police vehicles, with authorities saying the deployment was intended to prevent criminal activity, including attacks on businesses and looting. However, organisers [...] The post Police deployed in Nairobi CBD ahead of Linda Mwananchi rally appeared first on Kahawatungu.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 13 Sep 2026 06:39:44
Man drowns in sewage trench along Haile Selassie Avenue in Nairobi
A 37-year-old man drowned after falling into a sewage trench near Equity Bank along Haile Selassie Avenue in Nairobi. The incident was reported to Nairobi Railways Police Station. Police established that the deceased, identified as Isaac Kiplagat, had fallen into the trench and drowned. The body was subsequently moved to Nairobi Funeral Home, where it [...] The post Man drowns in sewage trench along Haile Selassie Avenue in Nairobi appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 13 Sep 2026 06:55:12
Gachagua afichua sababu kutotaja mwaniaji urais wa upinzani mapema
KINARA wa chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP), Rigathi Gachagua, amesema upinzani umeamua kuchelewesha kuunda afisi ya pamoja kwa sababu ya hofu ya kuingiliwa na serikali, huku akisisitiza kuwa lengo lao kuu ni kumng'oa Rais William Ruto mamlakani katika uchaguzi mkuu mwaka ujao. Akizungumza Ijumaa jioni mbele ya wafuasi wake mjini Portland, Oregon, Amerika anakozuru, Bw Gachagua alidai Rais William Ruto atashindwa kwa tofauti ya kura zaidi ya milioni saba. Alisema anatarajia kupokea simu kutoka kwa Rais Ruto usiku wa manane wa Agosti 10, 2027, akikubali kushindwa na kuomba kulindwa baada ya kuondoka madarakani. Gachagua pia alidai Rais amepenyeza watu wake ndani ya baadhi ya makundi ya upinzani ili kupata taarifa za siri kuhusu mikakati yao. "Majuzi tulikuwa katika kikao cha mkakati katika hoteli moja Nairobi. Kulikuwa na mmoja wa viongozi wa upinzani aliyekuwa amejiunga na muungano wetu akiwa na wanawake wawili. Hatukuwa hata tumemaliza kikao nilipoona taarifa ya kile tulichokuwa tunajadili ikiibuka kwenye simu yangu," alisema. Hata hivyo, alionya kuwa serikali ya upinzani haitawalinda wale watakaopatikana na makosa ya ufisadi, mauaji au utekaji nyara wa vijana waliokuwa wakishiriki maandamano. "Nataka iwe wazi kuwa serikali ya upinzani haitawalinda wezi wa rasilimali za umma, wauaji au waliotekeleza utekaji nyara. Wote watawajibishwa kwa mujibu wa sheria," alisema. Gachagua pia alikanusha madai kwamba anapanga kukutana na Rais Ruto wakati wa ziara zao nchini Amerika. "Puuzeni propaganda zinazoenezwa kwamba nina nia ya kukutana na Rais Ruto hapa Amerika. Hilo halipo kabisa katika mipango yangu," alisema. Alieleza sababu ya kucheleweshwa kwa sekretarieti ya pamoja ya upinzani, Gachagua akisema ni rahisi kuvurugwa na serikali.
read morekahawatungu.com
@kahawatungu Sun, 13 Sep 2026 06:08:29
Former President Moi's Physician David Silverstein Dies
Dr David Silverstein, the long-serving personal physician to Kenya's late retired President Daniel arap Moi, has died. The Moi family confirmed his death, mourning him as a compassionate doctor who left a lasting impression on those he treated. In a statement, KANU chairman Gideon Moi described Dr Silverstein as a physician who treated his father [...] The post Former President Moi's Physician David Silverstein Dies appeared first on Kahawatungu.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 13 Sep 2026 05:55:40
Polisi wazima jaribio la kutibua mkutano wa Profesa Kindiki
POLISI wa kutuliza ghasia Jumamosi walizuia jaribio la kundi la vijana kuvuruga mkutano wa kisiasa wa Naibu Rais Kithure Kindiki katika Uwanja wa Nembure, Kaunti ya Embu. Maafisa hao walirusha gesi ya kutoa machozi na kufyatua risasi hewani kuwatawanya vijana hao waliokuwa wakipiga kelele na kurusha mawe. Vurugu hizo zilianza wakati Profesa Kindiki alipokuwa akihutubia maafisa wa chama cha UDA kutoka vituo mbalimbali vya kupigia kura katika kaunti hiyo. Alipokuwa akizungumza, vijana waliokuwa nje ya uwanja huo walianza kupaza sauti na kurusha mawe kwa lengo la kuvuruga mkutano huo. Wakati mmoja walijaribu kuvamia uwanja huo lakini walizuiwa na maafisa wa usalama. Hatimaye polisi waliwarushia gesi ya kutoa machozi, hatua iliyozua mapambano ya kukimbizana kati yao na vijana hao yaliyodumu kwa saa kadhaa nje ya uwanja huku Kindiki akiendelea na hotuba yake bila kusitisha mkutano. Baadaye, vijana hao walitawanyika lakini walikusanyika tena baada ya mkutano kumalizika na kuzua vurugu katika eneo hilo. Walivamia barabara iliyo karibu, kuwashambulia madereva na wakazi huku wakichoma magari kadhaa, jambo lililozua hofu. Miongoni mwa magari yaliyochomwa moto ni la mwanahabari wa eneo hilo. Mfuasi mmoja wa UDA pia alijeruhiwa usoni baada ya kupigwa na jiwe na kupatiwa huduma ya kwanza.
read morekenyans.co.ke
@kenyans Sun, 13 Sep 2026 05:15:47
Police Boss Explains Ban on Large Political Rallies in Nairobi CBD
The announcement comes hours ahead of the Linda Mwnanchi rally in Nairobi, with the movement expected to tour areas in Nairobi before a mega rally at the Jacaranda grounds.
read moretaifaleo.nation.co.ke
@taifaleo Sun, 13 Sep 2026 04:55:40
Ziara ya Ruto Nyanza mtihani mkubwa baada ya kifo cha Raila
ZIARA ya siku tano ya Rais William Ruto katika eneo la Nyanza kuanzia Jumapili, Septemba 13, imeibua mjadala mpana wa kisiasa huku wachambuzi wakisema ni zaidi ya ziara ya kawaida ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo. Ziara hiyo inafanyika katika kipindi nyeti kisiasa baada ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, jambo lililoacha pengo kubwa la uongozi katika eneo ambalo kwa miongo kadhaa lilikuwa ngome yake ya kisiasa. Rais Ruto anatarajiwa kuzuru kaunti za Kisumu, Siaya, Migori na Homa Bay akizindua na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo barabara, maji na usafi wa mazingira, masoko, hospitali, nyumba za gharama nafuu, viwanja vya michezo pamoja na miundombinu mingine ya umma. Mbali na kuhudhuria ibada ya kanisa Kisumu, Rais pia anatarajiwa kukutana na viongozi mbalimbali na hata kuendesha kikao cha Baraza la Mawaziri katika Ikulu Ndogo ya Kisumu. Kwa serikali ambayo imekuwa ikitumia maendeleo kama silaha yake kuu ya kisiasa, ziara hiyo ni nafasi muhimu ya kuwashawishi wakazi wa eneo ambalo kwa muda mrefu lilimuunga mkono Raila Odinga na chama cha ODM. Hata hivyo, umuhimu wa kisiasa wa ziara hiyo unazidi miradi inayozinduliwa. Kifo cha Raila Odinga mnamo Oktoba 15, 2025, kiliondoa mwanasiasa aliyekuwa na ushawishi mkubwa zaidi Nyanza na kuacha swali kubwa kuhusu ni nani atakayerithi mtandao wake wa kisiasa na kura zake. Katika mahojiano maalum yaliyopita, Rais Ruto alikiri kuwa uwepo wa Raila ungeathiri kwa kiasi kikubwa mazingira ya kisiasa ya sasa. Alimtaja Raila kama mwanasiasa wa kipekee aliyekuwa na ujasiri, maono na uelewa wa masuala ya taifa. Vilevile alisema yeye na Raila walikuwa na sera walizokubaliana, ikiwemo mpango wa nyumba za gharama nafuu na huduma ya afya kwa wote. Ruto sasa anaonekana kutaka kuwashawishi wakazi wa Nyanza kuwa ushirikiano kati ya serikali yake na viongozi waliokuwa karibu na Raila unaweza kuendelea kunufaisha eneo hilo. Tayari baadhi ya viongozi wa zamani wa ODM wanahudumu katika serikali yake, wakiwemo Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi, Waziri wa Fedha John Mbadi, Waziri wa Madini Hassan Joho na Waziri wa Vyama vya Ushirika Wycliffe Oparanya. Kwa mujibu wa wachambuzi wa siasa, Rais atajaribu kuunganisha ujumbe wa maendeleo na ujumuishaji wa kisiasa kwa kuonyesha kuwa Nyanza haifai kuwa upande wa upinzani ili kupata rasilimali za kitaifa na uwakilishi serikalini. Lakini upinzani pia unajipanga. Makundi mbalimbali yanayowania urithi wa kisiasa wa Raila tayari yameanza kufanya ziara katika eneo hilo. Miongoni mwao ni vuguvugu la Linda Mwananchi ambalo limekuwa likisisitiza kuwa maendeleo peke yake hayawezi kuchukua nafasi ya uwajibikaji, utawala bora na kuheshimiwa kwa Katiba. Hali hiyo inakita ujumbe wa serikali wa maendeleo dhidi ya ujumbe wa upinzani unaojikita katika masuala ya utawala. Katika kaunti ya Kisumu, Rais anatarajiwa kuzindua mnara wa kudhibiti safari za ndege katika uwanja wa ndege, kukagua makao ya polisi na kuzuru barabara ya Mamboleo-Miwani-Chemelil-Muhoroni pamoja na miradi ya maji. Atazuru pia sekta ya Jua Kali. Katika Siaya, atakagua Daraja la Dhogoye, hospitali ya Siaya, miradi ya makazi, viwanja vya michezo na mtandao wa barabara katika maeneo ya Bondo, Ugenya, Alego Usonga na Rarieda. Mbunge wa Bondo Gideon Ochanda amesema Daraja la Dhogoye yatakuwa hatua kubwa kwa wakazi kutokana na umuhimu wake katika kurahisisha mawasiliano, usafiri na biashara. Migori nayo iko katika ratiba ya Rais ambapo atakagua barabara katika maeneo ya Uriri, Awendo na Suna Mashariki pamoja na kituo cha umeme cha Masaba katika Kuria Magharibi. Katika Homa Bay, Rais anatarajiwa kuzindua masoko, barabara za mji na miradi ya taasisi ya mafunzo ya matibabu ya KMTC ya Sindo. Wakati huo huo, viongozi wa eneo hilo wanataka miradi mikubwa kama Bwawa la Koru-Soin, Uwanja wa Moi Stadium na barabara ya Mamboleo-Miwani-Chemelil kukamilishwa haraka. Hatua za usalama pia zimeimarishwa kufuatia tukio la hivi majuzi Siaya ambapo vijana walidaiwa kujaribu kuzuia msafara wa viongozi waliohudhuria hafla ya kuwawezesha wanawake kiuchumi iliyoongozwa na Mama wa Taifa Rachel Ruto. Kamishna wa eneo la Nyanza, Onesmus Kyatha, amesema ziara hiyo inalenga maendeleo na kwamba maandalizi yote ya usalama yamekamilika ili kuhakikisha shughuli zinaendeshwa kwa utulivu.
read moreRight Column Content